Tupeane ujuzi: Kabla ya kuoa, dada zetu na mama zetu wanayapokeaje mawazo ya sisi kutaka kuoa?

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Habari wanajamvi, poleni na majukumu ya kila siku!
.
.
niende moja kwa moja kwenye mada, kwa mara ya kwanza kusema nyumbani kuwa unataka kuoa, dada zako na mama walichukuliaje?.
.
.
binafsi mimi ni kijana wa miaka 30 kwa sasa, nina mchumba tayari, lakini imekuwa kila nikisema nyumbani hata kwa utani tuu kuwa inabidi nioe, nimekuwa nikipingwa sana kuwa nitafute pesa kwanza!!
.
.
hali hii imekua ikinishangaza sana, sikai nyumbani, ninajitegemea kwa muda wa miaka mitano sasa, ninakipato changu, si haba, kila nikipanga walau nioe ah kidogo nasitishwa, nyumbani mimi ni wa kiume peke yangu, na wa pili kuzaliwa, kuwasaidia yupo dogo ambae namsomesha chuo, hivyo sijasahau ya nyumbani,
.
.
imekua changamoto sana kwangu, maana tayari hapa nilipo nina mtoto ambae mama yake alikuja kuolewa, huu uzinzi siupendi, na kwa kwetu wanaume ni ngumu sana kujizuia,
.
.
nimekua nikiwaza au labda wao wanaona ni kawaida kulala na wanawake tuu, inakuaje? maana nimeuliza mpaka lini, jibu ni tafuta pesa kwanza!!
.
.
naombeni mnipe ujuzi, Je ni kawaida kwamba mama na dada zetu huwa hawapendi hizi taarifa za ndoa.?
.
.
Je tufanyaje?
 
Back
Top Bottom