Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

ES


1. Ridhiwani anagombea ujumbe wa mkutano mkuu kama mwakilishi wa wilaya ya Bagamoyo. Hagombei NEC kama ulivyodhani hapo awali.

Ushahidi huu hapa:

http://dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=2046



2. Zitto kuteuliwa Naibu Katibu Mkuu ni habari inapewa uzito wa hali ya juu, badala yake kina Nchimbi na Amina ndio wanalaumiwa kweli kweli kuhusu kadhia wakati na Zitto nae alikuwa ni mhusika mkuu.


Katika enzi hii ya vijana kuaswa kuachana na maambukizi ya UKIMWI Zitto anaonekana kidume! kwa kutembea na mke wa mtu, hata kama kajipitisha?! Inamaana richmond ikijipitisha napo kosa litakuwa ni la richmond kujipitisha sio Zitto kula rushwa?



Lakini the bottom line mimi in my personal capacity nisingemshari Ridhwani aingie kwenye siasa kwa wakati huu kutokana na sababu nilizozitoa hapo awali
 
Mzee Mugongo mugongo,

Ridhiwani ni mmoja wa wagombea wa nafasi 20 za Halmasahuri kuu CCM (Wanaume), ambazo wana-ccm 60 wakiwemo Lowassa, na Sumaye wamezigombea na kupitishwa na kikako cha kamati kuu kilichokutana hivi karibuni Dodoma, Kikao hicho pia kilipitisha majina 39 ya wagombea wa kike wanaogombea nafasi 13 za ujumbe wa Halamshauri Kuu ya CCM, you have a point and I will take back the confusion between NEC na Halmashauri Kuu, lakini bado ninasema kuwa wamepitishwa na Mwanri anatakiwa kutangaza leo au kesho rasmi,

Unless wewe unajua zaidi ya walioshiriki kwenye kikako hicho cha kamati kuu ambako ndiko ninakotoa hizi data, tena kwa taarifa yako wengi kati ya hao wagombea wamekuwa wakijipanga line kwenye pm yangu kutaka kujua kama ninazo info zao za kuchaguliwa au kutopitishwa,

Mammbo mengine ndugu yangu ni kwamba katika maisha kuna kitu kinaitwa facts of life, wewe angalia mkono wako utaona vidole vyako havifanani kimoja kirefu kuliko vingine na mkono ni wako wewe mwenyewe, vilivyoundwa huwa vinaelea, wengi hapa wameelewa ninachosema kama hujaelewa nitafute kwenye pm nitakusaidia, kwenye malumbano ya siasa kama hapa forum, ni muhimu sana kutumia back channels kama kuna kitu huelewi!

Otherwise nitaendelea kuvimwaga nipe kama masaa mawili hivi nitamwaga vitu zaidi!
 
Komandoo,

Lete mavitu hapa!! Tunasubiri kwa hamu kupata data!!!
 
CCM yatema mawaziri wanane kuwania NEC

2007-08-02 10:27:47

Na Mary Edward, PST Dodoma


Wakati Chama cha Mapinduzi kimeshikwana kigugumizi kuwataja wagombea waliotemwa na waliopitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, imebainika kuwa, Mawaziri na Naibu Mawaziri wanane, wametupwa nje ya kinyang`anyiro hicho.

Mawaziri hao, wametemwa kwenye kikao cha mchujo cha siku mbili cha NEC kilichokutana mjini hapa juzi na jana.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu mbalimbali vimewataja baadhi ya vigogo walioenguliwa kuwania nafasi hiyo nyeti ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Salome Mbatia na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rita Mlaki.

Hali kadhalika, vyanzo hivyo vya habari, vimewataja Bw. Kisyeri Chambiri na Chacha Mwita Gachuma kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ndani ya chama hicho ambao safari hii wametupwa nje kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara.

Vigogo wengine wa CCM ambao wametemwa kwenye mchujo huo ni pamoja na Bw. Didas Masaburi na Chacha Nyamoyo Wambura? aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC kupitia Umoja wa Wazazi Tanzania.

Taarifa zaidi zilidai kuwa, mwenyekiti wa sasa wa Mkoa wa Mtwara aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC, alianguka na kupoteza fahamu kikaoni baada ya jina lake kuondolewa katika mchujo huo.


Je CCM sasa wapo makini au ndio mtandao unafanya vitu vyake?
 
Mtu wa pwani,

Sasa hiyo picha inaendana na wewe!! Naona umefuata nyayo za Komandoo!!
 
