Ubaguzi: Madiwani Zanzibar kulipwa mishahara huku wa Tanzania bara wakitumika kwa posho ya vikao

Muuza Kangala

Senior Member
Jul 21, 2021
192
1,872
Nchi ni moja na rais ni mmoja kwa nini madiwani wa Zanzibar walipwe mishahara huku hawa wa bara hawalipwi? Huu ni ubaguzi usiofaa.

Bajeti Zanzibar Sh2.59 trilioni.

=======

Madiwani Z’bar kulipwa mishahara​

Jesse Mikofu

Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) jana imewasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2022/23 ya Sh2.5 trilioni huku ikitarajia kuanza kuwalipa mishahara madiwani wadi ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo kwa Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya alisema kati ya Sh2.5 wanazotarajia kukusanya, mapato ya ndani ni Sh1.3 bilioni, misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo ni Sh687.95 bilioni, mikopo ya ndani na nje kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ni Sh515.0 bilioni.

Pia aliomba kuidhinishwa Sh17.60 bilioni kukusanywa na Serikali za Mitaa.

Kwa upande wa matumizi alisema kati ya hizo, Sh1,220.51 bilioni zimeelekezwa kwa ajili ya kazi za kawaida, Sh1,352.19 bilioni zimeelekezwa kwenye kutekeleza Mpango wa Maendeleo na Sh17.60 bilioni zinakwenda kutumika katika Serikali za Mitaa.

Waziri Mkuya alisema SMZ imepanga kuimarisha masilahi ya watumishi wa umma na imetenga Sh628.68 bilioni sawa na asilimia 24 ya bajeti kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi, ikiwemo na marekebisho mapya ya mishahara kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Alisema pia Serikali imedhamiria kuanzisha fao la kupoteza ajira ambalo litasimamiwa chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

Dk Mkuya alisema hadi kufikia Machi 2022, Deni la Taifa limefikia Sh1.2 trilioni na linalodhaminiwa na Serikali ya Mapinduzi ni Sh310.7 bilioni.

Alisema deni hilo limeongezeka kwa Sh76.3 bilioni, sawa na ongezeko la asilimia 33 ikilinganishwa na deni lililoripotiwa Machi 2021 ambalo lilikuwa Sh234.4 bilioni.

Waziri Mkuya alisema Serikali inapendekeza kufuta kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mashine za kielektroniki na karatasi za kutolea risiti wakati wa uingizaji na usambazaji (uuzaji) kwa mawakala wa uingizaji na usambazaji walioteuliwa na Serikali.

Alibainisha kuwa Serikali inapendekeza kufuta kodi ya VAT wakati Benki za Kiislamu ambazo hutozwa mara mbili wakati benki inaponunua bidhaa na wakati wa kuwasilisha bidhaa hiyo kwa wateja wake.

Serikali inapendekeza kuanza kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa huduma zinazotolewa mtandaoni ambapo jumla ya Sh6.0 bilioni zinatarajiwa kukusanywa kutokana na hatua hii.

Dk Saada alisema kwa mfanyabiashara ambaye mauzo yake hayazidi Sh5.0 milioni hatapaswa kulipia, mauzo baina kati ya Sh5 milioni hadi Sh7.5 milioni atatozwa Sh100,000, mauzo yasiyozidi Sh7.50 milioni hadi Sh10.0 milioni atatozwa Sh200,000.

Na mauzo kati ya Sh10.0 milioni hadi Sh12.50 milioni atatozwa Sh 300,000 na mauzo kati ya Sh12.50 milioni hadi Sh15 milioni atatozwa Sh400,000.

Kodi kampuni usafirishaji

Alisema kwa muda mrefu sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar imekuwa haikusanyi kodi ya mapato ya asilimia tano kwa kampuni za kigeni za usafirishaji wa abiria na mizigo, hivyo mwaka wa fedha ujao 2022/23 TRA–Zanzibar itaanza rasmi kukusanya kodi hiyo kupitia wakala wa Shirika la Meli na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar. Hatua hii inatarajiwa kukusanya jumla ya Sh1.3 bilioni.

