Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,420
- 2,271
Kamanda FM
P.S. Hivi huo mji wa pili ni Mwanza au Dodoma?
Picha zote ni kutoka katika Jiji la Mwanza.
Kamanda FM
P.S. Hivi huo mji wa pili ni Mwanza au Dodoma?
Wa kulaumiwa ni yule aliyevunja serikali za mitaa zilizoachwa na mkoloni.
hakuna haja ya kulaumu kila mtu kwa huo uchafu,laumu serikali za mitaa ambazo ni madiwani & mayors maana hao ndio wana jukumu la kutunga na kusimamia sheria za usafi za miji yao,kumbuka hizo serikali za mitaa zina uwezo wa kuweka sheria na kushtaki na kukusanya fees kwa ajiri ya usafi wa sehemu zao na wanapata pesa kutoka serikali kuu pia...sioni sababu ya kulaumu raisi au kila mtu huku tunajua waliopewa hiyo kazi ni kina nani,lazima watu wawajibike sio kulaumu kila mtu la sivyo itakuwa ni kusingiziana tuu kila kitu!
Bin Maryam, weye mchokozi sasa! Wataka tuanze umjadili mtuhumiwa mkuu wa kudhoofika kwa maendeleo?Wa kulaumiwa ni yule aliyevunja serikali za mitaa zilizoachwa na mkoloni.
Vipi kuhusu uwajibikaji wa mtu binafsi...huoni kwamba kila mtu ana wajibu wa kuweka mazingira anayoishi katika hali ya usafi wa hali ya juu?
Mkuu Mtanzania,
Mimi bado natofautiana na wewe. Solution za kutegemea wananchi zinafaa vijijini lakini si mijini. Vijijini wana njia zao za kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika. Mama mwenye nyumba chafu kwa mfano binti yake hapati mchumba. Huko ndiko solution kama kuchimba visima ili wakabiliane na shida ya maji kunawezekana. Solution hizi hazitafanya kazi mijini kwa sababu kuu mbili:
1. Miji haina wenyewe kwa hiyo zile taratibu za kuwekana sawa kijijini hazifanyi kazi. Mama mchafu anaweza kumpatia mchumba mwanae bila shida yeyote kama vigezo vingine vinavyothaminiwa mjini (pesa, uzuri n.k.) atakuwa navyo. Vile vile mjini anaweza kukuta watu ambao hawaoni uchafu kuwa ni tatizo.
2. Mlundikano wa watu mjini unahitaji usimamizi na utaalamu ambao mtu binafsi hatokuwa nao. Mahali kama Manzese hata wajioganaiz vipi tatizo la maji litahitaji mamlaka husika kushirikishwa. Hauwezi kuchimba kisima maana kila sehemu ina mwenyewe na upatikanaji wa maji safi utahitaji matumizi ya mashine ambazo ziko nje ya uwezo wa wananchi wengi.
Tukitazama hili la uchafu, hata wananchi wa Manzese wafanye nini bila kuwa na chombo kitakachoweza kuukusanya huo uchafu na kwenda kuutupa mahali panapostahili, juhudi zao zitakuwa bure. Mfano angalia vile vitrela vya kuchukua uchafu vinavyo overflow. In desperation wananchi wamefikia hatua ya kuchoma bila kuangalia madhara ya moshi ulio na sumu! Wengine wanawalipa watoto wa mjini kuchukua na kwenda kutupa taka hizo sehemu wanazojua wao.
Hii ndiyo inayonipelekea kusema kuwa katika mazingira ya miji ni lazima utawal uwajibike kwa kuweka nyenzo na system za kushughulikia suala la uchafu. Wakishafanya hivyo, ndiyo waweke bye-laws zitakazomwadhibu yeyote ambaye atasababisha uchafu maana hatokuwa na sababu. Singapore unalipa faini kama unatupa Big G chini, kama hauflush public toilet kwa sababu mapipa na vyoo havikosi maji kwa hiyo hauna sababu ya kufanya vinginevyo. Sehemu nyingi Ulaya wenye mbwa wana wajibika kukusanya choo cha mbwa wao kwa sababu sehemu ya kukitupia kiko kila sehemu. Mtu anayeacha kinyesi cha mbwa wake bila kukikusanya anaadhibiwa!
Utamlaumu vipi mtu kujisaidia nyuma ya mti kama hamna huduma ya vyoo vya umma? Utamlaumu vipi mtu kutupa maganda ya ndizi chini kama hamna sehemu ya kutupia? Na zaidi ya haya, utawalaumu vipi wote hawa kama hauwaadhibu wakifanya hivyo wakati vyoo vipo na vipipa vipo?
Miji inahitaji utawala unaowajibika ili ifanye kazi. Hili sidhani kama tunaweza kukwepa.
...true,lakini usifikiri watu wote wana hiyo akili ya uwajibikaji,lazima watu wawajibishwe kwa kutumia sheria na wa kufanya hiyo kazi ni hizo serikali za mitaa na ndio mana tunachagua madiwani na kuna viongozi wanaolipwa kufanya hizo kazi,ukilaumu kila mtu utaonekana mpiga kelele tuu na hakuna kitu kitafanyika,source ya huo uchafu ni hao viongozi wa hizo sehemu tuu na hakuna kingine!
Tatizo lako wewe na mlio wengi mna mentality tegemezi...kwamba ni lazima mshurutishwe kufanya jambo fulani la sivyo hakitafanyika chochote. Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe na kwa kulingana na maoni yako basi hata watu tunaowachagua wako kama sisi wananchi---meaning na wao hawana akili ya uwajibikaji---sasa unategemea nini..?
Bin Maryam, weye mchokozi sasa! Wataka tuanze umjadili mtuhumiwa mkuu wa kudhoofika kwa maendeleo?
...hata hiyo miji misafi duniani unayoiona usifikiri ilikuwa ni misafi kwa sababu ya tabia nzuri za watu,kwa taarifa yako ni sheria zilizotungwa na zinavyofuatiliwa na baadaye kuzoeleka na kuwa kama culture ndio sababu ya hiyo miji misafi kuwa hivyo,mentality ya watu kama nyie ni kulaumu tuu kila mtu tatizo linapotokea,kumbuka sio kila mtu ni mchafu sasa hao wachache wanaochafua unafikiri uta wa contain vipi kama hulazimishi sheria zifuatwe,mawazo yako yanaishia kulaumu tuu na kusubiri tabia za watu kubadilika ukitegemea kila kitu kitabadilika,nenda londoa then tupa ganda la ndizi barabarani uone kitakachokupata!
Tatizo lako wewe na mlio wengi mna mentality tegemezi...kwamba ni lazima mshurutishwe kufanya jambo fulani la sivyo hakitafanyika chochote. Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe na kwa kulingana na maoni yako basi hata watu tunaowachagua wako kama sisi wananchi---meaning na wao hawana akili ya uwajibikaji---sasa unategemea nini..?
Vipi kuhusu uwajibikaji wa mtu binafsi...huoni kwamba kila mtu ana wajibu wa kuweka mazingira anayoishi katika hali ya usafi wa hali ya juu?
Haya sasa nimeshajaza bin langu nifanye nini ?