Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Ninakunukuu,
Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Jibu.
Mkoa wa Tabora ulimegwa kutengeneza mkoa wa Tabora kufuatia Kapuya na Sitta kuogopana, ikabidi Kapuya aangukie Katavi.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi.

Jibu.
Hakuna serikali inagawa mikoa yenyewe, serikali inaweka vigezo, wanaoomba mikoa igawanywe ni wananchi wenyewe alafu serikali inaangalia kama vigezo vinatimia, visipotimia hata wananchi wakiandamana hawapewi mkoa.
We mtu unajiandikia tu kila kinachopita kwenye medulla yako. Hayo ndo majibu ya mtu mzima? Hata wazo na vijiramani unavyoonesha kwenye thrd ni kama huna historia ya nchi hii na huna muda au uelewa na kutafuta historia halisi ya ukerewe. Huko kwenu? Mbona hujitambui kama sisi tulio nje ya kisiwa?

Historia ya ukerewe kuwekwa mkoa wa Mwanza ni sawa na upareni kuwekwa Kilimanjaro. Sasa fanya homework yako kujua sababu maana kuna watu munashinda mitandaoni kuangalia ngono tu!
 
Ukabila unawatesa sana Watanzania kwa sasa kuliko wakato wowote. Kwa kuwa Wakerewe na Wakara wanasikilizana kilugha na Wajita wa Bunda ndio maana mnatamani sana hili litokee bila kuzingatia Wazinza, Walongo na Wasumbwa nao wana nasaba na nchi jirani za Uganda na Rwanda.

Kwa busara na kuzingatia upunguzaji wa gharama za kiutawala na mzigo kwa walipa kodi ingekuwa ni vyema kubadili tu jina la mkoa wa Geita na kuwa mkoa wa Chato ila makao yake makuu kuwa Geita kwa kumega kipande cha wilaya y a Sengerema ili kuepuka kuanzisha mkoa mpya.

Wilaya ya Kwimba ni mfano ulio hai kwa kuwa makao yake makuu yako Ngudu. Viongozi na wanannchi waanche ubinafsi kwamba lia kiongozi atokeapo paanzishwe mkoa sio vizuri mnawabebesha wananchi mzigo usiowahusu na hauna tija.

Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi
Usihangaike sana na Chato, tatizo kubwa kabisa ni Mkoa wa Katavi. Pinda atueleze aliwaza nini? mkoa wenye wakaazi wasiofika laki 4! Na hapo alitaka kuongeza ukubwa kwa kumega urambo, ikashindikana maana Urambo ndo historia ya Tabora yenyewe. Kwa ujumla kumega na kugawa mikoa ni ushamba tu wa viongozi wetu.
 
Ninakunukuu,
Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Jibu.
Mkoa wa Tabora ulimegwa kutengeneza mkoa wa Katavi kufuatia Kapuya na Sitta kuogopana, ikabidi Kapuya aangukie Katavi.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi.

Jibu.
Hakuna serikali inagawa mikoa yenyewe, serikali inaweka vigezo, wanaoomba mikoa igawanywe ni wananchi wenyewe alafu serikali inaangalia kama vigezo vinatimia, visipotimia hata wananchi wakiandamana hawapewi mkoa.
Sio kweli Asili ya uanzishwaji wa mkoa wa Katavi ni wilaya Nkasi ambayo tangu uhuru ilidumaa kimaendeleo ikiwemo miundo mbinu na huduma za jamii ukizingatiwa ni eneo lililokuwa limevamiwa na wafugaji na baadae baadhi ya wakimbizi badaada ya serikali kukubali kuwasajili uraia walichagua kuishi huko. Eneo kubwa la mkoa wa Katavi lilitokana na mkoa wa Rukwa, eneo la kusini mwa mkoa wa Kigoma na kipande kidogo kutoka mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Urambo kusini.

Hata hivyo pamoja na wanasiasa kulenga maslahi yao bado mkoa wa Tabora ndio mkubwa kuliko mikoa mingine hapo Tanzania
 
Mkuu,
Mwl hakuitendea mkoa wa Mara haki kwa kuchukuwa Ukerewe kuipeleka Mwanza. Hii siyo #haki, inabidi Ukerewe irudishwe Mara kwasababu JPM aliwaahidi Mwanza kwamba atawapa Wilaya nyingine, basi Ukerewe irejeshwe kwenye asili yake (Mara).
Ukerewe haijawahi kuwa upande wa Mara. Zamani kulikuwa hakuna mikoa na ilirithiwa kutoka kwa wakoloni ni majimbo ambapo huko kulikuwa kunajulikana ni 'Lake Province' baadae ikagawanywa na kuwa mikoa mitatu Mwanza, Mara, Ziwa Magharibi (kwa sasa Kagera) na Shinyanga.

