Tetesi: Ubalozi wa Tanzania Uturuki unashirikiana na jeshi la polisi la Uturuki kuwadeport Watanzania

Mtu wanakudeport wewe kama wewe na nguo ulizovaa tu vitu vyako vyote vinaachwa kama una biashara zako unaziacha. Ata kwa hili pia ubalozi hauna mamlaka ya kumtetea raia wake angalau achukue vitu vyake?
Sio wewe tu. Kuna watu Japan,UK na ata South Africa -Ukiwa illegal Aliens.Ajalishi wewe ni nani.. unarudishwa Kwenu . Why wewe unataka ufanyiwe hisani usizostaili?? Kinachotakiwa ni kufuata sheria za nchi husika akuna mbadala wa hilo.
 
Hapo ndo nawapendea wanaijeria mtu wao akidipotiwa nakufikishwa Nigeria wanamkataa wanasema siyo raia wao inabidi warudi naye.
Wenye akili hao
Sasa hawa wajinga unazamia nchi ya watu halafu unakaa na passport ya nini sasa
Passport unavuka nayo ukifika kama umeingia illegal unakaa nayo ya nini sasa
Tatizo hawajui maana ya kuzamia
 
Wewe msenge, mimi najaza kitabu cha 4 saivi cha passport na bado unaniita mshamba, huna cha kunifundisha kwenye maswala ya travelling. Tatizo lenu wabongo mnaoishi nchi za watu bila karatasi huwa mna expect privileges ambazo ni almost impossible kuzipata in this capitalism economy. Ndo maana nawa support immigration wanavyowanyima boarding pass JKNIA.
Mkuu matusi ya nini sidhani kama yupo msafiri hapo kitabu unajaza cha Nne unaenda Kenya na Zimbabwe kama unapanda ndege ni mihuri miwili tu kujaza kitabu inachukua muda mrefu...mimi nipo Tanzania baada ya kutafuta nje na kurudi kuwekeza nyumbani punguza ushamba basi mazee wa kutukana hovyo kisa una passport wenzio tulianza kuchukua zile za kubandua picha mpaka leo sijui idadi ya Passport nilizotumia maana zipo nyingi hata Nchi nilizosafiri nimeacha chache sana kwenye Dunia hii na bado naendelea na safari za matembezi tu sasa...
 
Sio wewe tu. Kuna watu Japan,UK na ata South Africa -Ukiwa illegal Aliens.Ajalishi wewe ni nani.. unarudishwa Kwenu . Why wewe unataka ufanyiwe hisani usizostaili?? Kinachotakiwa ni kufuata sheria za nchi husika akuna mbadala wa hilo.
SA wanawaweka John vorster pale wakichangishwa rand 250 wanatoka ukiona mtu karudishwa kutoka SA jua hakuna namna maana wanachukua rushwa hao balaa ila kwa wale waliopewa adhabu ya miaka mitano ukikamatwa ni jela au unarudishwa hakuna hela wanachukua hapo..
 
Mtu wanakudeport wewe kama wewe na nguo ulizovaa tu vitu vyako vyote vinaachwa kama una biashara zako unaziacha. Ata kwa hili pia ubalozi hauna mamlaka ya kumtetea raia wake angalau achukue vitu vyake?
Hapo inabidi wafanye namna bora ya kuwasaidia. Maana umekua kama umefanya kazi bure.

Lakini pia balozi yetu haiwasaidii waTz kupata VISA mpya kabla uliyoingia nayo haijaisha? Au mkishaingia mnajilipua ? Mna umoja huko? Maana mkiwa na umoja ni rahisi kupeana mbinu.
 
