Unajua kwamba Kuna diploma ambao wameishia form four?Ok.. ndio wameachwa mbali lakini twende ktk uwezo wao! pia kumbuka diploma na degree wote wameishia form six!! na ujue siku hizi dip na degree wote wanakuja kwenye shule za olevel ni baadhi wanaoenda a level...jiulize why..
Utakuwa umesoma diploma?Dgree mnajitahidi kuvutia kwenu,,lakini ukweli upo pale pale mwl wa degree ni too low kwa diploma ,,kuanzia kiutendaji,ufanisi wa ufundishaji na kila kitu,, nafikiri nlicho kiona hapa nikwamba watu waitukuza degree kimatamshi wakati ni vilaza wa kutupa?nenda na hiyo degree yako kafanye mtihani wa diploma uone kama hujatoka na sup zote! Ila kwa alie pitia dip then akaenda degree huyo kweli respect kwake .lakini sio hawa vikojozi wa fm 6 wanao vulia chupi ma prof ili wapate GPA ,,ni sufuri, tupu! Hata utendaji wao ni bure kanibisa, na wengine wajaribu kujenga hoja eti kuajiri mwl wa degree gharama ,,ghara gani unayo ongelea hapa?? Kwa wale wanao own shule wanajua utofauti uliopo kati ya degree na diploma kiutendaji sio kutukuza sifa tu kuwa na degree halafu kichwani huna kitu.
Diploma!kuelekea ajira mpya za walimu hebu tuwe wakweli wanaJF ni mwalimu yupi anaandaliwa vizuri kiuwezo na kimaadili pamoja na mbinu za kufundisha kati ya diploma na degree? ikumbukwe kuwa mwalimu wa diploma hufanya mtihani wa mwisho chini ya necta na akifeli somo moja (SUP) Haajiriwi wakati yule wa chuo kikuu husoma kwa semister..nina mifano ya watu kadhaa ambao walifeli diploma wakaamua kwenda chuo kikuu leo hii wana degree! pia hata shule nyingi za binafsi hawapendi wenye degree unless huyo mtu kapitia diploma kwanza! sitasema mengi najua kuna watu watanielewa tofauti....hata hivyo sina nia mbaya karibuni tujadili
Naam, kwa hapa ni kama umefunga mjadalaKabla sijasoma bachelor nilipokuwa na diploma niliamini hivyo kwa kuona walimu wengi wa bachelor kutokumudu vitu vidogo kama lesson plan but when I joined at university education ndo nimegundua kuwa mwl wa bachelor huandaliwa kwa content kubwa sana ili akawasaidie watu kuanzia kuwaongoza kuwafundisha wanafunzi wa diploma hadi darasa LA awali duniani kote na masuala ya lesson plan na scheme of work mkazo siyo MKUBWA sana kama diploma. Kwa sababu unaweza soma course zaidi ya 60 kwa miaka 3+ ambayo ni sawa na masomo ya diploma wakati diploma kwa miaka 2+ unasoma masomo 10+ tu yanayo jirudia rudia kwa miaka yote . hiyo humfanya mwalimu kuwa vuzuri kwa hicho kichache. Kama hutojali mwl wa diploma nenda bachelor ninacho zungumza utakifahamu.
Walimu wa primary si ndio hadi sasa wanarazimishwa washone sare kwa ajiri ya kupokea mwenge? Kaka siwashangai maana wengi wao wamepatikana kimagumashi, wanatumia vyeti vya wajomba zao, wengine wanaelimu ya darasa la nne wanafundisha la saba. Sasa ni lini watasimama na kudai haki zao? Wanaona hata hapo walipo ni neema tosha kabisa!
Kuwa muwazi mkuu sifa huna.Mkuu kweli nina diploma na kutokana na nilivyoona uwezo wa wale degree holder nimeona sina haja ya kuchukua degree maana hakuna walichonizidi ! pia kuhusu sifa kuanzia za form 6 hadi matokeo yangu ya dip yananiruhusu kuchukua degree...sasa nifuate nini huko? kuongeza mshahara au? maana maujuzi...hahaha!