Tusherehekee na tufurahi pamoja sikukuu hii muhimu - miaka 50 ya uhuru si haba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusherehekee na tufurahi pamoja sikukuu hii muhimu - miaka 50 ya uhuru si haba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Dec 9, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Leo ni siku muhimu sana kwa watanzania.Tunajivunia kufikisha miaka 50 ya kuwa nchi huru.
  Tukiachilia mbali siasa, nadhani leo ni siku ya kila mmoja wetu kufurahi apendavyo.
  Ukiweza jumuika na wenzio mcheze, muimbe, mrukeruke. Ukiweza fanya tafrija ule
  na kunywa na wenzio.Bahati mbaya sana, uchumi mifukoni hauruhusu.Labda tuwezeshwe!

  Nimefuatlia sherehe zinavyokwenda, na nimefarijika angalau
  kushiriki kwa macho ( kupitia TV).Waliostahili wamepokea nishani zao kwa michango
  yao katika kuleta uhuru na pia kwa utumishi uliotukuka.Aidha baada ya kupokea
  nishani hizo, basi ni raha tu.Watu wanajumuika pamoja kwenye cocktail,
  na huenda labda kutakua na maakuli badae.Sijui.Mradi ni raha tu, watu wanatabasamu
  kuashiria furaha wanajichanganya na kushiriki mazungumzo na kupongezana.

  Katika yote haya, nimejikuta nawafikiria wananchi walio wengi na kujaribu kujiuliiza. Hivi miaka
  50 hii, ni kwa vipi labda wangeweza nao kujisikia wanasherehekea? Je ni kwa kuangalia TV,
  kusikiliza redio au ni kusubiri simulizi?Huenda wengine walibahatika kushiriki maonyesho yaliyokuwa
  yanafanywa na wizara mbalimbali kwa zaidi ya mwezi mmoja, kuanzia viwanja vya Mnazi MMoja
  na hatimaye kilele leo kule Viwanja vya saba saba. Huenda pia walishiriki kwenye mkesha
  na kujionea fataki.Lakini sina uhakika ni vipi wananchi hata 50% wamefikiwa
  na sherehe hizi ukizingatia hali ngumu ya maisha yanayozikumba familia nyingi.

  Huenda ingepokelewa kwa wema sana kama serikali ingefanya matendo ya huruma kwa wanachi
  katika kipindi hiki cha sherehe kama:
  1. Kuwapunguzia angalau adha ya umeme,nauli nk
  2. Kuwapa huduma mbalimbali bure kwa kipindi maalum
  3.Kuziwajibisha taasis zile zenye usugu wa kero za wananchi mf. rushwa za matrafiki barabarani.
  4.Kuteua shule kadhaa za mfano na kuziewekea huduma kama vile madawati ya kutosha,
  kuwapa wanafunzi madaftari na huduma nyingine, kuwajengea waalimu nyumba za bei nafuu
  5.Kujenga angalau barabara mbili kila kata za kiwango cha lami na kuzipa majina ya waasis wa uhuru
  6. Kuweka mabomba na visima vyenye kutoa maji hasa maeneo yenye usugu wa maji n.k.
  Hii ni kwa uchache tu.
  Nadhani haya matendo yangekuwa alama ya kudumu katika vichwa na fikra za wananchi kila wakikumbuka
  miaka 50 ya uhuru kuliko shughuli nilizoziona zikifanywa kuashiria miaka 50 - kwangu nahisi kama vile
  kumbukumbu haitakuwepo.Khanga, tshirt, vipeperushi, siyo vitu vya kudumu.
  Viongozi wangu wasikivu, hamjachelewa sana.Bado mnaweza kufanya haya matendo mkawagusa wananchi.
  Pesa sidhani ni tatizo.Inahitaji nia na dhamira tu.Nia ikiwepo, njia itapatikana .
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hii nii siku njema ya furaha na kwa kweli ya kufurahia.. ila sijui kama imesherehekewa na maadhimisho yameenda yalivyopaswa..
   
 3. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,301
  Likes Received: 953
  Trophy Points: 280
  Watu wengi hatujasherehekea kwa furaha sana, maana kibano cha maisha kipo pale pale. bidhaa zipo juu, umeme nao wameshaomba kupandisha pei ya unit kwa 150%, mavazi, na nauri za kwenda mikoani zinazidi kupanda kwa kipindi hiki cha mwezi 12.
   