Tangu hapo Ukerewe ilikuwa ni sehemu ya Mwanza
 
Sio kweli Asili ya uanzishwaji wa mkoa wa Katavi ni wilaya Nkasi ambayo tangu uhuru ilidumaa kimaendeleo ikiwemo miundo mbinu na huduma za jamii ukizingatiwa ni eneo lililokuwa limevamiwa na wafugaji na baadae baadhi ya wakimbizi badaada ya serikali kukubali kuwasajili uraia walichagua kuishi huko. Eneo kubwa la mkoa wa Katavi lilitokana na mkoa wa Rukwa, eneo la kusini mwa mkoa wa Kigoma na kipande kidogo kutoka mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Urambo kusini.

Hata hivyo pamoja na wanasiasa kulenga maslahi yao bado mkoa wa Tabora ndio mkubwa kuliko mikoa mingine hapo Tanzania
Tabora na Morogoro wanakaribiana kwa ukubwa.
Angalia maeneo yalivyoharibiwa kwa tamaa za kisiasa na ukabila.
Iringa --> Njombe+ Iringa
Mbeya --> Mbeya + Songwe
Sumbawanga --> Sumbawanga + Katavi
Arusha --> Arusha + Manyara
Mwanza --> Mwanza + Geita
Shinyanga --> Shinyanga + Simiyu
Pwani --> Pwani + Dar es Salaam

Lakini tusisahau yalianza zamani Mkowa wa Mtwara > Mtwara + Lindi
Iko siku kila wilaya ya leo itakuwa mkoa.
 
Ukerewe haijawahi kuwa upande wa Mara. Zamani kulikuwa hakuna mikoa na ilirithiwa kutoka kwa wakoloni ni majimbo ambapo huko kulikuwa kunajulikana ni 'Lake Province' baadae ikagawanywa na kuwa mikoa mitatu Mwanza, Mara, Ziwa Magharibi (kwa sasa Kagera) na Shinyanga.

Tangu hapo Ukerewe ilikuwa ni sehemu ya Mwanza
We jamaa umekomaa lakini naona huna uangalifu. Mkoa wa Kagera mwanzoni uliitwa Bukoba baadaye ukawa Ziwa magharibi na sasa Kagera.
 
Tabora na Morogoro wanakaribiana kwa ukubwa.
Angalia maeneo yalivyoharibiwa kwa tamaa za kisiasa na ukabila.
Iringa > Njombe+ Iringa
Mbeya > Mbeya + Songwe
Sumbawanga > Sumbawanga + Katavi
Arusha > Arusha + Manyara
Mwanza > Mwanza + Geita
Shinyanga > Shinyanga + Simiyu

Lakini tusisahau yalianza zamani Mkowa wa Mtwara > Mtwara + Lindi
Iko siku kila wilaya ya leo itakuwa mkoa.
Kuna wilaya kongwe hapo Tanzania kama Nzega, Kilosa hazijawahi kuomba kuwa mikoa, maendeleo yao yako duni hadi leo ukiacha Nzega kwa sasa ilishafunguka vizuri baada ya kupata wabunge wanaojitambua kupigania masalahi ya wananchi wake. Igunga ni moja ya wilaya za muda mrefu lakini maendeleo yake ni duni sana na imetoa viongozi wengi tu bila kuiboresha kulingana jigrafia ya eneo ilipo njiani mwa barabara kuu ya Singida-Dom-Dar-Mwanza

Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi kwenye mkoa wa Morogoro ndio zenye changamoto kubwa sana ya barabara na huduma za kiutawala kutoka makao makuu ya mkoa. Barabara ya lami inaishia kiwanda cha sukari Kilombero baada ya hapo zaidi ya kilomita 200 ni za vumbi zikiwa na mashimo makubwa kana kwamba haichangiii chochote kwenye uchumi wa mkoa na nchi!!!
 
We jamaa umekomaa lakini naona huna uangalifu. Mkoa wa Kagera mwanzoni uliitwa Bukoba baadaye ukawa Ziwa magharibi na sasa Kagera.
Hata hiyo anayosema hakukuwa na wilaya siyo kweli, wilaya zilikuwepo na Ma-DC waliitwa AREA COMMISSIONERS, Tarime ilikuwa North Mara District. Babake JK alikuwa Area Commissioner pia. Walikuwepo weusi na weupe mfano babake Jenerali John Butler Walden wa TPDF (deceased) babake alikuwa Area Commissioner wa Tunduru aliitwa Stanley Walden na mamake Violet Nambela Mnyakyusa.
 
kwa hela gani kwa mfano? tuanze kuunganisha sehemu ambayo meli zinaweza kwenda? badala ya kuboresha reli na bandari indian ocean?
 
