Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

MwanaCCM

Senior Member
Feb 5, 2007
110
23
Ndugu wanaForum , nianze kusema Kidumu Chama Cha Mapinduzi!!! Kama siyo CCM niseme Habari Yako!!


Hawa ndio wakuu wa CCM kwa sasa.
leaders_kiswahili.jpg


Chama Cha Mapinduzi {CCM} kitaanza Uchaguzi wa Viongozi wake kutoka Ngazi ya Shina hadi Halmashauri Kuu ya Taifa kwanzia tarehe 20 Mwezi huu.. Kuelekea huko lazima kuwe na matukio au taarifa mbalimbali. Naam tuanze basi leo kwa habari ifuatayo nayo ni :-

'Ndumilakuwili CCM' K'njaro matumbo moto​

Kutoka Gazeti ; Mwananchi
Ally Sonda, Kutoka Moshi Anasema

BAADHI ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, wameanza utekelezaji wa agizo la kutowachagua viongozi ndumilakuwili katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika hivi karibuni.

Agizo hilo lilitolewa hivi karibuni na Mlezi wa Chama hicho mkoani humo, ambaye pia ni Waziri Mkuu, Edward Lowassa .

Mwananchi limebaini kuwa, utekelezwaji wa agizo hilo , unafuatia kuundwa kwa makundi maarufu kama kambi ya kampeni za baadhi ya wanachama wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Kambi hizo tayari zimeanza kazi ya kuwanadi wagombea wao na wakati huo huo, zikiwatangaza wagombea wengine vibaya.

Mwanakambi mmoja wa mgombea (jina la nafasi linahifadhiwa) ameliambia Mwananchi jana kuwa, makambi mengi yaliyoundwa ni ya kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi za uongozi ngazi za wilaya na mkoa.

Amezitaja baadhi ya nafasi ambazo tayari wagombea wake wameunda makambi ya kampeni kuwa ni ya uenyekiti wa mkoa, uwakilishi wa halmashauri kuu ya taifa kutoka Kilimanjaro , ukatibu uenezi na uweka hazina wa mkoa.

" Sasa hivi ndugu yangu wanaume na wanawake ngangari wapo kazini, kampeni hazijaanza lakini pitapita imeanza, ni lazima tutekeleze agizo la Lowasa.... wale ndumilakuwili lazima tuwajue mapema na tuwang'o, " alisema mwanakambi mwingine.

WanaCCM hao, walisema kuwa baadhi ya viongozi waliokisaliti chama hicho mwaka juzi kwenye uchaguzi Mkuu hususan Jimbo la Moshi Mjini, wana uwezo wa kujieleza kisiasa, hali ambayo imekuwa ikiwawezesha kurejeshwa tena kwenye uongozi.

" Hawa viongozi wetu wanaotoaga siri za mikakati ya Chama kupata ushindi na kuipeleka upande wa upinzani wana uwezo mkubwa wa kujieleza jukwaani wakati wakiomba kura..baadhi yao siasa wanaijua, lakini mwaka huu tunawangofoa, kauli ya Lowassa ni nzito lazima ifanyiwe kazi kwa faida ya Chama.

Mwananchi ilipomuhoji jana kwa njia ya Simu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kiliamnjaro, Vicky Nsilo Swai endapo ameunda kambi, alisema yeye hana haja ya kuunda kambi wala kikundi cha kampeni kwa madai kuwa wapiga kampeni wake ni wanachama wote.

" Wewe unataka niwe na kambi au unaniuliza kama nina kambi mimi sina kambi ya kampeni, kambi yangu ni wanaCCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, wanajua nimewafanyia nini kwa miaka mitano sasa," alisema Vicky na kukata simu yake.

Baadhi ya wanachama wamebainisha kuwa kiongozi yeyote wa CCM kuanzia ngazi za mashina hadi mkoa aliyetimiza wajibu wake baada ya kuchaguliwa mwaka 2002, atarejeshwa tena kwenye uongozi, endapo atawania tena, mwaka huu.

Akiwa mjini Moshi mwanzoni mwa mwezi huu Lowassa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, aliagiza wale wote waliokihujumu chama wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka juzi, wasichaguliwe tena kwenye uchaguzi wa chama mwaka huu.

