Uchaguzi 2010: Sauti ya wananchi iheshimiwe!

Wananchi wangapi waliomchagua? Sasa mbona kila kona wanalalamika kadri NEC wanavyotangaza? Ataufanyia kazi? Are you msemaji wa Kikwete? Halafu ni wakina nani wenye imani naye sana?....Hivi unafanya tafiti au ndo unabandika "facts" toka kichwani mwako?

Hahaha! Inabidi tu nicheke! Una maana Makamba and the co. out?
I mean hata JK out?....Aisee inabidi utuambie kama ndio mrithi mpya wa Chiligati :smile-big:

- Sitaki kuamini kwamba wewe ni msemaji wa Dr. Slaa, wananchi wamezungumza wamechagua wabunge na Rais, wasimaizi wa kimataifa wamesema kuna matatizo katika NEC lakini sijaona wakisema kura zimeibiwa au kuna uchakachuaji, na besides my point ni kwamba kwa matokeo yaliyotolewa tayari kwa maoni yangu wananchi wamesema wana imani na Rais, lakini wana tatizo na watendaji wake wa chini, ukitaka niamini toafuti niwekee evidence hapa mkuu kwamba uchaguzi umeibiwa na CCM maana inaelekea unao ushahidi mkuu weka hapa!

- Otherwise ni haki yetu wananchi kutafakari kutokana na facts zilizokwisha tolewa tayari., Tanzania ni yetu sote kwa hiyo ni haki yetu sote kuijadili na kuitafakari!

William.
 
Duh, hiyo tactic aliitumia Hitler na siamini kama ndo umeshaitumia hivyo!
Kila mtu asiyekubaliana nawe ni msemaji wa Slaa? Hapo umepotea!
Hizo "fact" zako ziko wapi? ndio hizo za NEC ambazo mpaka JF wapige kelele ndio warekebishe?
Hivi umetembea mitaani kuwasikiliza wananchi? We research gani unafanyia ktk Tv?
Acha hizo bwana!
 
Mkuu wangu,
Naona unafanya siasa za kishikaji hapa. Mimi nadhani somo kubwa hapa lingekuwa kwamba JK anatakiwa kufahamu kwamba sera zake hazikuuzika na kuwa amepoteza wabunge wake (incumbents) kwa sababu wananchi hawakubaliani naye. Na hakika kura nyingi za JK zimetokana na wanachama wa CCM chenyewe ambao walikataa katakata kukiangusha chama kutokana na makosa yaliyokwisha tokea. CCM ni wale waitwao die hard wanakufa na tai shingoni hivyo JK ashukuru sana wanachama wake na hasa wanawake ambao ndio wamempa ushindi mkubwa zaidi. Siku zote wanawake ni sehemu kubwa ya wapiga kura na JK hakulala toka upande huo...

Labda nikukumbushe tu kwamba nilisema toka mwanzo kwamba uwezekano wa kumshinda JK upo na hasa kama atasimama Dr.Slaa, nadhani uchaguzi huu sote hapa tunaamini kabisa kwamba Chadema wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na dr. hili pia halina ubishi na kama nilivyosema toka awali CCM wanaweza kabisa kushindwa ikiwa Upinzani wangefuata na kutimiza baadhi ya maswala muhimu sana ktk uchaguzi huu.

Kwanza kabisa ikiwa ni kukosa UMOJA baina ya vyama vya Upinzani jambo ambalo tumelizungumzia sana hapa JF toka uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 - Haikufanyika hivyo, lakini bado hatukukata tamaa na kuendelea kuwashauri Chadema kwa mengi ya msingi. Hivyo Chadema waliingia uchaguzi huu solo na kama chama mbadala ingawa walikuwa na mapungufu mengi na yaliyokuwa wazi.

