Ubabe hadi Canada? This time you're done

Ubabe hadi Canada? This time you're done

Pascal Mayalla,
Huwa nasikia waswahili wanasema, adui yako muombee njaa, nadhani wanaofurahia ni wale wanaye muombea Rais Magufuli njaa.

Ndege ni zao au zetu? Huwa naona kila zikija wanachama wa ccm ndio hualikwa, nahisi hawa ni zao, sasa wale wanaokosa mualiko nadhani ndio hufurahia.

Haya mambo ya jinsi gani watu wanapokea nadhani yako binafsi sana, hata wanaofurahia au kushangilia mtanange huu hawabadili chochote, the fact kwamba tunadaiwa.

Nadhani wangelipa tu ili kuondokana na fedheha hii.
Pascal Mayalla,
Huwa nasikia waswahili wanasema, adui yako muombee njaa, nadhani wanaofurahia ni wale wanaye muombea Rais Magufuli njaa.

Ndege ni zao au zetu? Huwa naona kila zikija wanachama wa ccm ndio hualikwa, nahisi hawa ni zao, sasa wale wanaokosa mualiko nadhani ndio hufurahia.

Haya mambo ya jinsi gani watu wanapokea nadhani yako binafsi sana, hata wanaofurahia au kushangilia mtanange huu hawabadili chochote, the fact kwamba tunadaiwa.

Nadhani wangelipa tu ili kuondokana na fedheha hii.
Tulipe tu hamna namna...
 
Japo ni kweli tunadaiwa, na siku zote dawa ya deni ni kulipa, lakini kukamatwa au kuzuiliwa kwa ndege yetu ni janga kwa taifa letu. Watanzania tunapaswa kuwa wamoja katika hili, kushirikiana na serikali yetu kwa moral support ndege yetu inasuliwe, lakini kunaonekana kama kuna uzalendo wa ajabu wa watu kufurahia na kuliongelea kiushabiki majanga kwa nchi yako


P
Mkuu.. Je unadhani ni kwann hali hii imefikia hapa??
 
Baba unaponunua vitu vya nyumbani, huwa unashauriana na watoto wako nyumbani?.
P
pasko bora ukae kimya unaongea ugoro sana siku hizi nyie ndio mnafanya hadi huyo magufuli na wasukuma wengine muonekane wa hovyo sana. Njaa inakuvua nguo pasko mtaolewa huko mbele ya safari
 
Bila shaka kama Taifa kuna sehemu tumekosea,Lazima kuna Kundi la watu ndilo linatengeneza hali hii ya Matabaka katika Taifa.Mbona zamani tulikuwa tunaongea lugha moja? Viongozi wetu walikuwa wanahimiza Umoja wa kitaifa,hili Leo hii linafanyika?Mimi huwa najiuliza Leo akiingia adui ndani ya Taifa letu hakuna watu watawaonyesha njia za kupita? Hali hii Leo tunaiona kama utani lakini kesho itatuumiza sana.Maendeleo bila kujenga umoja wa kitaifa Matokeo Yake ndo haya ya wengine kufurahia tunapopatwa na matatizo.UKWELI UTATUWEKA HURU.
Jiwe,ccm,tiss,pasko na wajinga wengine ndio wameleta huu mpasuko na ukumbuke kwamba kisasi hakiozi haya wanayoyafnya walioumizwa watalipa kisasi hata aada ya miaka 50 ya mateso ya ccm
 
Pole kwa Rais wa JMT kwa ndege yake kukamatwa.
Pole kwa Waziri Kabudi kwa TZ kusalitowa.
Pole kwa Waziri Mahiga kwa mateso kutuma vijana Canada
Pole kwa serikali yetu yote kwasababu ndege ni ya serikali.
Pole kwa CCM, kwasababu serikali ni ya CCM.
Pole kwa wanasheria watakaoteseka.
Pole kwa ATC ndege yao kukamatwa hivyo kuchelewesha kupiga pesa.
Pole kwa sisi Watanzania wote kwa ndege yetu kukamatwa na kututia hasara ambayo ni sisi tutaifidia.
Ndege ni rais Magufuli kwasababu ndiye aliyeamua kuinunua kwa cash money.
Ndege ni ya serikali kwasababu inamilikiwa na serikali 100%.
Ndege ni ya ATCL kwasababu ATCL ndio wanaitumia.
Ndege ni ya Sisi Watanzania wote kwasababu fedha zilizonunulia ni fedha zetu, na sisi ndio tunaoipanda.

