Tuwe na namba ya ziada kwajili ya biashara tu, kujaza status za matangazo ya biashara kwenye namba yako binafsi haipendezi.

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Yani kuna baadhi ya marafiki zangu huwa nawashangaa, wanaweka status za biashara utadhani sisi ni wateja wao.

Nina rafiki kila siku anaweka status za chupi, mwengine kila siku anaposti status za oili za pikipiki, mwengine tray za mayai, mwengine simu, n.k. huwa inafika mahali sasa natamani hata nizifungie status zao maana mimi huwa nategemea kukuta status za maisha yao wao kama wao lakini nakutana na status za matangazo ya biashara tu, inakera kwakeli

Napenda nikiingia status ya ndugu, kaka, dada, rafiki, mke, jirani, wanafamilia, n.k nikute hata kaposti picha yake ama hata kituko, haya mambo ya kuposti posti biashara yatafutiwe namba zake za ziada kwajili ya wateja.
 
Kila mtu akianza kuposti biashara zake ama mambo ya ofisini kwake kutakuwa hakuna hata maana ya status za watu wa karibu sasa..
Lakini kwa upende mwingine wateja ndio hao hao watu WA karibu,,,,we unasemaje juu ya hilo
 
Lakini kwa upende mwingine wateja ndio hao hao watu WA karibu,,,,we unasemaje juu ya hilo
Sawa, tafuta namba ya ziada uiwekee whatsapp business, nikitaka kuangalia status za biashara yako ntafungua namba yako ya biashara.

Namba yako personal iwe kwajili ya mambo personal
 
Sawa, tafuta namba ya ziada uiwekee whatsapp business, nikitaka kuangalia status za biashara yako ntafungua namba yako ya biashara.

Namba yako personal iwe kwajili ya mambo personal
Wazo sio Baya Lkn unadhan watu Wana Mda wa kufanya hivyo?

Kwa watu hawa ambao wako busy na mambo kibao ktk mitandao
 
Back
Top Bottom