Sababu za Jerry Silaa kukumbwa na mikosi

Sababu za Jerry Silaa kukumbwa na mikosi

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,910
Reaction score
3,232
111.jpg


Siasa za makundi na kushindwa kusoma alama za nyakati ndio vinatajwa kuwa sababu ya mikosi anayopata aliyekuwa Mbunge wa Ukonga na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

Mkosi wa hivi karibuni uliompata ni Kesi Ardhi Namba 000032646 ya Mwaka 2024, shauri hilo linatokana na tukio la Februari 29, 2024 ambalo Silaa, Manispaa ya Kinondoni na Naomi Raymond Kwayu wameamriwa na Mahakama kulipa fidia ya Sh3.18 bilioni kwa kubomoa nyumba ya makazi kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi jijini Dar es Salaam, pia imewaamuru wadaiwa hao kulipa fidia ya madhara ya jumla ya Sh40 milioni pamoja na gharama zote za kesi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za kesi, Silaa akiwa Waziri wa Ardhi wakati huo, alifika katika eneo husika na kusimamia ubomoaji wa nyumba hiyo.

Hukumu ya kesi hiyo ilitolewa Januari 21, 2026 na Jaji Sharmila Sarwatt aliyebatilisha uamuzi wa Waziri Silaa wa kubomoa ghorofa, unatokana na mgogoro wa umiliki wa kiwanja kilichopo Kitalu Namba 484 (2196), Block H, Mbezi Medium Density, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Hata hivyo, tayari Serikali imewasilisha notisi ya kusudio la kukata rufaa mahakamani hapo kupinga hukumu hiyo pamoja na tuzo (decree) yake.

Mkosi huo umekuja wakati bado Silaa akiwa kwenye maumivu ya kupoteza ubunge wa Jimbo la Ukonga katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 baada ya kuangushwa na Bakari Shingo wa ACT Wazalendo.

Silaa amekuwa miongoni mwa Wabunge watano wa CCM waliopoteza majimbo upande wa Bara.

Aliingia bungeni Mwaka 2020 na Mwaka 2023 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi Mwaka 2024, alipoteuliwa kuwa Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari.

Kabla ya kuwa Mbunge, Mwaka 2015 alichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Gombo la Mboto na baadaye akawa Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Jerry aliikosoa nini mamlaka?


Hakuwa na ushirikiano na wenzake

Kwa mujibu wa chanzo ndani ya CCM, inaelezwa kuwa miongoni mwa sababu za Jerry kupoteza Jimbo la Ukonga ni pamoja na misigano ya ndani kati yake na baadhi ya chama hicho.

“Jerry alipopata ubunge na kuwa waziri, alijisahau sana na kujenga kiburi miongoni mwa wenzake,” amesema mmoja wa makada wa chama hicho, ambaye hakutaka kutajwa.

“Achilia mbali kushindwa kutekeleza ahadi nyingi alizoahidi kwa jimbo lake kabla halijagawanywa, Jerry hakuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa chama katika jimbo la Ukonga,” ameongeza.

Akiwa Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Jerry alilalamikiwa na wadau wa habari kwa kutoonyesha ushirikiano nao kila walipomhitaji.

Novemba 7, 2024, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alieleza kutoridhishwa na kitendo cha Silaa, kukosa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Nane wa jukwaa hilo uliofanyika Dar es Salaam.

"Tukiwa kama Wahariri, hatufurahishwi na mwenendo wa Waziri Silaa. Amealikwa kwenye Mkutano wa PST, hakufika; amealikwa kwenye Tuzo za Waandishi wa Habari, hakuhudhuria; amealikwa Mbeya kwenye tukio la Wadau wa Habari, hakuwapo; na sasa Mkutano Mkuu wa TEF pia hajaja. Hii inaashiria kwamba Waziri hana nia ya kushirikiana na Wadau wa tasnia ya habari."

Makundi ya Urais

Kada mwingine aliyeomba kutotajwa, alisema pia Jerry alijikuta kwenye wimbi la mawaziri walioonekana kupishana na kundi la Rais Samia Suluhu Hassan.

“Unajua ndani ya CCM kuna makundi ya Urais na makundi hayo tayari yameshaanza kujipanga kuelekea 2030, sasa Mama (Rais Samia) aliwashtukia ndio maana wengi waliachwa kwenye kura za maoni na wengine hata waliposhinda ubunge hawakurudishwa kwenye Baraza la Mawaziri.”

Itakumbukwa, wakati Rais Samia akizungumza na wazee wa Dar es Salaam Desemba 2, 2025, alisema; “Nataka nizungumze na watoto wangu, vijana wangu wanaoangalia mbele 2030, safari hiyo isiende kutuvurugia nchi yetu. Nilizungumza na mawaziri wangu nikawaambia nawaangalia mmoja mmoja, una interest na huko kaa nje kafanye huko, usifanye ukiwa ndani ya safari yangu.”

Miongoni mwa makada wanaotajwa kuusaka Urais ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, akiungwa mkono na vigogo kadhaa ndani ya chama hicho.

Makamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alitemwa kwenye uwaziri tangu Julai 19, 2025 na hata kwenye mchujo wa kura za maoni za CCM katika Jimbo la Bumbuli, Makamba alienguliwa.

Makamba alikanusha madai ya mbio za Urais alipoulizwa na Waandishi wa Habari waliopiga kambi ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutaka kupata maoni yake baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, kilichoketi Julai 28, 2025 kutomteua kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge ndani ya CCM Jimboni kwake Bumbuli, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Alisema haamini kwamba kikao kikubwa na cha heshima kama cha Kamati Kuu kinaweza kufanya maamuzi ya uteuzi wa ubunge kutokana na mambo mengine yanayokuja huko mbeleni.

“Inawezekana hata Jerry alionekana kuwa na vinasaba vya makundi ya Urais ndio ikawa chanzo cha anguko lake. Kwa sababu hata ukiangalia uchaguzi huu haukuwa mgumu kwa CCM kusema kwamba angeshindwa na wapinzani wake,” alisema kada huyo.
 
Jerry silaa ni group ya akina marope. Wana circle yao hawa vijana wa ccm. Ni kweli walipishana na kundi la uraisi jingine.

Behaviour attitude na ego alizonazo Jerry Silaa kama una akili za kiswahili ni vigumu sana kuiva nae anafanana sana na Makamba jr usipowaelewa utawachukia ila ni watu wazuri tu sema wana uvulana kwa lugha ya magomeni ukisikia mtu mvulana kaa nae mbali.

Hii ya kwadharau wana ccm ukonga inasikika sikika.
 
Apumzike binamu ,karma is real ,kama uko hapa jerry binamu jua sikuwahi kukusamehe na karma naiomba iendelee kukutafuna ,napata habari kuwa sasa umerudi bar natamani usiishie kurudi bar ila urudi kule vikindu kwa Jose mbavu ili uelewe dunia duara bwana mdogo .

Umemuona Shingo huko ? Muone anavyozidi kukata mbuga ,kingereza kimegoma ila karma imembeba huyoo kwenda kutuwakilisha nduguze tuseme nini sasa kama sio karma njema.
 
Back
Top Bottom