Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Mwanakijiji.. tutake radhi yaani sie sawa na hii picha
y1pIjS-ngexYeXGBi9Ve2_ZOREQibbxzii9BaH1fROPZxMbuzwY95PlI92B3pDuswKl9SDAULad-P4

.

Huyo mbwa kalala au kafa ?
 
Hivi, tukianza kutoa elimu ya kusafisha mazingira na kuanzia kwa nyumba halafu mtaa, je tutapokelewa au tutadhihakiwa na kupuuzwa?
 
Rev.

I always say and I will say it. Tanzania tunahitaji viongozi wawajibikaji. watu tutaingia line tuu! Ukiwa na Meya mweye akili za maendeleo, lazima wananchi tutakuwa na mwamko wa kuwa wasafi. Mengi wengi wameshaelezea huko nyuma. Hivi jiulize, ukipitisha kama bylaws kwamba anayetupa taka hovyo mtaani/au taka ikikutwa hovyo karibu na kwako ulipe faini..na sheria ikatekelezwa kisawa sawa..what will happen?

Kinachotumaliza waafrika ni kwamba tuna sheria za aina mbili.. za walionacho (ruling class, their families, wasomi nk) na sheria za raia (wakulima, wanaoishi below 0.50$$ nk) sasa katika mazingira kama hayo..nadhani we need the redifination ya utawala wa sheria..maana kama utawala wa sheria ndo mlio nao huko ulaya na USA..nadhani huku Africa tuna kitu kingine tofauti kabisa.

Dawa ya uchafu ni ku-enforce sheria vikali watu watatekeleza tuu. LAZIMA TUFIKE POINT TUACHE KUENDESHA DOLA KAMA KAMPUNI AU BIASHARA YA REJA REJA (ILE YA KUPIGA BEI)...

Ndo maana mpaka leo mtu anaiba $$$ of millions anaambiwa arudishe na hatajwi hadharani..na wala hamna consequences..you got it? Only in Africa.

WATU WAKIPEWA MADARAKA WAKAJUA HAPA SIO ULAJI NI KUWAJIBIKA, I TELL YOU HATA WANAOGOMBEA HIZI NAFASI WATABADILIKA! UTAANZA KUPATA WASOMI NA WENYE MOYO WAKIINGIA KWENYE UONGOZI. But for now watu wanajua uongozi especially wa kisiasa..ni deal la kupata hela za mkato..and on and on...

Uchafu kwa sehemu za mjini ni kutunga na kutekeleza kwa makini by laws. mtu anapewa tenda ya kukusanya taka kwa sababu anafahamiana na meya..hana hata gari la kuzolea taka...only in Africa..
 
Hivi, tukianza kutoa elimu ya kusafisha mazingira na kuanzia kwa nyumba halafu mtaa, je tutapokelewa au tutadhihakiwa na kupuuzwa?

Hiyo ndio njia pekee ya kuweza kuwafikia wadau. Ni kwenda nyumba kwa nyumba.
Utekelezaji wake wakati mwingine unakuwa ni mgumu kutoka na mambo mbali mbali:
  • Muda wa zoezi unaweza kutopata watu wengi
  • Kuna tatizo la kiitikadi, na hasa unapofuatana na Diwani
  • Kwenye nyuma za kupangisha waakazi hukwepa na kusukumia kwa mwenye nyumba
  • Nyumba zenye uzio na mageti makubwa ni tatizo kuwapata wahusika
 
Thanks Kibu...typical bongo! Nakumbuka wakati sijahama pale Kimara....mkuu..nimekumbuka mbali sana...
 
Hivi, tukianza kutoa elimu ya kusafisha mazingira na kuanzia kwa nyumba halafu mtaa, je tutapokelewa au tutadhihakiwa na kupuuzwa?

Rev:

Elimu ni muhimu. Lakini siku zote tumeiangalia elimu kama silver bullet na hili ni kosa kubwa.

Wakazi karibu wote wa DSM wanajua kusoma na kuandika na wanaelewa fika kuwa uchafu sio kitu kizuri lakini bado wanaishi kwenye mitaa michafu.

Mada ni uchafu mitaani. Na nina uhakika mkubwa ndani ya nyumba za watu usafi hupo.

Kinachoshindikana na kusababisha uchafu mitaani ni baada ya watu kusafisha nyumba zao au kutumia products kukosa miundombinu ya ku-process uchafu au masalio ya products walizotumia.

