Uchaguzi 2010: Kibonde usijifanye kujua kila kitu, tafuta wataalamu wakusaidie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Kibonde usijifanye kujua kila kitu, tafuta wataalamu wakusaidie

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Aug 31, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Katika kipindi cha Jahazi cha tar 31/8/2010 mtangazaji Kibonde amejifanya kuwa mtetezi wa JK na CCM kwa kuliponda pingamizi ya Dr Slaa na CHADEMA kuhusu JK kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

  Kwa bahati mbaya sana katika kutekeleza jukumu hilo Kibonde alizidi kudhihirisha umbumbumbu wake hadharani pale alipodai kuwa "Rais anayo mamlaka ya kuagiza matumizi ya fedha za Serikali atakavyo"

  Kwa maoni yangu Kibonde ana ufahamu mdogo sana wa kitu kinachoitwa Separation of Powers between the State (Serikali), Legislature (Bunge) and Judiciary (Mahakama). Hajo ya CHADEMA katika sakata hili ni mgombea wa CCM Jakaya Kikwete na Serikali yake ni kufanya matumizi ya fedha za umma kwa kukiuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Kwa mujibu wa Katiba Bunge ndio lenye jukumu la kuidhinisha makusanyo na matumizi ya fedha za Serikali.

  Kutokea mawaka 2006 TUCTA iliwasilisha madai ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali kufikia kima cha chini cha Shs 315,000/=.

  Kutokea mwaka 2006 JK na Serikali yake hawakuchukua hatua zozote kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa maana ya kupeleka ombi kwa bunge la kufanya matumizi ya ya ziada katika kulipa mishahara ya watumishi. Hivyo Bunge la 2006, 2007, 2008, 2009 na hata la 2010 Kikwete na Serikali yake walishindwa kuwasilisha ombi hilo.

  Wakati Serikali ya JK ilishindwa kuwasilisha ombi la kuongeza mishahara ya watumishi wake wanyoinge. Inadaiwa katika kipindi hicho iliwaongezea mishahara na marupurupu za viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Majaji n.k na pia kulipa malimbikizo ya nyongeza hiyo. Kama tutakumbuka vizuri wabunge wenye jukumu la kupitisha matumizi ya Serikali walipoona vigogo wenzao Serikalini wamejiongezea mishahara na marupurupu; wabunge nao wakawasilisha mapendekezo ya kuongezewa mishahara na marpurupu na wakapata.

  Ni kwanini CCM , Kikwete na Serikali yake waliamua kuwadharau wafanyakazi kwa miaka minnne kutoka mwaka 2006, na kuendelea kuwadharau hata pale walipotishia kugoma mwi 2010? Jibu walifanya hivyo kwa kuwa walijua TUCTA inaongea peke yake, haina asasi ingine ya kuisaidia hivyo Serikali itaweze kutumia vitisho kuzima jeuri ya TUCTA na Mgaya.

  Kuteuliwa kwa Dr Slaa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kulikuja kama mshituko kwa CCM JK na watanzania walio wengi. Na hoja yake ya kwanza wakati anafanya mikutano ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbali mbali ilikuwa kutamka wazi wazi kuwa anazihitaji kura za wafanyakazi zilizokataliwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salam Mei 2010, na akachapisha fulana zenye ujumbe huo.

  TUCTA ilipoona imepata msemaji wa kusaidiana naye katika kudai haki za wafanyakazi zilizokuwa zikipigwa danadana kutokea 2006, haikubweteka ikatoa tamko kwa wanachama wake kuwa wampatie kura mgombea anayeonyesha kuhitaji kura za wafanyakazi, kwa kuwa haiwezekani "ukampatia pilau mtu asiyeihitaji".

  Ni kutokana na pressure hizi za kuanza kwa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2010 CCM, Kikwete na Serikali yake wakasalimu amri na kutoa nyongeza ya mishahara kutoka Shs 135,000/= kufika Shs 235,000/= kimya kimya. TUCTA, CHADEMA na wadau wengine wakataka kufahamishwa ni nini kinaendelea ndipo Rais akajitokeza katika mikutano ya Kampeni za CCM mkoani Mwanza kudai kuwa Serikali yake inawajali sana wafanyakazi na tayari imewaongezea mishahara.

  Sasa Kibonde atuambie katika mtirirko huu wa matukio, ni kweli CCM ya leo na JK wanawajali wafanyakazi? Walikuwa wapi kwa miaka minne kuwapatia wafanyakazi nyongeza hiyo?

  Hoja kubwa ya Dr Slaa na CHADEMA sio wafanyakazi kuongezewa mishahara, bali wafanyakzi kutumika kama busati la kusafisha miguu na kukumbukwa baada ua upepo wa kisiasa kuwa mbaya kwa CCM na mgombea wake Jakaya Kikwete. Tujiulize kwa mtirirko uliotajwa hapo juu, iwapo vyama vya siasa vingesimamisha watu wasio makini kama Dr Slaa katika nafasi ya Urais, nyongeza ya mishahara iliyokuwa ikipigwa danadana kwa miaka minne kutoka 2006 na iliyotolewa wakati wa kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu ingepatikana?

  Sambamba na hilo Dr Slaa na CHADEMA wanahaji kitendo cha Rais na Serikali yake kukikuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Ni ukiukwaji huu uliosababisha kuwepo kwa Kashafa ya EPA, Meremeta, Tangold, n.k.