Pili, Uongozi wa Chadema wamefanya baadhi ya makosa ya wazi kabisa ambayo pia tuliyazungumzia hapa kijiweni, mojawapo nilionya toka mwanzo ni kutojiandaa kusimamisha Wagombea Udiwani na Ubunge nchi nzima. Tatizo hili linaweza kutokana na uwezo wao mdogo kuiwezesha agenda hii kwani ruzuku wanayoipata sidhani kama ingeweza kuwahudumia wagombea wote, hivyo pengine Chadema bado ni chama kichanga ambacho kinahitaji kukua zaidi, lakini nakufahamisha tu kwamba nilipoona hivyo nilijua fika Chadema hawawezi kushinda uchaguzi huu kwa kupata wabunge 100 kama walivyotarajia kwani CCM isingeweza kutoa nafasi hizo kirahisi isipokuwa pale watakapoweza kubanwa sehemu zote. Na kibaya zaidi, Chadema ilipoteza baadhi ya Wabunge ktk maeneo muhimu ambayo wagombea wake walikuwa ni mapandikizi ya CCM.

Tatu, Uongozi wa Chadema walifanya kosa jingine kubwa sana kutoingia ktk uchaguzi wa Halamashauri ambao tumeona viongozi wa CCM wakizoa majimbo mengi na ndio waliofanya ama niseme kuiwezesha CCM kushinda mwaka huu, iwe kwa uchachuaji ama lolote lile maadam kuna zaidi ya vituo 7,000 vya kupigia kura sii rahisi kabisa kwa Chadema kuweza kuweka wawakilishi wenye uchungu ktk maeneo yote.. Hivyo Chadema kutojikita ngazi za chini ambazo ni muhimu sana imekuwa pigo kubwa kwa chama na dalili zake zilijitokeza mapema wakati wa kampeni za viongozi wake..

Nne, mchezo mchafu wa CCM kuhusisha dini katika uchaguzi huu pia umechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa Chadema kushindwa ktk baadhi ya maeleno kwani sii kila Muislaam au Mkristu anapenda chama kinachotawaliwa na Udini. Mara nyingi uongo ukizungumzwa sana hufikia watu wakaamini na haya tumeyaona hata hapa kijiweni kwani wapo watu walivutwa na udini kiasi kwamba hata mimi nilianza kujiuliza position yangu ktk siasa ikiwa swala la udini litachukua nafasi..Udini ni kuchezea akili za watu kufikia maamuzi ambayo huondoa kabisa utu na uzalendo wao, CCM walifanikiwa ktk hili.

CCM walitulisha chambo na WanaChadema kama samaki wengi wao walikula na kuuweka uchaguzi huu kama ni nguvu ya kuondoa Uislaam ktk ngazi ya Urais, haya yalikuwa makosa makubwa sana ya baadhi ya wanaChadema na hasa viongozi wa dini walipoingilia kati. Ifahamike tu kwamba CCM pamoja na kuwa wao ndio waanzilishi wa Udini walichotaka wao ni wananchi kukitazama chama Chadema kilivyoundwa kwa kufananisha na CCM.

Hivyo hata hao Masheikh walipokuwa wakimnadi JK haikuwa kosa tena pale Mapadre waliposimama nao kunadi Dr.Slaa. Na kibaya zaidi CCM waliweza kujitetea sana kwa kutokuwa na udini ndani ya chama wakieleza wazi jinsi muundo wa chama na hata nyadhifa za viongozi wake jambo ambalo sii zuri kiutawala lakini liliweza kuwapa nafasi zaidi ya Chadema. Najua fika wapo watu watapinga hili lakini ndivyo nilivyoliona mimi kuwa sababu mojawapo ya Chadema kutofanikiwa mwaka huu. Kwa hiyo ngoma ndio imekwisha tugange yajayo.

Mwisho mkuu wangu JK anatakiwa sasa kuongoza nchi kama rais, muda wa John Mtembezi umekwisha. Sasa ni juu yake yeye mwenyewe kuchagua..Kuendelea na siasa za Usanii huku akiendelea kukumbatia Ufisadi na kuwafanyia wale woote waliokuwa against yeye uchaguzi huu au kurudisha hadhi ya kiti cha IKULU na kuwawajibisha wote watakao fikwa na scandals zozote za kifisadi. Akubali mageuzi ktk sehemu nyeti ambazo ndizo zilikuwa nguzo ya Dr.Slaa hata kama zimetoka Chadema na kuacha kabisa zile hadithi za kuijenga Kigoma kama Dubai.

