Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, Mar 31, 2009.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hiki ni kipimo maalumu kama Sangara Operation ya CHADEMA imeleta matunda au, kuvurugana kwa wanahalmashauri kuu ya CCM kuna effect kwa wananchi na pia neno UFISADI limeeleweka kwa wanakijiji? stay tuned. Kipenga kimepulizwa na hawa ndo ya Makamba.

  Makamba aifananisha CCM na klabu ya mpira Yanga

  Na Boniface Meena

  HARAKATI za uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge cha jimbo la Busanda zimeanza kwa staili ya aina yake baada ya katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kuvitahadharisha vyama vingine vya siasa kuwa viende kwenye kinyang'anyiro hicho vikijua kuwa chama hicho tawala ni mshindi, akisema "CCM ni kama Yanga".

  Makamba ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza ratiba ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda baada ya mbunge wake, Faustine Rwilomba kufariki dunia mapema mwaka huu akiwa nchini India alikokuwa akitibiwa.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Makamba alisema kuwa vyama vinavyotaka jimbo hilo, havina budi kuelewa kuwa tayari CCM ni mshindi.

  "Jimbo ni mali ya CCM na tutalitetea kama Yanga walivyotetea ubingwa wao kwa kutwaa kombe kabla ya ligi kumalizika. Wanachama wakae mkao wa kugombea kiti cha jimbo hilo," alisema Makamba.

  Yanga ilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa soka wa Ligi Kuu ya Bara baada ya kufikisha pointi 48 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote kati ya 11 zilizosalia. Kila timu imebakiza mechi tatu kumaliza msimu.

  "Hili ni jimbo letu CCM hivyo tutalitwaa kama Yanga," alitamba katibu huyo, ambaye alilaumiwa sana baada ya CCM kushindwa kulitwaa jimbo la Tarime, ambako Chadema ilifanikiwa kutetea kiti chake kilichoachwa wazi na Chacha Wangwe.

  Kuhusu mkakati wa CCM katika uchaguzi huo mdogo, Makamba alisema kuwa hawezi kuweka hadharani mikakati ya chama chake kwa kuwa hayo ni mambo ya ndani.

  "Kuwania kiti tutawania lakini mikakati ya chama ni mambo ya ndani... we waambie Makamba atamba jimbo ni la CCM," alisema Makamba.

  Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema leo sekretarieti ya chama hicho itakutana kutengeneza utaratibu wa kuwania jimbo hilo.

  Alisema wanaangalia katiba ya chama ili kufanya uteuzi wa mgombea katika jimbo hilo.

  "Kesho(leo) sekretarieti ya chama itakutana kuangalia utaratibu ili kufanya uteuzi wa atakayewania jimbo hilo. Hivyo tusubiri kwa kuwa ni mapema," alisema Dk. Slaa.

  Hata hivyo, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Makamba kuwa tayari jimbo hilo ni mali ya CCM, Dk Slaa alisema "Makamba atakuwa mganga wa kienyeji" hivyo hawezi kuwa kama yeye.

  "Huyo ni mganga wa kienyeji," alisema Dk. Slaa.

  Wakati CCM na Chadema vikielezea uchaguzi huo, mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema alisema kwa sasa hafikirii jimbo la Busanda kwa kuwa anashughulikia uchaguzi mkuu wa chama chake unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

  "Bwana Boniface naomba nisizungumzie suala la Busanda wala wapi. Kwa sasa nahangaikia na uchaguzi wangu ndani ya TLP," alisema Mrema.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na mkurugenzi wa uchaguzi, Rajab Kiravu, uteuzi wa wagombea utakiwa uwe umefanyika ifikapo Aprili 28.

  Kiravu, katika taarifa hiyo, ameeleza kuwa Aprili 29 hadi Mei 23 itakuwa ni kipindi cha kampeni na Mei 24 itakuwa ni siku ya upigaji kura.

  Kutokana na hilo tume imewataka wadau wote kuzingatia ratiba hiyo.