  Naomba wana JF wanaofahamu mipaka ya Rais kuagiza matumizi ya fedha za umma wakati usiokuwa wa dharura (emergency) bila ya kupata idhini ya bunge watusaidie kumhabarisha Kibonde kupitia hapa
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,006
  Trophy Points: 280
  na anashindwa kujua kuwa JK sasa anagombea uraisi, na mabo ya Chama na Serikali ni vitu viwili separate
   
 3. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyo jamaa mie simsikilizagi kabisa. Ni bumbumbu asiyejijua kuwa ni mbumbumbu. Anaongea sana pumba. Anakera kwa kweli. Halafu Clouds ni miongoni mwa radio zilizonunuliwa na mafisadi kuupotosha umma.
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ... huyu kijana ..huyu! ..he need to be awekened...!!!!!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Alichanwa na Mr Sugu bado hajakoma huyu!...Ana matatizo ya kiafya makubwa yanayoathiri kabisa kauli zake!..Actually ni wa kumwonea huruma sana huyu kijana!
   
 6. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtachoka kumjadili huyo dogo. Kwani mfalme wa mbumbumbu ambaye amewatuma anaitwa nani?
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hawa wote ni vibaraka, leo hii CCM ikianguka utawasikia wakisema si tulisema, yule mgombea hakuwa aliyefaa. Wanaganga njaaa zao na watafanya lolote hata kama ni kulamba manyeoo ya watoa riziki, ili mradi tonge lipate mchuzi na kinywaji kidogo
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  A person who knows and he is aware that he knows, is a wise, follow him
  A person who knows but is not aware that he knows, remind him.
  A person who don't know and he is aware that he don't know, teach him.
  A person who don't know and he pretend to know, is a fool, leave him

  Red is Kibonde a.ka. domokaya of redio mawingu.
   
 9. A

  ALIBAALIO Member

  #9
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitu nilichojifunza kuhusu Kibonde ni uelewa mdogo wa mambo, na hii inatia shaka kama anaweza kutofautisha au kuelewa maana ya separation of power.

  Lazima ajue kwamba pesa yeyote ya serikali ili iweze kutumika lazima ipitishwe na bunge. Sasa Kibonde atueleze ni bunge lipi limepitisha hiyo bajeti ya mishahara? Amewatia aibu wanahabari wengi na ndio maana watu wanasema wanahabari na watangazaji wa vyombo binafsi wana elimu ndogo
   
 10. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  jina lake tu linatosha kuelezea uwezo wake mdogo..! KIBONDE!

  AJIRA YAKE NI KWA AJIRI YA SAUTI YAKE NA SIO UELEWA WAKE...! kichwani kuna VOID
   
 11. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi mmemjua leo Kibonde????
   
 12. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  wala usimuonee huruma, ngoja tusubiri ile sheria ya maambukizi
   
 13. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Ina maana huyu dogo ana ugonjwa wa kuambukiza???!!
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kibonde anaweza U MC wa kwenye maharusi na vicheni party sio siasa..Kwa kifupi ni MPUMBAVU na sio mjinga narudia ni MPUMBAVU na anapenda sana kujikombakomba kwa viongozi...
   
 15. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kigogo safi sna:A S 8: hahhah
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jamani Katika hii Tasnia ya Sheria Kibonde ni Bonge la kilaza so anafaa aelekezwe Taratibu maana Pamoja na Ukilaza wake vile vile ni Mzito wa Kuelewa Halafu Mwepesi sana wa Kusahau, Kwa Wanajamvi Mkiona Kichwa kigumu sana Basi Kipuuzeni TU
   
 17. H

  Haika JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Sie kwetu jina la 'kibonde' lilikuwa na maana fulani, sijui kwanini kapewa hili jina
  Je ni la utani au alipewa utotoni kwa kuonyesha dalili fulani?
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Achaneni naye huyo Kibonde hana point, tatizo la waandishi na watangazaji wengi wa Bongo ni kudhani they can analyze everything na mara nyingi wanakuwa hawana data. Ndo walewale kwakuwa wanatangaza habari za michezo wanataka kuwa makocha vilevile. Achaneni nao hao wasioona mbali. Very miopic!
   
 19. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,401
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huwa ananiacha hoi na analysis zake uchwara,kuanzia siasa,uchumi na hata michezo.Ujuaji wa kijinga ukiongeza na njaa zake basi unapata mchanyato wa ajabu!
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Naomba nianze na "request" kwa yeyote atakayeweza kupata CV ya E. Kibonde na wenzake woooote hasa Gadner. Tuzipata tujue kama kweli kuna tija kuendelea kujadili hawa watu au la!! Kutokana na maneno yao tu, nilikwisha acha kusiliza vipindi vyao, maana ni mbumbumbu wa wazi wzi tu! Katika watu wanakera zaidi ni Gadner, anapenda kueleza vitu wakati hajui kitu.

  Hawa nawalinganisha na mapaka yanayoranda randa chini ya meza ya mlaji kutafuta makombo!! Hawa watangazaji wetu wanachekesha sana, badala ya kujitahidi kusoma sana ili kuwa na uelewa wao wanakalia kudakia dakia vitu wasivjo jua.

  Kwa kuwa wanapenda Makombo, laziwa wawe cheap, and so wamenunuliwa tu na mafisadi tunaopambana nao, wafikishe upupu wao kwa wapiga kura. Ni watu wasiojua walikotoka na wanakokwenda.

  Mwenye CV ya Kibonde please!!!
   
Loading...