Ushindi wa JK ulikuwa LAZIMA, hapakuwepo na nguvu ya kutosha kumwangusha hivyo he is a survival na hasira zake tutaziona muda sii mfupi....By the way kusema kweli JK tunaweza sema ni rais mdhaifu kwa sababu nyingi sana ikiwa ni pamoja na kukumbatia Ufisadi na upande wapili wa shilingi kuwaachia Upinzani kumtia vidole vya macho in the name of Demokrasia!
 
Ushindi wa JK ulikuwa LAZIMA, hapakuwepo na nguvu ya kutosha kumwangusha hivyo he is a survival na hasira zake tutaziona muda sii mfupi....By the way kusema kweli JK tunaweza sema ni rais mdhaifu kwa sababu nyingi sana ikiwa ni pamoja na kukumbatia Ufisadi na upande wapili wa shilingi
kuwaachia Upinzani kumtia vidole vya macho in the name of Demokrasia!

Mzee Mkandara,

Maneno yako yamenichanganya kidogo, unaweza ukanyambua kidogo ulikuwa unamaanisha nini ?
 
Angarau umenifanya niulize baada ya kupigwa butwaa kidogo, nisaidie tafadhali, kuna vidfeo inaonyesha mh. Masha anawashukuru wananchi kwa kumgagua kwa kura zake 28,..... Ambazo ameshindwa na mgombea wa chadema 38,.... Je inakuwaje hapo, maana kwa mujibu wa gazeti la mwananchi ni kuwa mgombea wa chadema alishinda, na vurugu zilifanyika ili matakeo yatangazwe, ikawaje baadae, nimepagawa,

nafikiri kuna haja ya kufanya kama kenya walivyofanya kama amani ya busara haipo basi ya ncha ya upanga...

Kwanini hivyo, kwani Tanzania bila ccm haiwezekani?[/B]

What do you mean?...........
 
Mzee Mkandara,

Maneno yako yamenichanganya kidogo, unaweza ukanyambua kidogo ulikuwa unamaanisha nini ?
Mkuu wangu sina maana zaidi ya kusema kwamba Udhaifu wa kiongozi ngazi ya rais una sura mbili..Hiyo ambayo hukuielewa ni kutazama uchaguzi huu (demokrasia) ilivyomsuta.. Sijawahi kusikia Presidaa akitoa ahadi kwa wananchi vitu alivyoahidi kama sehemu ya kampeni zake isipokuwa Mayor wa miji husika (Flyover, madaraja, miji kama Dubai, Meli n.k). Sijawahi kuona rais mgombea akikwepa Mdahalo badala yake kufanya mahojiano na vyombo vya habari, Sijawahi kuona rais wa nchi akitangaza chama zaidi ya Utaifa hata kuvaa pin ya Taifa au kupeperusha bendera ya Taifa mahala popote ktk kampeni zake. Sijawahi kuona......
Haya yote ni Udhaifu kwa jina la demokrasia.
 
william upo komredi??
uchaguzi umekwisha ndo unaonekana. kulikoni?
 
Mkandara,

Umeandika mengi na kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe. Mimi nadhani CHADEMA hawatakiwi kujilaumu hata kidogo, bali wajipongeze na kuanza kujipanga kwa chaguzi zijazo. Mimi nina imani kubwa sana na Dr. Slaa kwani ameonyesha ya kuwa ni mtu makini na mwenye ushawishi wa hali ya juu. Kinachotakiwa kufanyika sasa, ni kuanza kukijenga chama! Kuhakikisha ya kuwa chama hiki kinakuwa sura ya kitaifa katika uongozi wake.

Pili wapinzani ni lazima wahakikishe ya kuwa hii NEC iliyokuwa invented na CCM inavunjwa na tutengeneze chombo kitakachowatendea haki kwa vyama vyote. Nadhani ili linaweza kufanyika kama wapinzani wakitumia nafasi ya Maalim Seif kushawishi serikali ya Muungano. Jaji Makame asingekubali Slaa ashinde kwani kwa kufanya hivyo angepoteza kazi yake. Mimi nadhani NEC inabidi iwe chombo huru na Rais asiwe na uwezo wa kumfukuza mwenyekiti wa NEC kazi, ili kuondoa mgogoro wa kimaslahi( conflict of interest). Bila ya kukifanyia hiki chombo cha NEC mabadiliko, wapinzani watashindwa kwenye kila chaguzi.
 
