Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Lissu ndiye yuko juu ya sheria !!! Kiasi muda huu uko huru kutumia lugha ya "faragha" hadharini!? Mna taabu ninyi...Kha!!
Hayuko juu ya sheria, na ndio maana ametaka na polisi nao wafuate sheria. Unataka kutushawishi kuwa tamko lolote la polisi hata ukiambiwa leo hakuna kulala ni sheria lazima utii?
 
Unazungumzia matamshi ya kumwambia Magufuli mwizi? Kwani ni uongo?
Kama hujui ni kuwa kisheria hiyo inaitwa defamation, na lissu anajua fika kuwa anavunja sheria ila kwa sababu haheshimu sheria zetu za Tanzania anajifanyia atakavyo. Sijui kama akipata madaraka atazilindaje kama haziheshimu akiwa mgombea.
 
Tatizo siyo IGP, tatizo ni Lissu kuamini anajua shréria kuliko yeyote nchi hii. Hiyo sheria yake sijui kama anakumbuka hata majukumu ya polisi ni yapi! Ni mwepesi wa kutunga hata sheria isiyokuwepo. Angeweza kuwa rais iko siku atauliza sheria inayomlazimisha mtu kutumia choo.

Kama TL hajui sheria hebu nieleze toka umjue ameshtakiwa mara ngapi na waliweza kumshinda kesi mahakamani mara ngapi, jana wamesema hawana shida naye tena mpaka uchaguzi uishe je unajua uamuzi huo umekuja kwa sababu gani?
 
Utapata tabu sana mwaka huu kwani matusi yote yaliyojaa ubongoni mwako utajikuta huna pa kuyatumia tena.
Upumbavu si tusi bali ni hali ya akili kupumbaa, ni mjinga asiyejijua kuwa ni mjinga maana akijua kuwa mjinga atafuta ujinga. Mpumbavu ni mjinga anayejiona anajua kwa hiyo hawezi kufuta ujinga wake so kapumbaa.

Kutuaminisha na wewe kuamini kuwa upinzani haufai, una makosa always ni upumbavu to the highest degree. Inatosha kusema unafanania, je bado unaona ni matusi?
 
Kama hujui ni kuwa kisheria hiyo inaitwa defamation, na lissu anajua fika kuwa anavunja sheria ila kwa sababu haheshimu sheria zetu za Tanzania anajifanyia atakavyo. Sijui kama akipata madaraka atazilindaje kama haziheshimu akiwa mgombea.
Kumpa tenda mume mwenza kujenga uwanja mkubwa wa ndege kijijini kwake ni wizi.

Vitambulisho vya machinga kuwauzia kwa 20,000/- kwa watu 1,000,000 tu ni shilling trillion 2 ambazo hazikaguliwi na CAG, na hajulikani zinaenda mfuko gani.

Kwa uchache tu
 
Huku ndio kuanguka kwa CCM.

MZIGO MZITO HAUCHUKULIKI
Lissu1.JPG
 
Kama hujui ni kuwa kisheria hiyo inaitwa defamation, na lissu anajua fika kuwa anavunja sheria ila kwa sababu haheshimu sheria zetu za Tanzania anajifanyia atakavyo. Sijui kama akipata madaraka atazilindaje kama haziheshimu akiwa mgombea.
Magufuli haheshimu katiba ya nchi sembuse sheria!
 
Hapo anakosea sana, Lissu unafanya makosa ya kijinga, unavunja sheria kwa makusudi ili ufanye ubishi, unafundisha watu kutoheshimu sheria.

Wewe umeshaamua kuwa lazima uwashe moto nchini na uvunje amani. Haitakubalika, lazima utii amri na sheria, unapoonewa tutakupigania, lakini ukionea tutaka sheria ichukue mkondo wake.
Na akiwa mkuu wa nchi atawezaje kuongoza nchi ambayo watu watakuwa huru kuvunja sheria?
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa, kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, maelezo utayakuta polisi na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote.

Jee pia kisheria polisi polisi wanaweza kukuita na unapoitikia wito kituoni ukawa huonekani kutoka tena? Maana tumeona mara nyingi hasa visiwani watu wakiitikia wito vituoni huwa hawaonekani kutoka vituoni na wahusika huanza kurushiana mpira kila mmoja akijidai kuwa hajui kinachoendelea na kuelekeza watu kwenda kumuuliza mtu mwengine.

By the way umesema kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, unaweza kutuelimisha zaidi juu ya hili? ni sheria gani, numba gani ya mwaka gani na inaweka wazi nini juu ya kuitwa mtu kituo cha polisi na anatakiwa mtu aitikie wito katika masaa mangapi baada ya kupokea wito n.k.
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa, kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, maelezo utayakuta polisi na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote.
Hii ni kwenye ipi?kwanini polisi wapewe mamlaka ya kumuita mtu yoyote yule?bila kumweleza kosa lake?
 
Yanajirudia yaleyale,hawa Polisi warudishwe shuleni kutoa ujinga wao kichwani,hizi ni aibu kwa wale wanaowateua
 
Back
Top Bottom