Hapo Hapo

Kutoka Gazeti la Mwananchi
Mussa Juma, Kutoka Arusha Anasema

CCM waguswa mgogoro wa wananchi, manispaa

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha kimeingilia kati mgogoro ulioibuka kati ya wakazi wa Muriet Kata ya Sokoni 1 na Manispaa ya Arusha baada ya kutakiwa kuvunja nyumba zao kupisha mradi wa upimaji viwanja.

Habari kutoka ndani ya CCM ambazo zilithibitishwa na Katibu wa Wilaya, Ngang'aso Ndekubali na viongozi wa CCM wa Kata hiyo na Murieti, zimeeleza hatua hiyo kuingilia kati mgogoro huo imekuja baada ya kubaini kuna mapungufu katika utekelezaji agizo la manispaa.

Viongozi wa juu ya chama hicho, juzi walipanga kufanya mkutano wa hadhara na wakazi hao, lakini walishindwa baada ya kuzuiwa na mvua iliyokuwa ikinyesha.

" Ni kweli tulikuwa tupite pale lakini tulikuwa na mambo mengine pia ikiwepo huu ugonjwa wa homa ya bonde la ufa, " alisema Ndekubali.

Hata hivyo, alisema kitendo cha wakazi hao kufungua kesi kinaweza kuwazuia kushughulikia suala hilo.

Kata ya Sokoni 1 kilipo kitongoji cha Muriet inaongozwa na Diwani wa Tanzania Labour Party (TLP), Michael Kivuyo na habari za uhakika zinaeleza kuwa kama manispaa hiyo, itavunja nyumba hizo Serikali ya CCM itaendelea kupingwa katika kata hiyo.

Kwa zaidi ya miezi miwili sasa kumeibuka mgororo mzito katika eneo hilo hasa baada ya Manispaa hiyo kuwapa notisi wakazi hao ya kuvunja nyumba zao, ndani ya siku saba, la sivyo itazivunja.

Notisi hiyo ilimalizika mapema wiki iliyopita, lakini hata hivyo, kabla ya manispaa hiyo kuanza kutekeleza amri hiyo, wakazi hao wamefungua kesi na kupinga kuporwa eneo lao.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Job Laizer amekuwa akidai eneo hilo ni mali yao ambalo walikabidhiwa na Shirika la Mifugo la TLMP miaka 20 iliyopita, wakati wakazi hao, wanadai ni mali yao na kwamba eneo holo linamilikiwa kimila tangu enzi za ukoloni na ndiyo sababu iliyoifanya manispaa hiyo, mwaka 1999 kuomba ekali 60.

NB: Nitaendelea kutoa taarifa kutoka katika makao makuu ya chama au kutoka katika vyombo vya habari mbalimbali! nchini.

Kusoma habari zaidi kuhusu Chama Cha Mapinduzi tembelea tovuti yetu www.ccmtz.org

CCM Oyeeeeeeeeeee!!!
 
Eh!

CCM nawatakia uchaguzi mwema natumaini sasa hivi mtawaweka viongozi wazuri na wenyekujali maslahi ya watanzania. Huko Moshi kuna habari nyingine kutoka gazeti la Uhuru linasema :-

CCM Kilimanjaro yatahadharisha wanaotoa rushwa kuwania uongozi

Na Rodrick Makundi, Moshi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Kilimanjaro kimewatahadharisha baadhi ya wanachama na viongozi wanaotoa rushwa kwa wapiga kura ili kuwarubuni wachaguliwe katika nyadhifa mbali mbali za uongozi.

Soma zaidi http://www.uhuru.info/Habari mchanganyiko.htm
 
Habari!! Hi News leo inakosoa Chama Cha Mapinduzi.

Katika hili tunaiambia CCM bayana; hapana


Gazeti la Tanzania Daima

KUNA taarifa zilizonukuliwa katika gazeti hili kwenye toleo lake la jana, zilizokuwa zikieleza kwamba, viongozi kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameanzisha mkakati mahususi wa kuwapata wanachama wapya wakitumia mbinu batili.

Viongozi hao wa CCM katika ngazi za chini, wamekaririwa wakiwaasa vijana kujitokeza na kukata kadi za uanachama wa chama hicho, ili kujihakikishia nafasi ya kupata mgawo wa mabilioni yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umaskini.

