CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,784
- 6,180
kuelekea ajira mpya za walimu hebu tuwe wakweli wanaJF ni mwalimu yupi anaandaliwa vizuri kiuwezo na kimaadili pamoja na mbinu za kufundisha kati ya diploma na degree? ikumbukwe kuwa mwalimu wa diploma hufanya mtihani wa mwisho chini ya necta na akifeli somo moja (SUP) Haajiriwi wakati yule wa chuo kikuu husoma kwa semister..nina mifano ya watu kadhaa ambao walifeli diploma wakaamua kwenda chuo kikuu leo hii wana degree! pia hata shule nyingi za binafsi hawapendi wenye degree unless huyo mtu kapitia diploma kwanza! sitasema mengi najua kuna watu watanielewa tofauti....hata hivyo sina nia mbaya karibuni tujadili