Mwananchi
 
Others

JF-Expert Member
Dec 28, 2013
1,108
2,298
Kwa upande wa matumizi alisema kati ya hizo, Sh1,220.51 bilioni zimeelekezwa kwa ajili ya kazi za kawaida, Sh1,352.19 bilioni zimeelekezwa kwenye kutekeleza Mpango wa Maendeleo na Sh17.60 bilioni zinakwenda kutumika katika Serikali za Mitaa.
Sh1,220.51 bilioni = Trilioni 1.51
Sh1,352.19 bilioni = Trilioni 1.19

Nna wasiwasi na Mwandishi wa Mwananchi, huyo Waziri wa Fedha au Viongozi waliohusika kuandika hayo Mapendekezo ya Bajeti.

Tabia za Bunge la JMT za kuogopa kutaja kiasi cha Fedha kama kilivyo ndiyo na wao wamezichukua ili kuwapumbaza Wananchi na Wadau.

Katika hali ya kawaida unawezaje kutamka au kuandika Bilioni 1,000?, Una Agenda gani!??
 
NGABAGILA

Senior Member
May 8, 2020
107
113
Nchi ni moja na rais ni mmoja kwa nini madiwani wa Zanzibar walipwe mishahara huku hawa wa bara hawalipwi? Huu ni ubaguzi usiofaa.

Bajeti Zanzibar Sh2.59 trilioni.
Ulichotakiwa kufanya ni kujenga hoja kuwa SERIKALI YA MUUNGANO iangalie uwezekano wa kuwalipa MADIWANI wa bara kuliko kumshushia mtu lawama kisa ni Rais mpumzisheni mama wa watu afanye kazi binadamu nyie viumbe wagumu Sana duh 🙈
 
jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
10,095
18,083
Mbona madiwani wa Tanganyika wanalipwa laki 3 kwa mwezi..bado posho za vikao vya halmashauri..acha ramli chonganishi tafuta taarifa sahihi.

#MaendeleoHayanaChama
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,962
3,173
Ulichotakiwa kufanya ni kujenga hoja kuwa SERIKALI YA MUUNGANO iangalie uwezekano wa kuwalipa MADIWANI wa bara kuliko kumshushia mtu lawama kisa ni Rais mpumzisheni mama wa watu afanye kazi binadamu nyie viumbe wagumu Sana duh 🙈
Anatwishwa hata mizigo ya jirani, ha haaaa!
 
MoroOne

Member
Dec 12, 2018
75
162
Tanzania bara madiwani wanalipwa mshahara wa laki 3, kwa mwezi tangu 2015 kipindi Mh. Kikwete anaondoka madarakani. Huko nyumba walikua hawalipwi. Pia wanna kuibua mgongo cha milioni kama 16 baada ya miaka 5, na posho ya mwezi kutoka kwa kila Halimashauri ya laki 1. Chunguza kabla ya kuandika ( posho za vikao zipo palepale.
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
10,876
24,095
Ulichotakiwa kufanya ni kujenga hoja kuwa SERIKALI YA MUUNGANO iangalie uwezekano wa kuwalipa MADIWANI wa bara kuliko kumshushia mtu lawama kisa ni Rais mpumzisheni mama wa watu afanye kazi binadamu nyie viumbe wagumu Sana duh
Hoja imeletwa na muuza kangala!! Huenda hata hajui ni wizara gani siyo za muungano.
 
Michael mbano

JF-Expert Member
Apr 4, 2022
820
560
Nchi ni moja na rais ni mmoja kwa nini madiwani wa Zanzibar walipwe mishahara huku hawa wa bara hawalipwi? Huu ni ubaguzi usiofaa.

Bajeti Zanzibar Sh2.59 trilioni.

=======

Madiwani Z’bar kulipwa mishahara​

Jesse Mikofu

Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) jana imewasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2022/23 ya Sh2.5 trilioni huku ikitarajia kuanza kuwalipa mishahara madiwani wadi ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo kwa Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya alisema kati ya Sh2.5 wanazotarajia kukusanya, mapato ya ndani ni Sh1.3 bilioni, misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo ni Sh687.95 bilioni, mikopo ya ndani na nje kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ni Sh515.0 bilioni.

Pia aliomba kuidhinishwa Sh17.60 bilioni kukusanywa na Serikali za Mitaa.