Fedha hizo ambazo kila mkoa umepewa kiasi cha shilingi bilioni moja na zikapewa jina la ‘mabilioni ya Kikwete’, hivi sasa zinaonekana kutaka kutumiwa katika misingi isiyokusudiwa.

Kwa sababu hiyo basi, sisi tunaamini uamuzi wa serikali kutoa fedha hizo ambazo matumizi yake yalipata baraka za Bunge, unapaswa kuchukua sura ya kitaifa zaidi kuliko kiitikadi.

Kutokana na mazingira hayo, tunapenda kujiaminisha kwamba, uamuzi wa baadhi ya viongozi wa ngazi za chini wa chama hicho tawala, kuamua kuzitumia fedha hizo kama ‘bingo’ ya kisiasa, haukubaliki na unakwenda kinyume kabisa cha uamuzi wa serikali kutoa fedha hizo.

Ingawa bado ni mapema kuweza kusema kwa uhakika iwapo uamuzi huo wa serikali utatoa matunda ya wazi au la, bado katika hatua hii ya awali, tungependa kuona kila kiongozi wa kisiasa au kiserikali anaweka mbele kwanza maslahi ya taifa badala ya chama chake au tumbo lake binafsi.

Tunasema hivi tukiwa na imani kwamba, uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete na hususan serikali yake kuamua kutenga kiasi hicho cha fedha, ulikuwa ukienda sambamba na kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Nne isemayo, “Maisha bora kwa kila Mtanzania.”

Ukiiangalia kaulimbiu hiyo na kuifanyia tathmini, utabaini inazungumzia Watanzania bila ya kuwabagua na wala haisemi ‘Maisha bora kwa kila mwana CCM’ kama inavyotaka kufanywa na viongozi wachache wahuni.

Wakati tukiweka bayana msimamo wetu na kueleza kukerwa na genge la viongozi wa aina hiyo, tunaamini kwa dhati kabisa, serikali haitakaa kimya na kuwaacha wahuni hao wakipotosha ajenda yake njema, ya kujaribu kuwaongezea kipato wananchi wake.

Ingawa ni ukweli usiopingika kwamba, serikali iliyoko madarakani inatokana na CCM, tunatambua pia, uhalali wa serikali hiyo unatokana na kura ilizopigiwa na wanachama wa chama hicho na wale wasio wanachama wake.

Ni kwa misingi hiyo, ndiyo maana Rais Kikwete, siku chache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa urais, alipokuwa akiwahutubia wana CCM wenzake, alitahadharisha kuhusu hali hiyo.

Kwa maneno yake, Kikwete aliwaeleza wana CCM kuacha tabia ya kuwakebehi wanachama wa vyama vya upinzani, akifahamu kwamba kura alizopigiwa, nyingi zilipigwa na Watanzania, ambao si wanachama wa chama hicho tawala.

Kwa kutambua hilo, ni imani yetu, viongozi wa CCM watafanya kila wanaloweza kuwaelimisha wenzao, ambao kwa sababu moja au nyingine, hawatambui lengo la msingi la serikali kutoa fedha hizo.

Wakati tukiamini hilo litatekelezwa, tunaamini pia kwamba, viongozi wa kiserikali ambao ndio watakaokuwa na dhamana ya kuzigawa fedha hizo, watafanya hivyo wakitambua kuwa, lengo la serikali halikuwa likiwalenga wanachama wa chama hicho tawala, bali Watanzania wote wenye sifa za kusaidiwa kukabiliana na umaskini.

Hapo Hapo {Intresting}

Kutoka Gazeti 'letu' la Uhuru
Na Rashid Mussa, Nachingwea anasema:-

Upinzani Lindi taaban

WANACHAMA wa vyama vya upinzani mkoani Lindi wameungana na maelfu ya wananchi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuzifanya kambi zao kubaki taaban.

Habari hizo za kuhama kwa wapinzani na kujiunga CCM, zimo katika taarifa ya nusu mwaka ya utekelezaji wa mradi wa uimarishaji uhai wa Chama iliyotolewa hivi karibuni mjini Nachingwea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, iliyosomwa na Katibu wa Mkoa wa Lindi, Stephine Kazidi, wanachama wapya 13,681 wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani waliamua ujiunga na CCM, wilaya ya Nachingwea ikiongoza katika mavuno hayo.

Nachingwea iliingiza wanachama 3,522 ikifuatiwa na Rwanga 2,299, Kilwa 2,421, Liwale 1912 Lindi vijijini 1,792 na Lindi mjini 1,735.

