Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

We jamaa umekomaa lakini naona huna uangalifu. Mkoa wa Kagera mwanzoni uliitwa Bukoba baadaye ukawa Ziwa magharibi na sasa Kagera.
Mmhhh wewe historia yako ulisomea wapi..ndio maana yule jamaa alisema historia iandikwe upya.
 
Ukabila unawatesa sana Watanzania kwa sasa kuliko wakato wowote. Kwa kuwa Wakerewe na Wakara wanasikilizana kilugha na Wajita wa Bunda ndio maana mnatamani sana hili litokee bila kuzingatia Wazinza, Walongo na Wasumbwa nao wana nasaba na nchi jirani za Uganda na Rwanda.

Kwa busara na kuzingatia upunguzaji wa gharama za kiutawala na mzigo kwa walipa kodi ingekuwa ni vyema kubadili tu jina la mkoa wa Geita na kuwa mkoa wa Chato ila makao yake makuu kuwa Geita kwa kumega kipande cha wilaya y a Sengerema ili kuepuka kuanzisha mkoa mpya.

Wilaya ya Kwimba ni mfano ulio hai kwa kuwa makao yake makuu yako Ngudu. Viongozi na wanannchi waanche ubinafsi kwamba lia kiongozi atokeapo paanzishwe mkoa sio vizuri mnawabebesha wananchi mzigo usiowahusu na hauna tija.

Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi
Mkuu,
Mimi nashangaa sana hata mgawanyo wa mkoa wa Morogoro ulivyo. Mvomero umeukalia vibaya Kilosa na Kilombero umeukalia vibaya Ulanga. Mwananchi wa kutoka Kilosa Kaskazini analazimika kupitia Mvomero au azunguke Kilosa Kusini ndipo afike makao makuu ya Mkoa, vilevile mwananchi wa Ulanga analazimika kuvuka Kilombero kufika makao makuu ya Mkoa. Eti hata Mzumbe ile iko Mvomero badala ya Morogoro Mjini??!!

Location-of-the-five-districts-within-Morogoro-region-Tanzania.png

Taswira kwa hisani ya Google
 
Sio kweli Asili ya uanzishwaji wa mkoa wa Katavi ni wilaya Nkasi ambayo tangu uhuru ilidumaa kimaendeleo ikiwemo miundo mbinu na huduma za jamii ukizingatiwa ni eneo lililokuwa limevamiwa na wafugaji na baadae baadhi ya wakimbizi badaada ya serikali kukubali kuwasajili uraia walichagua kuishi huko. Eneo kubwa la mkoa wa Katavi lilitokana na mkoa wa Rukwa, eneo la kusini mwa mkoa wa Kigoma na kipande kidogo kutoka mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Urambo kusini.

Hata hivyo pamoja na wanasiasa kulenga maslahi yao bado mkoa wa Tabora ndio mkubwa kuliko mikoa mingine hapo Tanzania
Sikusema Katavi imetokana na Tabora, nimesema Tabora ilimegwa (ikimaanisha pamoja na wilaya zingine za mikoa mingine) kupata mkoa wa Katavi, sasa kwa kuwa mafahari wawili hawalali zizi moja Kapuya imebidi aangukie Katavi na Sitta abakie Tabora.
 
kwa hela gani kwa mfano? tuanze kuunganisha sehemu ambayo meli zinaweza kwenda? badala ya kuboresha reli na bandari indian ocean?
Kifo cha majini na barabarani kipi kina uhakika wa kupata miili ya marehemu kirahisi? Tunaoishi ziwani ndiyo tunajuwa!
 
Chalinze tayari ni wilaya nenda ukapate huduma ofisi ziko mubshara barabarani kabisa kabla hujafika kiji cha Msolwa ndipo makao yake makuu yapo. JPM alikamilisha kitambo ila wanavuta muda ili wadai eti SSH ndio kaijenga. Na wilaya ya Bagamoyo iliongezewa eneo kutoka Tanga wilaya ya Muheza, Handeni na Pangani. Zamani Bagamoyo ilikuwa inaishia mto Wami kwa ng'ambo ya pili lakini kwa sasa unaenda vijiji zaidi ya vinne ndipo unakuta mpaka wake, Mbwewe na Kimange
Baghosha!
 
Sikusema Katavi imetokana na Tabora, nimesema Tabora ilimegwa (ikimaanisha pamoja na wilaya zingine za mikoa mingine) kupata mkoa wa Katavi, sasa kwa kuwa mafahari wawili hawalali zizi moja Kapuya imebidi aangukie Katavi na Sitta abakie Tabora.
Acha uongo wilaya ya Kaliua haiko Katavi bali iko Tabora ambako ndiiko alikuwa mbunge Kapuya baadae katolewa na mama mmoja kutoka CUF Magdalena Sakaya
 
Mkuu

hiyo ramani uliyotoa ni ya zamani kabla ya wilaya mbili kuongezwa ambazo ni Malinyi ikimegwa Kilombero na Ulanga, Morogoro vijijini ambayo inaanzia Mikese na eneo lote la mashariiki ya mlima Uluguru makao makuu yake yakihamishwa kutoka Morogoro mjini hadi kijiji cha Mvuha mpakani na pori la Selous, Kilosa pia ilimemegwa na kutengeza wilaya ya Gairo kwa hiyo mkoa una wilaya nane ambazo kijiografia hazioneshi kuwanufaisha wananchi wanapohitaji huduma za ngazi ya kimkoa.
Mkuu,
Umesahau na Ifakara (sasa ni mamlaka ya mji)
 
Acha uongo wilaya ya Kaliua haiko Katavi bali iko Tabora ambako ndiiko alikuwa mbunge Kapuya baadae katolewa na mama mmoja kutoka CUF Magdalena Sakaya
Urambo East Sitta, Urambo West Kapuya, sasa hivi kuna Jimbo la Urambo (Mhe. Margareth Simwanza Sitta), tusaidie kuitafuta Urambo West ya Kapuya imeenda wapi?
 
Usichanganye mambo Ifakara ni makao makuu ya wilaya ya Kilombero kama ilivyo Ulanga makao makuu ya wilaya ni Mahenge. Kwa hiyo hakuna wilaya ambayo sikuitaja.
Kiuchumi ina mamlaka yake kwasababu inakusanya mapato, ni Halmashauri ya Mamlaka ya Mji Mdogo (Ifakara Mji), sooner or later itakuja kuwa Wilaya ya Ifakara kama ilivyo Musoma Mjini na Musoma Vijijini, Kilombero itakuja kusimama kivyake kiutawala. Mzaha mzaha hutumbua usaha mkuu.
 
Back
Top Bottom