Kama kuna suala ambalo linakera pia ni uchafuzi wa mazingira. Sio kwamba huwa ni kero tu, lakini uchafu huleta magonjwa mbali mbali na hatimae vifo ambavyo mara nyingi ni vya kujitakia. Na mara nyingi itokeapo hivi..msemo wa Ni mapenzi ya Mungu hutumika. Mimi sidhani ni sahihi wakati Mungu alitupa akili na vipawa mbali mbali ili tuishi maisha bora. Na ni Mungu wa Upendo na Rehema, sio wa kuangamiza.
Nina pendekezo, kwa nini kampeni kabambe isianzishwe ili kuweka nchi katika hali ya usafi, tukianzia vitongojini, wilayani hatimae mijini.
Ninachopendekeza ni vyombo vya habari i.e "Radio, Magazeti na Television vitumike katika kuutangazia UMMA katika kudumisha usafi wa mazingira.
Mfano kama ni Radio kila siku, zijitolee kutoa matangazo ya bure kwa dakika moja tu, na iwe angalau mara tano kwa siku. Vitoe ujumbe unaoeleweka mfano USITUPE TAKA OVYO, UTAOKOA MAISHA YA KWAKO, BABA, MAMA AMA ndugu yako yoyote au ujumbe wowote ule utakaomgusa atakayesikia. Na magazeti na television vivyo2. Ninaamini hili likitenda ndani ya mwaka mzima tutaona mabadiliko sana katika mazingira tunayoishi. Tena sasa hivi mikoa mingi ina Radio stesheni, hii itatia msukumo sana ks at least ujumbe utagusa sehemu nyingi.
Ila Kampeni hizi zinatakiwa ziambatane na vitendea kazi, I mean mapipa ya taka kuwa sehemu mbali2. Viwanda vinavyotengeneza vyombo vya plastic, kwa nini visitengeneze yale mapipa ya taka ya plastic kama yanatengeneza basi upatikanaji wake uwe rahisi na bei rahisi kama ndoo au beseni unapozikuta katika maduka mengi. Watengeneze pia mifuko mikubwa ya plastic inayopatikana kwa urahisi kama vile ipatikanavyo mifuko midogo. Sidhani kama upatikanaji wa haya mapipa ukiwa rahisi, mtu atathubutu kuiba. Kampeni ikishaanza ina maana kutakuwa na mapipa ya taka sehemu nyingi, serikali then iweke mikakati aidha za kuongeza tender za sekta binafsi kuhakikisha takataka zinachukuliwa mara kwa mara na kwenda kutupwa dampo.
Hali ilivyo sasa INAKERA, mfano barabara ya Ali Hassan Mwinyi utakuta wakina mama wako busy wanafagia barabara. Lakini ks watu hawana hulka ya usafi , mara nyingi nimeshahudia niko nyuma ya gari tena yenye nakshi..haitachukua dakika 2 utaona chupa ya maji n.k imerushwa nje ya dirisha. Daladala ndio kabisa usiseme, upande huu viplastice vya maji vinarushwa, the other side mifuko ya plastic n.k. Hivi ni kwa nini mtu asiuhifadhi uchafu wako uje utupe kwenye pipa la taka unapofikia mwisho wa safari yako???. Halafu utastaajabia mtu huyu huyu akipita sehemu yenye rundo la uchafu, utamsikia mhhh!!! Aisee mji mchafu hadi unatia kinyaa. Amejisahau kuwa yeye kurusha kitu nje ya dirisha ni kuanzisha mrundikano wa uchafu usio wa lazima. Yeye atatupa, mwingine atatupa baada ya wiki mtaa hauelezeki..takataka kila sehemu, na harufu juu..Sasa hapo kweli tunategemea kuokoa afya zetu???. Sasa sio mitaa yote husafishwa kama Ali hassan Mwinyi. Mitaani uchafu unatupwa tu, hatimae mifereji yote inajaa uchafu..Ije mvua sasa..ndio balaa ..mifereji yote imeziba. Halafu tunaanza kulaumu, kumbe source ni ile mimi na wewe kutupa chupa ya maji na mfuko wa plastic n.k. Je kwa namna hii tutapona
???
Maoni binafsi, wahusika kama mnasoma humu please serikali ilisisitize hili kwa sababu ikifanikiwa kubadilisha MINDSET ya mtu ya kutotupa uchafu ovyo
mabadiliko yatakuwa makubwa sana. Hatuna miundo mbinu wala settlements za kuvutia sana basi tujitahidi tuwe na mazingira safi.
Mimi hainiingii akilini, mfano jijini DAR kuna mipango ya kuweka mabasi yaendayo kwa kasi, au uporomoshaji wa vikwangua anga wakati sanitation ni mbovu
.Ukweli badala ya kupendeza mji utaonekana ni CHAOS.
Kwa kumalizia, badala ya kukazana kuwapa kampuni binafsi tenda za kusafisha jiji, mkazo utiliwe pia katika kubadilisha MINDSET za watu ili waweze kuwa na hulka ya usafi, na jinsi ya kufanya hivyo dawa yake ni KAMPENI TU likewise kampeni za utumiaji Condom. Au sivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Samahani its a long article, lakini in short mimi binafsi "UCHAFU HUNIKERA SANA" na madhara yake ni mabaya wakati solution za kucontrol uchafu zipo nyingi....