Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Hii sheria ndio inaliza watu wengi. Labda kwenye thread hii badala ya kuhangaika na RA tungetumia muda huu kuwaelemisha Watanzania wengine kwa faida yao ya baadaye. Nina uhakika RA ni safi kwenye hili maana watu wangeshamvaa zamani.
this is flawed reasoning.. kwa vile hawajamvaa ina maana ni safi?
Kama mtu alizaliwa na mzazi mmoja ambaye hakuwa mtanzania wakati anazaliwa na kule kwao wanatambua mtoto kama huyo kuwa raia basi wewe una uraia wa nchi mbili na unaruhusiwa mpaka miaka 18. Baada ya hapo lazima uukane uraia wa hiyo nchi nyingine. Kwa mfano baba mwingereza na mama Mtanzania, kwa miaka mpaka 18 unakuwa na uraia wa nchi mbili, baada ya hapo kwasababu Tanzania haitambui uraia wa nchi mbili, inabidi uukane uraia wa UK ili ubaki kuwa Mtanzania.
Kundi lingine la kuangalia ni lile la Watanzania wanaoishi nje ya nchi kihalali ambako mtoto akizaliwa anakuwa raia pia. Hata kama hamjaomba huo uraia, kwasababu huyo mtoto anakuwa atomatically ni raia basi baada ya miaka 18 lazima aukane uraia wa nchi nyingine, vinginevyo siku anaingia siasa, wajanja watakuwa wanamsubiri.
Hiyo sheria wala hata sio lazima uchukue gamba, inatosha tu kwamba kwa sheria za nchi husika mtu kama huyo anakuwa raia.
Huko mbele tusipobadilisha sheria kuna Watanzania wengi waliozaliwa na wazazi wote Watanzania watakumbwa na sheria hii na kuleta matatizo hasa pale watakapojihusisha na siasa.
Wanasheria tuelemisheni ili watu wajifunze na wasifanye makosa hayo hayo hata siku za mbele.
Kuna watanzania wengi sio wafuatiliaji wa sheria na wanajikuta hata hawajui nini kinaendelea. Kwa mfano kuna Watanzania wengi ambao walikuwa wanasoma UK na kupata watoto kabla ya mwaka 1983, baada ya muda kurudi nyumbani. watoto wao wamehangaika kutafuta visa za kuja Ulaya bila kujua wao automatically ni raia wa UK hata kama wazazi wao wahakuwa raia. Baadhi yao mpaka wanashutuliwa na ubalozi ndio wanajua kumbe ni raia. Kwa wale ambao wamepoteza hata vyeti ndio imetoka tena.
naomba wengine mnaojua ongezeeni.
sidhani kama hapa kuna gumu.. sheria yetu ya awali ya uraia ilikuwa inasemaje? Na mabadiliko ya sheria hiyo baadaye yaliondoa tatizo gani? Tukielewa hiyo sheria tutaona kuwa hakuna ugumu mno kwani ni sheria hiyo hiyo ilitumika kumvua Jenerali uraia wake na wenzake wengine...
Na bado inaweza kutumika kuwavua wengine pia uraia huo kama ikiamuliwa kufuatwa (kama hii kesi inavyoeleza na kama ina ukweli).
Tatizo ni serikali ya CCM inaitumia sheria hii selectively..