Tuwaze mrejereo: Hivi DP World ingeletwa na Magufuli ingepingwa?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Sitaki kumchokoza mwendazake wala yoyote. Nimekuwa nikilisikiliza malumbano juu ya 'uuzwaji' au uwekezaji wa bandari ya Dar.

Je tatizo hapa ni mkataba au namna Serikali ya sasa inavyofanya mambo yake? Hivi kuna kosa kubwa kama kuvuruga uchaguzi ambapo Chama Cha Majambazi sorry mapindiuzi kilishinda viti vyote?

Sikuona malumbano, vitisho, kukamatana, mipasho na zilzali kama sasa. Je hapa tatizo ni ile hali kuwa paka akiondoka mipanya hujitawala au?
 
Binafsi nadhani yawezekana ingekuwa hivyo ila sio kwa vipengele vya mkataba kama vilivyo hapo Magufuli asingekubali hata kidogo.

DPW si wabaya, kibaya ni namna mkataba ulivyo.

Kumbuka sakata la bandari ya Bagamoyo.
 
Sitaki kumchokoza mwendazake wala yoyote. Nimekuwa nikilisikiliza malumbano juu ya 'uuzwaji' au uwekezaji wa bandari ya Dar.

Je tatizo hapa ni mkataba au namna serikali ya sasa inavyofanya mambo yake?
Mkuu Father of All , kwenye hili la DPW na Bandari zetu, ni wanamuonea tuu Mama!. Niliwauliza humu DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
Humo nilisema
Wanabodi,

Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza rais wetu Mama Samia, kwa kuendelea kuwa na ngozi ngumu!, maana kuna vitu vinasemwa, ikijiuliza kama angekuwa ni Magufuli, vingesemwa?. Hata huo mkataba wa IGA, tungeuona?, hata huko Bungeni ungepelekwa?. Mnyonge tumnyongeni jamani, haki yake mpeni!, kwenye hili la kupeleka mkataba huu wa IGA kuridhiwa na Bunge, ni jambo jema linalo stahili pongezi za dhati.

Paskali.
hakuna mwenye jibu!.
P
 
Sitaki kumchokoza mwendazake wala yoyote. Nimekuwa nikilisikiliza malumbano juu ya 'uuzwaji' au uwekezaji wa bandari ya Dar.

Je tatizo hapa ni mkataba au namna serikali ya sasa inavyofanya mambo yake? Hivi kuna kosa kubwa kama kuvuruga uchaguzi ambapo Chama Cha Majambazi sorry mapindiuzi kilishinda viti vyote?

Sikuona malumbano, vitisho, kukamatana, mipasho na zilzali kama sasa. Je hapa tatizo ni ile hali kuwa paka akiondoka mipanya hujitawala au?
Hatuipingi DP WORLD tunapinga contents zilizomo kwenye mkataba
 
Sitaki kumchokoza mwendazake wala yoyote. Nimekuwa nikilisikiliza malumbano juu ya 'uuzwaji' au uwekezaji wa bandari ya Dar.

Je tatizo hapa ni mkataba au namna serikali ya sasa inavyofanya mambo yake? Hivi kuna kosa kubwa kama kuvuruga uchaguzi ambapo Chama Cha Majambazi sorry mapindiuzi kilishinda viti vyote?

Sikuona malumbano, vitisho, kukamatana, mipasho na zilzali kama sasa. Je hapa tatizo ni ile hali kuwa paka akiondoka mipanya hujitawala au?
DP World siyo tatizo kabisa; tatizo ni mktaba unaowaleta. JPM hangekubali mktaba huo wa kijinga hivyo.
 
Angepingwa ila shida ni upatikanaji wa DP world na jinsi vipengele vya kisheria vilivyo kwenye mkataba.

DP world inaonekana imepatikana kiujomba ujomba hivi, kama favor kwa wajomba hivi.

Jambo lingine, Mzanzibari kutufanyia maamuzi ambayo yanaweza kua na matokeo mabaya ama ya muda mrefu watanganyika hilo ndio hatukubali.

Ndio maana Zanzibar wao wanajua hilo, mustakabali wa wazanzibari uamuliwe na Mzanzibari mwenzao, sio sisi mustakabali wa watanganyika uamuliwe na mtu wa taifa lingine.

Hata wakati wa USSR, hakujawahi kua na kiongozi nje ya urusi ya sasa, hakuna. Hawakua wajinga.

Sasa sisi wenye nguvu ndani ya muungano tunaletewa mtu mwingine wa taifa lingine kutufanyia maamuzi makubwa kama hayo. Kesho muungano ukifa utampata wapi amerudi kwao Zanzibar anakula karafuu ama kakimbilia ujombani huko anakula biriani
 
Ungeacha kumuunga mkono msukuma na mkristo mwenzio ningeshangaa sana.
Dada yangu kipenzi, FaizaFoxy mimi sijawahi muunga mkono mtu yoyote kwa sababu ya ukabila wala udini!, naunga mkono au kukosoa utendaji tuu wa mtu.

Mfano mzuri ni enzi ya JPM, mimi ni Mkristo wa RC na Msukuma, JPM ni Mkristo wa RC na Msukuma, nilimuunga mkono JPM kwa uchapakazi wake na sio kwa Ukristo wake, au Usukuma wake na kila alipo kosea, nilimkosoa!.

Sasa tuko na Mama, kwanza sisi wote ni binadamu, na kiubinadamu watu tuna udhaifu mbalimbali, mimi humu JF, nimejitanabaisha ni mmoja wa members wakweli daima, kwa kujieleza maeneo yenye udhaifu wa kibinaadamu, Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? udhaifu huu umekuja hata kwako, ndio maana japo mimi ni Mkristo, na wewe ni Muislamu wa swala 5, lakini nakupenda na nimekueleza!.

Namuunga mkono Mama kwa kumsaidia katika maeneo yanayonihusu, moja ya maeneo hayo ni eneo la uelimishaji umma. Kitu cha kwanza ni kuwafundisha Watanzania kuwa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda hivyo bado tunaendelea kumpa muda mpaka 2025, ndio tumfanyie tathmini, aendelee au itoshe, apumzike!.

Hivyo dini ya mtu, na kabila ya mtu, haihusu kumkubali au kumkataa.
P
 
Back
Top Bottom