Uchaguzi Monduli, CHADEMA waambuliwa kuulizwa nyie ni akinanani? Lowassa afanya new style ya siasa

Mtela Mwampamba

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
537
347
Kwa ufupi

  • Tukio hilo limetokea baada ya Lowassa kuibua staili mpya ya kampeni ya chama chake, ambapo badala ya kuhutubia amekuwa akiwapa nafasi wananchi kupanda jukwaani na kuzungumza.



Monduli. Kampeni za kuwania nafasi ya udiwani katika Kata ya Makuyuni wilayani Arusha juzi ziliambatana na tukio la kuchekesha baada ya wazee wa huko kupata wakati mgumu kutamka jina la
CHADEMA ambacho ni kifupi cha jina la Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Kata ya Makuyuni ina wakazi wengi ambao kwa kawaida huwa ni wafugaji na hawafahamu vizuri Lugha ya Kiswahili kutokana na maisha yao ya kijadi.
Mzee mmoja aliyetajwa kwa jina la Olengalepo aliwachekesha watu kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Naiti wakati aliposhindwa kutamka jina CHADEMA na badala yake kusema Sabena.
"Hawa Sabena (CHADEMA) kwani wametokea wapi?" alihoji Mzee huyo licha ya Mbunge wa Monduli, Lowassa kumwelimisha kwamba ni CHADEMA na siyo Sabena.
Mzee Olengalepo alichekesha zaidi watu wakati alipomjibu Lowassa."Hiyo hawezi mimi tamka, maana siijui." Jibu hilo lilifanya watu kuangua kicheko zaidi wakati wa mkutano huo ulioanza saa nane mchana kijijini hapo.
Tukio hilo limetokea baada ya Lowassa kuibua staili mpya ya kampeni ya chama chake, ambapo badala ya kuhutubia amekuwa akiwapa nafasi wananchi kupanda jukwaani na kuzungumza.
Lowassa anaongoza kampeni ya CCM ya kutetea kiti cha udiwani wilayani Monduli, ambao uchaguzi wake unafanyika Jumapili hii.
Goodluck Lerunya anawania nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM wakati Japhet Sironga ndiye anapeperusha bendera ya CHADEMA kwenye jimbo hilo.

Chanzo:gazeti la mwananchi
Tar.13/06/2013
 
Kama una akili timamu badala ya kurukaruka kwa furaha unapaswa kujiuliza kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kiwango cha elimu na upashamaji habari kwa Tanzania kiko chini kiasi kwamba kuna wananchi hawajui hata jina la chama kikuu ya upinzani? Kimsingi ni aibu kwa CCM kuwa bado tuna wananchi wenye uelewa mdogo kiasi hiki.
 
Huyo Mzee hata Kikwete asingeweza kutamka na pengine hata hamjui...irrelevant reference!

Mzee mmoja aliyetajwa kwa jina la Olengalepo aliwachekesha watu kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Naiti wakati aliposhindwa kutamka jina Chadema na badala yake kusema Sabena.
"Hawa Sabena (Chadema) kwani wametokea wapi?" alihoji Mzee huyo licha ya Mbunge wa Monduli, Lowassa kumwelimisha kwamba ni Chadema na siyo Sabena.
Mzee Olengalepo alichekesha zaidi watu wakati alipomjibu Lowassa."Hiyo hawezi mimi tamka, maana siijui."

 
Mtela mwampamba unapokua kimwili ujaribu na kukua kiakili, unaposema wazee wa uko wanashindwa kutamka jina la CHADEMA, kumbuka this is the second time mmerudi kufanya kampeni pale wewe na bosi wako mwigulu, tulimsikia Lowassa anaongea chonde chonde mkiichagua CHADEMA mtakuwa mmenichoma kisu, na leo hii Luawasa kaweka kambi kule

Mpaka hapo watu wa kule hawaijui chadema bado ? kumbuka awamu ya kwanza mlipoenda na siasa za kitoto na majitaka za matusi mlishushwa jukwaani

Kama umesoma kidogo tu unaweza kuelewa vizuri jambo hili, kwa wakati wa sasa chama kipi kinakuwa na uhakika zaidi ya ushindi kati ya kile kinachoshabikiwa na wazee au vijana , go back to study "demography"
 
ni aibu! Inadhihirhsha ufedhuli wa serikali ya magamba kutokuweka vipaumbele masuala ya msing kama elimu!! Mi nadhani kijana ungekaa na kutafakali madudu ya selikal yako na SIO KUROPOKA ROPOKA KAMA UMEFUMANIWA!!
 
Dogo unajua ukitaka kuheshimika ni kujilinda sana na kutoa ujinga , hilo linadhihirisha jinsi ulivyomtupu kichwani, hivi lile jina lako la chuoni unakumbuka lile la ganzi, ujajiuliza bado kwa nini uliitwa ganzi
 
ni aibu! Inadhihirhsha ufedhuli wa serikali ya magamba kutokuweka vipaumbele masuala ya msing kama elimu!! Mi nadhani kijana ungekaa na kutafakali madudu ya selikal yako na SIO KUROPOKA ROPOKA KAMA UMEFUMANIWA!!

Ndugu yangu kuna watu waliosoma na kuelimika lakini sio type za kina Mtela Mwampamba na Juliana , ukitaka kujua madhara ya Desa au pale SUA wanaita Simbi , mtu akirudi kwenye jamii unamuona waziwazi alivyomtupu kichwani, najiuliza hivi hawa walikuwa wanasoma kweli au walihesabu miaka tu pale chuoni
 
Mziki ni wa kwetu bila kupima DNA Vp mamilion yaende naijeria na usa? Kuwaponda wakubwa walioanguka ni kuwavunja moyo wachanga wanaoinuka ila mtela kwa hz utapiga deki nyumban kwa lowasa
 
Mimi nakumbuka pia pale Kiwira uchaguzi mdogo wa udiwani, bibi vizee walikuwa wanakuja kupiga kura wakionyesha ishara ya vidole viwili , kwa mtu muelewa kutamka au kushindwa kutamka jina la chama tena kwa wazee sio hoja ya kutuletea humu Mwampamba unatupotezea muda bure, endelea na kazi yako ya houseboy kwa mfalme wako, ila angalia asije akawa anakupa na tule tunguo twa nda.n ukawa unamfulia
 
Wee ni msemaji wa Chadema?
Bei yako kiasi gani? It seems uko cheap, anyone can afford you.
 
Kama una akili timamu badala ya kurukaruka kwa furaha unapaswa kujiuliza kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kiwango cha elimu na upashamaji habari kwa Tanzania kiko chini kiasi kwamba kuna wananchi hawajui hata jina la chama kikuu ya upinzani? Kimsingi ni aibu kwa CCM kuwa bado tuna wananchi wenye uelewa mdogo kiasi hiki.
Hii inaonyesha ni jinsi gani chama (CDM) kisivyo makini au kinafanya shughuli zake kwa upendeleo wa maeneo fulani ambapo kinaweza kutumia helikopta kwenye kampeni za udiwani Maeneo ya Arusha wakati kila siku kinadai ni ngome yake huku kuna sehemu nyingine nchini ambayo inahitaji resources zaidi, ukichukulia kuwa kwa sasa kina zaidi ya miaka 20 tokea kipate usajili kisiasa.
 
Kama una akili timamu badala ya kurukaruka kwa furaha unapaswa kujiuliza kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kiwango cha elimu na upashamaji habari kwa Tanzania kiko chini kiasi kwamba kuna wananchi hawajui hata jina la chama kikuu ya upinzani? Kimsingi ni aibu kwa CCM kuwa bado tuna wananchi wenye uelewa mdogo kiasi hiki.
Ni aibu kweli lkn kwa CCM ndio mtaji wao,wanatamani wote tungebaki hivyo au tuwe na akili kama za mleta mada,anafurahia wazee wa watu kutojua kiswahili sawasawa.
 
Back
Top Bottom