Kuna wilaya kongwe hapo Tanzania kama Nzega, Kilosa hazijawahi kuomba kuwa mikoa, maendeleo yao yako duni hadi leo ukiacha Nzega kwa sasa ilishafunguka vizuri baada ya kupata wabunge wanaojitambua kupigania masalahi ya wananchi wake. Igunga ni moja ya wilaya za muda mrefu lakini maendeleo yake ni duni sana na imetoa viongozi wengi tu bila kuiboresha kulingana jigrafia ya eneo ilipo njiani mwa barabara kuu ya Singida-Dom-Dar-Mwanza

Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi kwenye mkoa wa Morogoro ndio zenye changamoto kubwa sana ya barabara na huduma za kiutawala kutoka makao makuu ya mkoa. Barabara ya lami inaishia kiwanda cha sukari Kilombero baada ya hapo zaidi ya kilomita 200 ni za vumbi zikiwa na mashimo makubwa kana kwamba haichangiii chochote kwenye uchumi wa mkoa na nchi!!!
Mkuu,
Siyo hoja sana isipokuwa hapo Morogoro mimi napata shida sana kwa jinsi mgawanyo wa Wilaya ya Mvomero ulivyokuwa. Imepenyezwa katikati ikagusa Kilosa, Morogoro Mjini na Morogoro. Mtu wa kutoka Kaskazini ya Kilosa akitaka kupata huduma za ngazi ya Mkoa analazimika kupita wilaya nyingine ya Mvomero ndipo afike makao makuu ya Mkoa au azunguke hadi Kusini ya Kilosa kwanza kuikabili makao makuu ya Mkoa. Eti Mzumbe ile iko Mvomero??!!
Location-of-the-five-districts-within-Morogoro-region-Tanzania.png

Taswira kwa hisani ya Google
 
Mkuu,

Peleka na hili:

Wilaya ya Mafia ipewe mkoa wa Dsm toka mkoa wa Pwani. Tayari Pwani imeongezewa Wilaya ya Kibiti na mipango iko mbioni kuanzishiwa Wilaya ya Chalinze.
Chalinze tayari ni wilaya nenda ukapate huduma ofisi ziko mubshara barabarani kabisa kabla hujafika kiji cha Msolwa ndipo makao yake makuu yapo. JPM alikamilisha kitambo ila wanavuta muda ili wadai eti SSH ndio kaijenga. Na wilaya ya Bagamoyo iliongezewa eneo kutoka Tanga wilaya ya Muheza, Handeni na Pangani. Zamani Bagamoyo ilikuwa inaishia mto Wami kwa ng'ambo ya pili lakini kwa sasa unaenda vijiji zaidi ya vinne ndipo unakuta mpaka wake, Mbwewe na Kimange
 
Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mwanza
600px-Mwanza-Ukerewe.svg.png

Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mara (Bunda)
R.35716408d9461e35572cefe94851db0c

Hoja:
1. Ukerewe iko jirani na mkoa wa Mara kuliko mkoa wa Mwanza.
2. Ninadhani Ukerewe iondolewe mkoa wa Mwanza ipelekwe mkoa wa Mara.
3. Kama tumeweza kujenga Nyerere Bridge Kigamboni-Kurasini, Tanzanite Bridge, Magufuli Bridge (Kigongo Busisi) hatuwezi kushindwa kwa baadaye hali ya bajeti ikiruhusu kujenga daraja kuunganisha Bunda na Ukerewe. Marehemu Tom Mboya ali-reclaim land na kuunganisha nchi kavu na kisiwa cha Rusinga alikozaliwa.

Kisiwa cha Rusinga kikiwa kimeunganishwa na nchi kavu sehemu ya Mbita.

91908541f6580e0246a9ec0cd25446f2.jpg

Taswira zote kwa hisani ya Google.
Kwa maana hii
1-kibaha tuipeleke morogoro
2-bagamoyo -tanga
3 -mkuranga Lindi
Si ndio mkuu!!??
 
Mkuu,
Siyo hoja sana isipokuwa hapo Morogoro mimi napata shida sana kwa jinsi mgawanyo wa Wilaya ya Mvomero ulivyokuwa. Imepenyezwa katikati ikagusa Kilosa, Morogoro Mjini na Morogoro. Mtu wa kutoka Kaskazini ya Kilosa akitaka kupata huduma za ngazi ya Mkoa analazimika kupita wilaya nyingine ya Mvomero ndipo afike makao makuu ya Mkoa au azunguke hadi Kusini ya Kilosa kwanza kuikabili makao makuu ya Mkoa. Eti Mzumbe ile iko Mvomero??!!
Location-of-the-five-districts-within-Morogoro-region-Tanzania.png

Taswira kwa hisani ya Google
Mkuu

hiyo ramani uliyotoa ni ya zamani kabla ya wilaya tatu kuongezwa ambazo ni Malinyi ikimegwa Kilombero na Ulanga, Morogoro vijijini ambayo inaanzia Mikese na eneo lote la mashariiki ya mlima Uluguru makao makuu yake yakihamishwa kutoka Morogoro mjini hadi kijiji cha Mvuha mpakani na pori la Selous, Kilosa pia ilimemegwa na kutengeza wilaya ya Gairo kwa hiyo mkoa una wilaya nane ambazo kijiografia hazioneshi kuwanufaisha wananchi wanapohitaji huduma za ngazi ya kimkoa.
 
Back
Top Bottom