Kwa upande wa matumizi alisema kati ya hizo, Sh1,220.51 bilioni zimeelekezwa kwa ajili ya kazi za kawaida, Sh1,352.19 bilioni zimeelekezwa kwenye kutekeleza Mpango wa Maendeleo na Sh17.60 bilioni zinakwenda kutumika katika Serikali za Mitaa.

Waziri Mkuya alisema SMZ imepanga kuimarisha masilahi ya watumishi wa umma na imetenga Sh628.68 bilioni sawa na asilimia 24 ya bajeti kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi, ikiwemo na marekebisho mapya ya mishahara kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Alisema pia Serikali imedhamiria kuanzisha fao la kupoteza ajira ambalo litasimamiwa chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

Dk Mkuya alisema hadi kufikia Machi 2022, Deni la Taifa limefikia Sh1.2 trilioni na linalodhaminiwa na Serikali ya Mapinduzi ni Sh310.7 bilioni.

Alisema deni hilo limeongezeka kwa Sh76.3 bilioni, sawa na ongezeko la asilimia 33 ikilinganishwa na deni lililoripotiwa Machi 2021 ambalo lilikuwa Sh234.4 bilioni.

Waziri Mkuya alisema Serikali inapendekeza kufuta kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mashine za kielektroniki na karatasi za kutolea risiti wakati wa uingizaji na usambazaji (uuzaji) kwa mawakala wa uingizaji na usambazaji walioteuliwa na Serikali.

Alibainisha kuwa Serikali inapendekeza kufuta kodi ya VAT wakati Benki za Kiislamu ambazo hutozwa mara mbili wakati benki inaponunua bidhaa na wakati wa kuwasilisha bidhaa hiyo kwa wateja wake.

Serikali inapendekeza kuanza kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa huduma zinazotolewa mtandaoni ambapo jumla ya Sh6.0 bilioni zinatarajiwa kukusanywa kutokana na hatua hii.

Dk Saada alisema kwa mfanyabiashara ambaye mauzo yake hayazidi Sh5.0 milioni hatapaswa kulipia, mauzo baina kati ya Sh5 milioni hadi Sh7.5 milioni atatozwa Sh100,000, mauzo yasiyozidi Sh7.50 milioni hadi Sh10.0 milioni atatozwa Sh200,000.

Na mauzo kati ya Sh10.0 milioni hadi Sh12.50 milioni atatozwa Sh 300,000 na mauzo kati ya Sh12.50 milioni hadi Sh15 milioni atatozwa Sh400,000.

Kodi kampuni usafirishaji

Alisema kwa muda mrefu sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar imekuwa haikusanyi kodi ya mapato ya asilimia tano kwa kampuni za kigeni za usafirishaji wa abiria na mizigo, hivyo mwaka wa fedha ujao 2022/23 TRA–Zanzibar itaanza rasmi kukusanya kodi hiyo kupitia wakala wa Shirika la Meli na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar. Hatua hii inatarajiwa kukusanya jumla ya Sh1.3 bilioni.

Mwananchi
kumbuka zanzibari wana mihimili.Kwahiyo haya yamefanywa na serikali ya kule.Hongera
 
msonobali

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,206
1,016
Mbona madiwani wa Tanganyika wanalipwa laki 3 kwa mwezi..bado posho za vikao vya halmashauri..acha ramli chonganishi tafuta taarifa sahihi.

#MaendeleoHayanaChama
Unahakika na posho za vikao? Ile 600,000 aliyofuta mwendazake kwa madiwani ilisharudishwa usijisahaulishe
 
Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,049
1,649
Kwa taarifa yako, madiwani walikuwa wanalipwa mshahara kama laki tatu hivi, sijajua kwa awamu hi
 
Michael mbano

JF-Expert Member
Apr 4, 2022
820
560
Unahakika na posho za vikao? Ile 600,000 aliyofuta mwendazake kwa madiwani ilisharudishwa usijisahaulishe
madiwani hulipwa posho ya vikao au kamshahara kulingana na mapato ya halmashauri.Wapo wanaopata laki kwa kikao na wengine zaidi.Na mwisho wa mwezi wengine 250000 wengine ni zaidi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

5 Reactions
Reply
Top Bottom