Waslaaam wananchi wote JF,

- Bado tunaendelea kutafakari kilichojiri kwenye huu uchaguzi wa wabunge na Rais, baada ya kuyasikiliza kwa makini sana matokeo:

- Inaonekana kwamba kuna ujumbe mzito sana wa wananchi kwa Rais aliyechaguliwa, kwamba wananchi wana imani naye sana, lakini wana tatizo kubwa sana na watendaji wake, hasa mawaziri na wakuu wa Mikoa/Wilaya. Ni matumaini yangu kwamba amewasikia wananchi na ataufanyia kazi ujumbe wao mzito sana waliomtumia kupitia kwenye kura zao.

- Na ni matumaini yangu makubwa sana kwamba CCM kama chama, kimesikia kilio cha wananchi, kwamba wamechoshwa na viongozi magoi goi katika serikali yao na sasa wanataka mabadiliko!

Ahsanteni.

William.
aKIWEMO SWAHIBA WAKO LAU.
 
Huna la maana wewe mchumia tumbo. Baada ya kushindwa ule utapeli wako wa kuwapeleka watu majuu unajifanya muungwaaaaaana!!
 
Mkandara,

Umeandika mengi na kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe. Mimi nadhani CHADEMA hawatakiwi kujilaumu hata kidogo, bali wajipongeze na kuanza kujipanga kwa chaguzi zijazo. Mimi nina imani kubwa sana na Dr. Slaa kwani ameonyesha ya kuwa ni mtu makini na mwenye ushawishi wa hali ya juu. Kinachotakiwa kufanyika sasa, ni kuanza kukijenga chama! Kuhakikisha ya kuwa chama hiki kinakuwa sura ya kitaifa katika uongozi wake.

Pili wapinzani ni lazima wahakikishe ya kuwa hii NEC iliyokuwa invented na CCM inavunjwa na tutengeneze chombo kitakachowatendea haki kwa vyama vyote. Nadhani ili linaweza kufanyika kama wapinzani wakitumia nafasi ya Maalim Seif kushawishi serikali ya Muungano. Jaji Makame asingekubali Slaa ashinde kwani kwa kufanya hivyo angepoteza kazi yake. Mimi nadhani NEC inabidi iwe chombo huru na Rais asiwe na uwezo wa kumfukuza mwenyekiti wa NEC kazi, ili kuondoa mgogoro wa kimaslahi( conflict of interest). Bila ya kukifanyia hiki chombo cha NEC mabadiliko, wapinzani watashindwa kwenye kila chaguzi.
Bila shaka Chadema hawana sababu ya kujilaumu isipokuwa kujifunza zaidi kutokana na mapungufu au makosa ya awali.
Muhimu kilichonituma mimi kuandika mtazamo wangu ni kutokana na imani kwamba wananchi hawakumchagua JK bali wamekichagua chama CCM (ushabiki) tofauti na Chadema ambao Dr.Slaa ndiye amekuwa sababu kubwa ya ushindi wa Chadema..hivyo wakati wakisherehekea ushindi wao pande zote mbili inabidi JK mwenyewe afanye marekebisho makubwa juu ya uwezo wake mwenyewe ktk Uongozi wake kwani mwaka 2005 alikuwa sababu ya ushindi na mwaka huu ndiye amekuwa sababu kubwa ya kupoteza wabunge. Na Chadema nao wajikite zaidi ktk serikali za mitaa ambazo ndizo zimewapa kura zaidi CCM.

Kuhusiana na NEC mkuu wangu taifa letu bado kabisa changa sana ktk demokrasia hivyo ni vigumu sana kupata chombo huru ikiwa vyombo kama Jeshi la Polisi, UWT na Mahakama tumeshindwa kufanya hivyo kutokana na nguvu ya kuundwa chama kimoja ambacho miaka ya nyuma kila kiongozi wetu alitakiwa kuwa mwanaCCM. Nidhamu kubwa ya Utanzania wetu bado unahesabika kama ni unyenyekevu kwa chama tawala, kinyume cha hapo utaonekana huna adabu wala shukrani.