  Source: Mwananchi
   
  Last edited by a moderator: May 12, 2009
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kipenga kimelia jamani, naomba kuambiwa jimbo la Busanda lina kata zipi? CHADEMA hiki ni kipimo chenu kutokana na darasa mnalolitoa
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nilifikiri utasema upinzani hili ni jimbo lenu ,maana sioni tofauti ya Chadema na CCM waote wamoja si umesikia juzi wakimwandalia Mwakiembe kule wilayani kwake.
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hivi ile sheria ya kuahirisha uchaguzi mdogo kwa miezi 24 iliishia wapi? naona chaguzi ndogo zinafululiza sana siku hizi. Na ni wakati gani inapoamuliwa itumike?

  Hapa si bure; naona ni njama ya kuwachosha wapinzani na rasilimali zao ndogo kisha ikifika 2010 watakuwa taabani kiuchumi na kisiasa. Wale wanaofikiri sisiemu inapenda demokrasia, KALAGABAHO!!!
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hivi hizi pesa za kurudia uchaguzi mbona hazijawahi kukosekana hata siku moja kama zinavyokosekana pesa za kutengeneza barabara?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Waliona inawakwaza wakaamua kuibadilisha
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Au kama zilivyokosekana fedha za kuendelea na kikao cha Bunge kilichopita kilichokuwa kijadili masuala kadhaa muhimu
   
 8. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mwiba rudisha ule mwiba wako ili tuwe tunakuona kwa urahisi bwana, ndani ya hizo luvas huonekani vyema!
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CCM wajitokeza 12 kuwania nafasi, Vipi CHADEMA na CUF?

  Source: HabariLeo
   
 10. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kuwa kitasimamisha mgombea atakayewania nafasi ya ubunge katika jimbo la Busanda mkoani Mwanza, na tayari kimeshaanza mchakato wa kutafuta mgombea wa nafasi hiyo, na majina ya wanaowania yamewekwa hadharani. Jimbo hilo liko wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wake, Faustine Rwilomba aliyefariki Machi 12, mwaka huu nchini India.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chama hicho, Msafiri Mtemelwa, alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya Sekretarieti ya Kamati Kuu kukutana Machi 31, mwaka huu pamoja na Tume ya Uchaguzi (NEC) kutangaza tarehe ya uchaguzi katika jimbo hilo ambayo ni Mei 24, mwaka huu.

  “Chadema imedhamiria kupambana vikali kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda na ili kumpata mgombea mwenye sifa anayekubalika, fomu za kuwania nafasi hiyo zitatolewa Aprili 6, mwaka huu na mwisho wa kurudisha itakuwa Aprili 15,” alisema. Aprili 18, mwaka huu Kamati ya Utendaji ya Chama hicho itakutana kufanya uteuzi na taarifa yake itawasilishwa kwa Kamati Kuu ambayo itakuwa na uamuzi wa mwisho kupitisha jina la mgombea atakayewakilisha chama hicho.

  Mtemelwa alisema kuwa wagombea waliojitokeza mpaka sasa ni Fineas Magesa, Nazir Mneka, Oscar Ndalawa, Meshack Opurukwa na Baltazar Madaha na imefafanuliwa kuwa wote wana sifa na uwezo wa kugombea nafasi hiyo ingawa chama kitafuata taratibu za kupatikana kwa mgombea mmoja mwenye sifa. Utaratibu wa uchukuaji fomu ndani ya chama hicho bado unaendelea.
   
 11. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #11
  Apr 11, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kinachonifurahi juu ya uchaguzi wa Busanda ni ukweli kuwa vyama vya upinzani vilishapata darasa kwa makosa yaliyofanyika kule Mbeya, hasa katika taratibu za mwanzo za ukamilishaji wa fomu za wagombea.
  Naamini kuwa vyama vyote vitakuwa makini katika jambo ilo na mengine muhimu ya kitaratibu za mchakato nzima wa kupata wagombe wao. Na kama hali itakuwa hivyo basi ule ushindi wa uwanjani tunautarajia katika jimbo ili, tofauti na ushindi wa mezani.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,641
  Likes Received: 82,289
  Trophy Points: 280
  Joto la uchaguzi Busanda: Viongozi CHADEMA washushwa jukwaani
  Saturday, 18 April 2009 14:56

  ...Wananchi wazingira gari la polisi

  Na Reuben Kagaruki, Geita

  Majira

  VUGUVUGU la uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Busanda wilayani Geita mkoani Mwanza limeanza kupamba moto baada ya Polisi wenye bunduki aina ya SMG na mabomu ya machozi kuwashusha jukwaani viongozi wa kitaifa wa CHADEMA waliokuwa wakisalimia wananchi.

