Elections 2010 Uchaguzi 2010: Kibonde usijifanye kujua kila kitu, tafuta wataalamu wakusaidie

........niliacha kusikiliza kipindi cha jahazi kwa sababu ya Kibonde. I may resume tuning it on when he leaves broadcasting it. Kama kuna jambo analoshabikia huwa anachonga sana...mbaya zaidi huwa anatawaliwa na majungu zaidi,hapati muda wa kufanyia utafiti jambo. Kuna namna nyingi za bootlicking ila ya huyu Kibonde imezidi.
.....hey...hold on a second.....his name is Kibonde.....in swahili it sounds something numb,something brainless,....isn't it?
 
Jamani watanzania lazima tuelewe kwamba kibonde ni Kama wafanyakazi wengine kwenye private sector ...........lazima atetee kitumbu chake kwa nguvu zote. Alikuwa bias kwa sababu ya interest fulani fulani........Yaani jamaa si mwendawazimu wa kawaida ni mwehu aliyeshindikana kutibika kule Mirembe.

Ndugu zangu, wala msipoteze muda kumuwazia Kibonde. Kama lilivyo jina lake jamaa ni kibonde kweli kweli.
Wengine huwa tunamsikiliza ili walau tu-relax kidogo baada ya ma-stress ya ofisini. Na isitoshe naye anatumia nafasi ya kukaa studio kukipigia debe chama chake.
 
kibonde hana CV

mpuuzi sana huyo kijana na hana lolote

ujanja ujanja ndo unamweka mjini
 
Mnaouliza kuhusu maambukizi source hii hapa sikiliza wimbo wa MR II aliowachana Clouds FM
 
Popopoo KIBONDE, hana shule kabisaaa na akili yake ni mgando kabisa.Asitusumbua huyu Pipooooooooooooooooooos pawaaaaaaaaaaaaaa.
 
mmm alikosea kidogo jaman
no body iz perfect
kukopsea kupo
msameheni bure
 
Kikwetu Kibonde maana yake ni kopo la kunawia baada ya kumaliza kujisaidia haja kubwa.
 
Katika kipindi cha Jahazi cha tar 31/8/2010 mtangazaji Kibonde amejifanya kuwa mtetezi wa JK na CCM kwa kuliponda pingamizi ya Dr Slaa na CHADEMA kuhusu JK kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Kwa bahati mbaya sana katika kutekeleza jukumu hilo Kibonde alizidi kudhihirisha umbumbumbu wake hadharani pale alipodai kuwa "Rais anayo mamlaka ya kuagiza matumizi ya fedha za Serikali atakavyo"

Kwa maoni yangu Kibonde ana ufahamu mdogo sana wa kitu kinachoitwa Separation of Powers between the State (Serikali), Legislature (Bunge) and Judiciary (Mahakama). Hajo ya CHADEMA katika sakata hili ni mgombea wa CCM Jakaya Kikwete na Serikali yake ni kufanya matumizi ya fedha za umma kwa kukiuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Kwa mujibu wa Katiba Bunge ndio lenye jukumu la kuidhinisha makusanyo na matumizi ya fedha za Serikali.

Kutokea mawaka 2006 TUCTA iliwasilisha madai ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali kufikia kima cha chini cha Shs 315,000/=.

Kutokea mwaka 2006 JK na Serikali yake hawakuchukua hatua zozote kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa maana ya kupeleka ombi kwa bunge la kufanya matumizi ya ya ziada katika kulipa mishahara ya watumishi. Hivyo Bunge la 2006, 2007, 2008, 2009 na hata la 2010 Kikwete na Serikali yake walishindwa kuwasilisha ombi hilo.

Wakati Serikali ya JK ilishindwa kuwasilisha ombi la kuongeza mishahara ya watumishi wake wanyoinge. Inadaiwa katika kipindi hicho iliwaongezea mishahara na marupurupu za viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Majaji n.k na pia kulipa malimbikizo ya nyongeza hiyo. Kama tutakumbuka vizuri wabunge wenye jukumu la kupitisha matumizi ya Serikali walipoona vigogo wenzao Serikalini wamejiongezea mishahara na marupurupu; wabunge nao wakawasilisha mapendekezo ya kuongezewa mishahara na marpurupu na wakapata.