Hivyo, ili kukiwezesha chombo hiki kiwe huru na chenye kutoa haki (kulingana na mazingira yetu) chaguzi zijazo itabidi kushirikisha vyama vyote ktk kuunda upya NEC, nikiwa na maana wahusika wakuu (viongozi) wa NEC watatoka ktk vyama vyote shiriki. Jingine maswala ya uhesabuji kura utakuwa ukifanyika toka vituoni moja kwa moja badala ya kupelekwa sehemu nyingine hivyo tutahitaji Pc (laptop) zaidi ya 7,000 wireless ambazo zitatuma matokeo moja kwa moja makao makuu NEC ambako wao pamoja na wanahabari Radio na TV watashirikiana kutangaza matokeo hayo kila hatua yanapoletwa..
 
hapo kwenye nyekundu sijuhi ulifanya analysis gani, ukweli uklio wazi JK hakubaliki kabisa hata na watu wa vijijini ambao mara nyingi tunawaona wao huwa wanaifata CCM, ukiniambia watu bado wanaipenda CCM naeza kukukubalia lakini sio viongozi waliopo sasa

Sema wewe ndiyo humkubali, sisi huku vijijini tunamkubali
 
si kwamba naisapport CCM, ila asiekubali kushindwa si mshindani hata kama kura zimechakachuliwa swali, je zimechakachuliwa za chama kimoja cha upinzani au vyote? je kura zilizochakachuliwa zingemuwezesha Dk slaa kunyakua kiti cha urais? je wamechakachua kura za TZ bara tu? kwani zanzibar wamepishana kwa 1% ukiangalia yote haya kwa undani utapata majibu na nini cha kufanya mwaka 2015.
 
:A S angry:i as one of the mwananchi i like nothing about this current ccm; absolutely nothing, what i pray to god should happen ni mfumo mzima kubadilika hususan katiba, the hopefully we will start seeing what is happening now in kenya; watu waanze kutupwa ndani kwa makosa makubwa waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya - 'katiba must be changed period':doh:
 
Huna hoja William, it seems uko hapa kisiasa zaidi, huna hata aibu kuuambia umma kwamba Kikwete hakujua kama uongozi wake ni hovyo? Huyu si aliambiwa wazi na akina Warioba na Butiku, makamba akawaita wehu? Ulitaka aambiwe nini? How many times magazeti yameeleza jinsi ambavyo Kikwete amepwaya katika uongozi? You are too low real, sikuwahi kukufikiria kama na wewe unaweza kufika mahali ukawa mtumwa wa mafisadi this much?!

Tena akajibu kwa jeuri kwamba kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi kwa hiyo akalala kabisaaaaaaaa
 
- Mkuu siamini kwamba Dr. Slaa amekutuma hapa, halafu angalia tarehe za wewe kuingia hapa na mimi inaweza kukusaidia kujijibu maswali yako mengi ambayo ni nje ya masilahi ya taifa!

William.
Tarehe za kuingia si hoja. Kwa ID nyingi hapa JF mtu anaweza kuja kwa namna yoyote. Usiangalie tarehe angalia umetoa hoja gani hapa?
 
Waslaaam wananchi wote JF,

- Bado tunaendelea kutafakari kilichojiri kwenye huu uchaguzi wa wabunge na Rais, baada ya kuyasikiliza kwa makini sana matokeo:

- Inaonekana kwamba kuna ujumbe mzito sana wa wananchi kwa Rais aliyechaguliwa, kwamba wananchi wana imani naye sana, lakini wana tatizo kubwa sana na watendaji wake, hasa mawaziri na wakuu wa Mikoa/Wilaya. Ni matumaini yangu kwamba amewasikia wananchi na ataufanyia kazi ujumbe wao mzito sana waliomtumia kupitia kwenye kura zao.

- Na ni matumaini yangu makubwa sana kwamba CCM kama chama, kimesikia kilio cha wananchi, kwamba wamechoshwa na viongozi magoi goi katika serikali yao na sasa wanataka mabadiliko!

Ahsanteni.

William.

Mkuu William salute!!!

Ni kweli uliyoyasema hapo juu, lakini Rais wetu mteule ni sikio la kufa kamwe hataweza kuweka viongozi wachapaka kazi kwa ajili ya maswahiba zake. Sura utakazoziona za watendaji wote ni karibu zile zile so tutegemee business as usual. Ufisadi utakuwa pale pale na tutegemee miaka mitano ya dhiki kuu chini ya utawala wa muheshimiwa wetu.
 
