Ninachokiona hapa ni kujaribu kuorodhesha properties za attributes mbalimbali, tena ukiwa unaelezea za sumsung zaidi. Kusema maarufu, ina speed sana, inatumia storage aina ya emmc, etc., haviwezi kuwa calculated quantitative na qualitative measure. Unaelezea kuhusu sensor, megapixels, etc., kwa kusema kwa mfano sumsung ina sensor nzuri, au megapixel nyingi lakini sensor ndogo picha zitakuwa noisy or whatever. Maneno kama ndogo, nzuri, speed sana, ni maarufu, quality ndogo, kutaja spec bila kuielezea maana yake ni nini, na inachangia kwenye quality au performance ya simu kivipi hayawezi kuwa ni uchambuzi linganifu. Halafu unataja sensor kirahisi tu, na uhusino wake na megapixel na resolution ya picha. Hayo ni mambo ya signal processing na optics, yakiambatana na calculations. Unapoongelea picha unaongelea 3D object, kuna super calculations mpaka unapokuja kuiona image rendered na camera yako. Halafu kingine, mambo hayapo kirahisi kama unavyoyachukulia. Tatizo la humu hamtumii utaalamu, au huwa hamkiri kuwa sielewi vizuri au sielewi kabisa kitu fulani kinafanyaje kazi. Halafu kila kitu kina strength na weakness yake, simu sio exceptional.
Eleza technically, sio kulist technical terms, what do I mean? Badala ya kuandika 720p@240fps, autofocus, 1.4 GHz, 5 MP, etc., eleza 720p ni nini, 240fps ni nini, 1 GHz maana yake nini, MP ni nini, and then inamaanisha nini tunaposema 720p@240fps, 1.5 GHz, 12 MP, etc., huku ukilinganisha specs za sumsung na tecno, kwa kila attribute, then sum up kwa kuonyesha one is better than another.
Unaweza kufanya uchambuzi wa ubora wa kamera tu kama alivyoomba mwuuliza swali. Unapoongelea camera unaongelea mambo ya optics na signal processing. Waambie watu nini maana ya 12 MP, sensor, ni bora kwa sababu gani, kwa sababu ya material yake? Yapi? architecture yake? Ipi? Kwa sababu ya modeling (maths behind it), kwa sababu ya lens yake? Aina gani? Kwa sababu ya sampling rate? Kwa sababu ya resolution yake? etc., na kwa nini hivyo vyote ni bora kwa simu moja kuliko nyingine. Unapoongelea resolution na sensor, unaongelea light signals/photons na uwezo wa lens/camera kuona na kucapture signal, kwa quality gani (arseconds/pixels), na kwa umbali gani.
Ongea kama mtaalamu. Ujue huwezi kuulizwa swali, then dakika 2 tu tayari umepata majibu, serious? Wataalamu wanainvest muda, skills, energy, na resources zingine kufanya research, sio kitu chepesi kama unavyochukulia.