Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

We jamaa umekomaa lakini naona huna uangalifu. Mkoa wa Kagera mwanzoni uliitwa Bukoba baadaye ukawa Ziwa magharibi na sasa Kagera.
Pole sana. Mkoa wa Kagera ulikuwa ukiitwa Ziwa Magharibi baada ya vita vya Idd Amini ukabadilishwa na kuitwa Kagera
 
Kuna wilaya kongwe hapo Tanzania kama Nzega, Kilosa hazijawahi kuomba kuwa mikoa, maendeleo yao yako duni hadi leo ukiacha Nzega kwa sasa ilishafunguka vizuri baada ya kupata wabunge wanaojitambua kupigania masalahi ya wananchi wake. Igunga ni moja ya wilaya za muda mrefu lakini maendeleo yake ni duni sana na imetoa viongozi wengi tu bila kuiboresha kulingana jigrafia ya eneo ilipo njiani mwa barabara kuu ya Singida-Dom-Dar-Mwanza

Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi kwenye mkoa wa Morogoro ndio zenye changamoto kubwa sana ya barabara na huduma za kiutawala kutoka makao makuu ya mkoa. Barabara ya lami inaishia kiwanda cha sukari Kilombero baada ya hapo zaidi ya kilomita 200 ni za vumbi zikiwa na mashimo makubwa kana kwamba haichangiii chochote kwenye uchumi wa mkoa na nchi!!!
Igunga ni wilaya muda mrefu ? Hiyo imezaliwa na Nzega mwaka 1974
 
Kibara siyo makao makuu ya mkoa wa mara. Wilaya haiwezi kutegemea huduma za kiutawala kutoka wilaya nyingine bali kutoka makao makuu ya mkoa. Huduma za kimkoa ztakuwa mbali na halmashauri. Kupakana siyo tija bali ni uharaka wa huduma kutoka makao makuu. Ndo maana mpka leo nyerere anawazd wengi kifkra
1. Kuunganisha Ukerewe na Mwanza na kuunganisha Ukerewe na Mara wapi pana unafuu wa gharama?

2. Kwa kigezo cha idadi ya watu katika mkoa kutengeneza consumer market, Mara ina faida kiuchumi kwa Ukerewe kuliko Mwanza. Japokuwa Mwanza inakadiriwa kuwa na watu 2ml dhidi ya Mara 1.9m bado Mara inaizidi Mwanza kwa kuwa inapokea watu wa nchi jirani wanaovuka mpaka mara kwa mara kuja kutafuta huduma Mara. Ukerewe ina utajiri wa uchumi wa bluu, mbogamboga, ndege wa aina mbalimbali, matunda, ndizi nk, vyote hivi vinahitaji walaji wengi. Mara imepakana na nchi jirani hivyo Mara itakuwa na competitive advantage na comparative advantage over Mwanza kuhusu Ukerewe.

3. Dialects za Mara kama Kijita, Kiruri, Kikwaya, ni dialects zinazoshabihiana na Kikerewe kuliko Kisukuma. Kumbe asili ya Ukerewe ni Mara kuliko Mwanza.

Consider this Case Study.
Kutoka Wilaya ya Mafia kwenda Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani, mwananchi analazimika kwenda Wilaya ya Rufiji, aje Wilaya ya Kibiti, aje Wilaya ya Mkuranga, aje Mkoa wa Dsm ndipo aende Mkoa wa Pwani Kibaha. Kumbe basi kutoka Mafia mtu anatoka nje ya Mkoa wa Pwani anaingia Mkoa wa Dsm alafu anatoka Mkoa wa Dsm ndipo aende Mkoa wa Pwani Kibaha palipo Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani!!

Mafia ipelekwe Mkoa wa Dsm na Ukerewe ipelekwe Mkoa wa Mara.
 
Hakuna sehemu ya Tabora iliyopelekwa Katavi. Kaliua ni wilaya katika mkoa wa Tabora. Unazungumzia eneo lipi la Tabora lililopelekwa Katavi ?

Mhh. Unajua kutoka Ukerewe kwenda Musoma ni mbali sana kuliko kuja Jijini Mwanza ? Aidha nani aliyekudanganya kwamba ukerewe asili yake ni Mara ?


Dialects za Mara kama Kijita, Kiruri, Kikwaya, ni dialects zinazoshabihiana na Kikerewe kuliko Kisukuma. Kumbe asili ya Ukerewe ni Mara kuliko Mwanza. Dialects za Mara kama Kijita, Kiruri, Kikwaya, ni dialects zinazoshabihiana na Kikerewe kuliko Kisukuma. Kumbe asili ya Ukerewe ni Mara kuliko Mwanza. Lakini pia Kikerewe kwa uchache kina misamiati ya Kihaya kuliko Kisukuma na kuna simulizi kwamba asili ya Wahaya ni Ukerewe.
 
