Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Mzee Killtime,

Magazeti ya bongo wengine huwa hatusomi kabisaa, na ndio hasa maana ya kuwa hapa ni baada ya kugundua kuwa media yote ya bongo ni usaniii,

kujibu your hoja ni kwamba habari ni nyingi mno, lakini tatizo ni uthibitishaji, kabla ya kuziweka hapa, halafu hapa tunajitolea tu, hatulipwi kwa hiyo nilifikiri kuwa angalau utakuwa na shukrani kidogo kwa hizo chache tunazozileta, as opposed na forum zingine ambazo hakuna kitu kabisaa!

Hayo magazeti na sisi at this point ambapo CCM hawajatangaza rasmi majina, tunakua kwenye the same boat yaani ni data tu!

Ahsante Mkuu!
 
Nimesona Thread nzima, Sijaona hao waheshimiwa wenye link nzuri na NEC na CC, walivyoweza kutupatia kwa uhakika list ya waliopitishwa na waliotemwa!

..halafu info nyingine ni misleading!

Habari naziona za vipande vipande na Zingine zinatofautiana na za magazeti ya hapa nchini, kwa mfano issue ya Dada Salome Mbatia...

..ila ya huyu iko kinyume!magazeti yatakuwa sahihi zaidi.
 
"CCM yatema mawaziri wanane kuwania NEC

2007-08-02 10:27:47

Na Mary Edward, PST Dodoma

Wakati Chama cha Mapinduzi kimeshikwana kigugumizi kuwataja wagombea waliotemwa na waliopitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, imebainika kuwa, Mawaziri na Naibu Mawaziri wanane, wametupwa nje ya kinyang`anyiro hicho.

Mawaziri hao, wametemwa kwenye kikao cha mchujo cha siku mbili cha NEC kilichokutana mjini hapa juzi na jana.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu mbalimbali vimewataja baadhi ya vigogo walioenguliwa kuwania nafasi hiyo nyeti ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Salome Mbatia na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rita Mlaki.

Hali kadhalika, vyanzo hivyo vya habari, vimewataja Bw. Kisyeri Chambiri na Chacha Mwita Gachuma kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ndani ya chama hicho ambao safari hii wametupwa nje kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara.

Vigogo wengine wa CCM ambao wametemwa kwenye mchujo huo ni pamoja na Bw. Didas Masaburi na Chacha Nyamoyo Wambura? aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC kupitia Umoja wa Wazazi Tanzania.

Taarifa zaidi zilidai kuwa, mwenyekiti wa sasa wa Mkoa wa Mtwara aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC, alianguka na kupoteza fahamu kikaoni baada ya jina lake kuondolewa katika mchujo huo."

Mzee Dar na Killtime, mnasema hii habari ina ukweli zaidi ya habari zilizoko kwenye thread yetu? Kubainika ni ukweli as a fact? Halafu hayo magazeti wamechemsha kwa sababu Mbatia hakunyimwa kugombea ujumbe, ila ameondolewa kwenye bodi ya hazina(CCM), lakini bado amepewa nafasi ya kugombea nafasi hiyo ambapo atachuana na Mama Megji! Sisi na wao magazeti tuko boti moja, ni data tu, mpaka kesho CCM watakapotangaza na tutaendelea kuzichokonyoa!

Na the latest zinasema wenyeviti wengi wa CCM wa mikoa wamepigwa chini!
 
"CCM yatema mawaziri wanane kuwania NEC

2007-08-02 10:27:47

Na Mary Edward, PST Dodoma

Wakati Chama cha Mapinduzi kimeshikwana kigugumizi kuwataja wagombea waliotemwa na waliopitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, imebainika kuwa, Mawaziri na Naibu Mawaziri wanane, wametupwa nje ya kinyang`anyiro hicho.

Mawaziri hao, wametemwa kwenye kikao cha mchujo cha siku mbili cha NEC kilichokutana mjini hapa juzi na jana.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu mbalimbali vimewataja baadhi ya vigogo walioenguliwa kuwania nafasi hiyo nyeti ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Salome Mbatia na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rita Mlaki.

