Taifa letu linapitia nyakati ngumu za ugandamizaji wa haki, demokrasia na uhuru wa maoni.
Mambo haya hayakuanza ghafla bali yamekuwa yakizidi kuongezeka na kuota mizizi.
Leo mtu anayeikosoa Serikali au Rais, kutekwa, kupotezwa, kuuawa au hata kubambikiwa kesi mbaya, imekuwa ni jambo la kawaida.
Leo hii wagombea wa upinzani kuenguliwa karibia wote wakati wa uchaguzi, inaonekana ni kawaida.
Leo hii mgombea wa CCM kutangazwa kuwa ndiye mshindi, hata kama wapiga kura wote wanajua hakushinda, limekuwa ni jambo la kawaida.
Leo hii kusikia kuwa matrilioni ya kodi za Watanzania yametumika hovyo au kupotea au kuibiwa, ni habari za kawaida.
Wakati uovu huu ukiota mizizi, ni vema kama Taifa tukawatangaza rasmi maadui wa haki, demokrasia na uhuru wa maoni, wa Taifa letu. Kwa kuwa CHADEMA ni chama kilichojipambanua kwa uwazi kuwa ni chama kinachotetea demokrasia na haki ya Watanzania, ni vema kikaandaa siku maalum, na kuzialika taasisi na watu maarufu ambao wamethibitishia bila shaka, uzalendo wao kwa Taifa bila mashaka, na siku hiyo wakatangazwa maadui wa demokrasia na haki ya Watanzania. Maadui hawa wanaweza kuwa ni taasisi au hata watu binafsi. Watakapotangazwa, kuwepo pia na matukio yenye ushahidi wa wazi na wa kimazingira, jinsi walivyohusika kudhulumu haki ya wananchi. Wa wazi kabisa ambao wanaofahamika na kila mmoja, ni pamoja na:
1. CCM
2. Mahela aliyekuwa mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya 2020
3. Ramadhani, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi wa sasa.
4. Mchengerwa, waziri wa TAMISEMI aliyeharibu uchaguzi wa 2024
5. Waliokuwa wakuu wa jeshi la polisi mwaka 2020, 2024 mpaka sasa
6. Jaji mkuu wa kipindi cha 2019 mpaka 2024.
Wengine, ongezeni kwenye orodha hiyo.
Watakapokuwa wanatangazwa waovu hawa, kutolewe pia orodha ya taasisi na watu binafsi wazalendo wa kweli walioonesha mapenzi makubwa kwa Taifa letu, ambao wamewahi kuwa mstari wa mbele kutetea haki ya wananchi:
1. Jaji Nyalali
2. Jaji Kisanga
3. Jaji Warioba
4. CHADEMA
5. Tundu Lisu
6. TLS
7. TEC
8. Shura ya Maimamu
9. Askofu Shoo
10. Askofu Bagonza
11. Shekhe Ponda
12. Askofu Mwamakula
13. Prof Shivji
Wengine ongezeeni.
Tukio hilo liandaliwe kwa ustadi mkubwa kuhakikisha wananchi wote wanawatambua maadui zetu wakubwa wa haki yetu, lakini pia kuwatambua na kuwashukuru sana watetezi wetu wakubwa wa haki yetu.