Miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika; Aluta Continua

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,196
Leo Tanganyika inasherehekea miaka 62 ya uhuru wa bendera toka kwa mkoloni wa Kiingereza.
Nakumbuka wakati tunapata uhuru Hayati Mwl. JKN, baba wa Taifa alisema, pamoja na uhuru huo, bado kama nchi tulikuwa na kazi ya kufanya kuendelea na mapambano dhidi ya maadui watatu wa nchi yetu ambao ni:

1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Inasikitisha sana kuona ni wachache sana ambao wanafaidika na matunda ya uhuru huu "bandia" kutokana na kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa wameshindwa kutuongoza vyema katika kukabiliana na maadui hao watatu wa Taifa letu.

Imefikia hatua wale tunaowaamini kutuongoza, wanakwenda kutumikia matumbo yao na ya familia zao pamoja na marafiki zao. Na kwa bahati mbaya sana wakishapewa dhamana, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi hizo hata baada ya kustaafu!

Maisha yanazidi kuwa magumu kwa watu wa hali ya chini huku viongozi na wafanyabiashara wakubwa wakizidi kujilimbikizia ukwasi pasipo kujali maumivu ya wananchi wenzao.

Hivyo kama Taifa, tunahitaji kubadili uelekeo, tufanye kila linalowezekana kuwaondoa madarakani viongozi hawa na badala yake tuweke wazalendo watakaokuwepo kwa ajili ya kusimamia maslahi ya wananchi wote kwa ujumla na kuhakikisha kila mwananchi anafaidi keki ya Taifa. Na hili kulifanikisha hilo, tunapaswa kufanya kila linalowezekana tupate Katiba mpya.

Katiba Mpya itatusaidia kuwadhibiti viongozi wetu na kuwafanya watutumikie kwa uzalendo na uadilifu, watake wasitake!

Mungu ibariki Tanganyika,

Amin.
 
Wewe hiyo neno Tanganyika umeutoa wapi leo, wakati viongozi walisema Tanzania Bara
 
Tanganyika ni taifa pekee lililokufa katika umri mdogo sana.
3yrs

images.png
 
Back
Top Bottom