Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Ukerewe haijawahi kuwa upande wa Mara. Zamani kulikuwa hakuna mikoa na ilirithiwa kutoka kwa wakoloni ni majimbo ambapo huko kulikuwa kunajulikana ni 'Lake Province' baadae ikagawanywa na kuwa mikoa mitatu Mwanza, Mara, Ziwa Magharibi (kwa sasa Kagera) na Shinyanga.

Tangu hapo Ukerewe ilikuwa ni sehemu ya Mwanza
Makao makuu ya mkoa wa Mara yako karibu na wananchi wa Ukerewe kuliko makao makuu ya mkoa wa Mwanza ambao ndiyo mkoa unaohudumia wilaya ya Ukerewe.
 
Tupe mchanganuo wa faida tafadhali.
Zamani kabla Tom Mboya haja-reclaim Rusinga kuiunganisha na Mbita iliyoko nchi kavu, mtu alisoma shule chekechea (zamani bush) hadi form six hajaona gari kwa macho yake, anaenda kuonea Mbita, na maghorofa anakwenda kuyaona Nairobi University.

Aidha, kuna Wakara na Wakerewe hata na Wajita wanaweza kuogelea toka Buguma Bunda hadi Ramukoko Ukerewe lakini hawawezi kufanya hivyo toka Ukerewe hadi mwaloni Ilemela Mwanza.
 
Hivi unajua ni km ngapi hapo au unaongea,
Sawa ,humu tunaongeza tu lakini serikali ukitafakari gharama za mameri na vivuko , lakini pia kunaweza kuanzishwa eneo la utalii au watu kwenda kupumzika huko , hii ni kutokana na.mazingira ya kisiwa hicho, upo uwezekano watu wakatoka nchi jirani katika ukanda wetu achiliia mbali kutoka nje ya ukanda huu. Lakini kikubwa zaidi ni kuwarahisishia wananchi wa ukerewe na majirani zao usafiri kwenda na kutoka visiwani mwao.
 
JK alizimikiwa kivuko katikati ya ziwa kuelekea Ukerewe. SSH jenga daraja au reclaim ardhi kama Tom Mboya kule Rusinga.
 
Siyo kwamba ni karibu zaidi mtu wa Ukerewe kwenda Mwanza ukilinganisha na kwenda Musoma? Makao makuu ya mikoa hiyo miwili!
 
Tupe mchanganuo wa faida tafadhali.
Inadhaniwa (tafiti hazijafanyika) kwamba Ukerewe inayoundwa na visiwa 38 (archipelago of 38) ni sehemu pekee duniani (tena ndogo sana 530 km2 (200 sq mi)) ambayo imezalisha wanazuoni wa kiwango cha Uprofesa wapato 70 hadi mwongo mmoja uliopita 2011 - 2021.
 
Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mwanza
600px-Mwanza-Ukerewe.svg.png

Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mara (Bunda)
R.35716408d9461e35572cefe94851db0c

Hoja:
1. Ukerewe iko jirani na mkoa wa Mara kuliko mkoa wa Mwanza.
2. Ninadhani Ukerewe iondolewe mkoa wa Mwanza ipelekwe mkoa wa Mara.
3. Kama tumeweza kujenga Nyerere Bridge Kigamboni-Kurasini, Tanzanite Bridge, Magufuli Bridge (Kigongo Busisi) hatuwezi kushindwa kwa baadaye hali ya bajeti ikiruhusu kujenga daraja kuunganisha Bunda na Ukerewe. Marehemu Tom Mboya ali-reclaim land na kuunganisha nchi kavu na kisiwa cha Rusinga alikozaliwa.

Kisiwa cha Rusinga kikiwa kimeunganishwa na nchi kavu sehemu ya Mbita.