Ukosefu wa miundombinu ya ku-process uchafu au masalio ya products walizotumia sio suala la elimu ni suala la miundombinu za miji.

Vilevile tukumbuke kuwa wakazi wa mijini wa sasa na matumizi yao, kuna wakati wana-produce toxic waste ambao ni uchafu mbaya kwa mazingira na afya. Hivyo wananchi kujitolea kusafisha kwa kutumia mikono kama inavyoonekana kwenye picha ni kuhatarisha maisha ya wananchi.

Kuna digrii za mazingira, uongozi wa serikali, city planning na nyinginezo. Kama ni elimu basi tuangalie jinsi ya kutumia fani hizi katika maendeleo ya miji.
 
Hivi jamani hata kusafisha nyumba yako, bafu lako, choo chako, ua wako, mwili wako, kwapa lako, mdomo wako, n.k. unahitaji elimu kweli?
 
Hivi, tukianza kutoa elimu ya kusafisha mazingira na kuanzia kwa nyumba halafu mtaa, je tutapokelewa au tutadhihakiwa na kupuuzwa?

unajua Rev. tatizo sio kutolewa elimu, trust me unajua tanzania mambo mengi ambayo watu wanadhani hakuna yalikuwepo before, ni kwamba watu wamezoea kila fulani basi wao wanafall huko huko. hiyo elimu imetolewa na inaendelea kutolewa, watu wakizoea kitu esp. watanzania, basi jua kuna tabu !
 
Nyani tuliza boli...

Kinachozungumziwa hapa ni usafi wa mazingira na namna ya ukusanyaji na utupaji wa taka. Elimu inayohitajika hapa ni pamoja na;
  • Kujua aina za taka
  • kutenganisha taka
  • utunzaji wa taka kabla ya kutupwa
  • na wapi pa kutupa taka hizo
 
Ningependa kuuliza mliosoma kwenye shule za mabweni, je mambo huko yalikuwaje kwenye upande wa vyoo.

Shule niliyosoma ilikuwa ni lazima ujue ku-syncronize. Maana vyoo vya mashimo vilikuwa vinajaa maji sana hivyo ukiisi kuwa kitu kinadondoka basi ni lazima usimame haraka kabla maji machafu hayajakurukia. Na ukitoka huko inabidi upunge hewa kwa nusu saa kuondoa harufu.
 
Nyani tuliza boli...

Kinachozungumziwa hapa ni usafi wa mazingira na namna ya ukusanyaji na utupaji wa taka. Elimu inayohitajika hapa ni pamoja na;
  • Kujua aina za taka
  • kutenganisha taka
  • utunzaji wa taka kabla ya kutupwa
  • na wapi pa kutupa taka hizo

Aisee nimeanza kuhisi wewe una utaalamu wa haya mambo ya uzoaji taka/ usafi wa mazingira maana inavyoelekea unayaelewa sana!
 
Aisee nimeanza kuhisi wewe una utaalamu wa haya mambo ya uzoaji taka/ usafi wa mazingira maana inavyoelekea unayaelewa sana!

Usije ukanishambulia kwa staili ile ya FM....:)

Tukiandelea na somo la takataka ni vema wakati wa kutoa elimu hiyo kwa wadau kuelezea aina za taka na hasa za majumbani, ambazo ni:
  • Taka hatari(hazardous waste)
-betri
-taa za umeme zilizokwisha tumika
-rangi,gundi(glues) na vanishi
  • Biowaste
-taka za jikonizitokanazo na maandalizi ya upishi na mabaki ya vyakula
-majani ya chai
-mabaki ya maganda ya mayai,katooni za mayai
-taka toka katika bustani, majani n.k
  • Vyuma(metal)
-tins
-cans-makopo ya aluminium
-aluminium dishes
 
Usije ukanishambulia kwa staili ile ya FM
....

Kama FM ni mimi, sidhani kama nimewahi kukushambulia Kibunango! Au unamaanisha kuwa nina staili fulani ya kushambulia watu? Au ni kawaida yangu kushambulia watu?

Mimi sielewi nimeingiaje katika masuala yenu! Si mngemaliziana bila kunihusisha! Kama unamaanisha FM mwingine, niwie radhi.
 
[/COLOR]....

Naona umenielewa vibaya.. Nilikuwa na maana ya Nyani kukuita profesa ...:D

"I did'nt mean to offend you."
 
Back
Top Bottom