mkuu hardware ni zile zile ikiwa ufs 2.0 imetumika awe katumia sony, iwe samsung iwe tecno iwe huawei speed ni ile ile hivyo huna haja ya kutumia emmc ya tecno au ufs ya huawei kujua actual speed. same kwa ram ni mule mule na ukumbuke hapa mtengenezaji ni mmoja, ukikuta ufs kwenye one plus ujue katengeneza samsung na hata mfano 2019 huko ukakuta Tecno ina ufs ujue itatoka samsung.
hivyo kufanya comparison ya kitaalamu huna haja ya kuwa exactly device fulani kujua.
vitu kama ram, cpu, gpu etc ni rahisi kuvifahamu sababu unaangalia soc,
mfano mtu akisema simu yangu inatumia mediatek helio x20 mimi moja kwa moja nafahamu itakuwa na
-core 10 za cpu mbili zikiwa kubwa na 8 ndogo
-ram single chanell ddr3
-gpu ya mali T880 mp4
-4G
-bluetooth 4 etc
najuaje? ni mediatek wenyewe wakitangaza soc zao wanataja na specs zake, hapo manufacture hawezi badili kitu,
siku Tecno akitangaza simu ina helio x20 automatic nafahamu specs zake zinazohusiana na hio soc,
soc ya ddr3 ukaeka ddr4, au soc haikubali 4G ukaieka, unless ufanye tafiti za kufa mtu zitakazokuchukua miaka mingi. kwa ulimwengu huu nimeona Nokia na Motorola tu wakiwa excluded kwenye hizi rules.
so mimi nahitaji kuisoma kiundani soc(system on chip) ili niweze fahamu simu nyingi kwa mpigo, unakuta soc moja inatumiwa na simu tofauti tofauti 50, huwezi ukakaa chini ukakariri simu zote 50.
hizo camera za Tecno hazitolewi specs na ukitoa vi blog vyetu uchwara site kubwa zote hawaripoti tecno hivyo ni almost impossible kujua.
na ili nijue manual inabidi nizishike Tecno moja moja nianze kuziangalia na pengine inaweza hitaji hata root access kitu ambacho ni karibia hakiwezekani.
Comparison niliyotaka ufanye, haiwezekani kwa sababu hujui specs za tecno, na sababu ya msingi uliyotoa hawatangazi, na labda haiwezekani kufahamu (kwa mjibu wako). Sasa hapakuwa na haja ya kuanza kusema camera ya sumsung ni bora kuliko ya tecno au kufanya comparison nyingine yoyote kwa kuhisi, wakati specs za upande mwingine huzijui.
Halafu unafahamu kamwe, unapofanya ulinganifu, lazima vitu unavyovilinganisha viwe angalau vinakaribiana, mfano huwezi kulinganisha toleo la kwanza kabisa la iphone na sumsung galaxy s8.
Nashukuru kuwa umegundua habari nyingi ni za kishabiki, kwenye blogs na websites, wafanya tech reviews waliowengi wanalipwa, atafanya tech review ya sumsung au iphone au tecno ili kuvuta watu, yaani kazi yao ni kufanya simu ipendwe na iuze, kwa maana hiyo kuna bias kubwa sana.
Na usitegemee pia mtu humu akasifia simu ambayo haitumii (sio wote, bali walio wengi), lazima watavutia upande wao, achilia mbali watu kutokuwa na skills za kuelezea au kuelewa kitu) - unafahamu vizuri ligi zenu, sumsung and iphone fan boys.
Kampuni ya kibiashara inaweza kukuambia explicitly technology inayotumia, jinsi wanavyofanya design, na process zingine zote? Yes/No, kwa nini?
Maswali ya ziada:
1. Sumsung zimeanza kutengenezwa lini na tecno zimeanza lini? Nani anayekua haraka kibiashara na kiteknolojia (naongelea rate)?
2. Je, unafahamu kuwa kwenye ushindani, kuna makampuni ambayo hutumia watu kususia na kuzisema vibaya bidhaa za kampuni zingine ili kuua soko?
3. WhatsApp ina watumiaji wengi sana kuliko Telegram, at least kwa Tanzania labda na Africa, possibly duniani kote, je, ina maana WhatsApp ni bora zaidi kuliko Telegram?
4. Kwa nini watumiaji wa Snapchat Africa ni wachache zaidi kuliko watumiaji wa mabara mengine? Ndio tuseme yenyewe ni bora zaidi kuliko WhatsApp, Telegram, etc. kwa sababu labda inatumiwa Ulaya na Marekani?
5. Je, ni kitu gani kinachofanya product fulani iwe popular? Je, umeshawahi kujionea product ambayo wewe unadhani kuwa ilikuwa ni bora, lakini kwenye mauzo na popularity ikawa chini ukilinganisha na products zingine ambazo ni inferior?
7. Je, unajua kuwa unaweza kuwa unatumia kitu miaka nenda na usikijue undani wake? Yes/No? Kuthibitisha hili, Je, Jamiiforums imetengenezwa kwa kutumia framework gani?