Safi kabisa mkuu, hii ndiyo michango tunayohitaji michango yenye audio visuals hadi mtu unakosa pa kukosoa. Hii ni maarifa tosha mkuu, unajibu hoja kwa hoja badala ya matusi kwa hoja. Kuhusu uchumi Ukerewe ina potentials zifuatazo:-
1. Panastahili kuwa kituo/kisiwa cha utalii wa kiuvuvi (Fishing tourism), michezo ya majini (water sports e.g. wakeskating, canoe racing) utalii wa ndege (bird tourism. Duniani kote kuna species zaidi ya 18,000 zilizotafitiwa hadi sasa, Ukerewe ikiwa na mamia ya ndege zikiwemo: raptors, songbirds, shorebirds, vultures, cranes, swans, hawks, falcons, owls, and waterfowl, wengine kwa lugha ya kwetu ni Kalamindi, Osogo, Mire, Owichkombulo, Akuru, Odhedhe, Agak, Oyundi, Arumtidi, Undhwe, nk,).
2. Ukerewe kuna utalii wa kitamaduni.
3. Ukerewe kuna Utalii wa kitafiti (Research Tourism). Ukerewe ni sehemu pekee duniani iliyotoa Maprofesa zaidi ya 70, hivyo panafaa kwa utalii wa kufanya tafiti za asili ya wanazuoni hawa.
4. Kuna aina zaidi ya 500 ya samaki, na dazani za wadudu wa ziwani wakiwemo wanyama.
5. Ukerewe inazalisha matunda aina ya maembe dodo, machungwa, mapapai, ndizi, machenza, mapera, ndimu nk na zamani ilikuwa ndiyo inasupply Kanda nzima ya Ziwa.
6. Ukerewe inalima kwa wingi zao la "Manihot esculenta Crantz" (mihogo).
7. Ukerewe inaweza kujenga hoteli za kitalii kisiwani kwenye upepo mwanana wa latitudo 1° 30’ na 3° 00’ Kusini mwa msitari wa Ikweta na longitudo 31° 45’ Mashariki na 34° 10’ Mashariki, na kwamba badala ya Watalii kulala Mwanza kwenye jotoridi wanaweza kwenda kulala Ukerewe kwa boti au gari (barabara ikijengwa kuunganisha Mara na Ukerewe). Kijiografia Ukerewe inaangalia lango la Magharibi la hifadhi ya Serengeti pale Rubana (japo sasa hivi pamepewa mkoa wa Simiyu toka Mara), lango ambalo ni kubwa lakini halijaendelezwa kama lile la Mashariki na kufanya lango la Magharibi kupokea watalii wachache sana (moja ya sababu ni kutokuwepo hoteli za hadhi ya kitalii). Lango la Magharibi la hifadhi ya Serengeti ndilo lina wanyama wengi wanaokunywa maji ya ziwa Victoria na hivyo kufanya wanyama kuwepo kwenye lango hilo mfululizo kwa mwaka bila kuhama kutafuta maji kama kule lango la Mashariki na Kaskazini wanakohama nyumbu kila mwaka kwenda Masai Mara kutafuta maji na malisho.
NB.
Nipeni U-DC bila mshahara nikaibadilishe Ukerewe.