Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Tuunganishe Ukerewe na nchi kavu

Ukabila unawatesa sana Watanzania kwa sasa kuliko wakato wowote. Kwa kuwa Wakerewe na Wakara wanasikilizana kilugha na Wajita wa Bunda ndio maana mnatamani sana hili litokee bila kuzingatia Wazinza, Walongo na Wasumbwa nao wana nasaba na nchi jirani za Uganda na Rwanda.

Kwa busara na kuzingatia upunguzaji wa gharama za kiutawala na mzigo kwa walipa kodi ingekuwa ni vyema kubadili tu jina la mkoa wa Geita na kuwa mkoa wa Chato ila makao yake makuu kuwa Geita kwa kumega kipande cha wilaya y a Sengerema ili kuepuka kuanzisha mkoa mpya.

Wilaya ya Kwimba ni mfano ulio hai kwa kuwa makao yake makuu yako Ngudu. Viongozi na wanannchi waanche ubinafsi kwamba lia kiongozi atokeapo paanzishwe mkoa sio vizuri mnawabebesha wananchi mzigo usiowahusu na hauna tija.

Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi
Nakataa wazo la kuipeleka Ukerewe mkoa wa Mara, lakini kutangeneza daraja pale Ngoma/Kisorya ni wazo la msingi sana. Ukerewe inafanya biashara ya chakula na mkoa wa Mara kuliko Mwanza. Ukweli ni kwamba mkoa wa Mara unaitegemea UK kwa chakula kwa kiwango kikubwa na wao hawawezi kukanusha hili. Kwa upande wa Mwanza ni rahisi kwenda kwa meli kuliko kutumia hii barabara ya kupita Bunda kwani itahitaji masaa 5 wakati kwa meli ni masaa 2.30 hadi 3 na kama italetwa fast ferry itatumia saa 1 tu.
 
Sisi tuna jenga bandari bagamoyo kwanza
Tayari!!
IMG-20211106-WA0000.jpg
 
Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mwanza
600px-Mwanza-Ukerewe.svg.png

Ukaribu wa Ukerewe na mkoa wa Mara (Bunda)
R.35716408d9461e35572cefe94851db0c

Hoja:
1. Ukerewe iko jirani na mkoa wa Mara kuliko mkoa wa Mwanza.
2. Ninadhani Ukerewe iondolewe mkoa wa Mwanza ipelekwe mkoa wa Mara.
3. Kama tumeweza kujenga Nyerere Bridge Kigamboni-Kurasini, Tanzanite Bridge, Magufuli Bridge (Kigongo Busisi) hatuwezi kushindwa kwa baadaye hali ya bajeti ikiruhusu kujenga daraja kuunganisha Bunda na Ukerewe. Marehemu Tom Mboya ali-reclaim land na kuunganisha nchi kavu na kisiwa cha Rusinga alikozaliwa.

Kisiwa cha Rusinga kikiwa kimeunganishwa na nchi kavu sehemu ya Mbita.

91908541f6580e0246a9ec0cd25446f2.jpg

Taswira zote kwa hisani ya Google.
Huu ni ukweli kabisa kuna muingiliano mkubwa sana wa kundugu kati ya ukerewe na wilaya za mkoa Mara kama bunda na Musoma vijijini
 
Usihangaike sana na Chato, tatizo kubwa kabisa ni Mkoa wa Katavi. Pinda atueleze aliwaza nini? mkoa wenye wakaazi wasiofika laki 4! Na hapo alitaka kuongeza ukubwa kwa kumega urambo, ikashindikana maana Urambo ndo historia ya Tabora yenyewe. Kwa ujumla kumega na kugawa mikoa ni ushamba tu wa viongozi wetu.
Mwanzonk hata Mimi nilikuwa siungi mkono Katavi kuwa mkoa. Lakini baada ya kufika Rukwa na hatimaye Katavi kwa kazi zangu za uandishi nilikualiaa na wazo la kuipa hadhi ya mkoa. Awali mkoa wa Rukwa uliundwa na wilaya za Sumbawanga, Nkasi na Mpanda. Lakini ukichukua Sumbawanga na Nkasi kwa pamoja zinazidiwa kwa mbali na Mpanda. Lakini Jiografia ya Mpanda ilikuwa inawatesa sana wakazi wa wilaya ile. Katikati ya Mpanda na Nkasi kuna mbuga ya Katavi na hifadhi ya Lwafi ambazo zinatengeneza umbali wa km 160 hivi bila makazi yoyote. Lakini kutoka Mpanda hadi Sumbawanga ni zaidi ya km 250. Yaani mtu anatoka makao makuu ya wilaya kwenda mkoani km 250 ilikuwa mateso kwa wananchi.
 