SA wanawaweka John vorster pale wakichangishwa rand 250 wanatoka ukiona mtu karudishwa kutoka SA jua hakuna namna maana wanachukua rushwa hao balaa ila kwa wale waliopewa adhabu ya miaka mitano ukikamatwa ni jela au unarudishwa hakuna hela wanachukua hapo..
Watanzania na wa SA kiasi kuna huruma na kumbuka kuwa Askari wengi wa SA waliishi na kusoma TZ so ni kama Ndugu zetu. Japo Usela umetuzidi sana sisi Wabongo ndani ya Sauz Africa. Ata Sauz ukikamatwa na kupelekwa Lindera auna chance ya kurudi na chochote kile ulichokuwa nacho Kwako
 
tuliza kishimo we bwege. Kutetea raia wake toka lini ikawa msaada? Kama hili unaita msaada ni nini kazi ya ubalozi kwa raia zake
Tuwe wakweli kwenye suala hili, Ubalozi wa nchi yoyote ile hapa duniani una mipaka ktk kuwasaidia raia zake wanapokuwa huko nje ya nchi zao wanazoziwakilisha, hususani kuhusiana na masuala ya makosa ya jinai. Tambua Ubalozi wa nchi yako una mipaka ktk kukusaidia kwenye suala kama hili.
Kitu cha muhimu kuzingatia ni wewe mwenyewe Mhamiaji kwanza kutii Sheria za nchi husika, sambamba na kufuatilia kwa umakini kuhusu suala lako la uhalali wa kuendelea kuishi huko ktk nchi ya ugenini. Hakikisha unafuatilia vibali vyako vya kuishi huko mapema ktk mamlaka zinazohusika ktk nchi husika. Endapo kama umekwama kabla muda wako wa kuishi huko haujaisha, basi uwe na muda wa kutafuta Plan "B", ikiwamo na kupata muda wa kuokoa mapema mali zako unazomiliki huko ugenini kabla hata janga la deportation halijakukumba.
Tatizo lililopo ni kwamba wa-Tanzania wengi sana wamezoea maisha ya 'magumashi', janja-janja, uholela na kutaka Sana mambo ya magendo au kufanikisha mambo yao kwa njia za mkato, kama ilivyo kwa hapa nyumbani Tanzania, wenzetu huko nje ya nchi hawapendi kabisa maisha ya hovyo hovyo namna hiyo. Hapa Tanzania CCM ndiyo inawalea kwenye maisha ya hovyo namna hiyo, lakini kumbukeni kwamba kwenye nchi hizo huko ugenini hakuna CCM.
 
Turkye nayo ni nchi ya kuzamia?bora mtimuliwe kwa kweli mnafanyaga matendo mabaya sana hadi aibu.
 
Balozi kazi yake ni kutetea raia zake lakni ubalozi wetu wa Tanzania uliopo Uturuki haufanyi kazi hii badala yake umekuwa ukishirikiana na jeshi la polisi la Uturuki kuwaondosha watanzania nchini umo na kuwarudisha Tanzania.

Mchezo upo hivi Mtanzania akikamatwa na polisi kama hana makaratasi anapelekwa kituoni akifika kituoni polisi wanapiga simu ubalozini wanaongea nao kituruki sijui wanaongeaga nini baadae wanakupa sim unaongea na ubarozi.

Ukiongea na ubalozi unakuchombeza unakufariji mtu unafarijika unazani ukimaliza kuongea na ubalozi polisi watakutoa kumbe ndo imekula kwako hiyo kesho unatumiwa passport unarudishwa Tanzania utake usitake.

Ubalozi aukutetei ndo kwanza wanashirikiana na polisi. Vijana wengi wanaoishi Uturuki ambao awana makaratasi awatoki nje wanaogopa kukamatwa na polisi.

Ukikamatwa ujue ndiyo safari ya Tanzania imewadia na ubarozi aukutetei. Kama ubalozi unashindwa kutetea raia zake kazi ya ubarozi inakua nini?
Si useme wewe ni Mkenya
 
Hapo inabidi wafanye namna bora ya kuwasaidia. Maana umekua kama umefanya kazi bure.