Hali kadhalika, vyanzo hivyo vya habari, vimewataja Bw. Kisyeri Chambiri na Chacha Mwita Gachuma kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ndani ya chama hicho ambao safari hii wametupwa nje kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara.

Vigogo wengine wa CCM ambao wametemwa kwenye mchujo huo ni pamoja na Bw. Didas Masaburi na Chacha Nyamoyo Wambura? aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC kupitia Umoja wa Wazazi Tanzania.

Taarifa zaidi zilidai kuwa, mwenyekiti wa sasa wa Mkoa wa Mtwara aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC, alianguka na kupoteza fahamu kikaoni baada ya jina lake kuondolewa katika mchujo huo."

Mzee Dar na Killtime, mnasema hii habari ina ukweli zaidi ya habari zilizoko kwenye thread yetu? Kubainika ni ukweli as a fact?

..nusu ukweli nusu speculation!

..by far magazeti huwa na nyeti fulani,hata humu watu hu-post kutokana na hizo za mags!
 
Hali kadhalika, vyanzo hivyo vya habari, vimewataja Bw. Kisyeri Chambiri na Chacha Mwita Gachuma kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ndani ya chama hicho ambao safari hii wametupwa nje kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara.

Vigogo wengine wa CCM ambao wametemwa kwenye mchujo huo ni pamoja na Bw. Didas Masaburi na Chacha Nyamoyo Wambura? aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC kupitia Umoja wa Wazazi Tanzania.

Kisyeri Chambiri na Chacha Gachuma ni wazi kafara ya vurugu zao kule Musoma na kuachia CHADEMA kuchukua jimbo la Tarime. Hawa kina Chambiri wanajiona kama machifu wa Musoma na ndio chanzo kikubwa cha kuanguka CCM kule. Vilevile wana tuhuma nyingi mno...

Didas Masaburi ni wazi ubabe wake umemfikisha pabaya. Hata wakati ule wa kugombea ubunge wa Africa Mashariki alilazimisha kupitishwa ingawa hakuwa chagua la wakubwa wa CCM. Alifikia hata kuwatisha wenye chama hivyo wakashindwa kumtosa katika kuhesabu kura ambako inadaiwa kuna mambo yalifanyika kuwahisani kina KABOUROU. Yeye ndiye ilikuwa apigwe chini lakini wazee wa busara waka amua kutotoa mwanya wa vurugu ambazo zingelitokea miongoni mwa wabunge ambao walikuwa wakimshabikia. Sijui nini hatima ya mke wake ambaye ni mbunge wa viti maalum..mambo ya couple za kisiasa hayo.

Mengine yanawekwa kapuni maana yanatisha kidogo...

Tanzanianjema
 
Watakao wania NEC CCM hawa hapa

Maulid Ahmed, Dodoma
HabariLeo; Friday,August 03, 2007 @00:03

http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=3289
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), jana kilitangaza wagombea mbalimbali waliopitishwa kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.

Wagombea hao ni wale wanaowania uenyekiti wa chama hicho kwa ngazi ya Wilaya na Mikoa na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia katika makundi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Uenezi na Itikadi, waliopitishwa kwa Kundi la Tanzania Bara kuwania viti 20 vya NEC ni pamoja na Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba.

Wengine ni Abdulrahman Kinana, Novatus Makunga, Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Shyrose Bhanji, Juma Kapuya, Hamida Kilua, Lucas Kisasa, John Komba, Dk. Makongoro Mahanga, Mohammed Mamoon, Wilson Masilingi, Bernard Membe, William Ngeleja, Kingunge Ngombale-Mwiru, Salim Hamis Salim ‘Chicago’, Frederick Sumaye, William Lukuvi, Siwajibu Clavery, Jaka Mwambi, Job Ndugai, John Simbachawene, Abdul Adam Sapi, Frank Uhahula, Dk. Diosdorus Kamala, Said Kilahama, Nicolas Zakaria, Dk. David Mathayo, Aggrey Mwanri, David Holela, Isdore Shirima, Stephen Wassira, Christopher Gachuma, Enock Chambiri, Maurus Mhimbila, Profesa David Mwakyusa, Emmanuel Mwambulukutu, Amos Makala, Baanda Ayoub Salum na, Jackson Msome.