91908541f6580e0246a9ec0cd25446f2.jpg

Taswira zote kwa hisani ya Google.
Kuna kitabu cha Kiingereza nilikisoma zamani miaka ya 1990s (nilikiazima kutoka kwa Padri Roki Katabure, aliyekuwa paroko wa Parokia ya Itira kwa miaka mingi sana huko nyuma) kinasema miaka ya nyuma sehemu (ambayo kwa sasa imefunikwa na maji) kati ya ya bara na Ukerewe ilikuwa 'marsh area'. Na watu kutoka Ukerewe walikuwa wakienda upande wa bara kwa mguu na watu wa bara walikuwa pia wakienda Ukerewe kwa mguu. Hata wanyama kama simba, fisi, tembo na wanyama wengine kutoka Mbuga ya Serengeti walikuwa wakati ule wakitafuta malisho hadi Ukerewe. Wajerumani mwaka 1917 (sikumbuki vizuri kama ni mwaka huu kweli au la, lakini nakumbuka kusoma hivyo) walichimba 'channel' ili iwe rahisi kusafiri kutoka Mwanza kwenda Musoma kwa njia ya mkato kwa boat kupitia 'channel' hii kuliko kuzunguka sehemu ile nyingine ya Ukerewe. Na mwaka 1954 wakati wa ujenzi wa Owen Falls nchini Uganda, kina cha maji ya Ziwa Victoria kiliongezeka na miaka ya 1960s (nadhani miezi kadhaa kabla ya uhuru kulikuwa na mvua kubwa sana inayojulikana Ukerewe kama "Mvua ya Uhuru". Hivyo, kina cha maji kilipoongezeka eneo hili (marsh area) lilianza kumezwa na maji na kutokana na water erosion, baadhi ya sehemu za upande wa Ukerewe na wa bara ziliendelea kufunikwa na maji. Kwa sasa ukiwa upande wa Ukerewe au bara huwezi kuona watu upande ule au huu isipokuwa majengo tu. Hii inaonyesha water erosion iliyofanyika ni kubwa sana na kwa pontoon kama sikosei ni ama mwendo wa nusu saa au zaidi (sikumbuki maana ni muda mrefu sana sijasafiri kupitia njia hii ya pontoon).
 
Siyo kwamba ni karibu zaidi mtu wa Ukerewe kwenda Mwanza ukilinganisha na kwenda Musoma? Makao makuu ya mikoa hiyo miwili!
Ukerewe hadi Mwanza ni 54 km kwa njia ya majini, Ukerewe hadi Musoma Mjini kupitia Bunda ambako ni mzunguko ni 183 km kwa barabara, Ukerewe (Nansio) hadi Kibara na Musoma Mjini kupitia majini ni 3.8 km. Ukitokea Ukerewe hadi Bunda na kwenda Mwanza kwa barabara ni mbali zaidi ya kutoka Ukerewe hadi Musoma kupitia Bunda kwa barabara.
 
Madhali Jimbo lipo kwenye mikono ya CCM we hope they will do something kama legacy ya mama na kwa heshima ya Baba wa Taifa!
 
Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mara (Bunda)
Mkuu 'Douglas Majwala' kuunganika kwa ardhi siyo hoja ya sehemu sehemu moja kuwa kwenye mkoa mwingine.

Kwani wewe hujui kwamba Ukerewe ilikuwa imeunganika na nchi kavu hadi miaka ya 60 tu (1961) watu walikuwa wanavuka kwa miguu toka Ukewrewe kwenda Mwibara na Bunda; lakini bado ilikuwa ni wilaya katika mkoa wa Mwanza? Mtemi wa Ukerewe alikuwa na eneo hadi sehemu za huko nchi kavu Mara na hata visiwa vilivyoko Mara sasa hivi kama Irugwa ilikuwa ni sehemu ya Ukerewe.

Kwa hiyo hoja yako haina mashiko.
 
Ukerewe hadi Mwanza ni 54 km kwa njia ya majini, Ukerewe hadi Musoma Mjini kupitia Bunda ambako ni mzunguko ni 183 km kwa barabara, Ukerewe (Nansio) hadi Kibara na Musoma Mjini kupitia majini ni 3.8 km. Ukitokea Ukerewe hadi Bunda na kwenda Mwanza kwa barabara ni mbali zaidi ya kutoka Ukerewe hadi Musoma kupitia Bunda kwa barabara.
Kwa kuwa Mwanza ni karibu zaidi kuliko Musoma, naona ni bora zaidi ukerewe ibaki mwanza ili kupunguza usumbufu wa kusafiri mwendo mrefu kwenda mkoani. Kuwe tu na usafiri wa uhakika wa meli Nansio - Mwanza.
 
Ukerewe hadi Mwanza ni 54 km kwa njia ya majini, Ukerewe hadi Musoma Mjini kupitia Bunda ambako ni mzunguko ni 183 km kwa barabara, Ukerewe (Nansio) hadi Kibara na Musoma Mjini kupitia majini ni 3.8 km. Ukitokea Ukerewe hadi Bunda na kwenda Mwanza kwa barabara ni mbali zaidi ya kutoka Ukerewe hadi Musoma kupitia Bunda kwa barabara.
Hizi kilometer 3.8 umezipima tokea wapi mkuu? Haiwezekani kwa kila njia!
 
Mkuu,
Mwl hakuitendea mkoa wa Mara haki kwa kuchukuwa Ukerewe kuipeleka Mwanza. Hii siyo #haki, inabidi Ukerewe irudishwe Mara kwasababu JPM aliwaahidi Mwanza kwamba atawapa Wilaya nyingine, basi Ukerewe irejeshwe kwenye asili yake (Mara).
Huu ni upotoshaji, tena wa kijinga kabisa.
Ukerewe toka ukoloni haijawahi kuwa sehemu ya mkoa wa Mara.
 
Back
Top Bottom