Mkuu 'Douglas Majwala' kuunganika kwa ardhi siyo hoja ya sehemu sehemu moja kuwa kwenye mkoa mwingine.

Kwani wewe hujui kwamba Ukerewe ilikuwa imeunganika na nchi kavu hadi miaka ya 60 tu (1961) watu walikuwa wanavuka kwa miguu toka Ukewrewe kwenda Mwibara na Bunda; lakini bado ilikuwa ni wilaya katika mkoa wa Mwanza? Mtemi wa Ukerewe alikuwa na eneo hadi sehemu za huko nchi kavu Mara na hata visiwa vilivyoko Mara sasa hivi kama Irugwa ilikuwa ni sehemu ya Ukerewe.

Kwa hiyo hoja yako haina mashiko.
Mkuu Kalamu1,

Hapo ndipo unagundua mgawanyo huo wa mikoa ya Mara na Mwanza ulifanyika kwa staili kama ile ya ukoloni walivyogawa Lesotho na Estwani ndani ya Afrika Kusini.

Ukerewe iliungana na mkoa wa Mara (ardhi moja) lakini ilitengwa na mkoa wa Mwanza kwa maji kwa umbali wa kilomita 54. Yaani Mwanza inaacha nchi kavu inaingia hadi majini na kuvuka maji hayo kwenda kuifuata Ukerewe ambayo imeungana kwa ardhi na mkoa wa Mara. Kwa mantiki hiyo kumbe Sultan Jamshid Bin Abdullah alikuwa sahihi kuweka mipaka ya eneo la Usultani wake kutambuka kisiwa cha Unguja, kuingia baharini na kuvamia nchi kavu ya mkoa wa Dsm hadi Kimara.
Mantiki ya Mwl Nyerere ya kukataa mipaka ya Usultani kutambuka bahari hadi Kimara na kukubali Mwanza kutambuka ziwa hadi Ukerewe ambayo iliungana na Mara inakosa mashiko, ushawishi na uwiano wa haki.

Jipange upya mkuu.
 
Ukerewe haijawahi kuwa upande wa Mara. Zamani kulikuwa hakuna mikoa na ilirithiwa kutoka kwa wakoloni ni majimbo ambapo huko kulikuwa kunajulikana ni 'Lake Province' baadae ikagawanywa na kuwa mikoa mitatu Mwanza, Mara, Ziwa Magharibi (kwa sasa Kagera) na Shinyanga.

Tangu hapo Ukerewe ilikuwa ni sehemu ya Mwanza
Na kwa msaada tu viunga vya kisorya navyo vilikuwa ukerewe baadae ndo vikapelekwa bunda.
 
Makao makuu ya mkoa wa Mara yako karibu na wananchi wa Ukerewe kuliko makao makuu ya mkoa wa Mwanza ambao ndiyo mkoa unaohudumia wilaya ya Ukerewe.

Makao makuu ya mkoa wa Mara yako karibu na wananchi wa Ukerewe kuliko makao makuu ya mkoa wa Mwanza ambao ndiyo mkoa unaohudumia wilaya ya Ukerewe.
Siyo kweli. Musoma to Nansio ni mbali kuliko mwanza jiji to nansio. Panda basi kutoka musoma had ukerewe na mwingine apande boti ya mwendokasi kutoka mwanza to nansio uone. Anaetoka mwanza utakuta ameshamaliza kula na kuoga.
 
Ukerewe is the fifth-largest lake island in the world. With an area of 530 km2 (200 sq mi), it is also the main island in lake victoria and the largest lake island in Africa. Ukerewe Island is located in the ukerewe district of Tanzania, 45 km north of Mwanza to which it is linked by ferry. A ferry crossing of 3.8 km (2.4 mi) links the island to a dirt road on the eastern lakeshore, which runs to Kibara and Musoma.
Source: UKEREWE ISLAND - Tours Northern safari in ukerewe island
 
Sio kweli Asili ya uanzishwaji wa mkoa wa Katavi ni wilaya Nkasi ambayo tangu uhuru ilidumaa kimaendeleo ikiwemo miundo mbinu na huduma za jamii ukizingatiwa ni eneo lililokuwa limevamiwa na wafugaji na baadae baadhi ya wakimbizi badaada ya serikali kukubali kuwasajili uraia walichagua kuishi huko. Eneo kubwa la mkoa wa Katavi lilitokana na mkoa wa Rukwa, eneo la kusini mwa mkoa wa Kigoma na kipande kidogo kutoka mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Urambo kusini.

Hata hivyo pamoja na wanasiasa kulenga maslahi yao bado mkoa wa Tabora ndio mkubwa kuliko mikoa mingine hapo Tanzania
Ukubwa wa eneo sio hoja..tabora eneo kubwa ni mapori..sawa na lindi...ila kanda ya ziwa ni eneo lenye watu wengi na uchumi wake unakua kwa kasi sana hivyo uhitaji wa kugawa eneo ki utawala ni mkubwa sana..Mkoa wa chato uko mbioni kajinyonge sasa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tabora na Morogoro wanakaribiana kwa ukubwa.
Angalia maeneo yalivyoharibiwa kwa tamaa za kisiasa na ukabila.
Iringa > Njombe+ Iringa
Mbeya > Mbeya + Songwe
Sumbawanga > Sumbawanga + Katavi
Arusha > Arusha + Manyara
Mwanza > Mwanza + Geita
Shinyanga > Shinyanga + Simiyu

Lakini tusisahau yalianza zamani Mkowa wa Mtwara > Mtwara + Lindi
Iko siku kila wilaya ya leo itakuwa mkoa.
Mwanza geita..shinyanga simiyu wala sio ukabila mana wote hao ni wasukuma mikoa yote hiyo..kigezo kikubwa ni wingi wa watu na ukuaji wa kiuchumi wa maeneo hayo ndio mana yakagawa ki utawala.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tunazungumzia kuunganisha aridhi sio vikojoleo.
Naona unaanza kuwa promote wake na watoto wetu kuanza kusakwa
Hata falme zilipotaka kuungana waliunganisha vikojoleo kwa kuozesha mabinti na wana wao wakiume..muunganobwa kweli ni wadamu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukerewe is the fifth-largest lake island in the world. With an area of 530 km2 (200 sq mi), it is also the main island in lake victoria and the largest lake island in Africa. Ukerewe Island is located in the ukerewe district of Tanzania, 45 km north of Mwanza to which it is linked by ferry. A ferry crossing of 3.8 km (2.4 mi) links the island to a dirt road on the eastern lakeshore, which runs to Kibara and Musoma.
Source: UKEREWE ISLAND - Tours Northern safari in ukerewe island
Kibara siyo makao makuu ya mkoa wa mara. Wilaya haiwezi kutegemea huduma za kiutawala kutoka wilaya nyingine bali kutoka makao makuu ya mkoa. Huduma za kimkoa ztakuwa mbali na halmashauri. Kupakana siyo tija bali ni uharaka wa huduma kutoka makao makuu. Ndo maana mpka leo nyerere anawazd wengi kifkra
 
Sijui unaandika ukiwa wapi. Yaani Geita iitwe Chato ? Halafu mbona unadanganya hapa kwamba Kaliua ilikuwa Kigoma. Kwa taarifa yako Kaliua ni Tabora toka enzi na enzi. Muwe mnafanya utafiti kabla ya kutoa hoja.
Ukabila unawatesa sana Watanzania kwa sasa kuliko wakato wowote. Kwa kuwa Wakerewe na Wakara wanasikilizana kilugha na Wajita wa Bunda ndio maana mnatamani sana hili litokee bila kuzingatia Wazinza, Walongo na Wasumbwa nao wana nasaba na nchi jirani za Uganda na Rwanda.

Kwa busara na kuzingatia upunguzaji wa gharama za kiutawala na mzigo kwa walipa kodi ingekuwa ni vyema kubadili tu jina la mkoa wa Geita na kuwa mkoa wa Chato ila makao yake makuu kuwa Geita kwa kumega kipande cha wilaya y a Sengerema ili kuepuka kuanzisha mkoa mpya.

Wilaya ya Kwimba ni mfano ulio hai kwa kuwa makao yake makuu yako Ngudu. Viongozi na wanannchi waanche ubinafsi kwamba lia kiongozi atokeapo paanzishwe mkoa sio vizuri mnawabebesha wananchi mzigo usiowahusu na hauna tija.

Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi
 
Ninakunukuu,
Mpaka sasa kuna mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania umenyamaza kimya (TABORA) maana haujawahi kudai kugawanywa ila uliongezewa majukumu kwa kupewa eneo la Kaliua lililokuwa kwa kiasi kikubwa kwenye mkoa wa Kigoma lakini kwa sasa ni wilaya ya mkoa wa Tabora.

Jibu.
Mkoa wa Tabora ulimegwa kutengeneza mkoa wa Katavi kufuatia Kapuya na Sitta kuogopana, ikabidi Kapuya aangukie Katavi.

Msigawe mikoa kwa kufuata asili ya wenyeji walioko maeneo hayo bali kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za kijamii na uwezo wa kiuchumi. Wanasiasa mnaharibu mstakbari wa nchi.

Jibu.
Hakuna serikali inagawa mikoa yenyewe, serikali inaweka vigezo, wanaoomba mikoa igawanywe ni wananchi wenyewe alafu serikali inaangalia kama vigezo vinatimia, visipotimia hata wananchi wakiandamana hawapewi mkoa.
Hakuna sehemu ya Tabora iliyopelekwa Katavi. Kaliua ni wilaya katika mkoa wa Tabora. Unazungumzia eneo lipi la Tabora lililopelekwa Katavi ?
 
Mkuu,
Mwl hakuitendea mkoa wa Mara haki kwa kuchukuwa Ukerewe kuipeleka Mwanza. Hii siyo #haki, inabidi Ukerewe irudishwe Mara kwasababu JPM aliwaahidi Mwanza kwamba atawapa Wilaya nyingine, basi Ukerewe irejeshwe kwenye asili yake (Mara).
Mhh. Unajua kutoka Ukerewe kwenda Musoma ni mbali sana kuliko kuja Jijini Mwanza ? Aidha nani aliyekudanganya kwamba ukerewe asili yake ni Mara ?
 
Sio kweli Asili ya uanzishwaji wa mkoa wa Katavi ni wilaya Nkasi ambayo tangu uhuru ilidumaa kimaendeleo ikiwemo miundo mbinu na huduma za jamii ukizingatiwa ni eneo lililokuwa limevamiwa na wafugaji na baadae baadhi ya wakimbizi badaada ya serikali kukubali kuwasajili uraia walichagua kuishi huko. Eneo kubwa la mkoa wa Katavi lilitokana na mkoa wa Rukwa, eneo la kusini mwa mkoa wa Kigoma na kipande kidogo kutoka mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Urambo kusini.

Hata hivyo pamoja na wanasiasa kulenga maslahi yao bado mkoa wa Tabora ndio mkubwa kuliko mikoa mingine hapo Tanzania
We acha uongo hadi sasa Nkasi ni wilaya katika mkoa wa Rukwa. Wewe unatuambia kwamba eti iko Katavi ? Aidha hakuna eneo la Wilaya Urambo lililopelekwa Katavi.
 
Back
Top Bottom