Hakuna sehemu ya Tabora iliyopelekwa Katavi. Kaliua ni wilaya katika mkoa wa Tabora. Unazungumzia eneo lipi la Tabora lililopelekwa Katavi ?
Usikariri kwamba kumegwa eneo lazima limegwe eneo lenye watu, wanaweza kumega hata mapori yasiyokaliwa na watu na wanyama ambayo yayo hayo hayajulikani kwa wengi.
 
Kumaanisha kwamba ziwa lilikua limekauka ama?.
Tupe hii historia ilikuaje..mana wazee walishawahi nambia kati ya ukerewe na bunda watu walikua wanatembea tu kwa mguu..hakuna kuvuka maji.

#MaendeleoHayanaChama
Madhara ya mabadilikko ya tabia ya nchi hayo
 
Usihangaike sana na Chato, tatizo kubwa kabisa ni Mkoa wa Katavi. Pinda atueleze aliwaza nini? mkoa wenye wakaazi wasiofika laki 4! Na hapo alitaka kuongeza ukubwa kwa kumega urambo, ikashindikana maana Urambo ndo historia ya Tabora yenyewe. Kwa ujumla kumega na kugawa mikoa ni ushamba tu wa viongozi wetu.
Nakerwa na hii tabia ya kugawa mikoa hata Sumaye alipokua Waziri mkuu aliigawa Arusha na kuja na mkoa wa Manyara mpaka leo kugawa kwake sijaona maendeleo yoyote, akaja pinda naye akagawa mkoa wa Rukwa kisa ni kiongozi , akaja Magufuli naye akawa analeta division tena ya chato ni aibu kabisa, Sasa huu ubaguzi wa kila sehemu akitoka kiongozi kuteua mkoa tutafika kweli, huko tuendako mbona USA ina majimbo makubwa na hawagawi hovyo. Hapa ni kuishauri serikali kuongeza budget za kimaendeleo Hadi ngazi za chini na sio kugawa nchi kwenye vi portion vingi huku umaskini wa watu ukiwa palepale
 
Mkuu,

Peleka na hili:

Wilaya ya Mafia ipewe mkoa wa Dsm toka mkoa wa Pwani. Tayari Pwani imeongezewa Wilaya ya Kibiti na mipango iko mbioni kuanzishiwa Wilaya ya Chalinze.
Kwa hapo awali kibiti ilikuwa wapi?
 
Urambo East Sitta, Urambo West Kapuya, sasa hivi kuna Jimbo la Urambo (Mhe. Margareth Simwanza Sitta), tusaidie kuitafuta Urambo West ya Kapuya imeenda wapi?
Wewe trush kweli, hivi unashindwa kuelewa kwamba kuna jimbo la Kaliua? Hiyo Kaliua iko Katavi? Puumbavu zako.
 
Ingekuwa vizuri ndugu yangu kama ungejibu swali langu
Usikariri kwamba kumegwa eneo lazima limegwe eneo lenye watu, wanaweza kumega hata mapori yasiyokaliwa na watu na wanyama ambayo yayo hayo hayajulikani kwa wengi.
 
Mwanza geita..shinyanga simiyu wala sio ukabila mana wote hao ni wasukuma mikoa yote hiyo..kigezo kikubwa ni wingi wa watu na ukuaji wa kiuchumi wa maeneo hayo ndio mana yakagawa ki utawala.

#MaendeleoHayanaChama
Nui mtindo wa kijinga tu! Chato ilimegwa Bihalamuro kwa sababu za kibaguzi, baada ya wahaya kwa miaka mingi kuendelea kuiona Bihalamuro kama wavamizi wa mkoa wao.
 
Nakerwa na hii tabia ya kugawa mikoa hata Sumaye alipokua Waziri mkuu aliigawa Arusha na kuja na mkoa wa Manyara mpaka leo kugawa kwake sijaona maendeleo yoyote, akaja pinda naye akagawa mkoa wa Rukwa kisa ni kiongozi , akaja Magufuli naye akawa analeta division tena ya chato ni aibu kabisa, Sasa huu ubaguzi wa kila sehemu akitoka kiongozi kuteua mkoa tutafika kweli, huko tuendako mbona USA ina majimbo makubwa na hawagawi hovyo. Hapa ni kuishauri serikali kuongeza budget za kimaendeleo Hadi ngazi za chini na sio kugawa nchi kwenye vi portion vingi huku umaskini wa watu ukiwa palepale
Mikoa mikubwa ilisaidia sana kuondoa tatizo la ukabila. Wanavyoendelea kumega mikoa mikoa inageuka kuwa vipande vya kabila moja tu. Walipogawa mkoa wa Pwani na kuondoa Dar sijawahi kuona maendeleo ya ziada kwa sababu ya kugawa mkoa.
 
