Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Mar 26, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Chicken has come home to roost!

  Hivi tutamlaumu nani? Mwenye nyumba, diwani, katibu kata, meya, halmashauri, mbunge, DC, mkuu wa mkoa Waziri wa afya, Nyumba, Tamisemi, Mazingira, miundombinu, Waziri Mkuu au Raisi?

  Hivi tukipata mlipuko wa kipindupindu tutapona?

  [​IMG]
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 26, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Mimi nawalaumu wote maana ukichunguza kwa undani au hata kwa juu juu tu utagundua kwamba kila mmoja wa hao uliowataja wanahusika kwa namna moja au nyingine.
   
 3. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhani mwenye nyumba, kisha serikali za mitaa. Maana kama tatizo ni dimbwi basi wananchi wanaweza kujitokeza na kulijaza kifu, lakini kama tatizo ni mfumo wa maji machafu, then serikali ya mitaa ndio inanguvu na swala hilo.

  Rev au tuwalaumi mafisadi nini?
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ASANTE NYANI....! WAKATI NAANZA KUSOMA HUKU NIKITAFAKARI JIBU MUAFAKA......NILIPITA ULIMOPITA....! HAKUNA WA KUBAKI.....WOTE HAWAJA-PLAY ENOUGH KTK HILI.....LAWAMA ZIWAANGUKIE WOTE NA WOTE WAFANYE YANAYOWAPASA KUFANYA......NA SI KULAUMIANA KAMA ILIVYO JADI YETU....!
   
 5. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida yetu tunatafuta wa kulaumu badala ya kutafuta suluhisho, kwa mtindo huu basi mimi nasema tuwalaumu mafisadi wa Buzwagi, Richmond na waliokwiba pesa za EPA na waliokopa NSSF na hawajalipa hadi leo!:mad::(
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi natupia lawama viongozi. Nchi zote ambazo sasa hivi tunaona kuwa ni kioo cha usafi, hazikuwa siku zote hivi. Singapore ilikuwa bandari masikini na chafu kwa kila jinsi walipopata uhuru.

  Ni uongozi wao waliochukizwa na hali hiyo na kuweka sheria ambazo zilimwadhibu raia yeyote atakayeendekeza uchafu. Miji ya uingereza, ufaransa yote nayo ilikithiri kwa uchafu mpaka utawala ulipopitisha sheria ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa iliyokuwa kama tija wakati ule.

  Ni mlipuko wa mara kwa mara wa Cholera ndiko kuliwafanya wenzetu wapitishe sheria ambazo kwanza zililazimishe local authorities wajenge sewer systems na wakazi wote wa mjini kuunganisha kwenye hizo sewers! Wananchi walipinga sana wakiona kuwa ni utawala wa ubabe lakini utawala ulishinikiza mpaka hali ikakubalika. Bila uongozi ulioamka hamna kitakachofanyika.

  Hali hii ya uchafu kukithiri mara nyingi ni mijini na sio vijijini. Vijijini kila mwenye nyumba anawajibika katika sehemu yake na hapo awali sehemu kubwa ya uchafu uliokuwa ukizalishwa ulikuwa ni bio-degradable. Hapa mjini hakuna mwenye mji na bila uongozi kuweka sehemu na taratibu za kukabiliana na hali hii hakuna ambacho mwananchi wa kawaida anachoweza kufanya.

  Kama hakuna taratibu za kukusanya taka, mwananchi aishie katikati ya mji ni vigumu kuchimba shimo la kutupia taka zake. Ziwekwe taratibu na kuhakikisha kuwa zinafuatwa. Bahati mbaya taratibu hizo zinafanywa dili kiasi cha kumuondolea mwananchi hamu ya kuzitumia!
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Rev. Kishoka,

  Hapo sisi wote tunawajibika na matatizo ya TZ. Kila mmoja wetu au wengi wetu tukitimiza wajibu wetu, Tanzania itasonga mbele.

  Watu hapa wajuzi wa kuandika makala ndefu kulaumu wengine lakini ukifuatilia unagundua wengi hatuna tofauti na hao tunaowalaumu.

  Sirikali ikitimiza wajibu wake, ni kweli maendeleo yatakuja haraka. Lakini je serikali ikilala, kwanini na sisi wananchi tulale?