Wazee Mugongo na Komandoo ES,
Mnakosoana kiutu uzima na kiungwana bila matusi! At the end wanaofaidika ni wasomaji - ni mfano wa kuigwa.
 
Mzee Nungux2,

Heshima mbele, nia kuelimishana na kuelimisha sio matusi, na Mugongo ni good educator kwa heshima mbele!

Na ninakaribia kumwaga mavuts, bado ninazi-verify kwanza!
 
Sasa majina yaliyopitishwa na kamati kuu, kwa ajili ya wajumbe watakaogombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM(NEC), imethibitishwa kuwa yatatangazwa rasmi hapo kesho majira ya mchana,

Habari za ndani zinazidi kuthibitisha kuwa Rita Mlaki ametupwa nje, lakini Salome Mbatia ampitishwa kwa taaabu sana!

Wakulu hawapatikani kutoa data maana wako kwenye msiba wa mama yake Masima, aliyekuwa mgombea wa CCM mkoa Dodoma, na mkuu wa wilaya kwa muda mrefu sana, wakimaliza tu hapo msibani tutaziweka hapa info!



.....stay tuned.....!
 
Okay,

Mama Salome Mbatia, pamoja na kupitishwa kugombea NEC, lakini amepumzishwa kutoka nafasi ya bodi ya CCM ya hazina, badala yake amepewa Rostam, it was a bitter uchaguzi, mama amekasirika sana.

Makamu wa Malegesi, anyeitwa bwana Mzuri naye ametupwa kiroho mbaya, I mean nje!

Beatrice Shelukingo, amepitishwa!

Ahsante Wakuu!
 
Muungwana imebidi atumie nguvu za ziada, na arms twisting kumpitisha Mama Meghji, ambaye wajumbe wengi walikuwa wameamua kumtosa,

Hali ni shwari lakini ukweli ni kwamba sasa ni saa ya mtandao na tayari imeshika hatamu kutokana na uchaguzi huu!
 
Nchimbi atamfuata rafiki yake guninita

naona guninita anataka kurudi kwenye system ya ccm kwa kutoana jasho na hemed mkali kuwania uenyekiti wa ccm dar..sijui watampitisha..
kimsingi boyz 2 men lazima watatafuta namna ya kumuenzi guninita..kumbukeni guninita na sukwa said sukwa ndio majeruhi wa kwanza wa utawala wa mkapa ..baada ya umoja wa vijana mwaka 1995 kutangaza rasmi kuwa watawaunga mkono wagombea vijana yaani jk na lowassa...baada ya mkapa kuingia guninita alibwagwa na sukwa akawa demoted kuwa katibu wa chama wilaya huko tanga ..sijui yupo wapi leo....guninita aliingia CHADEMA baadaye akajitoa ..naona amerudi ccm baada ya dalili za muungwana kuingia.....kiukweli guninita ni mmoja wa majeruhi wa mwanzo wa safari ya jk ikulu zaidi ya miaka kumi iliyopita..nadhani anaweza kuwa na sababu ya kumuokota...
 
Mzee Dar,

Sijakuelewa vizuri, exactly rais wetu anapigwa fix na nani? Na toka aingie urais mwaka 2005, ni fix ipi aliyowahi kupigwa unayoijua?

..kwani observation yangu ilitokana na jibu la swali la mwisho la ssali.

Ni lazima tuwe waangalifu na hoja nzito kama yako, kwa sababu rais wetu kama wengine wote duniani wanapewa majukumu ya kila siku kwa kutumia sheria za nchi, na ni majukumu ambayo sisi wananchi tumeona kuwa a sitting president atayaweza kwa kusaidiwa na wasaidizi wake, sasa rais atapigwaje fix, na huku tumemchagua kutokana na kutuhakikishia wakati wa kampeni kuwa anao uwezo kuliko wagombea wengine wote, sasa fix itatoka wapi?

..nzito kama nini?hizo false info?

Jamani tuache kuwapa free pass viongozi wetu, ni lazima tuwawajibishe, maana kama alivyosema Bwana Reagan, "The buck stops here, at the president"

..hapewi mtu pass wala free yake! kwanza that sentence was coming from seemingly sad and at times lonely man!

..kuongoza ni kazi kubwa si mchezo,hasa sasa!
 
Nimesona Thread nzima, Sijaona hao waheshimiwa wenye link nzuri na NEC na CC, walivyoweza kutupatia kwa uhakika list ya waliopitishwa na waliotemwa!

Habari naziona za vipande vipande na Zingine zinatofautiana na za magazeti ya hapa nchini, kwa mfano issue ya Dada Salome Mbatia...
 
Back
Top Bottom