 4. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndg yangu mi bado naomba chumvi kwa jirani. Labda kama nikipata cha jioni, sijui.
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  kama saa moja hivi ilopita nilizungumza na mdogo wangu akiwa 'kwa mama' na kumuuliza 'vipi sikukuu ya uhuru' akanijibu hakuna lolote la maana, hali ni ngumu. ni kama hakuna sikukuu tu.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Hatuwezi kusherehekea sawa kwa maana kuna wanaoshereheka wakiwa wanapiga mihayo huku wengine wakigonga glasi za wine,mvinyo na champagne,Sina maana mbaya ila kikubwa ni kutengeneza kwanza vitu vinavyoonesha UHURU kabla ya kukimbilia kushereheka kinafiki

  Nyerere aliwahi kuandika na kusema 'Freedom&Development' na akasema hivi vitu ni sawa na kuku na yai ...kusherehekea Uhuru ni kusherehekea matunda na maendeleo ya Uhuru wenu,sasa leo,reli ni ileile,maradhi,umaskini na ujinga vimekithiri na kibaya zaidi urithi wa nchi yetu umeporwa huku shilingi ikishuka...tunashereheka nini?ardhi kuuzwa?mgao wa umeme?kufeli kwa wahitimu wa kidato cha 4?kuwa na serikali ya mashemeji,maswahiba na nyumba dogo ama labda kuwa na serikali isiyokuwa na uzalendo kwa wafanyakazi wake na wastaafu?

  Niwatakie sherehe njema wale wote wanaoona kuna la kushereheka na niwape pole wenzangu kama mie tusiojua nini hatma yetu masaa kumi yajayo.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndiyo tutathmini tuone watu wanaonaje hizi sherehe na zilivyoenda Mkuu.

  Kweli kabisa.Maisha yanafinya sana.Sherehe kama hii inakuwa siyo kipaumbele kwa mwananchi wa kawaida.Je, ni sahihi kusema ni sherehe ya serikali zaidi, na siyo ya wananchi?

  Sikukuu ilikuwepo.Sema ushiriki wa mdogo wetu huyu ndio umekuwa hafifu kwa sababu ya hali ngumu.
  Kusherehekea kungeweza kufanyika bila pesa?
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kimsingi, tuko pamoja kiongozi
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi nimechinja mbuzi kufurahi uhuru wa Tanzania, nawahadithia wanangu maana ya uhuru ..

  Uhuru ni continues struglle ..uhuru kiuchumi, kuwa huru kimawazo etc..
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii Mkuu!Watoto wengi waliozaliwa kuanzia miaka ya 80 hadi sasa,
  hawaijui historia ya nchi yetu.Umefanya jambo jema sana la kuigwa.
  Niependa ulivyotumia siku ya leo kukaa hususan na watoto.
  Je ulijaaliwa kupanua wigo na kujumuika na walio nje ya familia yako?
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pasipo kwanza kuziba pakacha habari zingine zote ni ndoto.. Ufisadi ni adui wa kwanza wa uchumi wa nchi yetu na hata kuleta maisha magumu iwe umeme hadi dawati la mwanafunzi shuleni. Huoni sasbabu ya kusherehekea kwa sababu ya uongozi mbovu ambao umeleta adha hizi zote..Bila kurudisha Miiko na maadili ya viongozi kwanza na kuhakikisha yanafanya kazi hakuna kitu tunachoweza kubadilisha - Good Governance inasimama mbele ya kila kitu...
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa.
  Lakini huoni kuwa tukisema tusafishe kila kitu kibaya ndipo mengine yafate, hakuna kitakachofanyika?
  Naweza kulinganisha tatizo la taifa letu na Mzazi - baba/mama aliyewakosea watoto wake vibaya sana kiasi ambacho
  watoto wamekuwa wajasiri wakapiga kelele, wakaibua uozo wa wazazi wale, wakawachambua barabara.Wazazi wale wakaona aibu wee, mwisho wakazoea. Watoto wakaenda kushtaki kwa babu na bibi, babu na bibi kumbe nao walikuwa na madhambi yao.Matokeo wakaamua nao kukaa kimya.Wazazi hata hivyo wakaanza kufikiria, wakaona kweli watoto wana point.Lakini watoto wale wakaweka demands kubwa mno kiasi wazazi wale wakajiskia kukata tamaa.Wasifanye lolote.Unadhani kwa mfano watoto wale wangesema - 1.baba, mama, tunachohitaji ni mtulipie ada tu tuendelee na shule au
  2. Baba,mama mmefanya makosa mengi sana maishani, mmekuwa hamna msaada wowote hadi sasa hivi, tunaona aibu hata kuwaita nyie wazazi wetu. Mkitaka tuwaheshimu, basi acheni ulevi, jengeni nyumba bora, tulipieni ada, tuisheni, na mtununulie kila tunachohitaji.

