Uchaguzi 2010: Sauti ya wananchi iheshimiwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Sauti ya wananchi iheshimiwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Nov 4, 2010.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Waslaaam wananchi wote JF,

  - Bado tunaendelea kutafakari kilichojiri kwenye huu uchaguzi wa wabunge na Rais, baada ya kuyasikiliza kwa makini sana matokeo:

  - Inaonekana kwamba kuna ujumbe mzito sana wa wananchi kwa Rais aliyechaguliwa, kwamba wananchi wana imani naye sana, lakini wana tatizo kubwa sana na watendaji wake, hasa mawaziri na wakuu wa Mikoa/Wilaya. Ni matumaini yangu kwamba amewasikia wananchi na ataufanyia kazi ujumbe wao mzito sana waliomtumia kupitia kwenye kura zao.

  - Na ni matumaini yangu makubwa sana kwamba CCM kama chama, kimesikia kilio cha wananchi, kwamba wamechoshwa na viongozi magoi goi katika serikali yao na sasa wanataka mabadiliko!

  Ahsanteni.


  William.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,594
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu, William, salamu zako tumezipokea. Nimefarijika sana kwa wewe kuwa ni miongoni mwa mliolitambua hili la "viongozi magoi goi katika serikali yao na sasa wanataka mabadiliko!" ambayo naamini ndio kwanza wameanza kutuma salamu, na vile JK ambaye ni kweli bado wana imani naye na ni matumaini yao, kikosi kazi kijacho, hakitakuwa na idadi kubwa ya magoi goi kama kilichotangulia, vinginevyo, 2015, watakamilisha hii kazi waliyoianza.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pasco mark my words, kikosi kazi cha watu kama Nchimbi, Mary Nagu,Mahanga will bring no difference and will be just business as usual. Kwanza teuzi nyingi zitakuwa nani alitusapoti nani alitusaliti. Pia kutakuwa na wale Yes sir kwa kila kitu, simply kwa sababu hawakupita ila uchakachuaji ndiyo uliwapitisha.

  Unless hiyo siyo Tanzania nnayoifahamu na muungwana nnayemfahamu.
   
 4. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Always Kiongozi wa GOI GOI ni GOI GOI+, Judgment day yao iko njiani yaja.
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye nyekundu sijuhi ulifanya analysis gani, ukweli uklio wazi JK hakubaliki kabisa hata na watu wa vijijini ambao mara nyingi tunawaona wao huwa wanaifata CCM, ukiniambia watu bado wanaipenda CCM naeza kukukubalia lakini sio viongozi waliopo sasa
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Habari yako William. I doubt kama ulikuwa na muda wa kutosha wa kutafakari kabla hujaandaka ulichoandika. To be honest huwa naziheshimu sana posts zako ndani ya jeief. Post yako ya leo inanifanya nijiulize kama nimekuwa nikifanya kitu sahihi au la. By the way sizungumzii siasa, nazungumza kama mtanzania wa kawaida ninayeipenda nchi yangu. Kama umefuatilia kwa karibu matokeo utakubaliana na mimi kwamba si kweli kwamba watz wanaimani sana na jk, huenda ilikuwapo hiyo imani 2005 lakini kwa sasa haipo period. Invisible alitufikirisha matokeo ya majimbo mawili moja ni Bukoba na jingine silikumbuki. Bukoba inaonyesha kwamba nusu ya watu waliopiga kura za urais hawakupiga za ubunge. This is almost impossible. Mathematically speaking matokeo ya urais yamepikwa tena kwa bahati mbaya na mtu ambaye hayuko smart kwenye hiyo kazi.

  Na unasema pia watu wanamtaka jk lakini hawawataki viongozi goi goi wa serikali yake. Huitaji Phd ya management kujuwa kwamba serikali goi goi inazalishwa na rais goi goi. Huwezi kuwa na rais strong ukawa na serikali goi goi never on earth., Rais ndiye anayeishape serikali, kwa maneno mengine kwa kuangalia tu serikali inavyotenda ndivyo n utendaji wa rais ulivyo.Ukiwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na watendaje wengine ambao ni hopeless maana yake ni kwamba rais naye ni hopeless kwani hao wote ni wateule wake, hakuna sababu ya kumpaka mafuta mtu kwa mgongo wa chupa kwenye hili.
   
