Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
IMG_8063.jpeg
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Rais anayesaini mikataba ya hovyo kuliko hata wa Chifu Mangungo; anayegawa bandari zetu zote na nia za usafirishaji kisirisiri kwa wageni; anayelazimisha Bunge kubariki uharamia huo, na anayenyang'anya watu wetu ardhi zao na kuwapa wageni, anastahili kukosolewa kwa staha gani?

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

IMG_8067.jpeg

Barua ya wito wa Polisi


====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
 
Back
Top Bottom