Viongozi walikuwa upinzani walisema kuwa wameamua kujiunga na CCM kufuatia neema ya maendeleo inayoanza kuchomoza mkoani humu ambayo haikutarajiwa katika miaka iliyopita hali iliyokuwa imewakatisha tamaa
wananchi wengi.

"Unajua mimi na wenzangu wengi tulisukumwa kujiunga na upinzani kutokana na hali mbaya ya kimaendeleo ya mkoa wetu," alisema Chande Hassani Issa aliyekuwa Katibu wa TLP Wilaya ya Kilwa.

"Kama viongozi tulianza kukosa hoja zenye nguvu mbele ya watu za kuisambaratisha CCM, baada ya kukumbwa na wimbi la kukimbiwa na wanachama waliokuwa wanajiunga na CCM kila siku," alisema Ally Likwinya aliyekuwa Mwenyekiti wa TLP Kata ya Namupa.

Viongozi wengine walioondoka na kujiunga CCM ni aliyekuwa Katibu wa TLP Wilaya ya Ruangwa, Kanjela Abdallah, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mkoa ya CHADEMA, Mohamedi Nalama.

CCM Oyeeeeeeeeeeeeeee!!!! Nani kama CCM?
 
Hali Zenu Wajukuu Zangu Wana Ccm,

Mimi Babu Yenu Naitwa Masanja Wa Majebele Natokea Mkoa Wa Ziwa.nina Taka Kujua Nini Ndani Ya Ccm Mwaka Huu?

Mjadala Wote Umekaa Kujadili Nani Kafanya Nini Na Nani Ameondoka Chama Kipi Kuja Ccm. Kuna Kitu Mimi Nataka Kujua Au Munielekeze.

Katika Miaka 30 Ya Chama Cha Mapinduzi, Tumeambiwa Mengi Ikiwemo Hoja Ya Kujenga Chama Madhubuti Chenye Nia Ya Kweli Na Watanzania. Mwenyekiti Ametuambia Kwamba Kazi Mwaka Huu Ni Kujenga Chama Kitakacho Kuwa Na Uwezo Ambao Usiowezwa Na Watu Wengine Wakiwemo Wapinzani. Sasa Mimi Nashangazwa Sana La Hili Lundo La Hawa Niwaite Maharamia Wa Siasa Ambao Wanaamia Ccm Kwa Ajili Ya Kupata Vyeo Tu.

Nimewasikia Baadhi Ya Watu Majina Nawahifadhi , Wakizungumza Vibaya Na Kwamba Mwaka Huu Lazima Wawewajumbe Katika Vikao Fulani Vya Chama . La Kushangaza Watu Hawa Ni Wamerudi Juzi Kwenye Chama. Juzi Wakati Naongea Na Chief Mwezangu Wa Uchagani , Akaniaambia Kwamba Bwana Tlp Jana , Aliyerudi Ccm Ameanza Safari Ya Kuhakikisha Anamuondoa Ndesamburo. Kwa Kweli Mimi Sipingani Naye Katika Hoja Yake Ya Kisiasa Lakini Wasiwasi Wangu Ni Kwamba Anaweza Naye Akawa Anatafuta Ukweli Fulani Ndani Ya Chama.mnasemaje Wana Ccm?

Pia Ni Kwamba Muangalie Sana Wale Watu Waliotayari Kutumia Hela Zao Kupata Vyeo. Nimesikia Baadhi Ya Watu Wakipambana Kuomba Nec Ya Chama. Ni Vyema Kugombea Ili Mtusaidie Sisi Wakina Majebele.lakini Ni Hatari Kwa Jinsi Mnavyotaka Kutoana Roho.

Mimi Niwaambie Tu Ni Vyema Mkapata Wanec Wazuri Katika Mwaka Huu Ili Bwana Jakaya Aweze Kutusaidia Vizuri. Sababu Ni Kwamba Sioni Kama Kweli Atatoka Katika Miaka Mitano. Huku Mwanza Ni Raha Tupu Kuwa Naye Mtoto Wetu.sasa Ombi Letu Ni Kwamba Tuwekee Mambo Mazuri Kwa Sababu Kuja Majebele Anakuja Mwaka Huu.
 