Pole hata hawa Watanzania wenzetu wanaofurahia na kushangilia ndege yetu kukamatwa nao pia wataifidia hii hasara maana ndege pia ni yao bila kujijua.
Pole wote.
P
Na hongera kwa wale ambao Kondaboy aliwaponda kwenye hotuba yake wakati ndege ikipokelewa.
Na hongera kwa wananchi ambao wamekuwa marginalized na utawala huu kwa sababu mbalimbali kama vile mitazamo yao ya kisiasa, makabila yao au ukanda wanapotokea au dini/madhehebu yao.
Hongera pia kwa waliopoteza ndugu zao kwa sababu za kisiasa.
Hongera kwa walioteswa na waliojeruhiwa na utawala huu kwa sababu za misimamo/mitazamo yao ya kisiasa.
Hongera watu wote wa vyama vya 'ushindani' ambao utawala huu hauwatendei haki.
Hongera kwa wananchi wote wanaomuona JPM ni mtesi na mkandamizaji.
 
I bet, nyuma ya mkulima kuna CIA au M16, kushinda hii vita ni nguma tusijidanganye,

Lumba alikuwa na back up ya Russia lkn operation barakuda ikamuondoa sembuse sasa tunategemea wale wavaa suti wanaozuia mkono wa Rais asimsalimie kanjibai...

Me naona nafuu kwetu tumlipe tu huyu mkulima vinginevyo sioni dalili ya ushindi kwetu kwenye huu mtanange.
 
Japo ni kweli tunadaiwa, na siku zote dawa ya deni ni kulipa, lakini kukamatwa au kuzuiliwa kwa ndege yetu ni janga kwa taifa letu. Watanzania tunapaswa kuwa wamoja katika hili, kushirikiana na serikali yetu kwa moral support ndege yetu inasuliwe, lakini kunaonekana kama kuna uzalendo wa ajabu wa watu kufurahia na kuliongelea kiushabiki majanga kwa nchi yako


P

Paschal, be honest, kama huyu jamaa anadai, na amefukuzwa nchini, atapaje fedha yake, uzalendo kwako una tofasiri gani. Kumtetea mtu anayeonewa pia ni uzalendo. Tunataka kulazimisha maana ya neno uzalendo ni kukumbatia mambo maovu, huko ndiko unakoelekea wewe?
 
[QUOTE="Pascal Mayalla, post: 33563036, Duh! awamu hii kiboko. Yaani watanzania wote wamekuwa watoto! kwa hiyo akina JPM ndo akina baba wetu. Haya ngoja awamu iishe turudi kuwa watu wazima halafu tutoe ushauri kwa nchi yetu.
 
[QUOTE="Pascal Mayalla, post: 33563036, Duh! awamu hii kiboko. Yaani watanzania wote wamekuwa watoto! kwa hiyo akina JPM ndo akina baba wetu. Haya ngoja awamu iishe turudi kuwa watu wazima halafu tutoe ushauri kwa nchi yetu.
 
TAHADHARI: Kama huna akili timamu usisome.!
__________________________________
Kuhusu kuzuiliwa kwa ndege yetu huko Canada, swali la msingi la kujiuliza ndege zetu zitaendelea kuzuiliwa hata lini? Hii ni ndege ya 3 tangu zimeanza kuzuiliwa.