Ni kwanini CCM , Kikwete na Serikali yake waliamua kuwadharau wafanyakazi kwa miaka minnne kutoka mwaka 2006, na kuendelea kuwadharau hata pale walipotishia kugoma mwi 2010? Jibu walifanya hivyo kwa kuwa walijua TUCTA inaongea peke yake, haina asasi ingine ya kuisaidia hivyo Serikali itaweze kutumia vitisho kuzima jeuri ya TUCTA na Mgaya.

Kuteuliwa kwa Dr Slaa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kulikuja kama mshituko kwa CCM JK na watanzania walio wengi. Na hoja yake ya kwanza wakati anafanya mikutano ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbali mbali ilikuwa kutamka wazi wazi kuwa anazihitaji kura za wafanyakazi zilizokataliwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salam Mei 2010, na akachapisha fulana zenye ujumbe huo.

TUCTA ilipoona imepata msemaji wa kusaidiana naye katika kudai haki za wafanyakazi zilizokuwa zikipigwa danadana kutokea 2006, haikubweteka ikatoa tamko kwa wanachama wake kuwa wampatie kura mgombea anayeonyesha kuhitaji kura za wafanyakazi, kwa kuwa haiwezekani "ukampatia pilau mtu asiyeihitaji".

Ni kutokana na pressure hizi za kuanza kwa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2010 CCM, Kikwete na Serikali yake wakasalimu amri na kutoa nyongeza ya mishahara kutoka Shs 135,000/= kufika Shs 235,000/= kimya kimya. TUCTA, CHADEMA na wadau wengine wakataka kufahamishwa ni nini kinaendelea ndipo Rais akajitokeza katika mikutano ya Kampeni za CCM mkoani Mwanza kudai kuwa Serikali yake inawajali sana wafanyakazi na tayari imewaongezea mishahara.

Sasa Kibonde atuambie katika mtirirko huu wa matukio, ni kweli CCM ya leo na JK wanawajali wafanyakazi? Walikuwa wapi kwa miaka minne kuwapatia wafanyakazi nyongeza hiyo?

Hoja kubwa ya Dr Slaa na CHADEMA sio wafanyakazi kuongezewa mishahara, bali wafanyakzi kutumika kama busati la kusafisha miguu na kukumbukwa baada ua upepo wa kisiasa kuwa mbaya kwa CCM na mgombea wake Jakaya Kikwete. Tujiulize kwa mtirirko uliotajwa hapo juu, iwapo vyama vya siasa vingesimamisha watu wasio makini kama Dr Slaa katika nafasi ya Urais, nyongeza ya mishahara iliyokuwa ikipigwa danadana kwa miaka minne kutoka 2006 na iliyotolewa wakati wa kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu ingepatikana?

Sambamba na hilo Dr Slaa na CHADEMA wanahaji kitendo cha Rais na Serikali yake kukikuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Ni ukiukwaji huu uliosababisha kuwepo kwa Kashafa ya EPA, Meremeta, Tangold, n.k.

Naomba wana JF wanaofahamu mipaka ya Rais kuagiza matumizi ya fedha za umma wakati usiokuwa wa dharura (emergency) bila ya kupata idhini ya bunge watusaidie kumhabarisha Kibonde kupitia hapa

Nakuunga mkono KAMANDA kwa ufafanuzi ulio makini, ni kweli KIBONDE asifikiri kuchambua siasa ni kama kuchambua mpira!
 
Kikwetu Kibonde maana yake ni kopo la kunawia baada ya kumaliza kujisaidia haja kubwa.

:becky:...Yaani kwa maana ya "Jamani Kibonde kiko wapi nataka kwenda ch**ni!" Duh. Siku yangu imekamilika mapemaa!