Wengine ni Aborgast Godogodo, Dk. Alex Msekela, Constantine Kanyasu, Amos Siyantemi, Mohammed Mkumba, Profesa Idris Mtulia, Profesa Samwel Wangwe, Andrew Chenge, Jared Kaduga, John Chiligati, Pascal Mabiti, Said Fundikira, Abeid Mwinyimsa, Charles Kagonji, Ibrahim Msengi, Hassan Ngwilizi na Hashim Chakiondo.

Kwa kundi la Vijana ambao wana nafasi 15, waliopitishwa ni Mwamini Lusingu, Abdallah Mayomba, Omar Kiliati, Zainabu Kawawa, Sixtus Mapunda, Vanessa Mugeta, Nape Nnauye, Jerry Slaa, Ashura Selemani, Neema Mwakabonga, Deogratius Ndejembi, Edwin Sanda, Melkiador Januari, Penias Kaindoa, Rajabu Katunda, Benno Malisa na Paul Kirigini.

Wengine ni Lutengano Mwalywiba, Sara Ally, Adela Ng’asigwa, Rose Juma, Magembe Magembe, Pili Jadir, Jenista Mboneko, Violet Mzikandaya, Raymond Mwangwala, Lucy Mayenga, Francis Mtinga, Suleiman Nchambi, Hussein Basheikh na Rodgers Shemwelekwa.

Kwa nafasi 15 za Wazazi Bara, wagombea ni Fortunata Kabeja, Enock Kalumuna, Selina Mkonji, Mohammed Nondo, Salum Tambarizeni, Tambwe Hizza, Mustapha Yakub, Mussa Azzan ‘Zungu’, Ruth Msafiri, Thomas Ngawaiya, Henry Shekifu, Richard Nyaulawa, Innocent Kalogeris, Margaret Makanga, Aziz Jawad Aziz, Dickens Shindika, Dk Zainab Gama, Adam Malima, Stella Manyanya, Athuman Mfutakamba na Mgosi Bakari.

Nafasi 20 za Umoja wa Wanawake (UWT), waliopitishwa ni Halima Mamuya, Sifa Swai, Asha Baraka, Khadija Kopa, Jackline Liana, Anne Makinda, Jane Mihanji, Fatuma Mkwawa, Rita Mlaki, Regina Chonjo, Sophia Simba, Margaret Sitta, Kate Kamba, Shamsa Mwangunga, Pindi Chana, Amina Mrisho Saidi, Janath Kayanda, Sakina Kabeza, Anne Malecela, Salome Mbatia na Zakia Meghji.

Wengine ni Jackline Noni, Anna Magowa, Dk. Rehema Nchimbi, Chiku Galawa, Halima Kihemba, Fatma Kimario, Elizabeth Mwaipwani, Gulazar Sabil, Margaret Mkanga, Lydia Boma, Zuhura Mikidadi, Hellen Bogohe, Esther Nyawazwa, Mwanaidi Kiongoli, Zainab Vullu, Esha Stima, Diana Chilolo, Tatu Ntimizi, Dk. Aisha Kigoda, Mwantumu Mahiza na Beatrice Shelukindo.
 
Ahsante,

Other than kuhusu Nchimbi, hayo memgine mliyokuwa mnaongea ni UONGO naomba mtubu kwa Mwenyezi Mungu, maana bwana hapa JF kila mtu anajifanya yuko karibu sijui na JK, wengine usalama wa taifa, wengine wako karibu na Hosea, bora tu kila mmoja atafuje njia ya kufanya tuamini post zake...

Sasa mumeumbuka, Mbatia yumo, Mlaki yumo;

Au ndio kampeni alizokuwa amezikataa JK za kupakana matope... Kama hujui jambo nyamaza tu.
 
Hata mimi nimeshangaa, habari nyingi tulizokuwa tunaletewa hapa ni uongo mtupu. Ni tofauti na wakati ule wa uchaguzi wa rais ambapo mambo mengi yalikuwa sahihi.