Usiwe mbishi bhana! Kwani nchi hii imeanza wakati wa vita ya Idd Amin?
Wakati wa ukoloni mkoa wa sasa wa Kagera ulikuwa ndani ya jimbo la ziwa. Ilipofika mwaka 1959 Jimbo la Ziwa liligawanywa na kupata jimbo la Ziwa Magharibi. Baada ya uhuru wa Tanganyika Mkoa wa Ziwa Magharibi uliendelea kutumia jina hilo hadi baada ya vita ya Idd Amin ulipobadilishwa jina na kuitwa Kagera.
 
Mkuu Kalamu1,

Hapo ndipo unagundua mgawanyo huo wa mikoa ya Mara na Mwanza ulifanyika kwa staili kama ile ya ukoloni walivyogawa Lesotho na Estwani ndani ya Afrika Kusini.

Ukerewe iliungana na mkoa wa Mara (ardhi moja) lakini ilitengwa na mkoa wa Mwanza kwa maji kwa umbali wa kilomita 54. Yaani Mwanza inaacha nchi kavu inaingia hadi majini na kuvuka maji hayo kwenda kuifuata Ukerewe ambayo imeungana kwa ardhi na mkoa wa Mara. Kwa mantiki hiyo kumbe Sultan Jamshid Bin Abdullah alikuwa sahihi kuweka mipaka ya eneo la Usultani wake kutambuka kisiwa cha Unguja, kuingia baharini na kuvamia nchi kavu ya mkoa wa Dsm hadi Kimara.
Mantiki ya Mwl Nyerere ya kukataa mipaka ya Usultani kutambuka bahari hadi Kimara na kukubali Mwanza kutambuka ziwa hadi Ukerewe ambayo iliungana na Mara inakosa mashiko, ushawishi na uwiano wa haki.

Jipange upya mkuu.
Huna hoja hata kidogo katika bandiko lako lote.
Mifano ya Lesotho na eSwatini wala haileti maana yoyote hapa, sasa sijui wewe uelewa wako upo vipi hasa.

Unaingiza "ukoloni" hapa kwa mantiki ipi? Kwani kuwepo na maji kati ya sehemu mbili katika nchi hiyo hiyo kunafanya pawe na mipaka kati yake?

Huu sio mjadala ninaoweza kupoteza muda wangu nao.
 
Haikuwahi kuwa, sasa tunataka iwahi kuwa sehemu ya Mara. Nadhani tuwaulize Wanaukerewe kwa njia ya referendum wanataka wawe Mwanza au Mara?
Wewe ndiye msemaji wa hao wana Ukerewe?

Kama kweli ndio wamekutuma upuuzi huu watakuwa wamepungukiwa akili kichwani. Inaonekana siku hizi 'furu' (samaki wadogo) wamekuwa adimu na akili za hao wakerewe zimepotea kama wewe ni mmoja wao; na tena wanakuamini kuwa na mawazo mgando kama haya.
 
Madhara ya mabadilikko ya tabia ya nchi hayo
"Mabadiliko Tabia Nchi" yamekuwepo karne na karne, hayakuanza leo na hayatakoma kesho!

Linalowezekana ni kuya'manage' tu, kasi yake, lakini hayazuiiliki; na wala huwezi kuyarudisha kama yalivyokuwa miaka 200 iliyopita.
 
Mikoa mikubwa ilisaidia sana kuondoa tatizo la ukabila. Wanavyoendelea kumega mikoa mikoa inageuka kuwa vipande vya kabila moja tu. Walipogawa mkoa wa Pwani na kuondoa Dar sijawahi kuona maendeleo ya ziada kwa sababu ya kugawa mkoa.
Ni kweli maana hyo ina encourage ukabila tu wa Bure tu nchini na kila kiongozi atakuwa ana mega mkoa na ku favor sehemu yake. Serikali ipeleke maendeleo Hadi ngazi ya chini kabisa sio kugawa gawa nchi kwa vi portion yasije kutokea mambo ya Ethiopia sasa
 
Back
Top Bottom