Waslaaam wananchi wote JF,
- Bado tunaendelea kutafakari kilichojiri kwenye huu uchaguzi wa wabunge na Rais, baada ya kuyasikiliza kwa makini sana matokeo:
- Inaonekana kwamba kuna ujumbe mzito sana wa wananchi kwa Rais aliyechaguliwa, kwamba wananchi wana imani naye sana, lakini wana tatizo kubwa sana na watendaji wake, hasa mawaziri na wakuu wa Mikoa/Wilaya. Ni matumaini yangu kwamba amewasikia wananchi na ataufanyia kazi ujumbe wao mzito sana waliomtumia kupitia kwenye kura zao.
- Na ni matumaini yangu makubwa sana kwamba CCM kama chama, kimesikia kilio cha wananchi, kwamba wamechoshwa na viongozi magoi goi katika serikali yao na sasa wanataka mabadiliko!
Ahsanteni.
William kabla hatujaanza kujadili tathmini za uchaguzi zilizotolewa na NEC wewe binafsi bila kujali itikadi yako kichama unatoa tathmini gani? Suala la uchaguzi huu ni dosari za makusudi ili kukipa nguvu chama tawala; kimsingi NEC si chombo huru hii ikumbukwe kilikuwa ni kilio tangu wakati wa mfumo vyama vingi ulipoanza; wapinzani wa kweli wakati ule waliliona lakini wengi waliingia kwenye mtego wa ruzuku ambao unaendelea hadi leo hii; kama wapinzani kweli wanataka kuleta mabadiliko wajitoe kwenye hii mifumo ya ruzuku serikali haipashwi kulea vyama kwa ruzuku jukumu la kulea vyama ni la wanachama wenyewe, dosari ni dosari tu iwe ndogo ama kubwa uchaguzi unatakiwa uwe huru na waki.