Utabiri wangu na pesa JK nilijua una jambo kubwa sana .Sasa mnaona si kuinua maisha ya Watanzania bali kuijenga CCM bado nina wasi wasi na pesa zenyewe .
 
Karume akemea makundi CCM Zanzibar

180px-Amani_Abeid_Karume.png

Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani, Ndg. Amani Abeid Karume

Na Salma Said, Zanzibar,
Gazeti la Mwananchi.


RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, jana amewakaripia vikali wabunge na wawakilishi ambao wanaanzisha makundi katika chama hicho na kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo.

Akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jengo la Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Rais Karume alisema kuwapo kwa makundi katika chama kunaweza kusababisha chama hicho kukosa ushindi.

Aliwataka wanachama wa CCM kujenga umoja na mshikamano, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Rais Karume ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani, aliwataka viongozi watendaji katika majimbo ya uchaguzi kushikamana na kukaa pamoja ili kukiletea ushindi chama chao.

“Mbunge akimbagua Mwakilishi basi ni sawa na kumbagua Diwani, tabia hiyo ni mbaya inaweza kuleta mgawanyiko mkubwa katika chama na kukikosesha ushindi,” alionya.

Ofisi hiyo ya CCM Mkoa iliyopo Amani, ambayo imo katika matengenezo, inahitaji jumla ya Sh55 millioni ili kukamilisha ujenzi huo ambao umesitishwa kwa muda mrefu sasa kutokana na ukosefu wa fedha.

Ujenzi wa jengo hilo lenye ghorofa mbili ulianza mwaka 1984 na ujenzi wake ulisitishwa mwaka 1995 baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi.
 
Mwanaccm
hivi Nchimbi anagombania uenyekiti wa vijana tena? Au hii ni zamu ya Amina?
 
Hallo Kaka Sama Hali Yako.?

Ninachokisikia Kikisemwa Hapa Dar Es Salaam Mjini Ni Kuwa Mh. Nchimbi Ambaye Kwa Sasa Ni Waziri Wa Masuala Yetu Ya Vijana Hatogombea Kutokana Na Kutofaa Katika Vigezo Husika. Ila Huyu Mama Amina Wa Mpakanjia Chifupa Ameshatangaza Kwamba Angependa Sana Hii Nafasi.

Sina Uwakika Kama Ni Kweli Anataka Ila Tukiangalia Vigezo Vilivyopo Katika Umri Na Mambo Mengine , Nafikiri Dada Ana Nafasi Ya Kugombea Japo Siwezi Kuzungumzia Suala La Kushinda.

Wengine Wapo Wanasemwa Japo Sina Uwakika Kama Watafaa Vigezo Vyao?
 
Mambo ya CCM makubwa kweli kweli,watu wameanza kupigana vikumbo kugombea nafasi mbalimbali kwenye Jumuiya za CCM.kama ujuavyo ukiweza kuwa m'kiti wa jumuiya yoyote kati ya hizo tano una access ya moja kwa moja kwa muungwana,EL na Bw.Makamba (ambaye sasa ana sauti baada ya EL).
Kikubwa kuliko vyote ni nani atayekuwa Makamu wa mwenyekiti,kwa sababu kuna CCM Asili na CCM Mtandao ambao wanaonekana kutofautiana sana.Mtandao ni wenye nchi sasa,na wanajua sana kupepeta mdomo ili mambo yao yakubalike!.Kuna habari kuwa watu kutoka nje ya nchi wamealikwa nyumbani kuhudhuria hivyo vikao (Baba Balozi?) Labda nao watapongezwa kwa kufungua Matawi ya CCM nje ya mipaka ya Nchi!.
Licha ya Amina Chifupa kuna maelezo kuwa wakuu wa wilaya wawili wakereketwa wa CCM wamechukua forms za Uongozi wa Umoja wa Vijana,pia Mbunge mmoja wa Bunge la EA amechukua form kwa ajili ya Jumuiya ya Wanawake.Kazi ipo!
 
Mpinzania azidi kumng'ang'ania mbunge wa CCM

Kutoka Gazeti la Mwananchi
Na Daniel Mjema, Moshi,


KESI ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela, inazidi kupata sura mpya baada ya mpizani wake, Peter Kuga Mziray, kudai kuwa hana imani na majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kilimanjaro.