  Katika 1 NA 2 kipi rahisi kufanyika?
  Samahani nimetoa mfano too simplistic kwa tatizo kubwa lakini ni
  kwa ajali ya kuchagiza majadiliano tu, in line with my thread.
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Uhuru ni mafanikio (tukio hilo ni vema likakumbukwa kwa juhudi zote na kwa raha zote), tulihitaji uhuru sana sana..

  Malengo ya uhuru kufikiwa au kutofikiwa ( ni jambo lingine ambalo litakuwa linabadilika kila wakati)

  Mimi naona watu wafurahie (tukio), wapambane na malengo ya uhuru..kufikiwa au kutofikiwa maana

  Malengo yanabadilika na wakati na mahitaji ya jamii..na hayana mwisho hadi kufa..
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  WoS,

  Hakuna au ni watawala wachache sana katika nchi hii wanaweza kufikiria katika huo mtazamo wako....Hayo mambo unayopendekeza hayajazi mifuko binafsi ya watawala na kwa hiyo hayawezi kupewa kipaumbele....

  Hebu jaribu kuuliza kiasi gani kimetumika kwenye hayo maadhimisho..Utashangaa,.. ila zaidi ya 50% zimeingia mifukoni mwa wakubwa na watendaji wengine walioshiriki kwenye maadhimisho hayo ....Kwa ufupi maadhimisho ya namna hii yanalipa sana katika mfumo wetu wa Bongoland!!!

  Bila mabadiliko ya msingi, naamini hakuna kiongozi yeyote yule serikalini anayeweza kufikiria mambo yanayaigusa jamii...Siyo leo tu bali hata miaka 50 mingine ijayo!!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  katika hili nadhani asilimia kubwa ya Watanzania tumepitia maisha haya. na hakika kwa kila uloyasema nimeyaona ktk maisha yangu sijui wewe. lakini Je, mafanikio yangu yametoka wapi? kwanza sikutaka kutazama nyuma wazazi wangu walifanya niniili niwalaumu isipokuwa kuyajua makosa waloyafanya na mimi nisiyarudie. Pili nimesoma kwa taabu sana wala sina haja ya kuyaweka hapa lakini siwezi kuwalaumu wazazi wangu kwa sababu hawakuwa na uwezo. Na kidogo walichokuwa nacho walinunua nyumba ya nyumba sita tukajirundika familia nzima ya watoto tisa..

  Leo hii kati ya hawa watoto tisa tupo tulokuwa na malengo mazuri na wengine wamepitia mitihani vile vile lakini sidhani kama kuna mmoja wetu anayewalaumu wazazi wetu kwa kutuzaa maskini ama kufanya makosa kwa sababu makosa waloyafanya ni ktk kuendesha maisha yao na mapenzi yao kwetu hayakuondoka hata wakati mmoja..

  Kifupi namshukuru Mungu sikuishi kama wao, nimetoka nje ya nchi na kutafuta riziki yangu ambayo ndivyo nilivyoandikiwa. Na ktk kujifunza na maisha nimegundua kwamba usafi unaanza kwangu, nyumbani kwangu na kwa kila nyumba ilokuwa safi yenye udhu ndivyo baraka huzidi kuongezeka. Ukiwa na roho ya kikorosho ukajiibia mwenyewe utakuwa unajidanganya mwenyewe maana mzazi wako kila kula raha na taabu zake anachosubiri yeye ni kuitengenza pepo yake...
  - Maasalaam..
   
 16. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I like this. Uhuru ni continuous struggle ... Sio kitu cha dakika moja. Ni kitu we people have to fight for continuously... Na kwa maana hii naona tunaweza kusema kua jana (in the 70's and 80's) tulikua huru kuliko leo (late 90's to date)...
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Duh! Waliozaliwa kuanzia 80 ni watoto! Kiasi Kikwete ajiite kijana
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Heheheheh.....Unashangaa kuwaweka waliozaliwa from 80s kundi la "watoto"? Nadhani umecheki context nilioandikia. Topical kasema alishinda na "wanawe" akiwaelezea historia ya uhuru etc. Sijui wanawe wana umri gani kwa kuanzia.Ndipo nikasema nilivyosema. Hata hivyo, by definition, waliozaliwa in the 80s ni watu wazima kwa kweli...lakini usisahau kwamba mtoto kwa mama/baba hakui na kwa nchi-mama, watabakia watoto hata wafikisha miaka 60 bado ni watoto wa Tanzania!..Kikwete kujiita kijana, sidhani kuna ubaya ( kama yeye aliwahi kijiita maana nijuavyo watu ndio humuona kijana).Mtu atajiita kijana/mzee anavyojisikia moyoni mwake.
   
Loading...