Ni kuipenda nchi yako kwa dhati ya moyo wako, hivyo kutanguliza mbele maslahi ya taifa kuliko hata maslahi binafsi.
Kama ilivyo katika ngazi ya familia, Baba wa familia akifanya kosa akatiwa ndani, huwezi kufurahia hata kama ni kweli baba yako ni mkosaji.
Hivyo kwenye hili la ndege, japo ni kweli tunadaiwa, lakini Mtanzania Mzalendo wa kweli wa taifa lake hawezi kufurahia, kushangilia, kubeza na kukejeli ndege ya taifa lake inapokamatwa, hili ni janga la kitaifa.
Huu ni uzalendo wa ajabu
Wanabodi, Jumatatu ya leo, nimeipata tena fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa. Leo nazungumzia Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, nchi yako inapatwa na majanga, halafu wewe unafurahi, huu ni Uzalendo wa aina gani?. Kiukweli huu ni Uzalendo wa Ajabu Kabisa kuwahi...
www.jamiiforums.com
P