Tundu Lissu apuuza wito wa DCI Kingai, asema hatoenda ofisini kwake

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Tundu Lissu.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewasili nchini leo Julai 26, 2023 kutoka Ulaya.

Akihojiwa juu ya kuitikia wito wa DCI Kingai unaomtaka afike ofisini kwa mahojiano, Lissu ametoa kauli inayoashiria kuwa hatakwenda.

“Kwenda (kwa DCI) kufanya nini? Unapoitwa na Polisi mahali popote lazima polisi akuambie anakuitia kosa gani. Ile barua imesema kuna kosa? ……”

Baada ya kutoa kauli hii Lissu aliondoka. Kauli hii inatoa tafsiri kuwa Mwanasheria huyo nguli hatokwenda ofisi ya DCI iliyompa wito wa kufanya naye mahojiano kufuatia matamshi aliyotoa kama alivyonukuliwa akisema kauli za Rais ni matope.

Pia soma: Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili
 
Hili liwe fundisho kwa mamlaka, wanapoleta maigizo yao, waangalie wanamuigizia nani, sio kujikurupukia tu, huwezi kumtisha mwanasheria, kwenye jambo linalohusu sheria, kienyeji.

Lissu itakuwa baada ya kupokea ile barua akajiuliza hivi naenda pale kufanya nini? kwani sheria inasemaje? akaona ujinga huu, siendi popote.

Walishaambiwa kuna watu wakuwatisha, lakini kwa Lissu aliyeonja mpaka ladha ya risasi zao zaidi ya kumi na sita, huyu kucheza nae kunahitaji akili ya ziada, wala sio hayo maigizo yao waliyoyazoea kila wakati. Kingai aibu kwake.
 
Hili liwe fundisho kwa mamlaka, wanapoleta maigizo yao, waangalie wanamuigizia nani, sio kujikurupukia tu.

Lissu itakuwa baada ya kupokea ile barua akajiuliza hivi naenda pale kufanya nini? kwani sheria inasemaje? akaona ujinga huu, siendi popote.

Walishaambiwa kuna watu wakuwatisha, lakini kwa Lissu aliyeonja mpaka ladha ya risasi zao zaidi ya kumi na sita, huyu kucheza nae kunahitaji akili ya ziada, sio hayo maigizo yao waliyoyazoea kila wakati.
Kwenda kwa DCI kufanya nini? Unapoitwa na Polisi mahali popote lazima polisi akuambie anakuitia kosa gani. Ile barua imesema kuna kosa? ……”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewasili nchini leo Julai 26, 2023 kutoka Ulaya.

Akihojiwa juu ya kuitikia wito wa DCI Kingai unaomtaka afike ofisini kwa mahojiano, Lissu ametoa kauli inayoashiria kuwa hatakwenda.

“Kwenda (kwa DCI) kufanya nini? Unapoitwa na Polisi mahali popote lazima polisi akuambie anakuitia kosa gani. Ile barua imesema kuna kosa? ……”

Baada ya kutoa kauli hii Lissu aliondoka. Kauli hii inatoa tafsiri kuwa Mwanasheria huyo nguli hatokwenda ofisi ya DCI iliyompa wito wa kufanya naye mahojiano kufuatia matamshi aliyotoa kama alivyonukuliwa akisema kauli za Rais ni matope.

Pia soma: Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili
Anajimwabafai.
 
Hili liwe fundisho kwa mamlaka, wanapoleta maigizo yao, waangalie wanamuigizia nani, sio kujikurupukia tu, huwezi kumtisha mwanasheria, kwenye jambo linalohusu sheria, kienyeji.

Lissu itakuwa baada ya kupokea ile barua akajiuliza hivi naenda pale kufanya nini? kwani sheria inasemaje? akaona ujinga huu, siendi popote.

Walishaambiwa kuna watu wakuwatisha, lakini kwa Lissu aliyeonja mpaka ladha ya risasi zao zaidi ya kumi na sita, huyu kucheza nae kunahitaji akili ya ziada, wala sio hayo maigizo yao waliyoyazoea kila wakati. Kingai aibu kwake.
Tungekuwa na watu kama Lisu 50 Tanzania ingekuwa mbali sn
 
Back
Top Bottom