KERO Changamoto ya umeme wa REA Kata ya Ipande, Chalinze

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa heshima na tadhima naomba JF ujumbe huu uwafie wahusika.

Kipindi umeme wa REA unasambazwa, mwaka 2017 aliyekuwa Waziri wa Nishati Menad Kalema alituahidi wana Ipande kwamba umeme utaenda nyumba hadi nyumba mpaka nyumba ya udongo ili mradi tu amelipia.

Baada ya hapo umeme mpaka leo hii mkoa wa Mbeya Wilaya ya Kyela kata ya Ipande kijiji cha Mbula umeme ulipita moja kwa moja hadi kwa diwani (CCM), center ya kata, shuleni (Secondary Ipande) zahanati na baadhi ya marafiki wa diwani walio muunga mkono uchaguzi wa mwaka 2020.

Kuna mdau kupitia uwezo wake binafsi inasemekana aliamua kununua transformer na kuomba ashushiwe umeme hadi kwake na majiran zake ambapo ulighalim nguzo za umeme 20 kwa ghalama binafsi.

Baada ya hapo unaambiwa mdau huyo aliumwa sana (kwa hila za kiimani japo siyo approved) na diwani aliyopo madarakani alimfata na kumtishia kuto rudia tena kuleta maendeleo kwenye kata yake akihofia ni harakati za kuja kugombea udiwani 2025 angali diwani wa sasa amedumu tangu 20000 had sasa.

Na wadau wakihoji ngazi za wilaya inaonekana diwani amejiridhisha ya kuwa umeme upo kila mtaa wakati siyo kweli.

Na hii yote inaobesha ni hasira za diwani mwenyewe kwa kukosa kura kwenye kijiji cha Mbula kata ya Ipande mwaka 2020 na kuonekana kupita kwake ni kwa hila.

Na anafanya hivi kwa kiapo cha kuwakomoa mpaka atakapo toka madarakani.

Je, ni haki kiongozi kufanya hivi? Na anazuia mamlaka ya kuu kwa kupeleka taarifa zisizo za ukweli?

Naomba JF kupitia mtandao wa huu.

Mhamasisheni Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya na Meneja wa TANESCO wakaongee na raia wa kata ya Ipande na kujionea kwa macho yao.

Kujiridhisha je, umeme upo au haupooo?
 
Huyo diwani yupo madarakani tokea 2000 mpaka sasa, ni kina nani wanaompigia kura?
 
Ila hapo Chalinze dizain kama pamelaaniwa (samahani kwa kutumia lugha ngumu kidogo)

Toka wakati wa Mh Mzee Kikwete yupo madarakani kama mbunge hadi anakuwa raisi kwa miaka kumi continuously ulikuwa ukipita mgeni ukaambiwa kiongozi wa juu wa kitaifa kama raisi anatoka hapo ungekataa,na amestaafu unaenda mwaka wa kumi pako vile vile na wakazi wake wala wasiwasi hawana.

Labda ni mambo ya kisiasa?nani anajua!
 
Back
Top Bottom