Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,893
- 11,376
FM,
Lete solutions zako za mjini sasa, maana kulalamika tumesikia, na tatizo liko pale pale. Unayeona kuna solutions za vijijini na zile za mjini, basi tuletee za mjini.
Watu wanaendelea kufa kwa magonjwa yatokanayo na uchafu, kwanini tusitafute solution?
Wakipewa Wazungu hayo maeneo, watapata solution, huku Watanzania bado tunasubiri serikali ije utuokoe. Kama mnaweza itoeni hiyo serikali, lakini
kama hamna uwezo wa kuitoa serikali mtafanya nini? Mtaendelea kuzungukwa na uchafu?
Tukitazama hili la uchafu, hata wananchi wa Manzese wafanye nini bila kuwa na chombo kitakachoweza kuukusanya huo uchafu na kwenda kuutupa mahali panapostahili, juhudi zao zitakuwa bure. Mfano angalia vile vitrela vya kuchukua uchafu vinavyo overflow. In desperation wananchi wamefikia hatua ya kuchoma bila kuangalia madhara ya moshi ulio na sumu! Wengine wanawalipa watoto wa mjini kuchukua na kwenda kutupa taka hizo sehemu wanazojua wao.
Hii ndiyo inayonipelekea kusema kuwa katika mazingira ya miji ni lazima utawala uwajibike kwa kuweka nyenzo na system za kushughulikia suala la uchafu. Wakishafanya hivyo, ndiyo waweke bye-laws zitakazomwadhibu yeyote ambaye atasababisha uchafu maana hatokuwa na sababu. Singapore unalipa faini kama unatupa Big G chini, kama hauflush public toilet kwa sababu mapipa na vyoo havikosi maji kwa hiyo hauna sababu ya kufanya vinginevyo. Sehemu nyingi Ulaya wenye mbwa wana wajibika kukusanya choo cha mbwa wao kwa sababu sehemu ya kukitupia kiko kila sehemu. Mtu anayeacha kinyesi cha mbwa wake bila kukikusanya anaadhibiwa!
Utamlaumu vipi mtu kujisaidia nyuma ya mti kama hamna huduma ya vyoo vya umma? Utamlaumu vipi mtu kutupa maganda ya ndizi chini kama hamna sehemu ya kutupia? Na zaidi ya haya, utawalaumu vipi wote hawa kama hauwaadhibu wakifanya hivyo wakati vyoo vipo na vipipa vipo?
Miji inahitaji utawala unaowajibika ili ifanye kazi. Hili sidhani kama tunaweza kukwepa.
Mimi natupia lawama viongozi. Nchi zote ambazo sasa hivi tunaona kuwa ni kioo cha usafi, hazikuwa siku zote hivi. Singapore ilikuwa bandari masikini na chafu kwa kila jinsi walipopata uhuru. Ni uongozi wao waliochukizwa na hali hiyo na kuweka sheria ambazo zilimwadhibu raia yeyote atakayeendekeza uchafu. Miji ya uingereza, ufaransa yote nayo ilikithiri kwa uchafu mpaka utawala ulipopitisha sheria ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa iliyokuwa kama tija wakati ule. Ni mlipuko wa mara kwa mara wa Cholera ndiko kuliwafanya wenzetu wapitishe sheria ambazo kwanza zililazimishe local authorities wajenge sewer systems na wakazi wote wa mjini kuunganisha kwenye hizo sewers! Wananchi walipinga sana wakiona kuwa ni utawala wa ubabe lakini utawala ulishinikiza mpaka hali ikakubalika. Bila uongozi ulioamka hamna kitakachofanyika.
Hali hii ya uchafu kukithiri mara nyingi ni mijini na sio vijijini. Vijijini kila mwenye nyumba anawajibika katika sehemu yake na hapo awali sehemu kubwa ya uchafu uliokuwa ukizalishwa ulikuwa ni bio-degradable. Hapa mjini hakuna mwenye mji na bila uongozi kuweka sehemu na taratibu za kukabiliana na hali hii hakuna ambacho mwananchi wa kawaida anachoweza kufanya. Kama hakuna taratibu za kukusanya taka, mwananchi aishie katikati ya mji ni vigumu kuchimba shimo la kutupia taka zake. Ziwekwe taratibu na kuhakikisha kuwa zinafuatwa. Bahati mbaya taratibu hizo zinafanywa dili kiasi cha kumuondolea mwananchi hamu ya kuzitumia!
Nchi hii ni muda mrefu sana hatujapata mtu wa kukosha nyoyo zetu. Labda miaka ya sabini waliyokuwepo walishuhudia idadi kubwa ya viongozi na mfumo wa kazi wa uwajibikaji.
Leo hii mimi naishi Mwenge ni kama nipo Peponi maana Serikali yangu haitambuwi mahala nilipo. Si kiongozi wa kitongoji, kijiji, kata, tarafa wala wilaya. Utaona karatasi ya Kata siku wakitaka kula pesa zetu kwa kigezo cha kupuliza dawa.
Je, katika mazingira ambayo viongozi ngazi ya kata hawawajibiki kwa wananchi ndani ya eneo lao ni kwa namna gani mwananchi atasimamia swala zima la usafi?
Sijafika ulaya lakini kichwa changu kinafanya kazi. Kama Baba mwenye Nyumba hatambui ongezeko la wageni kwenye nyumba yake ni namna ghani anakuwa kiongozi wa familia?
Wakati wa Mwalimu tulikuwa maskini kutokana na maliasili nyingi kuwa Iddle lakini hatukuwa na idadi kubwa ya viongozi uchwara.