  Kwa kushirikiana mmoja mmoja, wawili wawili, tunaweza kabisa kuondoa hilo tatizo.

  Huko nyuma niliwahi kuandika jinsi jamaa mmoja alivyoweza kuondoa tatizo sugu kwa solution rahisi sana huko kwao baada ya kutoka Ulaya. Alichoshwa na uchafu uliokuwa unazunguka maeneo yao pamoja na kwamba watu wote waliokuwa wanaishi huko walikuwa watu wenye kipato na nyumba za maana. Yeye alianza kwa kuwashawishi watu wachache ili watumie vijana waliokuwa wanakaa bure kukusanya takataka na kwenda kuzitupa mbali. Baada ya muda watu karibu wote wa eneo hilo wakajiunga na vijana pia wakaanzisha kikundi chao cha kukusanya takataka kwa mikokoteni.

  Sio optimum solution lakini ilifanya kazi na kila mtu akawa happy. Wangeendelea kusubiri serikali, mpaka leo wangekuwa wanasota na uchafu.

  Wakati mwingine mukiiumbua serikali hivyo, inaweza kushutuka na kufanaya kweli.

  Mbona kwenye elimu hatuisubiri serikali? Mbona tunapeleka watoto wetu kwenye mashule ya bei mbaya wakati ni wajibu wa serikali kutoa elimu kwa raia wake? Hivyo hivyo hata kwenye afya. Kwanini tunashindwa kwenye mambo mengine?

  Watu wakitoa pesa zao, itafika mahali watasema hapana, na kuamua kuwabwaga wanasiasa ambao hawafanyi kitu. Uchafu unaua ndugu zetu, kulalamika peke yake sio solution kabisa.
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Serikali yetu kwa muda mrefu imekuwa ikipata free ride kutoka kwa wananchi. Hakuna sehemu ya huduma ambayo imeona inawajibika kuanzia usalama wa raia(sungusungu), kinga za moto(imekuwa biashara ya machinga kwa wenye uwezo), shule ( private) hospitali (private) na mengineyo. Hao wananchi wakikusanya huo uchafu watautupa wapi maana dampo zimegeuzwa makazi? Kwa wenye uwezo kuwatoa watoto wao kwenye shule za serikali ndiko kulikochangia kwa kiasi kikubwa kudumaa kwa sekta ya elimu.

  Kwa wenye uwezo kupelekwa India, Uingereza na Marekani ukiachilia Hindu Mandal n.k. kumechangia kushuka kwa huduma za hospitali za serikali. Kwa wenye uwezo kuweza kuweka walinzi private kumechangia hali iliyopo katika vyombo vyetu vya usalama ambako huko mitaani mwananchi anaambiwa nenda kamlete mbaya wako hapa poli post. Kwa wenye uwezo kuweza kununua mashangingi kumefanya hali za barabara zetu kuwa kama zilivyo.

  Kwa wenye uwezo kuweza kujiwekea self konteina kwenye maofisi kumefanya hali ya vyoo vya wafanyakazi wa kawaida kuwa haisemeki. Inabidi wanachi waanze kudai huduma stahili kutoka kwa hao wanaowachagua kuwaongoza maana ni kodi yao itakayotumika.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Umachinga ninaouzungumzia kwenye biashara ya moto ni huu! Hawa wanapaki chini ya mwembe kungoja biashara. Nchi gani inayojiheshimu umeona hilo?
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Fundi Mchundo

  Unachoongelea ni chicken and egg scenario, nini kilianza kwanza? Shule zilikuwa mbovu kwanza na ndio watu wakahamisha watoto wao au watu walianza kuhamisha watoto wao kwasababu shule zilikuwa mbovu? Mimi nafikiri
  shule zilianza kuwa mbovu.

  Watu wakitaka kutafuta solution wataipata tu, kibaya ni hii tabia ya kukaa na tatizo bila kuhangaika na kufikiri. Hicho ndio kinatokea TZ kwenye mambo mengi ikiwemo suala la uchafu.

  Hata suala la maji, kuna solutions ambazo watu 20 wakikaa pamoja wanaweza kugundua ni bora kuliko kusubiri shirika la maji lisilojali wateja.

