Tupo Wenyewe Ulimwenguni?

Tupo Wenyewe Ulimwenguni?

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
7,252
Reaction score
21,396
Katika kupiga hesabu zangu na kuziangalia nyota, kuwaza na kuwazua nimefikia hitimisho kuna uwezekano mkubwa tupo wenyewe huku ulimwenguni.

Dalili zote zinanionyesha uhai uliopo duniani, ni wakipekee na unaweza usipatikane popote pale ulimwenguni.

Kuna sababu nyingi zinazofanya niamini hivo, ikiwemo sayari nyingi kuorbit rwed dwarfs, cyano bacteria kuwa chimbuko la hapa kwetu na ukiangalia namna kila kitu kimekuwa tuned kwa mpangilio kuruhusu uhai hapa duniani.

Unadhani tupo wenyewe au huenda wapo wenzetu ambao hatuna tekinolojia ya kuwatambua kama wapo.
 
Ikiwezekana kama hao viumbe wengine wapo basi waje watutafute na kututembelea.
Inawezekana ni micro organism wanaishi huko, maana kule chenobly kuba bacteria zimeota kwenye extreme radiation.
Nadhani bacteria hao ukiweza wapeleka huko mars kuna possibility wakasurvive na miaka 100ml mbeleni huenda tukazungumza mengine.
 
Ulimwengu una mabilioni ya miaka, na unatanuka bila mwisho. Kadri unavyotanuka, kuna sehemu zinakosa nishati ya nyota.

Ulimwengu ni mkubwa sana. Sehemu tuliyoweza kuiona(observable universe) ni kakipande kadogo.

Inawezekana miaka mingi kabla dunia haijawa, ziliwepo sayari nyingine zenye maisha ila kwa sasa zina giza tupu. Inawezekana hili likatokea kwenye sayari yetu pia huko mbele.

Inawezekana kuna sehemu za ulimwengu ambazo hatujaziona zinahifadhi uhai. Ukubwa wa ulimwengu unaleta utata.
 
Hatuna uwezo huo kwa sasa.
Ila huenda kuna aliens
Hakuna kitu kama hichi wala hakijawahi kuwepo hii ni ideal tu ambayo imekua established ili kuhide demons channels, na kuinvert na kuwaita eliens lakin kiuhalisia hakuna eliens kwasababu wao wanadai awareness ya eliens ni beyond normal thinking ya binadam imekuaje tukaco-oparate na eliens hata 1/2 ya thinking capability yao hatujafkia
 
Hio ni dhana tu mshamba_hachekwi unafahamu dunia imepitia shuruba ngapi za kuiangamiza ila bado imesimama?

Unafahamu ili uhai uwepo basi ni kuwepo kwa perfect conditions ikiwemo gravity?
 
Hio ni dhana tu mshamba_hachekwi unafahamu dunia imepitia shuruba ngapi za kuiangamiza ila bado imesimama?

Unafahamu ili uhai uwepo basi ni kuwepo kwa perfect conditions ikiwemo gravity?
Kwa kuwa ulimwengu ni mkubwa sana, inawezekana hizo "perfect conditions" zilikuwepo, zipo ama zitakuwepo sehemu nyingine.
 
Inawezekana kabisa tuko peke yetu, lakini bado hatuna ushahidi wa kutosha kusema hivyo.

Ulimwengu ni mkubwa mno, huenda uhai mwingine upo, ila umbali, muda na teknolojia vimetufanya tusiuone.

Siri kubwa si kama kuna viumbe wengine, bali ni njia ya gani tutaitumia kutambua uwepo wake🤔
 
Hakuna kitu kama hichi wala hakijawahi kuwepo hii ni ideal tu ambayo imekua established ili kuhide demons channels, na kuinvert na kuwaita eliens lakin kiuhalisia hakuna eliens kwasababu wao wanadai awareness ya eliens ni beyond normal thinking ya binadam imekuaje tukaco-oparate na eliens hata 1/2 ya thinking capability yao hatujafkia
Haya sijakuelewa point yako
 
Back
Top Bottom