 7. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mimi nimeangalia matokeo yaliyotangazwa, maana yanaonyesha kwamba Rais, Dr. Kikwete amepigiwa kura na wananchi wengi sana, isipokuwa nina wasi wasi kwamba wananchi either hawaridhiki na viongozi wake wa chini au chama, ingawa la viongozi wake wa chini linathibitishwa na idadi ya mawaziri walipigwa chini, isipokuwa ni mtizamo wangu tu maana Demokrasia inaruhusu na wewe kuwa na mtizamo wako!

  William.
   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Kwa vile unaongelea kutoka kwenye angle ya kura za urais kupikwa, then mjadala wote unakuwa hauna maana, mimi ninaongelea FACTS zilizotolewa na NEC bila kujali anything maana huu ni uwanja wa Great Thinkers siwezi kusema kura za Rais zimepikwa bila kutoa FACTS.

  - Kwenye hoja yako ya msingi ni kwamba Rais ni binadam mwenye mapungufu kama sisi wengine mara kwa mara anahitaji kukumbushwa mapungufu yake, ndio maana kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya jamhuri tunawapigia kura viongozi wetu wa taifa na local government, kwa mtizamo wangu wa matokeo ya huu uchaguzi ni kwamba mawaziri wengi wameshindwa, madiwani wa CCM wameshindwa sana, ndio niansema ujumbe hapa ni clear kwa Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi sana kwamba viongozi wake wa chini hawafai anahitaji kurekebisha hilo. Ni mtizamo wangu tu na wewe unaweza kuwa na wako unaotokana na kuamini kura zimepikwa, kitu ambacho mimi siamini hata kidogo.


  William.
   
 9. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  No umekosea sana kwenye tahminiyako, tumechoshwa na Kikwete mwenyewe, viongozi magoi goi wamezalishwa na Rasi goi goi, kilichotokea ni wizi tu wa kura lakini si mapenzi ya watanzania kwa kikwete, no way!
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Great Thinkers, tunatakiwa kuongea na FACTS mkuu!

  William.
   
 11. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Uchaguzi umekwisha na naona watu wametoa dondoo zao, nimestuka kiasi cha kuogopa jioni hii pale wakuu wa tume ya uchaguzi walipokiri hadharani kwamba madai ya Dr. Slaa kuwa kura za Geita zilikosewa ni sahihi na kwa sasa wamefanya mabadiliko hivyo hakupata kura 300, badala yake ni kura zaidi ya 20 elfu. Kwa nchi makini na watawala makini wasio magoi goi hii ilikuwa alama tosha ya mwenyekiti huyu kujiuzuru na kuhakiki majumuisho ya kura za urais upya kwa afya ya taifa. Bila kujari utashi wa vyama vyetu jambo hili ni aibu kwa Taifa na hata kwa mshindi atakayetangazwa maana nahisi majimbo yote yamekosewa kama hawatafanya uhakiki. Hivyo mtu aliyetangazwa kuwa asiyekubalika kwa umaa kama ndugu yangu William anavyodhani na hivyo kazi yake kuwa ngumu mno kuliko anavyodhani. Watanzania wa jana sio wa leo nami naamini kabisa hakuna amani ya kweli bila haki kama wanafanya makusudi kwa mtindo wa hujuma basi ni wazi kuwa nchi yetu haina amani na kuna siku nguvu ya uma itaishangaza nguvu ya mabomu na risasi. Siku chache kabla ya uchaguzi mgombea wa urais wa ccm alikiri hadharani kuwa sababu za kuwanadi mafisadi majimboni ni kwamba hao ndo watu alionao!! ajabu na aibu!! alimaanisha wazi kuwa ccm haina watu safi wanaokubalika bila dhuruma machoni pa umma wa watanzania.
  Naomba ndugu yangu William uongeze kwenye salamu zako kwa huyo mkuu ccm kuwa wananchi hawaridhishwi na chama kuendeshwa na nguvu ya pesa ya hujuma ya uchumi wa nchi na kama hili halitashugulikiwa basi 2015 hata Makame hataweza tena kuchakachua matokeo.
  Nawasilisha
   
 12. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #12
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Makondo heshima yako sana bro, ninasema hivi baada ya huu uchaguzi ni lazima wabunge wapya hasa wa Upinzani walivalie njuga tatizo hili la NEC, viongozi wote wa NEC ya sasa waondolewe haraka sana mara tu uchaguzi ukiisha na serikali itafute mbinu nataaluma mpya za kuikarabati hii tume iwe inafanana na siasa ya vyama vingi maaana sasa hivi imekaa kichama kimoja sana kwa maoni yangu.