  Kitu ninachoongelea mimi ni kwamba, hakuna tatizo lisilo na jawabu. Mtu ukikaa kimya na kusubiri mtu mwingine aje akutatulie matatizo yako, jua umeshashindwa. Kama ni wajibu wa serikali sawa, lakini fanyeni jambo ili hiyo serikali iamke, au iangushwe. Vinginevyo utakaa na uchafu mpaka miaka mingapi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mtanzania,

  Mimi bado natofautiana na wewe. Solution za kutegemea wananchi zinafaa vijijini lakini si mijini. Vijijini wana njia zao za kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika. Mama mwenye nyumba chafu kwa mfano binti yake hapati mchumba. Huko ndiko solution kama kuchimba visima ili wakabiliane na shida ya maji kunawezekana. Solution hizi hazitafanya kazi mijini kwa sababu kuu mbili:

  1. Miji haina wenyewe kwa hiyo zile taratibu za kuwekana sawa kijijini hazifanyi kazi. Mama mchafu anaweza kumpatia mchumba mwanae bila shida yeyote kama vigezo vingine vinavyothaminiwa mjini (pesa, uzuri n.k.) atakuwa navyo. Vile vile mjini anaweza kukuta watu ambao hawaoni uchafu kuwa ni tatizo.

  2. Mlundikano wa watu mjini unahitaji usimamizi na utaalamu ambao mtu binafsi hatokuwa nao. Mahali kama Manzese hata wajioganaiz vipi tatizo la maji litahitaji mamlaka husika kushirikishwa. Hauwezi kuchimba kisima maana kila sehemu ina mwenyewe na upatikanaji wa maji safi utahitaji matumizi ya mashine ambazo ziko nje ya uwezo wa wananchi wengi.

  Tukitazama hili la uchafu, hata wananchi wa Manzese wafanye nini bila kuwa na chombo kitakachoweza kuukusanya huo uchafu na kwenda kuutupa mahali panapostahili, juhudi zao zitakuwa bure. Mfano angalia vile vitrela vya kuchukua uchafu vinavyo overflow. In desperation wananchi wamefikia hatua ya kuchoma bila kuangalia madhara ya moshi ulio na sumu! Wengine wanawalipa watoto wa mjini kuchukua na kwenda kutupa taka hizo sehemu wanazojua wao.

  Hii ndiyo inayonipelekea kusema kuwa katika mazingira ya miji ni lazima utawal uwajibike kwa kuweka nyenzo na system za kushughulikia suala la uchafu. Wakishafanya hivyo, ndiyo waweke bye-laws zitakazomwadhibu yeyote ambaye atasababisha uchafu maana hatokuwa na sababu. Singapore unalipa faini kama unatupa Big G chini, kama hauflush public toilet kwa sababu mapipa na vyoo havikosi maji kwa hiyo hauna sababu ya kufanya vinginevyo. Sehemu nyingi Ulaya wenye mbwa wana wajibika kukusanya choo cha mbwa wao kwa sababu sehemu ya kukitupia kiko kila sehemu. Mtu anayeacha kinyesi cha mbwa wake bila kukikusanya anaadhibiwa!

  Utamlaumu vipi mtu kujisaidia nyuma ya mti kama hamna huduma ya vyoo vya umma? Utamlaumu vipi mtu kutupa maganda ya ndizi chini kama hamna sehemu ya kutupia? Na zaidi ya haya, utawalaumu vipi wote hawa kama hauwaadhibu wakifanya hivyo wakati vyoo vipo na vipipa vipo?

