Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

hakuna haja ya kulaumu kila mtu kwa huo uchafu,laumu serikali za mitaa ambazo ni madiwani & mayors maana hao ndio wana jukumu la kutunga na kusimamia sheria za usafi za miji yao,kumbuka hizo serikali za mitaa zina uwezo wa kuweka sheria na kushtaki na kukusanya fees kwa ajiri ya usafi wa sehemu zao na wanapata pesa kutoka serikali kuu pia...sioni sababu ya kulaumu raisi au kila mtu huku tunajua waliopewa hiyo kazi ni kina nani,lazima watu wawajibike sio kulaumu kila mtu la sivyo itakuwa ni kusingiziana tuu kila kitu!
 
Vipi kuhusu uwajibikaji wa mtu binafsi...huoni kwamba kila mtu ana wajibu wa kuweka mazingira anayoishi katika hali ya usafi wa hali ya juu?
 
Interesting fact is that on the pictures that show Watu wa Jiji wakisafisha na kuzoa taka, there is someone who will belittle them for what they do, by being disrespectuflly verbally and even throw more trash jsut because they can tawanya uchafu kukomoa.

Now this is the attitude problem, which many of us are at fault!
 
Vipi kuhusu uwajibikaji wa mtu binafsi...huoni kwamba kila mtu ana wajibu wa kuweka mazingira anayoishi katika hali ya usafi wa hali ya juu?

...true,lakini usifikiri watu wote wana hiyo akili ya uwajibikaji,lazima watu wawajibishwe kwa kutumia sheria na wa kufanya hiyo kazi ni hizo serikali za mitaa na ndio mana tunachagua madiwani na kuna viongozi wanaolipwa kufanya hizo kazi,ukilaumu kila mtu utaonekana mpiga kelele tuu na hakuna kitu kitafanyika,source ya huo uchafu ni hao viongozi wa hizo sehemu tuu na hakuna kingine!
 
Mkuu Mtanzania,

Mimi bado natofautiana na wewe. Solution za kutegemea wananchi zinafaa vijijini lakini si mijini. Vijijini wana njia zao za kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika. Mama mwenye nyumba chafu kwa mfano binti yake hapati mchumba. Huko ndiko solution kama kuchimba visima ili wakabiliane na shida ya maji kunawezekana. Solution hizi hazitafanya kazi mijini kwa sababu kuu mbili:

1. Miji haina wenyewe kwa hiyo zile taratibu za kuwekana sawa kijijini hazifanyi kazi. Mama mchafu anaweza kumpatia mchumba mwanae bila shida yeyote kama vigezo vingine vinavyothaminiwa mjini (pesa, uzuri n.k.) atakuwa navyo. Vile vile mjini anaweza kukuta watu ambao hawaoni uchafu kuwa ni tatizo.

2. Mlundikano wa watu mjini unahitaji usimamizi na utaalamu ambao mtu binafsi hatokuwa nao. Mahali kama Manzese hata wajioganaiz vipi tatizo la maji litahitaji mamlaka husika kushirikishwa. Hauwezi kuchimba kisima maana kila sehemu ina mwenyewe na upatikanaji wa maji safi utahitaji matumizi ya mashine ambazo ziko nje ya uwezo wa wananchi wengi.

Tukitazama hili la uchafu, hata wananchi wa Manzese wafanye nini bila kuwa na chombo kitakachoweza kuukusanya huo uchafu na kwenda kuutupa mahali panapostahili, juhudi zao zitakuwa bure. Mfano angalia vile vitrela vya kuchukua uchafu vinavyo overflow. In desperation wananchi wamefikia hatua ya kuchoma bila kuangalia madhara ya moshi ulio na sumu! Wengine wanawalipa watoto wa mjini kuchukua na kwenda kutupa taka hizo sehemu wanazojua wao.

Hii ndiyo inayonipelekea kusema kuwa katika mazingira ya miji ni lazima utawal uwajibike kwa kuweka nyenzo na system za kushughulikia suala la uchafu. Wakishafanya hivyo, ndiyo waweke bye-laws zitakazomwadhibu yeyote ambaye atasababisha uchafu maana hatokuwa na sababu. Singapore unalipa faini kama unatupa Big G chini, kama hauflush public toilet kwa sababu mapipa na vyoo havikosi maji kwa hiyo hauna sababu ya kufanya vinginevyo. Sehemu nyingi Ulaya wenye mbwa wana wajibika kukusanya choo cha mbwa wao kwa sababu sehemu ya kukitupia kiko kila sehemu. Mtu anayeacha kinyesi cha mbwa wake bila kukikusanya anaadhibiwa!

Utamlaumu vipi mtu kujisaidia nyuma ya mti kama hamna huduma ya vyoo vya umma? Utamlaumu vipi mtu kutupa maganda ya ndizi chini kama hamna sehemu ya kutupia? Na zaidi ya haya, utawalaumu vipi wote hawa kama hauwaadhibu wakifanya hivyo wakati vyoo vipo na vipipa vipo?

Miji inahitaji utawala unaowajibika ili ifanye kazi. Hili sidhani kama tunaweza kukwepa.

