Ni vita NEC CCM
Mwandishi Wetu
SALOME Joseph Mbatia hatunaye. Amefariki dunia kwa ajali ya gari Jumatano iliyopita akiwa Njombe, mkoani Iringa. Kifo cha mama huyo mchapakazi aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55, kimemkuta akiwa katika harakati za kisiasa, akiwa katika hatua za mwisho za kujinadi aweze kupenya katika tundu la Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mpinduzi (CCM).
Hadi mauti yanamfika, Salome alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa anawania kupitia Kundi la UWT (Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania).
Na saa mbili kabla ya kifo chake, alikuwa mjini Iringa alikoacha vipeperushi vyake ili wapiga debe waendelee kumnadi huku yeye akiendelea kusaka kura wilayani Njombe. Kwa bahati mbaya, amefariki kabla ya kutimiza ndoto yake.
Salome alikuwa mmoja kati ya kundi kubwa la wana-CCM waliopitishwa kuwania nafasi 85 za ujumbe wa NEC kutoka makundi mbalimbali.
Lakini mchuano mkubwa zaidi unaofananishwa na 'vita ya kisiasa' unaonekana kuwa katika 'Kapu' la 'vigogo' 59 linalopaswa kutoa watu 20 tu!
Pengine ni kutokana na ugumu huo, kwa takriban miezi miwili ziara za viongozi wengi wa chama na serikali mikoani zilikuwa hazikauki - lengo kubwa likiwa kujinadi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa (CCM).
Katika kapu, kuna wazito kama Waziri Mkuu, Edward Ngoyai Lowassa, Frederick Tluway Sumaye, waziri mkuu aliyemwachia 'ziwa' Lowassa, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Rajab Makamba, naibu wake, Jaka Mwambi, naibu katibu mkuu wa zamani, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu, orodha ndefu ya mawaziri na manaibu waziri pamoja na wabunge mashuhuri.
Wagombea wengine waliopitishwa katika kundi hilo ni pamoja na mkongwe wa siasa tangu enzi za TANU, 'babu' Kingunge Ngombale-Mwiru anayekabana koo na wajukuu zake katika kapu la CCM.
Kwa sasa, Kingunge mwenye umri wa zaidi ya 70, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia siasa na uhusiano wa jamii.
Wengine ni Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Shy-Rose Bhanji, Enock Chambiri, John Chiligati, Siwajibu Clavery, Dk. David Mathayo, Said Masoud Fundikira, Christopher Mwita Gachuma, Arbogast Godogodo, David Holela, Jared Kadunga, Charles Kagonji, Dk. Deodorus Kamala, Constantine Kanyasu, Profesa Juma Kapuya na Alhaj Said Kilahama.
Wengine katika kundi hilo ni Haidah Kilua, Abdulrahman Kinana, Lukas Kisasa, John Komba, William Lukuvi, Pascal Mabiti, Dk. Milton Mahanga, Amos Makala, Novatus Makunga na Mohamed Yakub Mamoon.
Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Wilson Masilingi, Maurus Mhimbira, Mohammed Mkumbwa, Dk. James Msekela, Dk. Ibrahim Msengi, Jackson Msome, Profesa Idrisa Mtulia, Profesa David Mwakyusa, Aggrey Mwanri, Abeid Mwinyimsa na Job Ndugai.
Orodha ni ndefu kwani inawahusisha pia William Ngeleja, Dk. Banda Salim, Salim Khamis Salim, Abdul Adamu Sapi, Isidore Shirima, George Simbachamwene, Amos Siyantemi, Dk. Hashim Twaakyondo, Frank Uhaula, Profesa Samuel Wangwe, Stephen Wassira 'Tyson' na Nicholaus Mateso Zacharia.
Katika kampeni hizo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba kuna baadhi ya vigogo (majina tunayo), walilazimika kufanya kila linalowezekana lengo si kushinda ujumbe wa NEC tu bali pia kushika usukani katika pointi.
Mathalan, kigogo mmoja wa CCM amekuwa akizunguka na kusisitiza apigiwe kura akidai kwamba itakuwa aibu kwake kupenya kwa kura chache katika kundi hilo la 'kifo'.
Inadaiwa amekuwa akisisitiza kwamba ana uhakika wa kushinda, lakini anataka ushindi wa 'kishindo' utakaoonyesha kukubalika kwake badala ya kushika nafasi kwa mfano ya kumi katika nafasi hizo 20.
"Anasema waziwazi kwamba ana uhakika wa kushinda, lakini anataka kuongoza
" kimeeleza chanzo chetu.
Mtazamo huo pia upo kwa kigogo mwingine wa juu serikalini anayedaiwa kukosa usingizi na kuhimiza 'wakubwa' mikoani na wilayani kuhamasisha apigiwe kura ili aibuke kinara zaidi ya wengine katika kundi hilo.
Hao ni 'wakubwa', lakini na wengine pia hawakulala, kila mmoja anapigana kikumbo kivyake kuhakikisha anaibuka na ushindi katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia Novemba 3 mjini Dodoma. Mkutano huo ni maalumu kwa uchaguzi.
Mbali ya wagombea watakaochuana kuwania nafasi 20 za 'Kapu' na wengine waliokwishapatikana kwa tiketi ya mikoa, wagombea wengine na makundi yao ni kama ifuatavyo;
KUNDI LA UWT:
Katika kundi hili ambalo hayati Salome Joseph Mbatia alikuwa mmoja wa wagombea, wanaowania kuingia NEC ni Halima Mohamed Mamuya, Mbunge na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT.
Wengine ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Semamba Makinda, Waziri Sofia Mnyambi Simba, Waziri Margareth Simwanza Sitta, Sifa Amani Swai, Asha Ramadhani Baraka, Khadija Omar Kopa, wanahabari Jacqueline Liana na Jane Claude Mihanji.
Pia wamo Waziri wa Fedha, Zakia Hamdani Meghji, Kate Magdalena Kamba, Fatuma Adam Sapi Mkwawa, Rita Louise Mlaki, Chonjo Reginald Regina, Shamsa Selengia Mwangunga, Pindi Hazara Chana, Hajjat Amina Mrisho Said, Janath Mussa Kayanda, Sakina Said Kabeza, Anna Kilango Malecela, Jacqueline Noni, Anna John Magowa, Dk. Rehema Jonathan Nchimbi, Chiku Abdallah Sumbu Gallawa, Halima Meza Kihemba, Fatuma Kimario, Elizabeth Sanga Mwaifwani, Gulzar A. Sabir, Margareth Agness Mkanga, Lydia Thecla Boma, Zuhura Bashekhe Mikidadi, Ellen Makungu Bogohe, Ester Kabadi Nyawazwa, Mwanaidi Maliki Kiongoli, Zainab Matiku Vulu, Esha Hassan Stima, Diana Mkumbo Chilolo, Tatu Mussa Ntimizi, Aisha Omari Kigoda, Mwantumu Bakari Mahiza na Beatrice Matumbo Shelukindo.
KUNDI LA VIJANA:
Katika kundi hili wamo Mwamini Lusingu, Abdallah Ramadhani Mayomba, Omari Yusufu Kiriati, Zainab Rashidi Kawawa, Sixtus Raphael Mapunda, Vanessa Mugeta, Nape Moses Nnauye, Jerry William Slaa, Ashura Abubakar Suleiman, Neema Heri Mwakabonga, Deogratius Ndejembi, Edwin Mgante Sanda, Melkiado January, Penias Peter Kaindoa, Rajab Thabit Katunda, Beno Malisa, Paul Herman Kirigini, Lutengano George Mwalwiba, Sarah Msafiri Ally, Adela Albert Ng'atigwa, Rose Kashinde Juma, Magembe Boniphase Cornel Magembe, Pili Mwajiri Jabiri, Jasinta Venant Mboneko, Violete Mzindakaya Mpogolo, Raymond Stephen Mwangwala, Lucy Mayenga, Francis Issack Mtinga, Suleiman Masoud Nchambi, Hussein Mohamed Bashe na Rojas Yakob Shemwelekwa.
KUNDI LA WAZAZI:
Wanaowania U-NEC kwa tiketi ya wazazi ni Thomas Ngawaiya, Fortunata Moses Kabeja, Enoc Kalumuna, Selina Adolf Mkonyi, Mohamed Nassoro Nondo, Salim Shomvi Tambalizeni, Richard Hiza Tambwe, Mustafa Yakubu, Mussa Azzan Zungu, Ruth Msafiri, Henry Daffa Shekifu, Richard Said Nyaulawa, Innocent Kalogeris, Danhi Beatus Makanga, Azizi Jawad Aziz, Dickens Kulwa Shindika, Dk. Zainab Amiri Gama, Adam Kighoma Ali Malima, Mhandisi Stella Martine Manyanya, Athuman Rashid Mfutakamba na Mgosi Semtumbi Bakari.
Je, baada ya mchakato mzito wa kusaka kura, ni nani atakayeibuka na ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri katika medani ya siasa nchini? Tusubiri.
Source: Tanzania Daima