Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Wanaomuita wanajua kaishashinda ndio maana wanatafuta sababu tu. IJP anasema afike polisi Kilimanjaro. Barua afike polisi kaenda maalumu hiyo yote ni mashinikizo.
Hakuwa na flyover, sgr sticker, vituo vya afya, madaraja,wala kushinda corona hata siku moja hakupiga goti kuomba kura. Sasa hivi vyote anavyo na kavinadi miaka mitano kwenye vyombo vya habari lakini kaona havimsaidii kaamua kupiga goti.
Mwenzie anasubiriwa mpaka giza na umati mkubwa wa watu. Pale hakuna msanii wa kutumbuiza zaidi ya mziki wa DJ. Pale watu hawazuiliwi kutoka kama kule ukiingia inakuwa mateka. Mgombea akianza hutuba foleni ya kutoka inaongezeka kwani wanajua ndio mwisho wa burudani.
Huku kwa Lisu kusudio la wananchi ni Lisu mwenyewe akiongelea kuhusu ustawi wao haki zao na maendeleo yao.
Mie ni mlemavu wa kufungulia TBC1 Lisu hana coverage kubwa lakini cha ajabu wananchi wanajaa kwenye mikutano yake.
 
Jibu lako linarudi kwenye maana hiyo ya kuwa kwa vile Lissu ni mgombea, basi yeye yuko juu ya sheria. Lolote atakalofanya la kuvunja sheria za nchi hailiwezi kuchunguzwa na vyombo vha sheria vilivyopo bali tume ya uchaguzi tu: myopic view of the law hata kama unadhani wengie hatujui sheria. Polisi hawajasema Lissu ana jinai yoyote ndiyo maana wanataka kumhoji kuona kama kweli kuna suspicion ya jinai au la; wanaoamua kuwa Lissu kavunja sheria za jinai ni mahakama siyo polisi.
Teavher kwenye hili tulia na kulifuatilia vizuri... gukizungumzia utii wa sheria raia hakuna aliye juu ya sheria hata mmoja.. kwahiyo tunaposimamia sheria basi tusimamie kisheria... ndio maana hata kama mtu akitenda jinai kama atasumbuliwa bila sababu wakati wa kukamatwa kwake polisi anakua amevunja sheria..

Kwa suala la Lissu polisi ndio wamenza kuvunja sheria jee wao wapo Juu ya Sheria?

Na je Mkuu ukipokea wito wa Polisi kutaka wakakuhoji kwa nini haumnunuliagi OCD bia, utaenda?
 
Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
Yaani wewe ndiyo una mashaka na uanasheria wa Tundu Lissu, inadhuru nini?
Umesoma alichojibu Tundu Lissu au ulikiruka kwa kuwa haumpendi?
Amesema hivi;
Barua ya Polisi siyo wito wa kirafiki ni tamko la kisheria.
Hapo amekiri jinsi utendaji wa Polisi ulivyo na nguvu kisheria lakini ili nguvu hizo za kisheria za jeshi hilo ambazo limepewa na sheria, ziwe ngyvu kweli na halali, nalo linapaswa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Unapomtaka aende, anaenda vipi? Aende kwa kufuata wito uliotolewa kinyume cha sheria? Wito wa Kirafiki?
 
Tundu Lissu katika Ukurasa wake wa Twitter, ameweka Barua ya Polisi na kuandika Maneno haya "Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho."

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro
View attachment 1587622
View attachment 1587514
Amkamate jiwe kwanza anayetishia wapiga kura huko tunduma
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Kwa sheria ipi wewe?Acha kukariri desturi za kigaidi za Polisi.Kwa hio wewe sa hivi askari anaweza kukuta tu uende kituoni kumsalimia?
 
Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
Haijalishi sababu.Ni lazima hata polisi anapokukakamata akutamkie kosa lako.Haweza kukwambia Maelezo utakuta Polisi.Hawezi kukupotezea muda.Kama anataka kukuhoji anakufuata wewe mahali ulipo na kukuhoji na iwapo kuna sababu ya kukuweka kizuizini ndo anatafuta kibali cha kukukamata.Watanzania amkeni msiwe kama mbuzi kwenye banda.
 
Back
Top Bottom