Mkuu wangu,
Naona unafanya siasa za kishikaji hapa. Mimi nadhani somo kubwa hapa lingekuwa kwamba JK anatakiwa kufahamu kwamba sera zake hazikuuzika na kuwa amepoteza wabunge wake (incumbents) kwa sababu wananchi hawakubaliani naye. Na hakika kura nyingi za JK zimetokana na wanachama wa CCM chenyewe ambao walikataa katakata kukiangusha chama kutokana na makosa yaliyokwisha tokea. CCM ni wale waitwao die hard wanakufa na tai shingoni hivyo JK ashukuru sana wanachama wake na hasa wanawake ambao ndio wamempa ushindi mkubwa zaidi. Siku zote wanawake ni sehemu kubwa ya wapiga kura na JK hakulala toka upande huo...

Labda nikukumbushe tu kwamba nilisema toka mwanzo kwamba uwezekano wa kumshinda JK upo na hasa kama atasimama Dr.Slaa, nadhani uchaguzi huu sote hapa tunaamini kabisa kwamba Chadema wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na dr. hili pia halina ubishi na kama nilivyosema toka awali CCM wanaweza kabisa kushindwa ikiwa Upinzani wangefuata na kutimiza baadhi ya maswala muhimu sana ktk uchaguzi huu.

Kwanza kabisa ikiwa ni kukosa UMOJA baina ya vyama vya Upinzani jambo ambalo tumelizungumzia sana hapa JF toka uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 - Haikufanyika hivyo, lakini bado hatukukata tamaa na kuendelea kuwashauri Chadema kwa mengi ya msingi. Hivyo Chadema waliingia uchaguzi huu solo na kama chama mbadala ingawa walikuwa na mapungufu mengi na yaliyokuwa wazi.

Pili, Uongozi wa Chadema wamefanya baadhi ya makosa ya wazi kabisa ambayo pia tuliyazungumzia hapa kijiweni, mojawapo nilionya toka mwanzo ni kutojiandaa kusimamisha Wagombea Udiwani na Ubunge nchi nzima. Tatizo hili linaweza kutokana na uwezo wao mdogo kuiwezesha agenda hii kwani ruzuku wanayoipata sidhani kama ingeweza kuwahudumia wagombea wote, hivyo pengine Chadema bado ni chama kichanga ambacho kinahitaji kukua zaidi, lakini nakufahamisha tu kwamba nilipoona hivyo nilijua fika Chadema hawawezi kushinda uchaguzi huu kwa kupata wabunge 100 kama walivyotarajia kwani CCM isingeweza kutoa nafasi hizo kirahisi isipokuwa pale watakapoweza kubanwa sehemu zote. Na kibaya zaidi, Chadema ilipoteza baadhi ya Wabunge ktk maeneo muhimu ambayo wagombea wake walikuwa ni mapandikizi ya CCM.

Tatu, Uongozi wa Chadema walifanya kosa jingine kubwa sana kutoingia ktk uchaguzi wa Halamashauri ambao tumeona viongozi wa CCM wakizoa majimbo mengi na ndio waliofanya ama niseme kuiwezesha CCM kushinda mwaka huu, iwe kwa uchachuaji ama lolote lile maadam kuna zaidi ya vituo 7,000 vya kupigia kura sii rahisi kabisa kwa Chadema kuweza kuweka wawakilishi wenye uchungu ktk maeneo yote.. Hivyo Chadema kutojikita ngazi za chini ambazo ni muhimu sana imekuwa pigo kubwa kwa chama na dalili zake zilijitokeza mapema wakati wa kampeni za viongozi wake..

Nne, mchezo mchafu wa CCM kuhusisha dini katika uchaguzi huu pia umechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa Chadema kushindwa ktk baadhi ya maeleno kwani sii kila Muislaam au Mkristu anapenda chama kinachotawaliwa na Udini. Mara nyingi uongo ukizungumzwa sana hufikia watu wakaamini na haya tumeyaona hata hapa kijiweni kwani wapo watu walivutwa na udini kiasi kwamba hata mimi nilianza kujiuliza position yangu ktk siasa ikiwa swala la udini litachukua nafasi..Udini ni kuchezea akili za watu kufikia maamuzi ambayo huondoa kabisa utu na uzalendo wao, CCM walifanikiwa ktk hili.

