Waziri TAMISEMI fuatilia posho za mafunzo ya maafisa tarafa na watendaji kata mkoa wa Lindi

zama mpya

New Member
Mar 8, 2023
1
2
Tunaandika haya kwa uchungu, na masononeko baada ya kufanyiwa ukatili wa kutudhulumu stahiki zetu za posho kwa maafisa tarafa na watendaji wa kata.

Mh. Waziri Manispaa ya Lindi inaundwa na majimbo mawili ya Lindi mjini na Jimbo la Mchinga ambayo zamani ilikua ipo Halmashauri ya Lindi vijijini kwa sasa Mtama.

Katika mafunzo hayo kumefanyika ukatili mkubwa kutoka kwa afisa wa TAMISEMI aitwae Ibrahim Minja kwa kutudharau ma kutoa majibu ya kebehi na majivuno makubwa.

Wakati wa kujaza fomu za malipo tulijaza na madaraja ya mishahara tukiambiwa kwamba posho italipwa kwa kuzingatia vigezo hivyo.

Lakini cha kuchekesha Halmashauri nyingine kama vile Mtama wao waliwalipa kwa kuzingatia vigezo hivyo lakini ilipofika kwa manispaa wote tumelipwa kiwango sawa (Flat rate) shillingi 75,000 tu.

Lakini pia kwa watendaji kutoka jimbo la Mchinga ambako kimsingi ni vijijini wao wamelipwa hela ya siku mbili tu tena half perdiem wakati ili wawahi mafunzo hayo iliwalazimu wafike siku ya Tarehe 25 na kulala, lakini Bwana Minja yeye akaamuru walipwe siku mbili.

Umbali kutoka kata za jimbo la mchinga mpaka lindi mjini ni kata ya mchinga ambako ni kilometa 31 kata nyingine zote zilizobaki umbali wake mpaka mjini Lindi ni kilometa 50,60,70,80.Mazingira yake ni vijijini kabisa.

Kwa kweli hakuna haki iliyotendeka jimbo la mchinga limepachikwa tu katika manispaa ya lindi lakini ukweli ni kwamba mazingira yake umbali na miundombinu yake sio rafiki kata nyingi za mchinga usafiri wa umma mwisho ni saa 6-7 mchana ukikosa hapo utalazimika kuchukua usafiri wa bodaboda ambao ni gharama au ulale katika nyumba za wageni. Siku ya mwisho ya mafunzo watu wametoka ukumbini saa 12 jioni ,muda huo magari yameshaisha yote ikawalazimu walale tena mjini.

Mh. Waziri weu mpendwa wa TAMISEMI tunatambua wewe ni mcha MUNGU mpenda haki na usiyependa dhuluma isipokuwa kuna watu wachache serikalini kwa ulafi wao wanataka kuichonganisha serikali na watumishi wake, tunakuomba suala la stahiki za posho hususani perdiem kwa watumishi wa jimbo la Mchinga ulitolee maelekezo maalumu kwenye zoezi hili la mafunzo lakini pia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 na mazoezi mengineyo ili kuondoa sintofahamu na kinyongo nawatu kupoteza uzalendo na imani kwa Serikali.

Tuna imani na wewe Baba Mchengerwa sema neno ili watumishi wako kutoka jimbo la mchinga wapate kupona. Tunaomba jimbo la ,mchinga liangaliwe kwa busara ili kutokuwaumiza watumishi wake.
 
Shukuruni kwa hicho kidogo mlichopata hayo mafunzo hayakuwa yanawahusu Sana maana watu waliopo zaidi karibu na wananchi ni watendaji wa vijiji hivyo ufinyu wa bajeti ndo ukafanya nyie muitwe japo najua hayo mafunzo hayawezi leta tija tarajiwa maana yamekwenda sehemu isiyo sahihi
IMG-20231122-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom