Tuwekane sawa: Dini hujenga mitazamo ya mtu, vyama vya siasa vichukue mikondo ya kimakundi

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam,
Hoja: Kuhuhusu mitazamo, mantiki, ufikiri na misingi ya maamuzi.

Nimeona mivutano na uongo mwingi kuhusu dini, imani, madhehebu,, makabila, ukanda, jinsia nakadhalika kutumika katika kukanya, kuzuia, kuhimiza na kuogofya kutumika kama misingi ya kifikra katika kufanya maamuzi au kutoa maoni ya Kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hoja zangu.
1. Dini huwa sehemu ya Utamaduni wa mtu. Mfano, Mh. Samia ni Muislam na ni Mzanzibari, na ni Mwanamke. Huyu Ana utamaduni wa Kutoka katika makuzi hayo, hivyo namna yake ya kufikiri itaathiriwa kwa kiasi flan na hayo. Sasa hicho kiasi kinaweza kuwa kikubwa au kidogo.
2. Makamu wa Rais, Mh. Mpango ni mkiristo Mkatoliki. Nae anadondokea kwenye hizo mila na kona za kufanya maamuzi kutoka katika hayo maeneo.
3. Zitto, Mbowe, Jusa, Padre Kitima, Shehe Ponda, Mzee Mwinyi, Kikwete, Mkapa etc. Na hata sisi tulioko hapa Jukwaani. Tunaathiriwa kwa namna flani kufikiri na kuamua tukiongozwa na vihisishi vya dini, kabila, ukanda, makuzi etc. Hivyo hatuwezi kuwa na vyama Neutral, taifa Neutral, Siasa Neatral. Ni uongo.
CUF ni ya Waislam, ACT Ni CUF katika rangi tofauti, UDP ililenga Wasukuma na Wakulima, CHADEMA ijiweke wazi kuwa ni chama chenye Mkondo wa Ukristo. Kitafanikiwa.
Sababu
1. Hakuna Chama hasa kinachobeba agenda za Wakristo, hakuna Chama hasa kinachobeba agenda za wabara walio wengi wanaojitambua katika zama za usasa. Wakrito tafuteni chama.
2. Wakulima, kama wanataka kutoka walipo lazima wawe na chama.kinachobeba hoja zao. Wakiinvia bungeni hoja zao ni wakulima.
3. Wafanyakazi nao hivyo hivyo.

Hii ndio maana ya vyama vingi. Hapo Ccm itapata upinzani utakaosaidia kusogeza taifa mbele
 
Kama tuna kiongozi ambaye fikira zake zinachochewa na dini ama kabila huyo ni kiongozi mpumbavu. Anapaswa kuwa kiongozi wa dini na sio kiongozi wa Taifa ambalo limejipambanua katika misingi ya kuongoza pasipo kujali dini ama kabila.
 
Kama wenye dini wanashindwa kuwa nyutro wakiwa katika siasa na madarakani basi tukubali tu wasio na dini ndio watuongoze.
 
Hoja yako ni ya msingi sana, ndio maana sio vyema kuwakabidhi madaraka ya aina yoyote watu wanaojionyesha au wanaoonekana sana mbele ya umma kwamba wameshika dini yao sana, au feminist sana au (anti-feminists) sana/local Andrew Tates n.k.
 
Haifai kuwa na kiongozi ambaye anaipa kipaumbele dini au kabila lake kuliko taifa, kiongozi WA hivyo ni rahisi kuzongwa na watu WA dini yake au kabila lake na kuanza kuinfluence maamuzi muhimu kwa ajili ya nchi.
 
Kama tuna kiongozi ambaye fikira zake zinachochewa na dini ama kabila huyo ni kiongozi mpumbavu. Anapaswa kuwa kiongozi wa dini na sio kiongozi wa Taifa ambalo limejipambanua katika misingi ya kuongoza pasipo kujali dini ama kabila.
Uwe makini, huenda mpumbavu ninwewe ambae umeshindwa kujua humpendi alie madarakani kwa kuwa tu sio muumini wa madhehebu yako. Nimekuambia dini zinaamua mengi maishani mwetu hadi kwenye kuamua baya na Zuri. Jitazame
 
Hoja yako ni ya msingi sana ndio maana sio vyema kuwaweka watu wanaojionyesha sana mbele ya umma kwamba wameshika dini yao sana, au feminist sana au (anti-feminists) sana/local Andrew Tates n.k.
Kwanini unataka wajifiche ? Hili ndio tatizo la hii nchi. Kusema hatuna dini. Kwanini kwenye katiba tusiseme Tanzania ni Taifa la Kikristo na Kislam lkn linalotambua uwepo wa dini nyingine? Halafu kutokea hapo tukajenga msingi mpana wa maadili ya taifa.?

Mfano, Kula Rushwa Uislam unasema unyongwe, Ukristo unasema ya Kaisari mwachie kaisari, hapo tunapata upenyo, tunasema kaisari anasema anyongwe. Tunapitisha sheria kali kwa wala rushwa kuwa hukumu ya kifo. Uislam na Ukristo vinakutana kwenye kujenga Taifa. Unaonaje hapo
 
Hoja yako ni ya msingi sana, ndio maana sio vyema kuwakabidhi madaraka ya aina yoyote watu wanaojionyesha au wanaoonekana sana mbele ya umma kwamba wameshika dini yao sana, au feminist sana au (anti-feminists) sana/local Andrew Tates n.k.
Unamaanisha Padri Slaa alivyo wakusanya maaskofu pale Temeke ... maaskofu wa chadema..tuwe nae na tahadhari??
 
Tatizo letu ni unafiki...

Kuna dini ambazo ni "foreign agent"..
Kitu kikipitishwa Vatican hawana ubavu wa kukipinga kabisa....

Na hao ndo hawaoni aibu kuvaa majoho na kupanda majukwaani..
Wewe ukiuliza mbona hivi wao ndo wanakushambulia kuhusu dini
 
EU countries zote ziko openly kuwa ni nchi za kikristo....
Vyama vyao kama Christian democratic party huko Ujerumani viko so openly....hata kuizuia Turkey ni suala la dini na linajadiliwa so openly...

Sisi Mtu anamuona Pengo ,Padri Slaa na Askofu Mwamakula eti ni watu neutral.. wazalendo....akili gani hizi?
Dpworld wangekuwa wanatoka Italy wangekuja front hivi?
 
Unamaanisha Padri Slaa alivyo wakusanya maaskofu pale Temeke ... maaskofu wa chadema..tuwe nae na tahadhari??
Toka hapo, sogea mbele kidogo. Huyu Slaa, Zitto, Rostam, Pengo, Mbowe, Malecela, Nyerere, Samia, wewe, faizafox, etc wote fikra zetu zinajengwa kwa kiasi flan ( kikubwa au kidogo ) na Dini zetu
 
EU countries zote ziko openly kuwa ni nchi za kikristo....
Vyama vyao kama Christian democratic party huko Ujerumani viko so openly....hata kuizuia Turkey ni suala la dini na linajadiliwa so openly...

Sisi Mtu anamuona Pengo ,Padri Slaa na Askofu Mwamakula eti ni watu neutral.. wazalendo....akili gani hizi?
Dpworld wangekuwa wanatoka Italy wangekuja front hivi?

Na wewe inawezekana unawashambulia hao ama kutokana na madhebu yako, au maslahi yako. Hatuwezi kuwa Neutral
 
Kwanini unataka wajifiche ? Hili ndio tatizo la hii nchi. Kusema hatuna dini. Kwanini kwenye katiba tusiseme Tanzania ni Taifa la Kikristo na Kislam lkn linalotambua uwepo wa dini nyingine? Halafu kutokea hapo tukajenga msingi mpana wa maadili ya taifa.?

Mfano, Kula Rushwa Uislam unasema unyongwe, Ukristo unasema ya Kaisari mwachie kaisari, hapo tunapata upenyo, tunasema kaisari anasema anyongwe. Tunapitisha sheria kali kwa wala rushwa kuwa hukumu ya kifo. Uislam na Ukristo vinakutana kwenye kujenga Taifa. Unaonaje hapo
Wasijifiche ila dini zao ziwe ni mambo yao binafsi na sio ya nchi kiujumla kwa sababu hazina msaada wowote katika nchi.

Pia kulifanya taifa la kidini hakutasaidia kubadilisha chochote. Zambia katika katiba yao wanajitambulisha rasmi ni taifa la Kikristo lakini bado hawana tofauti kubwa sana na mataifa mengine ya Africa katika matatizo yao, zitazame pia Afghanistan, Pakistan, Bangladesh, pamoja na kujitambulisha kidini lakini bado ni nchi za hovyo tu.
 
Toka hapo, sogea mbele kidogo. Huyu Slaa, Zitto, Rostam, Pengo, Mbowe, Malecela, Nyerere, Samia, wewe, faizafox, etc wote fikra zetu zinajengwa kwa kiasi flan ( kikubwa au kidogo ) na Dini zetu
My friend kinachoshangaza mtu kumuita FaizaFoxy ana udini...
Wakati anae muita hivyo yeye mkatoliki ..anaamini Pengo ni mtakatifu na mapadri na Maaskofu wake ni watu wa Mungu....yaani kiwango cha foolishness cha baadhi ya watanzania ni cha ajabu sana
 
Na wewe inawezekana unawashambulia hao ama kutokana na madhebu yako, au maslahi yako. Hatuwezi kuwa Neutral
Mimi Nina point out kitu kiko so openly....
Labda ningekuwa mkatoliki nisingeweza kukiona...ningekuwa blinded by faith..
 
Wasijifiche ila dini zao ziwe ni mambo yao binafsi na sio ya nchi kiujumla kwa sababu hazina msaada wowote katika nchi.

Pia kulifanya taifa la kidini hakutasaidia kubadilisha chochote. Zambia katika katiba yao wanajitambulisha rasmi ni taifa la Kikristo lakini bado hawana tofauti kubwa sana na mataifa mengine ya Africa katika matatizo yao, zitazame pia Afghanistan, Pakistan, Bangladesh, pamoja na kujitambulisha kidini lakini bado ni nchi za hovyo tu.
Sasa ili ufanikiwwe hapo, kwanza lazima utambue uzito na ukubwa wa dini na madhebu katika kujenga mitazamo na maamuzi. Pili dini au madhehebu makubwa yakutane kuweka misingi ya maadili kitaifa huku ikiheshimu kwa kiasi wengiene ( kwa kiasi) . Halafu dola sasa iunde mifumo imara kutoka katika dini au madhehebu hayo. Hapo tutatoka. Tanzania inafaida ya mchanganyiko kuliko Zambia. Mfano kwenye katiba mpya tuseme tu, Waislamu katika makundi yao leteni maoni, wakristo, Wasio amini hayo nao walete. Halafu tunaweka pamoja. Utakuta mengi yanafanana. Una9naje hapo
 
Mimi Nina point out kitu kiko so openly....
Labda ningekuwa mkatoliki nisingeweza kukiona...ningekuwa blinded by faith..
Walau unaona changamoto inayokukabili. Unakiona kwa kuwa haumo, na ulimo hauoni kwa kuwa umo. Ukitulia kidogo utaona maana ya kuathirika na aina ya utamaduni wako katika kufanya maamuzi.
Yaaani, Badala ya Tume ya warioba kwenda kuhoji mtu mmoja mmoja ingehoji dini, madhehebu, mila na tamaduni. Tungepata katiba bora sana
 
Uwe makini, huenda mpumbavu ninwewe ambae umeshindwa kujua humpendi alie madarakani kwa kuwa tu sio muumini wa madhehebu yako. Nimekuambia dini zinaamua mengi maishani mwetu hadi kwenye kuamua baya na Zuri. Jitazame
Nikijitazama sioni dhehebu lolote karibu yangu. Sijawahi/Sitowahi ku judge mtu kwa msingi wa dini au kabila lake.
 
Walau unaona changamoto inayokukabili. Unakiona kwa kuwa haumo, na ulimo hauoni kwa kuwa umo. Ukitulia kidogo utaona maana ya kuathirika na aina ya utamaduni wako katika kufanya maamuzi.
Yaaani, Badala ya Tume ya warioba kwenda kuhoji mtu mmoja mmoja ingehoji dini, madhehebu, mila na tamaduni. Tungepata katiba bora sana
Actually kama umefatilia mara zote huwa naongea as a neutral...but simbishii anae nihukumu . ..
Ambacho nimegundua huwezi Ku acknowledge neutrality kama wewe sio neutral pia...
 
Sasa ili ufanikiwwe hapo, kwanza lazima utambue uzito na ukubwa wa dini na madhebu katika kujenga mitazamo na maamuzi. Pili dini au madhehebu makubwa yakutane kuweka misingi ya maadili kitaifa huku ikiheshimu kwa kiasi wengiene ( kwa kiasi) . Halafu dola sasa iunde mifumo imara kutoka katika dini au madhehebu hayo. Hapo tutatoka. Tanzania inafaida ya mchanganyiko kuliko Zambia. Mfano kwenye katiba mpya tuseme tu, Waislamu katika makundi yao leteni maoni, wakristo, Wasio amini hayo nao walete. Halafu tunaweka pamoja. Utakuta mengi yanafanana. Una9naje hapo
Haya ni baadhi ya mataifa ambayo dini imepuuzwa sana na yameendelea sana,
1.China
2.Japan
3.Sweden
4. Czech
5. Estonia
6.Ufaransa
 
Back
Top Bottom