CCM walitulisha chambo na WanaChadema kama samaki wengi wao walikula na kuuweka uchaguzi huu kama ni nguvu ya kuondoa Uislaam ktk ngazi ya Urais, haya yalikuwa makosa makubwa sana ya baadhi ya wanaChadema na hasa viongozi wa dini walipoingilia kati. Ifahamike tu kwamba CCM pamoja na kuwa wao ndio waanzilishi wa Udini walichotaka wao ni wananchi kukitazama chama Chadema kilivyoundwa kwa kufananisha na CCM.

Hivyo hata hao Masheikh walipokuwa wakimnadi JK haikuwa kosa tena pale Mapadre waliposimama nao kunadi Dr.Slaa. Na kibaya zaidi CCM waliweza kujitetea sana kwa kutokuwa na udini ndani ya chama wakieleza wazi jinsi muundo wa chama na hata nyadhifa za viongozi wake jambo ambalo sii zuri kiutawala lakini liliweza kuwapa nafasi zaidi ya Chadema. Najua fika wapo watu watapinga hili lakini ndivyo nilivyoliona mimi kuwa sababu mojawapo ya Chadema kutofanikiwa mwaka huu. Kwa hiyo ngoma ndio imekwisha tugange yajayo.

Mwisho mkuu wangu JK anatakiwa sasa kuongoza nchi kama rais, muda wa John Mtembezi umekwisha. Sasa ni juu yake yeye mwenyewe kuchagua..Kuendelea na siasa za Usanii huku akiendelea kukumbatia Ufisadi na kuwafanyia wale woote waliokuwa against yeye uchaguzi huu au kurudisha hadhi ya kiti cha IKULU na kuwawajibisha wote watakao fikwa na scandals zozote za kifisadi. Akubali mageuzi ktk sehemu nyeti ambazo ndizo zilikuwa nguzo ya Dr.Slaa hata kama zimetoka Chadema na kuacha kabisa zile hadithi za kuijenga Kigoma kama Dubai.

Ushindi wa JK ulikuwa LAZIMA, hapakuwepo na nguvu ya kutosha kumwangusha hivyo he is a survival na hasira zake tutaziona muda sii mfupi....By the way kusema kweli JK tunaweza sema ni rais mdhaifu kwa sababu nyingi sana ikiwa ni pamoja na kukumbatia Ufisadi na upande wapili wa shilingi kuwaachia Upinzani kumtia vidole vya macho in the name of Demokrasia!

- Mkuu wangu Bob, heshima sana ni sawa una point nyingi sana na nzito sana, lakini mimi muono wangu unazingatia sana namba ya viongozi wengi wa Upinzani waliposhindia, yaani kwenye local governments. Kwa maana ya kwamba wananchi walikuwa wamechoshwa na viongozi wa serikali za mitaa yao na hasa ma-RCs na DCs ambao overall ndio wasimamizi wa mipango ya maendeleo, as opposed na sera za Rais, ambazo mimi sina uhakika kama zipo zaidi tu ya maneno ya siasa. Ndio maana ninaamini kwamba ilikuwa ni kura against uongozi mbovu zaidi kuliko sera, I mean nini sera ya CCM kwa serikali za mitaa?

William.
 
si kwamba naisapport CCM, ila asiekubali kushindwa si mshindani hata kama kura zimechakachuliwa swali, je zimechakachuliwa za chama kimoja cha upinzani au vyote? je kura zilizochakachuliwa zingemuwezesha Dk slaa kunyakua kiti cha urais? je wamechakachua kura za TZ bara tu? kwani zanzibar wamepishana kwa 1% ukiangalia yote haya kwa undani utapata majibu na nini cha kufanya mwaka 2015.
Naona ndio unatoka usingizini na hujui nini kinaendelea. Dr Slaa hajakataa kwamba anaweza kushindwa, hapana. Yeye hoja yake ni kwamba basi tarakimu zote ziwe sahihi! na kama ziko sahihi na akashindwa si hiyo ndio demokrasia? ya nini sasa kufanya forgery na kutafuta hata kuwanunua wagombea walioshinda dakika za mwisho?
 
Back
Top Bottom