  Miji inahitaji utawala unaowajibika ili ifanye kazi. Hili sidhani kama tunaweza kukwepa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Takataka barabarani....
  [​IMG]

  [​IMG]


  Wengine hupenda kutupa takataka kwenye mito...sijui pengine ni rahisi kwao..
  [​IMG]

  Hata hivyo Usahau kuwa takataka wanazutupa kwenye mito huishia baharini au ziwani,ambako tunapata vitoweo vyetu
  [​IMG]

  [​IMG]


  Pamoja na juhudi za ujezi wa miundo mbinu... lakini sio wote wapendao kutupa taka zao katika sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo, badala yake....
  [​IMG]

  [​IMG]


  Kwa wanaokerwa na tatizo la uchafu ni swala la uwamuzi tu, bila kusubiri serikali, kwani tatizo bado lipo kwenye elimu ya usafi..
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]


  Baada ya wananchi kuelewa ni wepesi kushiriki katika usafi..
  [​IMG]

  [​IMG]  Lengo ni kuwa na miji safi kwa Afya zetu na Mazingira kwa ujumla..
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Pesa za vita Comoro wanazo lakini kutengeza nyumbani hakuna
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ukiangalia hiyo picha ya nyumba na maji machafu utagundua kuwa si mvua ya siku moja tu ambayo imeleta uchafu mkubwa namna hiyo.

  Kwa rangi ya tope, ni rahisi kubaini kuwa maji machafu ni kawaida kuizunguka hii nyumba mpaka kuna kuwa na algae. Angalia ule ukuta wa uzio, tayari umepata algae, angalia nyasi kubwa za kuzalisha mbu, si mvua ya siku moja inatosha kurutubisha nyasi hizo kwa kiwango kikubwa hivyo!

  Jiulize, kipindupindu na malaria ambazo zitaikabili familia iliyoko kwenye nyumba hii, ni lawama kwa Serikali pekee?

  Ni kweli killa mtu niliyemtaja anastahili lawama. Mwenye nyumba kwa kuendelea kuacha uchafu na maji machafu ya bafuni na chhoni yaendelee kumwagika mtaani, Diwani, kata na meya, kwa kukosa kutembelea maeneo yao na kuhamasisha usfai wa mazingira ama kutunga sheria, DC na Waziri kwa kushindwa kuhakikisha kuwa kuna mfumo bora wa miundombinu ambayo utajenga mabomba na mifereji ya chini ya ardhi ya kuondoa maji machafu, kushindwa kudhibiti ujenzi holela wa nyumba bila kufuata mipango miji kuhakikisha nyenzo na huduma muhimu zinapatikana katika maeneo haya, kushindwa kupitisha sheria kudhibiti uholela wa majumba na uchafu, kukosekana kwa utashi wa kupata maisha na afya bora.

  Ni vigumu kupiga vita maradhi kama tutaendelea kuwa maskini wa mawazo na vitendo na kuachilia uchafu kama huu au hizi picha alizoonyesha Kibunango uendelee na kuzagaa.

  Mbaya zaidi ni kujengwa kwa lile tabaka la wenye kustahili kuishi mahali safi (matajiri na wageni) ambapo Halmashauri za jiji hata Serikali huhakikisha usafi wa mitaa, mifereji, barabara unafanyika.

  Ni jukumu letu sote kutaka kuishi mahali safi, pasipo na uchafu au harufu ya uozo. Mfano huu wa mtaani ni mdogo sana. Nenda masokoni, Tandale, Kisutu, Kariakoo na magenge mengine ambako ndipo unajinunulia chakula, hali za masoko haya ni taabani na hakuna mfumo bora wa uchukuzi wa takataka au kuwepo kwa maji safi na mifereji ya kuondoa maji machafu.

  Si ufisadi au Comoro ambako tutalaumu Serikali kwa kushindwa kulazimisha usafi uwe kipaumbele. Ni lazima tuwe na utashi na kutaka mahali bora. Ni lazima tuwajibike kama familia, kata na jamii. Ikiwa wawakilishi na viongozi hawafanyi kazi zao, si kuna njia za kuwawajibisha kama kura?

  Ni ajabu sana kuwa vijijini ambako tunadhani hakuna maendeleo au wako nyuma kwa kuwa wanakwenda kuteka maji maili moja na vyoo vyao vya shimo, wana usafi wa hali ya juu mara elfu kuliko ndugu huyu wa Mwananyamala au hizo picha nyingine.

  Swali ni hili, ikiwa Vijijini tunakuona shamba na kuna utaratibu na uratibu bora, kwa nini basi tusimrudishe huyu ndugu na wengine wa mijini huko vijijini wakajifunze Usafi kwa nyenzo nyepesi?
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kibunago,

  Pamoja na kuniondolea appetite ni lazima nikushukuru kwa hizo picha na hasa kwa kuweka contrasts humu humu nchini kwetu.