Lakini pia balozi yetu haiwasaidii waTz kupata VISA mpya kabla uliyoingia nayo haijaisha? Au mkishaingia mnajilipua ? Mna umoja huko? Maana mkiwa na umoja ni rahisi kupeana mbinu.
Umoja uliopo unashirikiana na ubalozi kwaiyo usitehemee kupata msada kutoka kwao
 
Wenye akili hao
Sasa hawa wajinga unazamia nchi ya watu halafu unakaa na passport ya nini sasa
Passport unavuka nayo ukifika kama umeingia illegal unakaa nayo ya nini sasa
Tatizo hawajui maana ya kuzamia
Nafikiri unajipotosha wewe mwenyewe binafsi na pia unapotosha umma hapa. Siku hizi kuna Sayansi na Teknolojia kubwa sana ktk kuwatambua watu, hata kama hautakuwa na Passport au kitambulisho chochote kile ukiwa ugenini unaweza kutambuliwa kuwa wewe ni nani na umetokea wapi hasa /nchi gani. Kwa hiyo kuficha Passport siyo njia sahihi ya kutokutambulika huko nje ya nchi.
 
Turkye nayo ni nchi ya kuzamia?bora mtimuliwe kwa kweli mnafanyaga matendo mabaya sana hadi aibu.
Ni kweli kabisa unachosema, wa-Tanzania wengi wawapo huko nje ya nchi huwa wanalitangaza jina la nchi vibaya, wanaichafua sana taswira ya nchi ya Tanzania kwa kujihusisha na vitendo viovu vya uhalifu na uvunjifu wa Sheria za wenyewe. Hali hii ndiyo imesababisha watu Wema kupata ugumu kwenye masuala ya ku-renew viza ktk nchi nyingi hapa duniani.
Waovu wachache Ndio wanaosababisha ugumu wa maisha kwa watu wengine wengi.
 
Nafikiri unajipotosha wewe mwenyewe binafsi na pia unapotosha umma hapa. Siku hizi kuna Sayansi na Teknolojia kubwa sana ktk kuwatambua watu, hata kama hautakuwa na Passport au kitambulisho chochote kile ukiwa ugenini unaweza kutambuliwa kuwa wewe ni nani na umetokea wapi hasa /nchi gani. Kwa hiyo kuficha Passport siyo njia sahihi ya kutokutambulika huko nje ya nchi.
Sasa nijipotoshe kivipi
Kwa taarifa yako nilifanya kazi sana ya ukalimani nchi ya wazungu na wengi wa waafrika walikuwa wanajilipua kwa kutaja nchi ambazo zina vita na wanapokelewa
Kama wabongo mpaka wengine walijiandikisha kama warundi au wacongo na hata wasomali

Walikuja kukamatwa wengi baada ya kuchomana kwa ujinga wao na magomvi ya kijinga na wengi walirudishwa

Kama uko nje ya nchi na umeishi Ulaya au States au Canada na Australia utanielewa lakini kama hujavuka border tutaboshana bure tu hapa
 
Hiyo ilikuwa zamani kabla Sayansi na Teknolojia haijakuwa, lakini siyo siku hizi. Nchi nyingi kwa sasa zinatumia sana Teknolojia ktk kuwatambua watu. Labda endapo kama haujawahi kabisa kujisajiri katika mifumo ya nchi yoyote ile hapa duniani ya Utambuzi, Utoaji Hati za kusafiria, au haujawahi kabisa kuomba na/au kupata Viza ya kuingia ktk nchi yoyote ile.
Mathalani, kwa sasa hivi nchi nyingi zinatunza Taarifa za wasafiri wote (international migrants) kwenye mfumo wa 'Visa Information Systems (VISAIS)', taarifa hizo kwa sasa zinatunzwa permanently in perpetuity, tofauti na miaka ya nyuma ambayo taarifa hizo zilikuwa zinatunzwa kwa muda wa miaka mitano tu, baada ya hapo zilikuwa zinafutika na kutoweka kutoka kwenye mfumo.
 
Back
Top Bottom