Ni wakati wa mfumo wa chama ulikuwa uhami wala kuhamia sehemu bila Balozi wako kubariki. Ilikuwa ni kosa kumpokea mgeni pasipo kumtambulisha kwa balozi. Mitaa ilikuwa ni misafi maana sera ya kujitegemea ilitumika vizuri lakini leo hii serikali sijui ipo na inafanya nini.
Nchi yetu ndipo mahali wananchi wanatangulia mbele serikali nyuma yao. Tunavamia kwanza maeneo ya kuishi ndo serikali inakuja kupima na kubomoa. Tabata Dampo, ni mfano. Je, uchafu ule mwananchi alaumiwe vipi? Tambua sisi ni wanyama ni kwa kuwapa watu fulani dhamana ya kuelekeza fikra zao katika kuwasimamia wengine ndipo ubinadamu wetu unatofautiana na wanyama wengine.
Hakika Serikali inapaswa kubeba lawama imetuacha tuwe wanyama badala ya kuwa binadamu.
Mafanikio uliyoona miaka ya zamani yalikuwa ni yale ya serikali za mitaa alizoacha mkoloni. Kuanzia 1972 ni kichwa cha mwenda wazimu.
Kachimbe jalala....
uchafu ni suala personal, dont expect mtu anye nje then aexpect serikali ije izoe ma*vi yake !
Kama uchafu wa taka taka, watanzania saa nyingine tunakuwa nyuma katika usafi wenyewe, najua kwamba kuna magari ya manispaa na city ambayo hupitia taka katika maeneo fulani si chini ya mara 2 kwa wiki, lakini utakuta watu bado tu wanatupa taka ovyo !
Kwa mbongo mazoea yana tabu, hata ukiweka tank ya kunywa maji safi, yeye atataka tu maji ya bombani, ukileta magari ya taka yeye atatupa tu taka anapojua yeye, hata ukimjengea uwanja safi wa soka, basi watavunja tu viti ili mradi wakae chini, SABABU ? eti wamezoea kuangalia mechi wakiwa wamekaa chini. Angalieni watu walivyochafua vyoo siku ile kwenye mechi iliyochezwa katika wanja jipya ! Watu walihara balaaaaaaa, na wengine wakadiriki hata kupaka ukutani na wengine kuweka machata yao, we have a longggg way to go folks !
SASA NANI ALAUMIWE ??
uchafu ni suala personal, dont expect mtu anye nje then aexpect serikali ije izoe ma*vi yake !
Kama uchafu wa taka taka, watanzania saa nyingine tunakuwa nyuma katika usafi wenyewe, najua kwamba kuna magari ya manispaa na city ambayo hupitia taka katika maeneo fulani si chini ya mara 2 kwa wiki, lakini utakuta watu bado tu wanatupa taka ovyo !
Kwa mbongo mazoea yana tabu, hata ukiweka tank ya kunywa maji safi, yeye atataka tu maji ya bombani, ukileta magari ya taka yeye atatupa tu taka anapojua yeye, hata ukimjengea uwanja safi wa soka, basi watavunja tu viti ili mradi wakae chini, SABABU ? eti wamezoea kuangalia mechi wakiwa wamekaa chini. Angalieni watu walivyochafua vyoo siku ile kwenye mechi iliyochezwa katika wanja jipya ! Watu walihara balaaaaaaa, na wengine wakadiriki hata kupaka ukutani na wengine kuweka machata yao, we have a longggg way to go folks !
SASA NANI ALAUMIWE ??
Jamii ya watu waliozoea kuona uchafu, na uchafu huo kwao haunuki tena, yaani wameuzoea kiasi kwamba harufu yake hainusiki tena; basi jamii hiyo huwa imezoea uchafu.
Kuna wazo zuri ambalo sasa limewanufaisha wengi, lile ambalo katoa Mtanzania, kuwa kuna haya ya kuwatumia vijana wakao maskani kukusanya taka kwa kulipwa.Kuna ubaya gani wa kuanzisha magari taka ambayo yatasomba takataka zilizowekwa kwenye mifuko maalum angalau mara moja kwa wiki badala ya kuitupa uwani au upenuni.
So what happened? why regress and not progress? It seems somewhere after several years of self autonomy and our independence, we changed the direction on everything! Look at Production, Education, Cleanliness, Morals, Accountability, Efficiency, Motivation, following Law and Order etc.
We need to examine what happened and why it is affecting us to the point we are just cool with everything, the Que Sera Sera, Ndivyo tulivyo attitude!
I think it is time we sit down and not writing up new plans and policies but revisit everything we have done from the day Mkoloni left todate and do a thorough analysis that can provide constructive feedback to correct our ills and short comings.
If we fail to make effort to do that, we will never make any progress and our efforts will be similar to a dog trying to bite its own tail!
Kwa maoni yangu, tunaupungufu mkubwa wa watu wanaojua kukusanya na kutumia pesa kama resource za maendeleo. Ukiwa mwalimu usiwaangalie wanafunzi wako na kusema vijana hawa wameshiba sana basi wanaweza kusoma na kuzalisha chakula cha kujilisha. Na ukiwa kiongozi wa nchi, usifikiri kuwa watu watatoka kazini na baadaye wafanye kazi za kusafisha mitaa. Tunaishi mijini na miji yote imeendelea kwa kodi za watu. Na kama mji hauendelei basi kuna ulakini katika ukusanyi au matumizi ya kodi.
Usafi ni tabia, mtu mwenye tabia ya uchafu hawezi kuuchukia uchafu! Ndio maana tuna mafisadi!
kama upi? suala hapa ni taka...Kama ndio hivyo basi tuna watu wengi sana wenye tabia hii ya uchafu maana huko uraiani kuna uachafu uliokithiri
kama upi? suala hapa ni taka...
Wa kila aina...
unajua kuwa hata mdomo uweza kuwa mchafu, ingawa sio taka taka?..