FM,

Lete solutions zako za mjini sasa, maana kulalamika tumesikia, na tatizo liko pale pale. Unayeona kuna solutions za vijijini na zile za mjini, basi tuletee za mjini.

Watu wanaendelea kufa kwa magonjwa yatokanayo na uchafu, kwanini tusitafute solution?

Wakipewa Wazungu hayo maeneo, watapata solution, huku Watanzania bado tunasubiri serikali ije utuokoe. Kama mnaweza itoeni hiyo serikali, lakini
kama hamna uwezo wa kuitoa serikali mtafanya nini? Mtaendelea kuzungukwa na uchafu?
 
...true,lakini usifikiri watu wote wana hiyo akili ya uwajibikaji,lazima watu wawajibishwe kwa kutumia sheria na wa kufanya hiyo kazi ni hizo serikali za mitaa na ndio mana tunachagua madiwani na kuna viongozi wanaolipwa kufanya hizo kazi,ukilaumu kila mtu utaonekana mpiga kelele tuu na hakuna kitu kitafanyika,source ya huo uchafu ni hao viongozi wa hizo sehemu tuu na hakuna kingine!

Tatizo lako wewe na mlio wengi mna mentality tegemezi...kwamba ni lazima mshurutishwe kufanya jambo fulani la sivyo hakitafanyika chochote. Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe na kwa kulingana na maoni yako basi hata watu tunaowachagua wako kama sisi wananchi---meaning na wao hawana akili ya uwajibikaji---sasa unategemea nini..?
 
...hata hiyo miji misafi duniani unayoiona usifikiri ilikuwa ni misafi kwa sababu ya tabia nzuri za watu,kwa taarifa yako ni sheria zilizotungwa na zinavyofuatiliwa na baadaye kuzoeleka na kuwa kama culture ndio sababu ya hiyo miji misafi kuwa hivyo,mentality ya watu kama nyie ni kulaumu tuu kila mtu tatizo linapotokea,kumbuka sio kila mtu ni mchafu sasa hao wachache wanaochafua unafikiri uta wa contain vipi kama hulazimishi sheria zifuatwe,mawazo yako yanaishia kulaumu tuu na kusubiri tabia za watu kubadilika ukitegemea kila kitu kitabadilika,nenda londoa then tupa ganda la ndizi barabarani uone kitakachokupata!
 
Bin Maryam, weye mchokozi sasa! Wataka tuanze umjadili mtuhumiwa mkuu wa kudhoofika kwa maendeleo?

Kizazi cha sasa cha watanzania kinaweza kujifunza mambo mbalimbali kwa kuangalia makosa yetu ya nyuma, kuyarekebisha makosa hayo na vilevile kutumia maarifa ya wenzetu hili tuweze kuendelea. Kwa mtaji huu aliyefanya makosa kwa kujaribu si mtuhumiwa hata kidogo.

Swali la kujiuliza ni kuwa serikali za mitaa za wakati wa mkoloni ziliendeshwa na wazawa ambao elimu yao ilikuwa sio kubwa sana lakini walileta ufanisi mkubwa katika uongozi wa miji, kwanini leo katika nchi huru na viongozi wenye madigrii miji ni michafu?
 
...hata hiyo miji misafi duniani unayoiona usifikiri ilikuwa ni misafi kwa sababu ya tabia nzuri za watu,kwa taarifa yako ni sheria zilizotungwa na zinavyofuatiliwa na baadaye kuzoeleka na kuwa kama culture ndio sababu ya hiyo miji misafi kuwa hivyo,mentality ya watu kama nyie ni kulaumu tuu kila mtu tatizo linapotokea,kumbuka sio kila mtu ni mchafu sasa hao wachache wanaochafua unafikiri uta wa contain vipi kama hulazimishi sheria zifuatwe,mawazo yako yanaishia kulaumu tuu na kusubiri tabia za watu kubadilika ukitegemea kila kitu kitabadilika,nenda londoa then tupa ganda la ndizi barabarani uone kitakachokupata!

Ni wazi sikatai kwamba kuwa na sheria ni muhimu lakini pia uwajibikaji nao ni muhimu vile vile na ndio maana kwenye bandiko langu la kwanza kwenye mada hii nilisema wote waliotajwa ni wa kulaumiwa. Mtu huhitaji polisi kuja kusimamia usafi wa choo, bafu, jiko, au ua wako! Kutupa takataka barabarani...hapo labda unahitaji polisi atakayekukamata akikuona unatupa uchafu. Sasa hapo huoni kwamba wote tuna wajibu?
 
Tatizo lako wewe na mlio wengi mna mentality tegemezi...kwamba ni lazima mshurutishwe kufanya jambo fulani la sivyo hakitafanyika chochote. Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe na kwa kulingana na maoni yako basi hata watu tunaowachagua wako kama sisi wananchi---meaning na wao hawana akili ya uwajibikaji---sasa unategemea nini..?