Msimamo huo wa Mziray umekuja wakati Mahakama Kuu jana ilianza mchakato wa kusikiliza ombi lake la kupatiwa kibali cha kuongezewa muda ili afungue maombi ya kukadiriwa kiwango cha dhamana anachostahili kukiweka.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, hakuna kesi yoyote ya kupinga matokeo ya uchaguzi itakayosikilizwa kabla ya mlalamikaji kulipa fedha za dhamana ya gharama za kesi ambayo kisheria inafahamika kama security for costs.

Hata hivyo wakili wa Serikali, Juma Ramadhan, aliiomba mahakama chini ya Jaji Mfawidhi, Njengafibile Mwaikugile, iwape siku 21 ili waweze kuwasilisha majibu ya hati ya kiapo cha Mziray.

Mziray anayejiwakilisha mwenyewe mahakamani, alipinga ombi hilo akisema mawakili wa serikali ni wasomi waliobobea na wanaweza kujibu hati yake kwa siku zisizozidi tatu.

Mziray aliiambia mahakama kuwa kuna wakati katika maombi kama hayo,aliwahi kupewa siku tatu kuwasilisha majibu na akashangaa kwanini upande wa Serikali upewe siku 21.

Hata hivyo, Jaji Mwaikugile alimtahadharisha Mziray kuacha kuwa na jazba kwa kuwa anaweza kupoteza mwelekeo wa kesi yake.

Jaji Mwaikugile alikubaliana na hoja za wakili wa serikali kuwa wanahitaji muda ili kutafuta taarifa za ukweli ikiwamo kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi ili waweze kujibu kiapo hicho.

Jaji aliupa upande wa serikali hadi Machi 15 kuwasilisha majibu hayo na kesi hiyo itatajwa Machi 19 na pia akaagiza Kilango, aarifiwe kuhusu kufunguliwa kwa maombi hayo.

Wakati hayo yakijiri mahakamani, jana Mziray alikabidhi mahakamani barua aliyomwandikia Jaji Kiongozi akisema hana imani na jinsi Mahakama Kuu kanda inavyoshughulikia maombi yake ya dhamana ya fedha.

Katika barua hiyo, Mziray amemuomba Jaji kiongozi kuipangia kesi hiyo Jaji mwenye uzoefu na kesi za uchaguzi nje ya Moshi.
 
Labda pia atagombea Nape Nnauye! Tunae huku India,ingawa alibwagwa na Nchimbi uchaguzi ulopita basi sasa labda anaweza jaribu tena
 
Heka Heka za Uchaguzi Mkuu wa CCM Zanzibar!! Zapamba Moto!!! Habari ya leo inatoka

Gazeti la Mwananchi
Na Salma Said, Zanzibar


Zanzibar wachangamkia fomu za CCM

WANANCHI wengi visiwani hapa, wamejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika mwaka huu.

Uchukuaji wa fomu hizo ulianza juzi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Visiwani na wanachama wa chama hicho wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu hizo bila ya woga ili chama kipate viongozi makini.

Akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Amani mjini hapa, Katibu wa CCM, Mkoa wa Mjini Magharibi, Ramadhan Abdallah, aliwataka wanachama wa chama hicho kutokuwa na hofu na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuchukuwa fomu.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho na mchakato wa kuwatafuta wagombea katika kuwatumikia wananchi kwenye maeneo yao mbali mbali.

“Uchaguzi huu ni muhimu sana, hivyo wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi jitokezeni kwa wingi kuchukua fomu ambazo zinatolewa bure bila ya malipo,” alisema.

Alisema majina ya wanachama wote waliochukuwa fomu yatafikishwa katika kamati za siasa za wilaya na kufanyiwa mchujo na halmashauri ya tawi kabla ya kupelekwa jimboni kwa uteuzi kamili.

Mwisho wa kurejesha fomu ni Machi 28 ambapo mchakato wa uteuzi wa wagombea utafanyika kati ya Machi 17 na 31. Pia wajumbe wanne watamsaidia Mwenyekiti wa shina katika uchaguzi.

Katika mikoa yote ya Unguja na Pemba, kumekuwepo na wanachama wengi walionekana wakijaza fomu katika matawi yao kwa ajili ya kutafuta nafasi za ngazi mbali mbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Matawi ambayo yameongoza kwa uchukuaji fomu nyingi ni Magogoni, Sebuleni na Amani ambayo yote yapo katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Awali akizundua kampeni za uchaguzi katika ofisi za CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk Mohamed Gharib Bilali, aliwataka wanachama kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu na kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama.

