WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Leo ni siku muhimu sana kwa watanzania.Tunajivunia kufikisha miaka 50 ya kuwa nchi huru.
Tukiachilia mbali siasa, nadhani leo ni siku ya kila mmoja wetu kufurahi apendavyo.
Ukiweza jumuika na wenzio mcheze, muimbe, mrukeruke. Ukiweza fanya tafrija ule
na kunywa na wenzio.Bahati mbaya sana, uchumi mifukoni hauruhusu.Labda tuwezeshwe!
Nimefuatlia sherehe zinavyokwenda, na nimefarijika angalau
kushiriki kwa macho ( kupitia TV).Waliostahili wamepokea nishani zao kwa michango
yao katika kuleta uhuru na pia kwa utumishi uliotukuka.Aidha baada ya kupokea
nishani hizo, basi ni raha tu.Watu wanajumuika pamoja kwenye cocktail,
na huenda labda kutakua na maakuli badae.Sijui.Mradi ni raha tu, watu wanatabasamu
kuashiria furaha wanajichanganya na kushiriki mazungumzo na kupongezana.
Katika yote haya, nimejikuta nawafikiria wananchi walio wengi na kujaribu kujiuliiza. Hivi miaka
50 hii, ni kwa vipi labda wangeweza nao kujisikia wanasherehekea? Je ni kwa kuangalia TV,
kusikiliza redio au ni kusubiri simulizi?Huenda wengine walibahatika kushiriki maonyesho yaliyokuwa
yanafanywa na wizara mbalimbali kwa zaidi ya mwezi mmoja, kuanzia viwanja vya Mnazi MMoja
na hatimaye kilele leo kule Viwanja vya saba saba. Huenda pia walishiriki kwenye mkesha
na kujionea fataki.Lakini sina uhakika ni vipi wananchi hata 50% wamefikiwa
na sherehe hizi ukizingatia hali ngumu ya maisha yanayozikumba familia nyingi.
Huenda ingepokelewa kwa wema sana kama serikali ingefanya matendo ya huruma kwa wanachi
katika kipindi hiki cha sherehe kama:
1. Kuwapunguzia angalau adha ya umeme,nauli nk
2. Kuwapa huduma mbalimbali bure kwa kipindi maalum
3.Kuziwajibisha taasis zile zenye usugu wa kero za wananchi mf. rushwa za matrafiki barabarani.
4.Kuteua shule kadhaa za mfano na kuziewekea huduma kama vile madawati ya kutosha,
kuwapa wanafunzi madaftari na huduma nyingine, kuwajengea waalimu nyumba za bei nafuu
5.Kujenga angalau barabara mbili kila kata za kiwango cha lami na kuzipa majina ya waasis wa uhuru
6. Kuweka mabomba na visima vyenye kutoa maji hasa maeneo yenye usugu wa maji n.k.
Hii ni kwa uchache tu.
Nadhani haya matendo yangekuwa alama ya kudumu katika vichwa na fikra za wananchi kila wakikumbuka
miaka 50 ya uhuru kuliko shughuli nilizoziona zikifanywa kuashiria miaka 50 - kwangu nahisi kama vile
kumbukumbu haitakuwepo.Khanga, tshirt, vipeperushi, siyo vitu vya kudumu.
Viongozi wangu wasikivu, hamjachelewa sana.Bado mnaweza kufanya haya matendo mkawagusa wananchi.
Pesa sidhani ni tatizo.Inahitaji nia na dhamira tu.Nia ikiwepo, njia itapatikana .