  William.
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Inategemea kuwa nani anasema kuwa facts zipi ni genuine. Facts za nec zinanifanya niwe na wasiwasi nazo ukiangalia inconsistencies nyingi zilizojitokeza na kuzingatia conflicts of interests za wahusika wake. Time will tell kama uchaguzi huu ulikuwa sauti ya wananchi au la, na bahati nzuri muda huo unakuja kwa kasi sana. mark my words.
   
 14. F

  FIRST PRIORITY Member

  #14
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angarau umenifanya niulize baada ya kupigwa butwaa kidogo, nisaidie tafadhali, kuna vidfeo inaonyesha mh. Masha anawashukuru wananchi kwa kumgagua kwa kura zake 28,..... Ambazo ameshindwa na mgombea wa chadema 38,.... Je inakuwaje hapo, maana kwa mujibu wa gazeti la mwananchi ni kuwa mgombea wa chadema alishinda, na vurugu zilifanyika ili matakeo yatangazwe, ikawaje baadae, nimepagawa,

  nafikiri kuna haja ya kufanya kama kenya walivyofanya kama amani ya busara haipo basi ya ncha ya upanga...

  Kwanini hivyo, kwani Tanzania bila ccm haiwezekani?[/B]
   
 15. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umepewa facts kwenye #11

  Tafakari chukua hatua
   
 16. F

  FIRST PRIORITY Member

  #16
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  - Makondo heshima yako sana bro, ninasema hivi baada ya huu uchaguzi ni lazima wabunge wapya hasa wa Upinzani walivalie njuga tatizo hili la NEC, viongozi wote wa NEC ya sasa waondolewe haraka sana mara tu uchaguzi ukiisha na serikali itafute mbinu nataaluma mpya za kuikarabati hii tume iwe inafanana na siasa ya vyama vingi maaana sasa hivi imekaa kichama kimoja sana kwa maoni yangu.

  William.


  ni kweli kabisa, japo sijafahamu sana kuwa huwa hawa watu wa nec wanachaguliwa na nani... ila ukweli hawafai hata robo..... wanatangaza matokeo wasiyokuwa na hakika nayo... uchakachuaji + uoga = uzembe na kuharibu nchi
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nilisoma zamani hadhithi ya mtu mmoja aliyekua analamba miguu ya "bwana wake".... na sijui kwanini kila siku nakuona wewe kama mlamba miguu wa bwana ukitegema kupewa kitu... bahati mbaya huna chochote chenye ubora zaidi ya kuendesha watu maarufu wa bongo

  nashindwa kuelewa sauti ya wananchi gani wasiozidi 505 iheshimiwe, na nashindwa kuelewa wasio kwenye takwimu zako waheshimiwe na nani

  ch akujivunia ni kwamba hata mwanangu mwenye 10 years kaniambia "baba huyu analelewa na watu anaowapenda na kuwajali?
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  just FYI... dont think you can rate people as great thinkers or great suckers as you wish because i have seen you abusing this word now.... paki lori kakojoe ulale
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  he is just a great stinker
   
 20. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  William, wewe ni uzao wa CCM na umekulia katika mfumo huo huo wa kiCCM na utawala. Ni mmoja kati ya wale ambao wakiambiwa kuna watanzania wanashinda na njaa kwa kuwa wamekosa hata maboga ya kula wanashangaa kwanini wasingekula pilau. Kwa hiyo katika namna yoyote utakayoongea kumsifia boss wako na chama cha mafisadi mimi sitaona ajabu sana.

  Lakini ni lazima ukubali kwamba ni upuuzi na ufinyu wa mawazo kusema eti Kikwete amefanya vizuri lakini watendaji wake ndo wamefanya vibaya. Hao watendaji wake walijiweka wenyewe madarakani? Kwanini asingewaondoa kama alijua wanafanya vibaya? Kwani Kikwete tulimpeleka Ikulu akacheze mziki kule au asimamie rasilimali za nchi na kuitoa nchi kwenye shida na matatizo makubwa ambayo wananchi wake wanakabiliana nayo kila kuchwapo, kuipeleka kwenye maisha nafuu?

  Kwa Kikwete kurudi madarakani, naamini tutakuwa na miaka mitano mingine ya kupiga mark time. Naionea huruma nchi yangu Tanzania.
   
Loading...