Aliwataka vijana kujitokeza zaidi katika kuwania nafsi hizo kwa vile wao ndio tegemeo na kizazi kinachohitajika ndani ya chama.

Alisema milango ipo wazi kwa wanachama waliokuwa tayari kugombea nafasi za uongozi na kuwahimiza akina mama nao kujitokeza kwa wingi na kuacha kutegemea nafsi za upendeleo.

Papo Hapo!! Tunduru kuna Habari kutoka

Gazeti 'letu' la Uhuru

‘Mtutura ana sifa zote za ubunge’​
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Tunduru, ni mtu makini na wasifu wake unakidhi sifa za kuwa mbunge.

Mgombea huyo ni Mtutura Abdallah Mtutura (pichani), mwenye umri wa miaka 44.

Mtutura kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha, tawi la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya wasifu wake, Mtutura alisoma shule ya msingi Muungano, na baadaye kujiunga na sekondari ya Ndanda, alikosoma hadi kidato cha nne mwaka 1980.

Mwaka 1981 hadi 1983 alisoma kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Minaki, na baadaye alikwenda kulitumikia taifa kwenye Jeshi la Kujenga Taifa, kabla ya kujiunga na Chuo cha Ufundi cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kidatu, alikosoma masuala ya uhandisi wa mitambo.

Mtutura alipata stashahada katika uhandisi wa mitambo na aliajiriwa na TANESCO mwaka 1984, ambako alishika nyadhifa mbalimbali hadi mwaka 1999.
Mwaka 1984-1988 alikuwa kwenye uendeshaji wa mitambo Kidatu, Morogoro na katiya mwaka 1988- 1995 alikuwa Makao Makuu ya TANESCO; akiwa mtalaamu wa mitambo kabla ya kupewa kazi ya ofisa usafiri makao makuu hadi mwaka 1999.

Mwaka huo huo, aliamua kujiunga na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ambako ni Ofisa Msaidizi wa Utawala hadi leo.
Kwa upande wa kazi za Chama, Mtutura tangu akiwa Chuo cha TANESCO alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wa tawi.

Mwaka 1999 na 2004, alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM tawi la Kichemchem, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam. Pia alikuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi na mjumbe wa Halmashauri ya Tawi.

Mwaka 2004 aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha, Tawi la CCM Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
Sasa mtu aliyesomea ufundi mitambo wa umeme anakuwa mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ama kweli CCM wanavituko; kwao kila kitu kinawezekana!
 
Mwanasiasa kule Mara mweka hazina wa CCM wa Mkoa ama Wilaya alikuwa hajui kusoma wala kuandika ila alijua kuhesabu pesa tu , lakini alipeta hadi majuzi alipo ondolewa anaitwa Mr. Msomi Bwana . Alikuwa owner wa Senser Band those days . Hii ndiyo CCM .
 
Ndugu Zangu Assalam Aleykum,

Mjadala Huu Mzuri Sana. Hebu Tuwaweke Wazi Hawa Wanaotaka Kuiangalia Hii Nchi Katika Miaka Ishirini Ijayo Maana Naona Hii Mineno Imezidi.

Kila Kukicha!

Anayewajua Wanaotamani Ukubwa Hawabandike Ubaoni.
 
Leo! Nimekuja na habari katika gazeti la Tanzania Daima huko Magu.

CCM Magu hoi

Kutoka gazeti la Tanzania Daima,
Na Osoro Nyawangah


HALI katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, mkoani Mwanza, ni mbaya kutokana na upungufu mkubwa wa wanachama waliolipa ada kwa mujibu wa katiba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, mbele ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, na uongozi wa chama hicho wilaya, uhai wa chama hicho unatishiwa kutokana na wanachama kushindwa kulipia ada zao za uanachama.

Akisoma taarifa ya chama ya wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Mukidoma kinachoendelea kujengwa wilayani hapa, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya, Dunia Mussa, amemwambia Dk. Shein kuwa, licha ya chama hicho kuwa na mashina 7,226 kina asilimia 20 tu ya wanachama walio hai.