Ya kwanza ilizuiwa Canada kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni ya ukandarasi ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL), nyingine ilizuiliwa Afrika Kusini kufuatia kesi iliyofunguliwa na mkukima Hermanus Steyn, na huyohuyo ndiye amezuia tena ndege hii ya sasa.

Tukitaka kuwa WAZALENDO wa kweli tutafute suluhu ya kudumu ya tatizo hili. Nimemsikiliza Prof.Kabudi akiongea na Rais JPM kwa kujibagaza kama kawaida yake. Akijitutumua na kuongea kwa tashwishwi na tamathali nyingi za semi, lakini hajatoa suluhisho la kudumu, badala yake ameishia kumpotosha Rais.

Kabudi ameongea kana kwamba tatizo la msingi ni Canada, na amefanikiwa kushawishi watanzania waamini hivyo. Akafika mbali na kusema alimuita Balozi wa Canada na kumwambia eti serikali imekasirika sana (hii kauli ya kifutuhi tuipuuze. Tuhesabu tu kwamba Kabudi alitaka kufurahisha umati kama kawaida yake).

Lakini je tatizo ni Canada. Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada, si Afrika kusini, wala si Chato. Tatizo la msingi ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya serikali na serikali kuangukia pua. Kwa hiyo badala ya kudeal na Canada tudeal na kesi hizo. Unless otherwise ndege zetu zinaweza kukamatiwa hata Burundi.

Kwa mfano kesi iliyoshikilia ndege kwa sasa ni ya mkulima Hermanus Steyn. Huyu alikua mlowezi aliyemiliki mashamba makubwa sana ya kilimo mkoani Arusha. Mwaka 1982 serikali ya Nyerere ikataifisha mashamba yake, magari yake 250, ndege ndogo 12, mifugo na majengo.

Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.

Serikali ya Rais Mwinyi ikamlipa $20M kama ilivyopendekezwa na kamati ya akina Chenge. Wakati huo sarafu yetu bado ilikua na nguvu. $20M zilikua kama TZS 44M hivi kwa wakati huo. Mkulima Steyn akapewa lakini hakuridhika. Akaendelea kudai kiasi kilichobakia. Na amekua akidai tangu wakati huo hadi sasa bila kulipwa. Kiasi kilichobakia kilikua $16M lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu pamoja na riba kimefika $33M, sawa na TZS 70 Bilioni kwa sasa.

Serikali ya Tanzania ilipoona anasumbua sana kudai fedha hizo ikampiga marufuku kukanyaga ardhi ya Tanzania. Steyn akaona atapoteza haki yake. Akachukua hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa ushindi na kwenda kusajili tuzo yake katika Mahakama ya Afrika kusini. The Arbitration act, cap.15 inamruhusu kufanya hivyo.

Akaomba mali za serikali ya Tanzania zilizopo Afrika kusini zikamatwe ili kufidia deni lake. Kifungu cha 30 cha sheria hiyo kinatoa masharti ya kufanya hivyo (conditions for enforcement of foreign awards). Na ndipo ndege yetu aina ya Airbus A220-300 ilipozuiwa nchini humo.

Lakini ikaachiwa baada ya mahakama ya Guateng kujiridhisha kuwa Hermanus alikosea kusajili "tuzo" yake mahakamani hapo (procedural irregularities). Sasa mkulima huyo amesajili "tuzo" hiyo nchini Canada, na ndio maana ndege yetu nyingine imekamatwa.

Jambo ambalo Kabudi anapotosha kwa makusudi ni kusema kuwa tulimshinda mkulima Hermanus Steyn on merit. Uongo mtupu. Kama tulishinda on merit why the matter is not res judicata?

Hatukumshinda Steyn on merit. Yani hatukumshinda katika kesi ya msingi ya kutaka alipwe fedha anazotudai. Tulimshinda kwa "technicalities" za kisheria (procedural irregularities) baada ya yeye kukosea kusajili tuzo hiyo kwenye mahakama ya Guateng.

