Tupo Wenyewe Ulimwenguni?

Tupo Wenyewe Ulimwenguni?

Eeh mkuu umenifanya niwaze sasa, ila kweli kuna jambo hapo. Nimesoma flani kwamba hata kama kuna viumbe wengine, umbali kati ya nyota ni mkubwa mno hata kama wangekuwepo, hawangeweza kufika hapa. Na sisi pia hatuna teknolojia ya kufikia huko. Lakini kama ni kweli tupo peke yetu, basi hiyo inamaanisha sisi ni bahati sana kuwa na dunia hii nzuri. Haha, lakn hiyo bia ya bar unayoahidi ni poa, ngoja nikumbuke baadaye! kweli
 
Inawezekana kabisa tuko peke yetu, lakini bado hatuna ushahidi wa kutosha kusema hivyo.

Ulimwengu ni mkubwa mno, huenda uhai mwingine upo, ila umbali, muda na teknolojia vimetufanya tusiuone.

Siri kubwa si kama kuna viumbe wengine, bali ni njia ya gani tutaitumia kutambua uwepo wake🤔
Nanukuu: "Siri kubwa si kama kuna viumbe wengine, bali ni njia gani tutaitumia kutambua uwepo wake"
Hii imekaa vizuri na ndipo kwa kutokujua njia ya kutamba uwepo wake tunajikuta tunaishia kwenye Kuamini i.e. Imani. Kwa mfano tupotunaoamini uwepo wa viumbe wanaoitwa malaika, majini n.k. na hatujawahi kuwaona - tuaamini ivo ivo maisha yaendelee.
 
Mnaamini nyie na sio mimi bwashee
 
Katika kupiga hesabu zangu na kuziangalia nyota, kuwaza na kuwazua nimefikia hitimisho kuna uwezekano mkubwa tupo wenyewe huku ulimwenguni.

Dalili zote zinanionyesha uhai uliopo duniani, ni wakipekee na unaweza usipatikane popote pale ulimwenguni.

Kuna sababu nyingi zinazofanya niamini hivo, ikiwemo sayari nyingi kuorbit rwed dwarfs, cyano bacteria kuwa chimbuko la hapa kwetu na ukiangalia namna kila kitu kimekuwa tuned kwa mpangilio kuruhusu uhai hapa duniani.

Unadhani tupo wenyewe au huenda wapo wenzetu ambao hatuna tekinolojia ya kuwatambua kama wapo.
Unaambiwa mpaka kufikia hapa tulipo ki technology yetu yote na mwisho wa upeo wetu tuna uwezo wa ku explore only 5% ya vitu tunavyoviona ulimwenguni na kushika kama sio kuvifikia ila kuna kama 95% ni darkness hatuna uwezo bado wa kuviona au kuvishika kama sio kuvifikia..

Kuna stories kuhusu aliens hakuna science ya moja kwa moja ambayo imesha prove uwepo wao au kusema kua ni viumbe hai wengine wanao exist sayari nyingine, bado ni stories tu.. kama wapo na wana uwezo kweli kuliko binadamu why waishi au waje duniani kwa kujificha ficha, wanaogopa nini sasa kama wanamuogopa binadamu basi sisi ni bora zaidi kuliko wao..right.?!
 
Viumbe wengine wapo duniani hapa unadhani ni nani anayesimamia misingi ya dunia hii?
Kwann huwezi kutoka nje ya ufahamu wako au ukilusha kitu kinaludi chini hiyo nguvu ushawah kuiona VIUMBE WENGINE WAPO DUNIANI SIYO BINADAMU TU wapo viumbe wengi tu
 
Kwa jinsi ulimwengu ulivyokuwa mkubwa (infinite) na unavyoendelea kuwa expanded, bado tuna mengi ya kugundua na kujifunza, pasina shaka mbali na wale 👽 aliens tuliokwisha sikia fununu zao upo uwezekano wa viumbe wengine wa ajabu katika maeneo mengine ya hii observable universe tunayoweza kuiona tu achilia mbali sehemu zingine za mbali ambazo even with powerful telescope hatuwezi kuziona.
 
Kuna uwezekano mkubwa uhai mwingine upo mahali fulani katika Ulimwengu, lakini huenda si uhai wa aina yetu, huenda uko mbali sana, au bado hatuna teknolojia ya kuuona.

Mpaka sasa hatujamgundua mwingine lakini Ulimwengu ni mkubwa kiasi kwamba kusema “tupo wenyewe” ni hitimisho kubwa sana kutoka kwenye taarifa ndogo tulizonazo.

Kutokuwepo kwa ushahidi si sawa na ushahidi wa kutokuwepo.
 
Kwa jinsi ulimwengu ulivyokuwa mkubwa (infinite) na unavyoendelea kuwa expanded, bado tuna mengi ya kugundua na kujifunza, pasina shaka mbali na wale 👽 aliens tuliokwisha sikia fununu zao upo uwezekano wa viumbe wengine wa ajabu katika maeneo mengine ya hii observable universe tunayoweza kuiona tu achilia mbali sehemu zingine za mbali ambazo even with powerful telescope hatuwezi kuziona.
Habari za uwepo wa Aliens ni Myth, hawapo.
 
Back
Top Bottom