“Chama chetu kilijizolea wanachama wapya wengi kutokana na ushindi mkubwa wa kishindo tulioupata na kufikisha wanachama 24,000, lakini kati ya hao ni wanachama 4,917 tu waliolipa ada na ambao kwa mujibu wa katiba wako hai,” alisema Mussa.

Alisema, hali hiyo imesababishwa na mazoea yaliyojengeka miongoni mwa wanachama, ya kulazimika kulipia ada zao kipindi cha uchaguzi huku wengi wakitegemea kulipiwa ada hizo na wagombea ambao kwa kipindi hicho watakuwa wakihitaji sana kura zao.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili, katibu mwenezi huyo alisema kuwa idadi ya wanachama walio hai hailingani na idadi ya viongozi wa mashina, hali ambayo inaonyesha kuwa, baadhi ya viongozi wa chama hicho pia wameshindwa kulipia ada zao kikatiba.

Aidha kutokana na kupungua kwa kipato kutokana na kuchelewesha ulipaji wa ada, Mussa amemweleza Dk. Shein kuwa, chama hicho kimejiandaa kuanzisha vyanzo vingine vya mapato ikiwemo mkakati wa kujenga vibanda vipatavyo 50 katika eneo la ofisi za wilaya na kuvikodisha kwa wafanyabiashara.

“Licha ya kuongeza kipato kutokana na mapato toka Kampuni ya Vodacom walioweka mnara wa mawasilianao katika viwanja vyetu, pia tumekamilisha taratibu za uchoraji ramani kwa ajili ya mradi wa kujenga vibanda ambavyo tutavikodisha kwa wafanyabiashara,” alisema Mussa.

Dk. Shein ambaye yuko mkoani Mwanza kukagua shughuli za maendeleo, amewashukuru wananchi wa Wilaya ya Magu kwa kuichagua CCM na kuwahakikishia kuwa, itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa maisha ya Watanzania yanaboreshwa.
 
CCM Oyeeeeeeeee!!! Kidumu Chama Cha Mapinduzi!.....

Leo nimekuja na hii habari kutoka huko Pemba, nayo ni kampeni katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi!!!

CCM yaanza kujiimarisha Pemba

Kutoka gazeti la Tanzania Daima,
na Saada Said, Zanzibar


MANAIBU waziri sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wiki ijayo wataanza kampeni maalumu ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisiwani Pemba.

Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa wiki mbili, imeandaliwa makusudi kwa ajili ya kuiimarisha CCM ambayo haina mvuto wa kisiasa kisiwani humo.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Machano Othman Said, jana aliiambia Tanzania Daima kuwa, CCM imewatuma kwenda Pemba kwa ajili ya kufufua uhai wa chama hicho kisiwani humo baada ya kubaini kuwa hakina mvuto kwa wananchi wa huko.

“Tunaondoka kwenda Pemba Jumapili, kwa ndege ya Costal na kama tulivyoagizwa na serikali yetu, sisi tunatekeleza agizo hilo,” alisema Machano.

Machano ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni, alisema serikali imewatayarishia nyumba za kukaa zilizoko eneo la Chake Chake katika kipindi watakachokuwa kisiwani humo.

Alisema yeye binafsi tayari ameshaitisha kikao katika jimbo lake na kuwaaga kutokana na kuhamishwa eneo la kazi na kuhamia kisiwani Pemba.

Machano alisema uhamisho huo utachukua muda wa wiki mbili pekee na baadaye watarejea Unguja hadi hapo watakapopangiwa tena na serikali.

“Tutakaa wiki mbili tu, baadaye tutarudi mpaka hapo tutakapopangiwa tena na serikali, lazima turudi kwa sababu kuna vikao vya Baraza la Wawakilishi mwezi wa Aprili, itatubidi turudi tu,” alisema Machano.

Uamuzi wa kuwapeleka manaibu waziri kisiwani humo, ulifikiwa mwezi uliopita kwa lengo la kwenda kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na jamii ikiwemo inayofadhiliwa na wahisani.

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili walisema mpango huo wa SMZ unaonekana kuwa wa kisiasa zaidi na hauna chembe ya kuendeleza miradi ya maendeleo.

Manaibu waziri wengine waliomo katika msafara huo ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Khatib Suleiman Bakari, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Jabir Makame na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mahmoud Thabit Kombo.

Wengine ni Naibu wa Afya na Ustawi wa Jamii, Shawana Buheti na Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee
 
Back
Top Bottom