Kwa lugha rahisi ni kwamba Hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa Hermanus tuzo ya $36M bado haijabatilishwa. Na Hermanus anaweza kuisajili tuzo hiyo katika nchi yoyote ya Jumuiya ya madola. Kwahiyo hata ndege ikiachiwa Canada, anaweza kusajili tuzo yake India, Kenya, Zambia, Australia, au nchi yoyote yenye mali za Tanzania zinazoweza kufikia thamani ya tuzo hiyo, na mali hizo kukamatwa.

Kwahiyo Kabudi anapoishangaa Canada, ni kukosa umakini tu. Ameongea kama "layman" ambaye hajui sheria kabisa. Vijana wa LLB1 pale UDSM, Mzumbe au SAUT wanamshangaa.

Mali zetu zimekamatwa zaidi Canada kwa sababu ndio nchi yenye mali nyingi za Tanzania kwa sasa (ndege zote za Bombadier zinatengenezwa huko). Hata Brazil ambapo Kabudi anashauri tukanunue ndege, zinaweza kukamatwa pia kama Steyn akiamua kwenda kusajili tuzo yake kwenye mahakama za huko.

Hivyo basi tunahitaji kupata suluhisho la kudumu badala ya kupiga 'ngonjera' kwamba kuna watanzania wanatumiwa na mabeberu kutuhujumu. Hakuna cha "beberu" wala "mbuzi jike" anayetuhujumu, ni makosa yetu wenyewe. Tutafute mbinu za kuyatatua badala ya kujificha kwenye visingizio vya mabeberu. Na tusimpotoshe Mheshimiwa Rais.

Nini kifanyike?
1. Serikali imuondolee mkukima Hermanus Steyn marufuku iliyompiga ya kuingia nchini. Ikumbukwe anahangaika huko nje kwa sababu amezuiwa kuja nchini. Kabla hajapigwa marufuku ya kuja Tanzania alikua anakuja kudai haki yake hapa. Alipozuiwa ndipo akaamua kuichukua "tuzo" yake mahakama kuu na kwenda kuisajili huko nje.

2. Kamati ya Chenge na Mkulo iitwe na kuulizwa msingi wa kupendekeza Steyn alipwe kiasi kidogo tofauti na "tuzo" aliyopewa na mahakama kuu. Kama sababu hizo zitakua na mashiko, zitumiwe kumshawishi Steyn akubali kiasi alicholipwa na kufuta shauri hilo mahakamani.

3. Kama serikali haikubaliani na option hizo mbili hapo juu, basi ikate rufaa au iombe "judicial review" kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya kumpa Steyn tuzo ya $36M. Na maamuzi yatakayotolewa kwenye rufaa hiyo yaheshimiwe na pande zote mbili.

Vinginevyo tutaishia kuwalaumu "mabeberu", kesho tutawalaumu "majogoo", keshokutwa tutawalaumu "mitetea" pasi na sababu zozote za msingi. Kama mkulima huyu kudai haki yake ni ubeberu basi Mahakamu kuu ya Tanzania ndio beberu kuu maana ndiyo iliyompa ushindi wa tuzo hiyo. Tuache porojo. Tudeal na msingi wa tatizo.

Tuanzie na sababu za Nyerere kutaifisha mali za Steyn, kisha twende kwenye hukumu iliyotolewa na mahakama kuu na kumpa ushindi. Then tumalizie na ripoti ya kamati ya akina Chenge. Halafu tumuite Steyn tukae nae mezani tuyamalize. Tuache kurukaruka kama maharage yaliyokosa maji.!