:becky::becky:
 
kibonde ni mchumia tumbo tu kama wachumia tumbo wengine.....

anachokifanya hakina tofauti sana na wale maprofesa wa UDSM walioacha kufundisha wakaenda kujiunga na mafisadi wa chama tawala ili nao waigie katika system ya ulaji..naomba nimkumbuke mwalimu wangu Dr Msekela katika hilo........

napenda kuelewa kwa nini kibonde anafanya analofanya na kwa hivyo sipati shida sana...ni tumbo tu.....

tazama vijana wa leo wenye degree na vihiyo kama kibonde...wengi wanatamani siasa kupitia ccm kwani huko wanaamini ni rahisi kupata madaraka na hivyo kukaa sambamba na walaji na ulaji...ikiwa wasomi wengi ambao tungetaraji wawe front kuipinga ccm wanaikimbilia, vihiyo wafanyeje???????? ni kwa mantiki hiyo nawapa big up sana vijana waliojitoa muhanga kugombea uongozi kupitia upinzani.. kwangu hawa ndio wapinzani wa kweli maana wanajua kuwa they stand a big chance to loose lakini wanasimamia kile wanaamini...

kibonde na ujinga wake ni ushahidi wa pale tumefika kama Taifa...we are screwed up...

we are going thru hell, we must keep going and never give chance kwa wapumbavu kama efraim kibonde kutupoteza...

wanaotaka kumchana waendelee lakini better we behave na kumchana kwa hoja juu ya alichokisema na sio personality...hatutofika kama nasi tutakuwa na cheap thinking...

ni mtazamo tu........
 
Tusker Bariiiidi,

Mzee haujambo rafiki?

Mimi nimeahamia Kilimanjaro sasa- unajua ladha ya Tusker imebadilika sana baada ya kuchukuliwa na SBL ..hivyo nikashindwa!

Ila bado tupo pamoja!
 
Wasanii wa mjini hao sidhani kama wana ata CV midomo ndo CV zao.Tena utakuta leo jioni lazima waijadili jamii forums kwa kuwakosoa.
Unaweza kuta kwa wanayoongea wengi wanawasifu kuwa wanaongea point ndo maana wanadiliki kuyaingilia mambo mazito kama hayo
 
Nakuunga mkono KAMANDA kwa ufafanuzi ulio makini, ni kweli KIBONDE asifikiri kuchambua siasa ni kama kuchambua mpira!

hata mpira unahitaji utaalamu kuuchambua...

kwa watu wenye kujua mpira lakini, sio kama hapa bongo ambapo unachohitaji ni kujuana na mtangazaji tu..kama ni mshikaji mnakutana bills au wapi basi unapewa shavu nawe unakuwa mchambuzi wa masuala ya soka

lakini kwa vyombo makini si kila mwenye kuupenda anaweza kuwa mchambuzi hapana....

tazama supersport hakuna wapumbavu pale wanaochambua soka......
 
kibonde na wenzake wengi ni COMEDIANS WA UTANGAZAJI kama alivyo Mpoki na Masanja.
 
Mtu mwenye hombwe kichwani usibishane naye daima hombe ili itoke nikujazwa sasa mjazaji hayupo!!Huyo ni Kinbonde!:mad2::mad2::mad2:
 
jamani sikupenda kuingia jamvini asubuhi hii.Kibonde , nimjuavyo mimi , aliwahi kuwa rafiki yangu kipindi nikiwa hapo Dar, hatua kwa hatua tukaanza kutofautiana kwasababu yakupenda kujikomba, nakumbuka mkienda maeneo ya starehe lazima atafute watoto wa waheshimiwa walipokaa akakae nao, atatafuta watu maarufu mjini kama kina Taji Liundi akae nao , atawalamba miguu, atawanyenyekea......naamini hajabadilika, bado anaendelea na mwenendo huo, nimjinga fulani hivi, hana a wala b, hana mbele wala nyuma. ni mtu wakutafuta cheap popurality,.najua hua anaingia humu, siruhusiwi kutaja ID yake, lakini najua atanipigia simu kwa maoni yangu, lakini uzuri ni kuwa jamaa anajua kua siku hizi simpendi.Endelea na kujipendekeza kwa Rais, endelea kujipendekeza kwa utawala, unasubiri uteuzi wa ukuu wa Wilaya kama ambavyo umekua ukitamba kwenye vilinge kadhaa.
 
kibonde mnamuonea......
kwanza amesha declare yeye ni kada wa ccm,
pili kipindi chake ni kama comedy fulani..
sio kipindi serious......

nyinyi mnaomchukulia serious ndio mnapata tabu...

mimi namchukulia kama entertainer hivi....simchukii.....
The Following User Says Thank You to The Boss For This Useful Post:

Teamo (Today)​
 
Back
Top Bottom