  Ukiangalia kwa makini utaona kuwa uchafu unalundikwa kwenye no man's land, kuanzia mini dampos hadi open drains. Hivi kama kweli hao waliopewa mandate ( wako jamani) ya public health wangewajibishwa hii hali ingekuwepo? Wangewajibishwa si kwa kushindwa kuondoa uchafu bali kutokua na mipango ya kukabiliana nao! Hao askari wa jiji ambao wanafukuzana na machinga wangemwagwa katika maeneo yenye open drains permanently na kuwajibika kuhakikisha hakuna taka inayoingia humo.

  Hizo operesheni usafi ziwe za kudumu na si kwa kuleta watu kutoka nje kufanya usafi bali kuwalazimisha wakazi na watumiaji wa maeneo husika kuwajibika!

  Iko kazi kweli.

  P.S. Hivi huo mji wa pili ni Mwanza au Dodoma?
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Rev. Kishoka

  Kweli tupu, Mkuu.

  Lakini huyo anayeishi karibu na hayo maji angefanya nini? Ajaze kifusi au ahame? Hapo zamani palikuwa na kamto kanapeleka maji ya mvua naturally kutoka sehemu za msasani, kijitonyama kupitia bwawa lachumvi na kuendelea msasani mikoroshini hadi baharini. Wakubwa wakajaza kifusi bwawa la chumvi na kugawana viwanja. Pale ambapo maji yalijitahidi kupita nakwenyewe waliziba wakagawana viwanja. Wenye mamlaka wakawapa ofa na building permits. Kazi imebaki kwa hao walalahoi ambao maji kwao sasa yana simama hayana mahali pa kwenda. Katika vitongoji palikuwa na sehemu za wazi ambazo wananchi waliweza kutupa taka ( si hygienic lakini aheri kuliko hii ya sasa) lakini hao hao wenye mamlaka wamegawa sehemu hizi kwa wenye nazo. Hizi sehemu zingefaa kuwa collection points, sasa hazipo. Mimi ndiyo maana sehemu kubwa ya lawama nawatupia wao. wao ndiyo wanaotakiwa kuongoza development ya miji yetu bila kuathiri afya za wakazi wake na hawafanyi hivyo. Hao health inpektas kwa nini wasifunge hayo masoko mpaka hali iwe ya kuridhisha? Haya ya siku moja katika mwaka kugawana T-shirt, kuimba ngonjera na kugawana vijibahasha na kufagia vijisehemu hakuta tufikisha mbali!

  Niliwahi kusimuliwa kuwa kuna wakati huko Makutupora JKT kuna kijana alijisaidia nje ya bweni kwa kuogopa kwenda kwenye vyoo vilivyokuwa mbali. walipoulizwa hakuna aliyekiri kufanya kitendo hicho. basi afande akawaagiza wote waishio kwenye bwalo hilo kuwa ikifika wakati wa disko jioni kila mmoja amuonyeshe kipande cha ule mzigo kwenye kiganja chake ama sivyo wataipata. Kwa vile afande yule alikuwa anajulikana kwa suluba, watu ilibidi wamegeane ule mzigo. Toka hapo hakuna aliyerudia tena mchezo huo wakijinga!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Pamoja na udahifu wa serikali zetu za mitaa na ungozi usafi uchafu pia ni hulka na silka za mtu!
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hakuna anayezaliwa msafi. Ni malezi na mafunzo ndiyo yanayotufanya hivyo!
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Fundi,

  Nimejiuliza, hivi Mkubwa wa nchi akiziona hizi picha zimechapisha kwenye magazeti na wakati wa kikao cha baraza la mawaziri akasema "I do not want to see this again" will the reaction be to stop publication and taking more pictures by Waziri wa Habari or efforts to clean the area?

  Msichape hizi picha zimemkasirisha Rais na kuliaibisha Taifa, I believe will be the reaction top down kutoka kwa viongozi na si kuhakikisha kuna mipango bora ya kuondoa takataka!
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Touche, Mkuu! Inawezekana kabisa na wale waliopiga wakachukuliwa hatua!!!
   
Loading...