Huyo mama Rita mmemsema bure kumbe yumo bado kwenye kapu la wanawake. Hivi hizi habari mlizitoa wapi? Hivyo hivyo kwa huyo mtoto wa JK.

In future kama huna uhakika na habari, usiilete hapa. Kwa kuandika majungu tutapoteza heshima ya JF
 
Hii list nayo pia ina walakini haijasema lolote kuhusu wajumbe wa kutoka kwenye mikoa!!!Yaani akina Mwandosya, Mangula etc...
 
Hata mimi nimeshangaa, habari nyingi tulizokuwa tunaletewa hapa ni uongo mtupu. Ni tofauti na wakati ule wa uchaguzi wa rais ambapo mambo mengi yalikuwa sahihi.

Huyo mama Rita mmemsema bure kumbe yumo bado kwenye kapu la wanawake. Hivi hizi habari mlizitoa wapi? Hivyo hivyo kwa huyo mtoto wa JK.

In future kama huna uhakika na habari, usiilete hapa. Kwa kuandika majungu tutapoteza heshima ya JF

Mtanzania,

Kwanza hongera CC, NEC, kwamba wanaweza kutunza siri zao, mpaka vyombo vyote vya habari pamoja na wanaojifanya mahiri JF kutolewa nje! na kuanza kubuni kutokana na MIOYO YAO[/B, alishasema JK, kwamba amefurahi kwamba yaliyosemwa kwenye magazeti sio kweli.... Wakati ya Zitto kuwa Naibu Katibu mkuu ilijulikana hata kabla mkutano haujaisha

Pili: hili ni fundisho kwamba mengi ambayo tunashabikia hapa mengine hayana lolote zaidi za zuhuma zisizokuwa na mshikio,,, kwa maana nyingine ni mazingira tu yanafanya watu tuamini JF wanayoandika lakini mengine uongo mtu!

Tatu:Kama haya mambo marahisi ambayo yali-involve watu wengi mmeongea uongo je mambo ya watu waili tu kama ya NGONO mnawezaje kuwa na ukweli kama si uzandiki tu

Nne: Nasikitika kwamba hili lisipokemewa hapa JF, kuna siku chombo hiki kitashuka chini kama vyombo vingine vilivyowahi kupuuzwa, Nadhani ingekuwa bomba member akiandika uongo na ukathibitishwa kwamba ni uongo ashushe daraja, kama alikuwa JF Senior expert ashushe chini
 
kushushwa daraja ?? IPPMEDIA wenyewe walikosea, sasa nao washushwe daraja kibiashara, sh*t happens men ! lakini kama ni excess uongo basi apuuzwe, na sio kama ulivyosema, mie nilisema na nilikuwa wa kwanza kusema mtoto wa jk jina lake halikupitishwa, and i still stand with what i say na wengine wakaanza bandwagon, na kusema kapitishwa wakidhani either nitakuwa wrong au yeye aliyesema hivyo atakuwa right ! well, i still stand with what i say and i know wapi nilipopata hizo info kwamba hakupitishwa !
 
Kilitime,

Nakubaliana na wewe. Hata baadhi ya magazeti mambo mengine wanachukua hapa. Sasa kama tunaandika majina ya watu ka makosa kiasi hivyo ni vibaya sana kwa reputation ya JF.

Mimi ningetaka wale wote walioandika habari za uongo hapa angalau waombe msamaha kama ambavyo IPPMEDIA wameomba msamaha.

Tukionekana mara mbili au tatu, tunasema mambo ambayo baadaye yanakuja kujulikana ni uwongo, huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa JF.

Hakuna haja ya kukurupuka na kuandika uongo, ni bora kuvuta muda na kupata habari za uhakika.

Niko dissapointed na quality ya info ambazo tulikuwa tunapata kwenye thread hii ya NEC ya CCM. Inabidi tujisafishe wenyewe. Mambo yakiwa hivi, mwaka 2010 JF si itakuwa balaa?
 
KadaMpinzani,

Sina tatizo na msema kweli hata kidogo! kama wewe ni miongoni mwao hongera,

Lakini binafsi nimechoka na UDAKU!!!
 
hii ni dunia kijana na kuna mengi mnoooooooooo kuchoka nayo, otherwise u just gonna have to give up on life kama umechoka the so called UDAKU ! kwani wee hujui watu walipolelewa, tz !
 
Kilitime,

Nakubaliana na wewe. Hata baadhi ya magazeti mambo mengine wanachukua hapa. Sasa kama tunaandika majina ya watu ka makosa kiasi hivyo ni vibaya sana kwa reputation ya JF.

Mimi ningetaka wale wote walioandika habari za uongo hapa angalau waombe msamaha kama ambavyo IPPMEDIA wameomba msamaha.

Tukionekana mara mbili au tatu, tunasema mambo ambayo baadaye yanakuja kujulikana ni uwongo, huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa JF.

Mtanzania,

Wakati najiunga na JF, nilidhani ni chombo fulani ambacho kinachambua mambo kwa kutopendelea mtu, taasisi, lakini kadiri muda ulivyoenda nikaona JF inanuda CHADEMA CHADEMA hivi, na wale niliokuwa nawaheshimu kwa uchambuzi wao nikawaona wamezibwa pazia la rangi za bluu za CHADEMA, na hii ni hatari sana, ndio maana naendelea kusema sisi tusiokuwa wananchama na washabiki wa vyama ndio tunahaki kamili ya kujadili mambo yenye masilahi ya vyama... Ndio maana kwenye bunge la jamhuri kanuni zinataka utangaze maslahi kwenye jambo unalochangia ili kusiwe na conflict of interest! Sasa hapa JF watu wame-declare kwamba wao ni CHADEMA damu alafu wanatuletea umasaku kujifanya wanachambua mambo ya CCM bila upendeleo... Kwa jina la... NAWASHINDWE NA KULEGEA.
 
hii ni dunia kijana na kuna mengi mnoooooooooo kuchoka nayo, otherwise u just gonna have to give up on life kama umechoka the so called UDAKU ! kwani wee hujui watu walipolelewa, tz !

KadaMpinzani,

Inasikitisha kwamba unashabikia UDAKU na unaamini hatuwezi ishi au habarishana bila kusema ukweli.

Kubuni uongo just kwa sababu ya mazingira yanaruhusu hivyo, ni sawa sawa na mganga wa kienyeji ambaye siku zote anatumia mazingira ya mgonjwa wake,,, kubuni kwamba amelogwa na mwanamke mweusi jirani yake (of which lazima uwe na jirani mweusi na mwanamke kwa mazingira ya nchini kwetu) hii husabisha wagonjwa kuamini hivyo... Hivi hivi ndivyo mlivyomzuishia ZITTO kwamba ameonja tunda la mwanamke aliyeolewa just b'se walikuwa kwenye mazingira ya kuwa pamoja.
 
Wazee hebu niulize kwani waht is the beef?

Nilisema Salome Mbatia, Anne Kilango Malecela, Mama Meghji, Lowassa, Sumaye, Masha wamepita, Beatrice Shelukingo, wamepita!

Error of margin, ni Ridhiwani huenda hakupita kama nilivyosema, sasa 8 vs 1, kuna mtu ananialaumu kwamba tulileta udaku? are serious au huelewi unachosema?

Mbona magazeti makubwa ya dunia kila siku yana corrections sasa hapa JF kuna nini tofauti au ni gele tu hiyo?

Acheni hizo wakuu, mnachoshusha ni heshima za majina yenu sio heshima ya forum, hata siku moja haitashuka, forum namba moja!
 
"Mama Salome Mbatia, pamoja na kupitishwa kugombea NEC, lakini amepumzishwa kutoka nafasi ya bodi ya CCM ya hazina, badala yake amepewa Rostam, it was a bitter uchaguzi, mama amekasirika sana.

Makamu wa Malegesi, anyeitwa bwana Mzuri naye ametupwa kiroho mbaya, I mean nje!

Beatrice Shelukingo, amepitishwa!"

Haya ndiyo tulisema na yametokea kama tulivyosema! Udaku uko wapi?
 
Back
Top Bottom