Malisa GJ
 
Pascal Mayalla,
My brother pascall, we were not happy coz of our plane being detained in south africa, no no no, we were happy coz this awamu ya tano thinks that they are clever than even God himself, if you see a president who kills, orders 37 bullets to be pumped into an opposition mp, orders the military to buy korosho yet korosho is nowhere near things like rockets, sumarines or fighter jets,a president who denies people right to express themselves, what else do you expect from the majority of those who such a dictator president is opressing??? i can tell you pascal my brother for free, lots of us will be more than happy if God sends this person(you know who i am talking abaut) to hell fire where he RIGHTFULLY BELONGS, nice weekend bro

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌👯👯👯👯👯👯👯👯👯👯👯!
Nakazia!
 
Pascal Mayalla,

Wakati wa kujadili taarifa ya kashfa ya Richmond bungeni Spika alitahadharisha Bunge (wale ccm) dhidi mshikamano wa kichama kwenye uovu. Viongozi wetu hawajatupatia maelezo yoyote kwanini hawataki kulipa deni na badala yake mdai amepigwa marufuku nchini!
 
Tatizo waziri Prof. Palamagamba Kabudi hajatuweka wasi Watanzania pamoja na Rais wetu Dr John Joseph Pombe Magufuli kwa kusema tulishinda kesi kule Africa Kusini. Hebu tujiulize Je,tatizo ni Canada au Africa Kusini? Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada wala Afrika Kusini wala USA. Tatizo lipo kwenye kesi ya msingi iliyofunguliwa na Mkulima Hermanus Stely dhidi ya serikali ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania na kushinda. Kwa hiyo badala ya kupamabana na Canada na kumwita Beberu anachukia maendeleo yetu akishirikiana na Watanzania ambao siyo wazalendo tupambane na kesi hizo mahakamani. Bila kupambana na hizi kesi zote kisheria kupitia mahakama zote ambazo tumeridhia ambazo serikali zetu kuanzia kwa Mwalimu mpaka sasa tunadaiwa ndege zetu au mali za serikali yetu zitaendelea kukamatwa popote pale.

Mfano huyu mkulima Hermanus Stely alifungua kesi mahakama ya hapahapa nchini 1982 akidai fidia ya $36M baada ya serikali ya wakati huo chini ya mwalimu Nyerere kutaifisha mifigo yake, nyumba zake,magari, matrekta na ndege ndogo 12 hivi. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi " hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo.

Hapa ndiyo waziri hajatuweka sawa kuhusu hii kesi pamoja na ile ya kule Canada ya mwanzo kabisa kuwa tulishinda kesi ya msingi kuhusu madai ya mkulima ya $36M? Je, vipi kuhusu mdai wetu wa kwanza pia aliyeshikilia ndege yetu ya kwanza hukohuko Canada tulimshinda?

Majibu yake mtusaidie wataalamu wa sharia lakini tunajohofia ni kusuhu kesi za msingi tulishinda?

Mfano Je mahakama ya Africa Kusini ilibatilisha hukumu iliyompa mkulima Hermanus Stely tuzo ya $36M?, maana hiyo ndy kesi ya msingi

Swala la kuhusika kwa nchi halina mashiko ,kwa mikataba ambayo tumeingia kama taifa hata Kenya or India mali zetu zinaweza kukamatwa.

Waziri atupe majibu yaliyo sawa siyo kusema kuna nini huko Canada na tunaweza kwenda hata Brazil (kama issue ni mahakama bado itakamatwa tu) bali ni kutuweka sawa kuhusu mambo ya kisheria kuhusu kesi na hukumu iliyotolewa, watanzania wa leo tuna uelewa wa juu sana na ndege yetu Dreamline ilivyoachiliwa kule Africa Kusini hamukuonyesha jinsi mlivyo shinda kesi ya msingi . Yawezekana labda mlimshinda mkulima kupitia taratibu tu za kimahakama kuhusu usajili wa hiyo tuzo yake ya msingi lakini kesi yake ikabakia pale pale na ndiyo maana imeweza kupokelewa Canada.

Watanzania tunaumia sana maana hizi ni kodi zetu, tunataka majibu yanayoeleweka na kama kuna uzembe mahali watu wawajibike.
 
Back
Top Bottom