  Katika sakata hilo, polisi nao walijikuta wakizingirwa na wananchi wenye hasira wakishinikizwa kumwachia huru kijana mmoja aliyekamatwa na askari hao wakitaka kumpeleka kituoni.

  Tukio hilo lilitokea jana mjini hapa katika kijiji cha Katoro baada ya msafara wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA kuwasili kijijini hapo na kupokewa na umati wa watu pamoja na msafara ya pikipiki na magari.

  Baada ya msafara huo kufika kijijini hapo viongozi wa kitaifa wa CHADENA wakiongozwa na Mkurugenzi wa Oganazesheni na Mafunzo wa chama hicho, Bw. Benson Kaigala walianza kupanda jukwaani
  kusalimia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kuwapokea.

  Wakati viongozi hao wakitambulishwa na kusalimia wananchi ndipo walifika askari wakiwa ndani ya gari la Polisi namba TP 1155 aina ya Land Lover wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Geita Bw. Kimei na kuwataka viongozi hao washuke jukwaani kwa kuwa mkusanyiko huo haukuwa halali.

  Hata hivyo vingozi wa CHADEMA waliendelea na ratiba yao ya kutambulishana ndipo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akiwa na bunduki aina ya SMG akiongozana na askari kanzu walipoenda
  moja kwa moja kwenye gari la matangazo la chama hicho lililokuwa likitumiwa kama jukwaa na kuwaamuru wateremke chini na kuondoka.

  Hata hivyo hatua hiyo ilipingwa na viongozi wa CHADEMA wakidai hawafanyi mkutano wa hadhara bali wamesimama kusalimiana na
  wananchi waliojitokeza kuwapokea.

  "Polisi msitutishe sisi hapa hatufanyi mkutano bali tumesimama kuwasalimia wananchi kwani chama chetu hakina tofauti na CCM," alisema Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa CHADEMA, Bw. Msafiri
  Mtemelwa.

  Hata hivyo Polisi hao waliendelea na msimamo wao ambao ulionekana wazi kuwakera wananchi waliokuwa na shauku ya kuwaona viongozi wa kitaifa.

  Kufuatia hali hiyo wananchi walianza kuwatia moyo viongozi hao wa CHADEMA wakidai kama waliweza kupambana na vitendo vya aina hiyo katika uchaguzi wa Tarime ambapo walimwagwa askari wengi iweje waogope askari wachache.

  Baada ya viongozi wa CHADEMA kutii amri ya Polisi na kuanza kuwatangazia wananchi waondeke ndipo polisi walimkamata kijana mmoja, Bw. Safari Manyama na kutaka kuondoka naye.

  Baada ya wananchi kuona hivyo walizingira gari la polisi na kuliweka katikati huku wakishinikiza aachiwe huru wakidai kuwa hakuna kosa lolote. Hata hivyo polisi walikataa kumwachia ndipo wananchi walianza kuvutana nao huku na wao wakijiandaa kufyatua hewani mabomu ya machoni.

  Baada ya wasiwasi kuzidi kuongezeka viongozi wa CHADEMA waliwafuata Polisi na kuwasihi wamuachie kijana huyo kwa kuwa siku zote mtutu wa bunduki haujawahi kuibuka na ushindi. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Polisi walikubali kumwachia kijana huyo hali iliyowafanya wananchi waanze kushangilia kwa kuimba nyimbo za kukipongeza chama hicho.


  Wakati huo huo Kamati Kuu wa CHADEMA inatarajia kumtangaza mgombea ubunge wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda
  kesho (Jumatatu).

  Baada ya kutangazwa kwa mgombea huyo timu ya kampeni ambayo tayari imewasili mjini hapa itaenda kupiga 'kambi' mkoani Kagera kwa takribani siku tisa ikiendelea na mikutano yake ya Operesheni
  Sagara ikisubiri muda wa kampeni ufike.