Nyani Ngabu:

Hili suala la maendeleo ya miji sio jipya duniani. Iwapo mtu mmoja itabidi atoke nje asafishe mazingira yalio karibu yake na Usiku awepo kwenye ulinzi wa sungusungu kwa sababu ni wajibu wake kulinda mji wake basi ule msemo wa wakati wenzetu wanatembea sisi tuwe tunakimbia katika kutafuta maendeleo tuachane nao na turudi kuishi maisha ya kizamani kila mtu katika kijiji chake.

Mathematically speaking viongozi wetu sio reflection yetu. Kwa sababu natural selection au unbiased experiment haikufanyika kuwapata viongozi hao.
 
naomba nitoe wazo kwani mwaka mmoja hivi uliopita niliandika makala ile ya "Taifa lililozoea uchafu" kwenye Kulikoni.

Jamii ya watu waliozoea kuona uchafu, na uchafu huo kwao haunuki tena, yaani wameuzoea kiasi kwamba harufu yake hainusiki tena; basi jamii hiyo huwa imezoea uchafu.

Sasa watu waliozoea uchafu, na kuuona ni wa kawaida, hawawezi kuusafisha. Kwanini wasafishe kitu ambacho hakinuki? Akija mgeni na mara ya kwanza akanusa harufu ya uchafu huo; na kuwaambia "inanuka" wale watu wanaweza kumshangaa, "mbona tumeuzoea" watasema.

Lakini watu wale wale wakiondoka eneo hilo na kwenda eneo lenye usafi, na kunusa harufu ya usafi, wakaipenda, na wakaona ni tofauti na harufu ile waliyoizoea (ya uchafu) basi watu wale wakirudi kwenye jamii zao, watanusa tena harufu ya uchafu.

Sasa, endapo wale walioona usafi na kuuonja uzuri wake wanaporudi kwenye jamii zao zenye uchafu, wakakenua pua zao kwa kukereka na uchafu, lakini baada ya muda wakasahau harufu ya usafi waliyoonjeshwa wakazoea tena uchafu basi watu hao ni wasaliti wa usafi.

Sasa, kimsingi kabla ya kuweza kuondoa uchafu, ni lazima mtu aukatae kwanza, auone ni kero, auchukie, umuudhi, na kumtia kinyaa! Asipokuwa na hisia hizo dhidi ya uchafu, basi mtu huyo hana msingi au msukumo wa kuundoa; kwanini aondoe kitu kisichomkera?

Hivyo, kabla ya kutaka kusafisha uchafu ni lazima kwanza kama mtu mmoja mmoja na kama jamii tuukatae uchafu, tuuone ni mbaya, unatudhalilisha na ni kinyume na maslahi ya jamii na mtu binafsi hapo ndipo tutaweza kusema na kuanza kutenda kuundoa uchafu.

Hapo basi hatutasubiri serikali kuu au ya mitaa au wazungu waje na kutuonesha kuwa uchafu ni mbaya.

So, by extension, kabla hatujaweza kubadili vitu vibaya na vichafu, lazima kwanza tuvikatae na kuviona kuwa havifasi na tusivizoee moyoni.

Kijana aliyevaa vizuri na kujimwagia manukato ghali anapopita karibu na shimo la taka, hasikii harufu ya uchafu na atasema yeye ni msafi; atakuwa anasema kweli. Nyumba nzuri ambayo ina kila aina ya amenities za kisasa iliyojengwa karibu na dampo au kwenye kuta zake ndipo dampo limehamia, basi mwenye nyumba anaweza kusema ana nyumba safi;

Lakini kwa kadiri kwamba uchafu ule unawaangalia wote wawili, ni uthibitisho kuwa usafi wao hauuhisiani na mazingira kwani wao wanaishi safi katika uchafu! (oxymoronic). Ni sawa na Mwanyika aliposema kuwa yeye ni "Safi milele na milele" wakati ushahidi wote unaonesha kuwa ofisi yake ni chafu!

Swali la kuponder:

Je mtu msafi ni yule asiyegusa uchafu, au yule ambaye ameondoa uchafu?
 
Mimi naona wa kulaumiwa ni watanzania woooote! Maana sisi wote ni watanzania, na kwa ujumla wetu, naweka lawama hapo kwa sababu sis watanzania tunachukulia mambo "as is". Yaani hatuoni ajabu barabara ni za mashimo, maji machafu kutoka kwenye vyoo yapo tu mitaani (lakini tunapita njiani hapohapo tukiyaruka!), matakataka yanazagaa tu hovyo(lakini na sisi tunatupa hapohapo). Sasa basi wote - Mpangaji, Mwenye nyumba, diwani, katibu kata, meya, halmashauri, mbunge, DC, mkuu wa mkoa Waziri wa afya, Nyumba, Tamisemi, Mazingira, miundombinu, Waziri Mkuu au Raisi ambao wote ni wananchi, tunatakiwa tunaone haya yote kama ni mambo yaliyo kinyume na kanuni za afya na usalama na aidha tuyakemee, tuyarekebishe na hatimaye kuyaondoa kabisa. Kama kila mtanzania akielewa ubaya wa.. na akishupalia swala la uhaba wa maji, umeme, kuzagaa kwa maji machafu, au barabara mbovu, rushwa, etc. nadhani somo litaeleweka tu, na taifa letu litakuwa swaaaafi kabisa!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom