Tujikomboe kutoka katika utumwa wa kiakili, hakuwa wa kutukomboa ili ni sisi wenyewe, hakuna mtu kutoka ughaibuni atakayeleta neema hapa nchini, ila ni kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa peke yake. Tuelimishe jamii yetu, tujifunze kutoka kwa wenzetu na kuiga yaliyo bora kwetu. Somo la kwanza waislam igeni toka kwa wakristo namna wanavyofanikisha utoaji elimu na huduma za afya. Milipewa chuo kikuu na Mkapa (Mkristo) ili mjikomboe kielimu, wakati mkisuasua kuomba misaada na kubaki kulaumu na kutengeneza uadui na wakristo, nendeni basi mkajifunze kwa wamoreviani, kanisa lenye waumini wachache lililoanzisha chuo kikuu takribani miaka 8 iliyopita jijini Mbeya, leo wana campus Tabora na D'salaam. Wanachangishana wanasonga mbele na jana walifanya tamasha la kwawa uwanja wa sokoine (Fund rising), ili kutafuta fedha za ujenzi wa bweni la wanawake. Waislamu wote wa Tanzania mkichangishana shilingi elfu tano kila mmoja mna uwezo wa kujenga chuo kikuu kikubwa kizuri.