  Kampeni katika jimbo hilo zinatarajia kuanza Aprili 29,mwaka huu ambapo CHADEMA itazindua kampeni zake Mei mosi. Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Oganazesheni na Mafunzo, Bw. Kaigaila alisema wanachama wawili wa chama hicho wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

  Aliwataja wanachama hao ambao jana walipigiwa kura za maoni kuwa ni Bw.Magesa Finias na Bw. Nasoro Bakari. Alisema taratibu zote za kampeni za chama hicho zimekamilika na kinachosubiriwa sasa ni uzinduzi. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Bw. Kabuzi Rwiromba.
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Naona Tanzania kumekucha. wananchi wamechoka na dhuluma na vitisho kwani CCM wamezidi kutumia nguvu za dola kwani hawajiamini. Jamani YES WE CAN! Ni lazima tuwahabarishe ndugu zetu huko mikoani kwamba aendelee na misismamo yao na tukishikamana tutawatimua CCM in 2010!
  There is always hope.....
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,641
  Likes Received: 82,289
  Trophy Points: 280
  Susuviri, Watanzani wamechoka na manyanyaso wanayofanyiwa wao na viongozi wa upinzani na vitengo mbali mbali vya CCM alias Polisi, FFU n.k. wanayoyafanya polisi na FFU hayana tofauti na yaliyokuwa yanafanywa na polisi wa Zimbabwe kwa Tsavangarai na wafuasi wake. Wakiendelea na manyanyaso yao kutakuwa na mauaji ya kutisha kati ya polisi, FFU na wananchi kama siyo huko Busanda basi katika uchaguzi wa 2010, Mungu apishilie mbali.
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  lakini kazi bado ipo hasa kwenye elimu ya upigaji kura, watu wameshachoka mda mrefu lakini wanaonekanaga majukwaani tu lakini kwenye upigaji kula kunakuwa hakuna showup
  cha muhimu chadama inawapasa kuwa makini na vibaraka waliopo ndani ya chama(ZITTO NA WENZIE) kwa maana kuna kila dalili ya kukimaliza chama mda si mrefu kama alivyotaka kufanya Wangwe
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Haya ya Polisi ni matokeo ya katiba mbovu.

  Mwenyekiti wa kama ya usalama ya mkoa ni Mkuu wa mkoa na wilayani ni mkuu wa wilaya. Hawa wote ni makada maarufu wa ccm ni wengi wao ni wale waiokosa nafasi mbalimbali za uongozi kama ubunge. Sasa hapa jeshi la polisi litatekeza je haki wakati Mkuu wao (ambae ni Mkuu wa Mkoa au wilaya) ambae ameagizwa ahakikishe ccm tu ndio inashinda!

  Lazima mabadiliko ya katiba yafanyike, ili demokrasia ya kweli iwepo. Sijui itakuwa je siku ccm ikianguka katika hali hii ya katiba yenye mapungufu makubwa, nao watashika makali, mwishowe ni kutolitendea haki taifa!

  Nono.
   
 17. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Wananchi wa mikoani naona ndio wameamka zaidi, natumaini wakati muafaka ukifika watanzania wote wapenda nchi yao tutakuwa tayari kuondokana na udhalimu!!
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Misafara ya akina Makamba huko mikoani/wilayani husimama vijijini na viongozi hao kusalimia wananchi. Kwa mtazamo wa polisi, masalimiano hayo huwa ni halali, lakini ya vyama vya upinzani huwa ni haramu.

  Kweli, CCM huwa inashinda chaguzi kupitia migongo ya taasisi zake nyingi -- hasa hii ya polisi. watashindwa tu siku umma ukiamua. Ipo siku.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa mnamfahamu, Phinias Magesa ndiye aliyeteuliwa na Chadema kuwa mgombea wao
   
 20. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakuna namna CCM inaweza kushinda uchaguzi bila kubebwa na polisi, tume ya uchaguzi, umwagaji mkubwa wa fedha na silaha yao kubwa sana KUNUNUA SHAHADA ZA WAPIGA KURA hasa.

  Phinehas pambana hadi kieleweke

  CHADEMA tunaomba mtupe raha watanzania kw akuimwaga CCM huko Busanda.
   
Loading...